Header Ads

WABUNGE UKAWA WALIOADHIBIWA NI WAHUNI TU



Na Happiness Katabazi

NENO Mhuni Utumiwa kupachikwa Mtu yoyote anayefanya matendo ambayo Si ya kistaarabu na kuungwana Mbele ya Jamii iliyostaarabika ,heshimika na inayojari Utawala wa sheria na Kanuni na asiye heshimu mamlaka wala kiongozi anayemuongoza mahali pake pa Kazi.

Nimelazimika kutumia neno la Mhuni kwasababu makala yangu ya Leo Inajadili uamuzi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa Adhabu ya kuwasimamisha idadi hiyo ya wabunge kutoudhuria Katika vikao Vya Bunge vilivyosalia kabla ya Julai 9 Mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge Hilo baada ya wabunge Hao Kukiri Kutenda vitendo Vya kihuni (utovu wa nidhamu ) ndani ya Bunge.

Baada ya kuwakuta na hatia kushindwa kuheshimu Kiti cha Spika na kupiga makelele ovyo Mithili ya watu waliopandisha Mapepo au wagonjwa wa Maradhi ya akili.

Spika Makinda alisema ametumia Kifungu cha 74(1) cha Kanuni za Bunge kuwadhibu wabunge hao.

Bila kumung'unya maneno Mimi binafsi nawaita wabunge hao WAUKAWA  ni wahuni kwasababu  mhuni siku zote ni mtu asiyetaka kuheshimu Sheria na Kanuni na kufanya vitendo vya kihayawani ambavyo  vinamshushushia heshima hata yeye binafsi Mbele ya watu waliostaarabika.

Hivyo wabunge hao wahuni ,uhuni ule walioufanya ndani ya Bunge wakuoiga makelele utafikiri wamekumbwa na Mapepo wachafu 'Mashetani" siyo tu umelipaka matope Bunge letu Kuwa Kumbe ndani ya Bunge letu tuna wabunge (watunga Sheria/Kanuni) ni wahuni,na uwenda wana Kichaa cha muda ' Temporaly Insanity' ambao hawajui Sheria na Kanuni wanazozitunga na hawaziheshimu na ni vinara wakazivunja na Spika Makinda amekiri Hilo Kuwa Bunge hilo la 10   Lina malizika lakini wabunge Wengi hawajui Kanuni. Nimechoka kabisa.

Maana Mtu mwenye akili timamu kichwani hawezi kufanya ushenzi uliofanywa na wabunge Hao wa UKAWA ndani ya Bunge. Ni ayawani na MTu mwenye wazimu kichwani ndiyo anaweza kufanya uhuni ule wa kupiga makelele ndani ya Bunge na kudharau mamlaka ya Spika wa Bunge kwa Kiwango kile kilichofanywa na wabunge hao wahuni toka UKAWA wiki iliyopita ambao Kutwa wamekuwa walijinasibu Kuwa wanaweza kuongoza Tanzania.Ajabu.


Zaidi ya  Wabunge  40 wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni (Ukawa), wamepewa adhabu ya kutoingia vikao vyote vya bunge hadi litakapovunjwa na Rais, Julai 9, kulipwa nusu mishahara na posho.

Jumla ya wabunge wa upinzani  90, waliotolewa siku ya kwanza (Julai 3) ni 11, na Julai 4 ni 35 hivyo kufanya idadi ya waliofukuzwa kuwa 46, huku 43 ambao hawakuwepo ndani ya Bunge kutoguswa na adhabu hiyo. 


Hatua hiyo imefikiwa baada ya wabunge hao kuwa kwenye harakati za kupinga miswada mitatu ya mafuta na gesi, kuingizwa bungeni kwa hati ya dharura na kujadiliwa kwa pamoja. 

Julai 3 Mwaka huu. wabunge 11 walitajwa kwa utovu wa nidhamu Bungeni, na kati yao, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini na Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa, wamepewa onyo baada ya kujutia makosa yao.

Waliotimuliwa Ijumaa iliyopita  ni John Mnyika (Ubungo), Tundu Lissu (Singida Mashariki) na Pauline Gekulu ( Viti Maalum) wote wa Chadema.
Wengine ni Filex Mkosamali (Muhambwe) na  Moses Machali (Kasulu Mjini) wa NCCR-Mageuzi.Wabunge  wawili wakipewa adhabu ya kutohudhuria vikao viwili.

