Mgomo wa Vyuo Vikuu ni Matokeo ya Uzembe wa Watawala
Na Happiness Katabazi
JUMAMOSI iliyopita, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Pro.Rwekaza Mukandara alitoa tamko la Chuo hicho la kuruhusu wanafunzi wote kurejea masomoni isipokuwa viongozi wao 56.
Kwa kiasi kikubwa uamuzi huo umetekeleza masharti yaliyotolewa na vyama vya siasa kwamba wanafunzi warejeshwe vyuoni bila masharti.
Tamko la chuo lilisema kwamba japokuwa asilimia 41 tu ya wananchuo wote ndiyo waliotekeleza masharti yaliyokuwa yametolewa na chuo na chuo sasa kimeamua kuwarejesha masomoni wanafunzi wote bila kujali kama wamelipa au hawajalipa asilimia 40 ya ada kwa wale wa mwaka wa kwanza na fedha za matibabu kwa wote.
Kulingana na tamko hilo chuo kiko tayari sasa kushirikiana na bodi ya mikopo kuchuja wanafunzi ili wapatiwe mikopo kulingana na mahitaji.
Kwa wachunguzi wa mambo tamko hilo la Professa Mukandara limeonyesha wazi jinsi gani uzembe wa watawala unavyoweza kuliletea taifa hasara.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, peke yake kimepata hasara ya Sh Milioni 100 kila siku tangu kilipofungwa April 17 mwaka huu.Kiasi hicho ni jumla ya bilioni tatu.Hiki ni kiasi kikubwa sana ukilinganisha na Sh Milioni 500 ambazo wangelipwa wanafunzi kama madai yao ya gharama ya mafunzo kwa vitendo walipwe.
Ni jambo la kushangaza kama watawala wa chuo au hata serikali wanaamini kuwa dai la nyongeza ya gharama ya elimu kwa vitendo kutoka sh 3,500 hadi 6,500 wanazodai hazilingani na gharama halisi.Ukweli ni kwamba kiasi walichodai wanafunzi ni kidogo mno kulingana na gharama halisi za maisha.
Tujadili hoja ya gharama za elimu ya Juu sera ya kuchangia haipo tena.Wanafunzi na wazazi wao wanalipia asilimia 100 na serikali haichangii chochote.
Hayo ndiyo mantiki ya sheria ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ya mwaka 2004.Kwa mujibu wa sheria hiyo gharama yote ya elimu ya juu itabebwa na mwanafunzi mwenyewe na mzazi wake mfadhili wake.
Serikali inawajibika kuipatia bodi ya mkopo kiasi cha fedha kinachotosha mikopo ya wanafunzi waliodahiliwa na vyuo vikuu.
Mgogoro uliopo hivi sasa ni matokeo ya uongozi wa serikali ya awamu ya nne kukiuka sheria ya uanzishwaji wa bodi ya mikopo ya mwaka 2004.Serikali ya awamu ya nne imetafsiri mikopo ya wanafunzi kuwa ni ufadhili(scholarship) na hivyo kuamuru kuwa kigezo cha kutoa mkopo kiwe daraja kwanza kwa jinsia zote na daraja la kwanza na pili kwa jinsia ya kike.
Sasa sio tu kwamba serikali haikuwa na mwelekeo wa kutoa amri hiyo kwa mujibu wa sheria ya bodi ya mikopo bali amri hiyo ilinyang’anya bodi ya mikopo madaraka na wajibu wake wa kuchuja na maombi ya mikopo ya wanafunzi walikanga na kigezo cha mhitaji.
Matokeo ya hili ni kwamba serikali kupitia bodi ya mikopo ilijikuta inatoa mikopo kwa waombaji wasiyostahili na kuwanyima wake wanaostahili.
Tamko la Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mukandara kuwa sasa kigezo kilichowekwa na sheria ya mikopo ya wanafunzi kitafuatiwa au kuzingatiwa ni jambo jema lakini pia ni ushaidi kuwa utawala wa chuo na serikali unakiri makosa yake.
Hivi ndiyo inatufanya tuone kwamba kuzuiliwa au kufukuzwa kwa viongozi 56, si sahii na ni mwendelezo wa kiburi cha watalawa.Wao wanataka ‘Kondoo wa kafara’ watakaoikosha serikali na uongozi wa chuo ili wasionekane kuwa wamekosea au kushindwa.
Tujiulize kama hao viongozi wa chuo wana elimu mwafaka kuhusu Utawala Bora?. Je si wakati mwafaka sasa wa kuanzisha chuo cha viongozi?.
Tunajua fika uongozi wa sasa wa wanafunzi wa UDSM ni mpya na bila shaka usio na uzoefu na maharifa ya uongozi.'Kubangaiza' kama ambavyo uongozi huo umefanya sasa katika suala hili la mgomo wa wanafunzi kunaweza kiliangamiza taifa au kuliletea hasara kubwa.
