Header Ads

ANSBERT NGURUMO CHALI

Na Happiness Katabazi

NGURUMO ni Mwandishi wa habari Mwandamizi nchini na ni Mwandishi wa Safu maarufu ya "MASWALI MAGUMU "  Katika  Gazeti la Tanzania aliwai Kuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti  hilo na ni miongoni mwa waandishi waanzilishi wa Gazeti Hilo la Tanzania Daima.

Ngurumo alikuwa  ni mgombea Ubunge ndani ya Chadema jimbo la  Jimbo la Muleba Kaskazi Mkoani Kagera. Jimbo Hilo lilikuwa likiongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage.

Leo umefanyika uchaguzi wa kula za maoni wa Chama hicho na kwa upande wake ameshindwa kutimiza ndoto yake ya Kuwa mbunge baada ya kuangushwa  vibaya na mpinzani wake ndani ya Chama hicho aitwaye  Injinia Najim Kassange kula 247 na Ngurumo amepata kula 55. 

Kwa Matokeo hayo ni wazi zile ndoto za Ngurumo kwenda Bungeni zimeyeyuka. 

Ila Chadema na nyie hata huruma kidogo hamna kwa kaka yangu? Kuwapiganieni kote kule kupitia makala zake lakini mmempa za uso?

Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu mwishoni mwa wiki alikuwepo huko jimboni kaja kumnadi Ngurumo na akamsifia sana  ni kiongozi makini lakini mkapuuza Lissu na Leo mkambwaga vibaya hivi Ngurumo?Aisee Mnatisha sana  Chadema Muleba Kaskazini.

Pole Ngurumo hiyo ndiyo siasa na hiyo ndiyo Demokrasia, nisisikie unahama CHADEMA eti kwasababu hujapitishwa  Kuwa Mbunge, vumilia huko huko.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi.
21/7/2015

No comments:

Powered by Blogger.