Miswada iliyozua mtafaruku ni ule wa Sheria ya Petroli wa mwaka 2015, Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa mwaka 2015 na Muswada wa Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji wa mwaka 2015.

Spika Anne Makinda akifafanua hoja hiyo, alisema wabunge hao hawajui kanuni, "nilitamani mjue kusoma kanuni, nilifikiri mnajua kumbe tunamaliza kipindi wala hamjui, mngekuwa mnajua utaratibu wa kupinga kikanuni upo, tumefanya miswada mingi sana inasomwa kwa wakati mmoja...nipeni muda niwaletee orodha ya miswada hiyo."

Alisema kanuni zinaruhusu kwa kuwa maudhui ya miswada ni mmoja, hivyo hakuna kanuni iliyovunjwa.

Spika Makinda alisema kuwa ametumia kanuni ya 74(i) kuwatimua wabunge hao kwa kushindwa kuheshimu kiti kwa kupiga kelele.

Kwa siku tatu mfululizo, Spika Anne Makinda amekuwa akipata shida kuendesha chombo hicho cha kutunga sheria kutokana na mbinu waliyogundua wapinzani ya kupiga kelele kukwamisha shughuli za Bunge.

Ijumaa iliyopita Spika Makinda,  aliamua kuwapeleka wabunge 11 mbele ya Kamati ya Maadili kwa makosa ya kudharau kiti chake na chombo hicho kikaibuka na adhabu ya kuwafungia wabunge wanne kutohudhuria vikao vyote vilivyosalia, wengine wawili kufungiwa vikao viwili.

Hakuna ubushi Kuwa Bunge hili lililoongozwa na Spika Makinda tulishuhudia mazuri na vitendo Vya utovu wa nidhamu Mara kwa Mara vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya wabunge ambao hawa jiheshimu kwahiyoa lugha zisizofahaa na kubishana na Spika wakati mwingine bila kuwepo na Sababu za Msingi za kufanya hivyo.

Tulimshuhudia Spika Makinda na hiyo Kamati yake wakiwachekea sana na kulea vitendo vile Vya kihuni vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya wabunge ikiwemo Kuzusha vurugu ndani ya Bunge na kusababisha vikao Vya Bunge kuahirishwa   kwasababu ya  vurugu, matumizi ya lugha chafu hali iliyosababisha heshima ya Bunge letu kuporomoka na Makinda kushindwa kuwachukulia Hatua na Kuishia Kulalamika tu utafikiri kulikuwa Hakuna Kanuni za kuwashughulikia wabunge wahuni wanaovunja Kanuni.

Hali iliyosababisha baadhi ya watu kuanza kumhisi vibaya Spika Makinda Kuwa enda Ananufaika na vitendo hivyo Vya kihuni na utovu wa nidhamu uliokuwa ulifanywa na baadhi ya wabunge Ndio maana Bunge lake lilikuwa linashindwa kutumia Kanuni kuwashikisha adabu.

Na baadhi ya wasomi Washeria chinichini walifika hatua ya Kusema kuna haja ya kufanyika Mabadiliko ya Kikatiba ili Nafasi ya Spika ishikiliwe na Spika ambaye amesomea fani ya Sheria kwasababu wanaamini endapo Spika mwenye taaluma ya Sheria Kamwe hawezi kulea uhuni huo ,atasimamia Sheria na Kanuni na atatumia Kanuni na Sheria kuwadhibu wabunge wasiyotaka kuheshimu Kanuni na Sheria na mfano mzuri Enzi za Msomi wa Sheria Samuel Sitta alipokuwa Spika wa Bunge,hakulea wabunge wahuni waliokuwa wajivunja Sheria na Kanuni akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini(Chadema), Zitto Kabwe alimtimua Bungeni kwa kuvunja Kanuni.

Lakini mwishoni mwa wiki Spika Makinda kupitia Kamati ya Bunge aliizinduka usingizini na kuwadhibu wabunge Hao wahuni ambao walifanya vitendo Vya utovu wa nidhamu.