Tuwaombe sasa viongozi Chuo wameze wembe au kiburi chao kwa kuwarejesha viongozi wa wanafunzi na kisha kukaa nao kujadili matatizo ya wanafunzi ili ufumbuzi unaokubalika na pande zote upatikane.
Tunachokiona hivi sasa ni kuzuka kwa mtafaruku mpya pale wanafunzi watakaporejea na kujikuta hawana viongozi na hivyo kuanza madai kuwa viongozi wao warejeshwe.
Mlipuko utakaotokana na hili unaweza ukawa mbaya zaidi kwakuwa viongozi halali wa wanafunzi watakuwa hawapo na hivyo harakati hizo zinaweza kukosa nidhamu na zikaleta uharibifu,ghasia,majeruhi na hata vifo.
Ieleweke wazi kwamba nyakati zimebadilika na akili na mioyo ya watu imebadilika.Huu siyo wakati wa utawala wa kidkteta na huu siyo wakati wa kutishiana na ‘mashushushu’ kujaza makachero UDSM au hata FFU kunaweza kukawa chanzo cha hali ya wasiwasi na kuhatarisha amani na utulivu ndani ya vyuo vikuu.
Busara na hekima iwarejee watawala wa Chuo Kikuu watambue wajibu wao wakuwalea vijana na kuwaelimisha.Busara na hekima hiyo hiyo iwarejee viongozi wa Wizara ya Elimu ya Juu na serikalini kutambua wajibu wao wa kutumia kodi ya wananchi kuakikisha kwamba watoto wa Tanzania wanapata elimu.
Hasirani isiwe utamaduni wetu kwa kiongozi au raia kufikiri kwamba nchi hii inaweza kuongozwa kwa vitisho kwa mfano, wapo viongozi wamesikika wakisema mgomo wa wanafunzi wa vyuo vikuu umechochewa na vyama vya upinzani.Hao ni wazushi ,wasanii na wachochezi wakubwa.
Hawa hawaoni mzizi wa mgomo huu katika kushindwa kwa serikali kutekeleza sheria ya nchi kuhusu mikopo ya wanafunzi.Hawa hawana hata busara ya kuona kuwa ahadi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete, pale Dimond Jubilee ilikuwa ndiyo kichocheo kikubwa cha mgomo huu.
Je ni vyama vya upinzani vilitoa ahadi alioitoa Rais Kikwete, kuwa hakuna mtoto wa maskini atakayefukuzwa kwa kukosa ada?. Je ni vyama vya upinzani vilivyowakusanya wanachuo 2500 pale Dimond Jubilee kuwa kirimu kwa kapero na fulana zenye rangi ya njano na kijani na kuwazawadia wasomi hao kadi za kujiunga na UVCCM?
Je Professa Mkandara na Waziri wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolwa hawakuudhulia tukio hilo?Nani sasa anafanya siasa vyuoni au chama gani kinafanya siasa vyuoni?
Tuelewane watoto wanaosoma vyuo vikuu wengi wao ni watoto wa Watanzania,wanaweza kuwa na vyama au wasiwe navyo lakini itakuwa ni Uhayawani mkubwa kuwanyanyasa na kuwavunjia haki zao za kibinadamu kwa sababu yoyote ile.
Mungu ibariki Afrika,Mungu inusuru Tanzania
O755312859:katabazihappy@yahoo.com:www.katabazihappy.blogspot.com
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano Mei 16,2007

4 comments:
Keep it up .You seems to be a serious woman i do appreciate what your doing.
Dont allow money to drive your way of thinking but you have to drive money by ur self.
Mtandao w ccm unatumia sana pesa hivyo usiw mtu wa kununulika kwa urais kwani fikra pevu ndio msingi wa mafanikio.
je umeolewa? ama una mchumba?kwani kazi yako imenifanya nikupende.
Mh jamani hiki chuo kikuu basi kifungwe moja kwa moja wampe Muhindi wao. Maanake hao viongozi wanaonyanyasa watoto wa walipa kodi wao hawajali walishapata kura zao na kodi zao, Na on top of that scholarship zote zinazotoka wanawapa watoto wao waende ulaya, Halafu huku wanawahunia watoto wa Tz tena hapo hapo nyumbani, So go figure wale wanaowapeleka Asia kusoma sio ndio wanawasahau kabisa, Mh jamani this is so sad Lakini raisi yeye anaona jambo la maana ni kulalamika kuwa waandishi wa habari hawampi heshima, sasa wampe heshima ya nini wakati yeye hafanyi kazi yoyote ile. Asafiri tu. Mh na wazungu wanamkaribisha wanamuona mshamba tu hana akili. Yaani ni aibu kweli akifika ulaya na wakati the only University in his country imefungwa na yeye anatabasamu tu, this is what white people call NIGGER.
Post a Comment