Napongeza uamuzi huo wa Makinda wa kuamuru Kamati ya Bunge iwashughulikie wabunge hao licha uamuzi huo umekuja ukiwa umechelewa sana Kwani zimebaki siku Chache Bunge kuvunjwa na wabunge baadhi ambao walishabobea Katika Nyanja ya kufanya vurugu bungeni walishafanya sana uhuni ndani ya Bunge na kufanikiwa kulipaka matope Bunge letu KWA Kipindi chote cha Uhai wake .

Baba wa Taifa Marehemu Julias Nyerere aliwahi Kusema hivi ; " Uhuru bila mipaka ni sawa na wendawazimu".

Na nikweli kabisa, Uhuru wa kujieleza ndani ya Bunge letu linaloongozwa na Makinda tumeshuhudia kuna wakati ulivuka mipaka na limegeuka kuwa kama lina baadhi ya wabunge ni wendawazimu maana wanafanya vitendo vya kiuwendawazimu licha Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatoa Uhuru kwa wabunge kujadili Kwa Uhuru ndani ya Bunge.

Ibara ya 100 ya Katiba hiyo inasomeka hivi : " 100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri  Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo".

Lakini Tulishuhudia baadhi ya wabunge waliokuwa na Chuki zao kijinga  ,kutumiwa na wafanyabiashara kutumia Uhuru huo kuwatuhumu watu ambao sio wabunge ndani ya Bunge Hilo, kujadili hoja za kizushi na kupaka matope wabunge wenzao na baadhi ya mawaziri ,wakuu wa Wilaya na wafanyabiashara wakati wakijua wazi unapomjadili Mtu ndani ya Bunge wakati mtu Huyo siyo mbunge wala waziri ambaye anaweza.

Na Katika Sakata la Escrow ,Spika Makinda alitamka ndani ya Bunge Kuwa wabunge waache tabia ya kutumiwa vibaya na wafanyabiashara Kuja kuamishia magomvi ya wafanyabaisha na watu wengine ndani ya bunge.

Niitimishe kwa Kusema Kuwa nimefurahishwa sana na uamuzi wa Kamati hiyo ya Bunge ya kuwatia adabu wabunge Hao wahuni wasiyojiheshimu kwanza wao binafsi ,Kanuni na kuto heshimu Kiti cha Spika.

Maana wahuni hawa walikosa adabu Katika baadhi ya vikao Vya Bunge walivyokuwa wasishiriki na kwakuwa walikuwa Hawachukulii hatua walikuwa Tayari wameishaota mapembe ambayo Ijumaa yamekatwa na Bunge na Kuonyeshwa Kuwa hawako juu ya Kanuni za Bunge.

Na Wengi wenu Nyie wabunge wahuni mliotimuliwa mnahali Mbaya Katika Majimbo yenu kwakuwa baadhi ya Wapiga kula wenu wanasema hamjawaletea maendeleo yoyote badala yake mlitumia  muda mwingi kubwatuka ovyo bungeni na Kwenye vyombo Vya Habari  na sasa ndiyo Mmeishafungiwa kuudhulia vikao Vya Bunge ambalo Bunge Hilo Uhai wake unakoma Julai 9 Mwaka huu, kwa maana hiyo nyie mmejiondosha mapema kwasababu ya vitendo vyenu Vya utovu wa nidhamu.

Na kwa baadhi yenu mmeishasoma alama za Nyakati Kuwa mna nafasi finyu sana ya kutetea nafasi Zenu za Ubunge, mkaamua muanzishe vurugu Hilo la kupinga miswaada hiyo kwa njia ya kihuni ili mliotimuliwa Ndio mpate Sababu ya kwenda Kuwaahada wananchi wenu Kuwa mmetimuliwa na Bunge wakati bado mlikuwa mkitakeleza majukumu yenu ya kuwapiga nia wapira wenu. Mmechemsha ,hadanganyiki Mtu.

Ukweli ni kwamba mmefurushwa bungeni kwasababu Nyie mmefanya vitendo Vya kihuni yaani utovu wa nidhamu ambavyo havipaswi kufanywa na wabunge . 

Ni Wasela Mavi peke yake ndiyo wanapaswa Kutenda uhuni ule mliojifanya wakuligeuza Bunge Kama Soko au klabu ya Pombe chafu ambayo kila Mtu anazungumza bila kufuata mpangilo.

Waswahili siku zote wanasema Muungwana Asifiwi ushenzi,sasa Nyie baadhi ya wabunge wa UKAWA,mnasifiwa kwa ushenzi.

Acheni hiyo tabia ,siyo sifa nzuri hata kidogo,mmejidhalilisha na rekodi imebaki Kuwa Nyie ni wabunge ambao ni wabovu wa nidhamu .Hivi hata watoto wenu, wake Zenu na wakwe Zenu na watu wanaowaheshimu mnafikiri watawaheshimu   tena Kama dhamana?

Ninavyofahamu Mimi Demokrasia ya vyama Vingi,haikuqnzishwa  kwa kuwapatia ruhusa wapinzani wakiwemo wabunge wao kupinga mambo yanayofanywa na Chama kinachounda  serikali iliyopo madaraka CCM kwa njia za kihuni kama hizo za wabunge wa upinzani kuamua kupinga miswaada bila kufuata Na kuheshimu Kanuni.

Jifunzeni kupinga mambo kwa kutumia lugha zenye staha,ustaarabu na siyo uzushi, makelele na Zogo mwisho wa siku hata kama mlichokuwa mkikipinga mlikuwa sahihi,mnaonekana ni wahuni kwasababu ya kushindwa kutumia njia za kistaarabu ,nidhamu na Kanuni kupinga mambo.

Haya Kama siyo mnawazimu ni kitu gani?mmetumia njia za kihuni kupinga miswaada ile isisomwe na imesomwa?Hivi mweu hapa ni nani Kama siyo Nyie wabunge wa UKAWA mlioadhibiwa ambao wengine baada ya Kuitwa Kwenye Kamati ya Bunge mmekiri Kutenda kosa? Watu wazima ovyoooooo.


Julai 5 Mwaka huu, Bunge  waliokuwa Ndani ya Bunge  walipitisha Muswada wa Sheria ya Petroli wa Mwaka 2015, ambao ni miongoni mwa miswaada ya sekta ya mafuta na gesi iliyokuwa ikipigiwa kelele na wabunge wa upinzani.

Nyie ni watu wazima,maji heshimu na mjitambue ,huo usela Mavi mnaoufanya huku mkiwa mnahadhi ya Ubunge unawashushia heshima kwanza Nyie Binfasi,familia zenu na Taifa letu.Mmelidhalilisha sana vazi la Suti Kwani mtu unapovaa suti Unatakiwa uwe na staa kwasababu vazi la suti linaheshima yake lakini nyie kwakuwa ni wahuni licha mlivaa suti ham kujificha mkaendelea kufanya uhuni wenu wa kupiga makelele huku mkiwa nimevalia suti.

Wabunge Nyie wahuni mliotimuliwa ,rudi mkamueleze Yule 'Bwana yenu' anayewatuma kupinga miswaada hiyo kwasababu tu amenyimwa vitalu Vya gesi kwasababu Hana sifa za kupewa na hata Kwenye Sakata la Esrow aliwatumia sana kwasababu alikuwa na Chuki Binfasi dhidi ya Aliyekuwa waziri mmoja lakini mwisho wasiku aliumbuka tena mkamwambie Huyo bwana wenu Kuwa hivi sasa ananguvu Kama zamani maana serikali,na Jamii imeisha baina tabia yake chafu ya uzushi,Chuki pindi anapokosa Ulaji Katika eneo Fulani.

Niitimishe kwa Kusema Kuwa nimefurahishwa sana na uamuzi wa Kamati hiyo ya Bunge ya kuwatia adabu wabunge Hao wahuni wasiyojiheshimu kwanza wao binafsi ,Kanuni na kuto heshimu Kiti cha Spika.

Kwani Ibara  ya 13  (1) ya Katiba ya nchi inasema hivi ; "  Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria".

Hivyo wabunge  hawapo juu ya Sheria , wanapovunja  Sheria,Kanuni ni lazima wachukuliwe hatua na Bunge lilipo wakuta na hatia ya kuvunja Sheria wabunge hao wa UKAWA limewachukulia hatua za kisheria kwa mujibu Kanuni za Bunge na huo ndiyo Utawala wa Sheria.Sheria ni Msumeno na msumeno huo umewakata wabunge hao wa UKAWA  na Sheria hainaga macho.Kanuni hizo za Bunge Nyie wabunge mlishiriki kuzitunga na Kanuni hizo hizo zimewameza.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
6/7/2014







No comments:

Powered by Blogger.