MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO USIRUDIE TENA KUFANYA USHETANI HUU
MITHALI 20: 1 Katika Biblia inasema : " Mvinyo hudhihaki ,kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo Hana Hekima".
Nimelazimika kutumia nukuu hiyo ya Biblia Kuonyesha matendo ya kishetani yaliyotendwa Jana hadharani na Kiongozi wa Kanisa la Maombezi nchini lenye masikani yake Ubungo Kibangu Dar Es Salaam,Anthony Lusekelo yana baraka za kitabu cha Mithali 20:1 Katika Biblia Kwani matendo Yale aliyoyatenda ambayo nimeyaamisha ndani ya makala hii yalithibitisha Hana Hekima .
Jana 23/11/2016 nikitoka nyumbani kwetu Sinza C nakuelekea University of Bagamoyo eneo la Kawe Beach Dar es Salaam Ambapo chuo hicho kimepakana na Ofisi ya Redio Times kwaajili ya kukamilisha mambo yangu ya kitaaluma.
Hatua chache kabla ya kufika chuoni hapo ni kama nyuma Tatu kurudi nyuma kushoto kuna Ukumbi unaitwa Mtana Multipose Hall na katikati kuna barabara ya vumbi inayotenganisha nyumba zilizopo upande wa kushoto na kulia .Ni barabara ndogo ambayo Dereva hawezi geuza Gari hadi aende Mbele zaidi.
Upande wa kulia wa ukumbi huo wa Mtana Multipose Hall kunanyumba ya ghorofa ambayo inalimdwa na walinzi wa makampuni ya walinzi ambayo ni Waaafrika na wanaishi pia raia wa kigeni .
Nyumba ina namba KAW / MZN/ 1348 ambayo imebandikwa katika ukuta wa geti la nyumba hiyo na mabango ambayo yanayoonyesha nyumba hiyo nalindwa na kampuni ya ulinzi nyuma ya nyumba hiyo ni Bahari ya Hindi .
Saa 12: 32 asubuhi nilipita Katika njia hiyo nikiwa nimepanda usafiri wa Bajaji wa kwaajili ya kwenda Chuoni kukamilisha mambo yangu ya kitaaluma nilipofika katika eneo la nyumba hiyo yenye namba KAW /MZN / 1348
inayotenganisha nyumba zilizojengwa upande wa kulia na kushoto na Kabla ya kufika chuoni ambapo ni mwisho kabisa ya barabara hiyo nyembamba nilikuta Gari limesimama katikati ya barabara yenye namba za usajili T126 DFN huku watu kama nane wakiwa wamesimama pembeni ya Gari Hilo huku wakimtazama mtu mmoja aliyekuwa akiongea kwa sauti ya juu karibu na nyumba hiyo.
Mimi nilipofika karibu nione kuna nini na kwanini Gari limeziba njia na nani Kaziba njia Yule anayeongea kama kuna ugomvi ninani niliposogea Karibu nikabaini aliyekuwa anafoka ni Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu " Mzee wa Upako.
Nilishtuka nikamtaka Dereva anishushe Mara Moja licha safari yangu ilikuwa haujafika mwisho licha ni Hatua Chache kufika chuoni Kwangu ili niwahi kwenda kumsihi Mchungaji Lusekelo aondoke eneo lile Mara Moja Kwani yeye ni kiongozi wa Kiroho na Mtumishi wa Mungu haifahai kidini, kujibizana na watu tena hadharani.
Nilimkaribia Mchungaji Lusekelo na kumshuhudia kwa macho yangu akiwa anatoa lugha za matusi na zisizofaa kwa wakazi wa nyumba Namba KAW / MZN/ 1348 huku akiwa amesimama nje ya geti la nyumba hiyo ambayo wanaishi Raia wa kigeni huku akisikika akisema wamezidi kumchokoza kwa kumuita yeye ni Mlevi.Nilihisi kuchanganyikiwa kabisa maana sikuamini nilichokuwa nilikushuhudia.
Mzee wa Upako ni miongoni wa wasomi wa makala zangu sana na zaidi ya Mara Tatu alishanipigia simu kunipongeza kwa ujasiri wangu wa kuandika makala zenye Lengo la Kujenga nchi na Akawa anasema ananiombea kwa Mungu azidi kunilinda.
Namimi pia nimekuwa nimekuwa Nilikuatilia mahubiri yake kupitia Chanel Ten Mara kwa Mara ila sikuwahi kubahatika kuonana ana kwa ana na yeye hadi Jana saa 12 asubuhi nilipomuona akiwa Katika Hali ile ambayo siyo ya binadamu wa kawaida .
Ambapo nilimsabahi nikamwambia Mimi ni Muhumini wake na ni mwanafunzi wa Univeristy of Bagamoyo chuo ambacho kipo nyumba ya pili kutoka nyumba ya pili kutoka nyumbani kwake.
Licha ukweli ni kwamba Mimi siyo Muhumini wa Kanisa lake .Niliamua kuficha jina langu ili asinijue kwani ningemtajia jina langu tu lazima angenifahamu kuwa mimi ni Mwandishi wa habari ambaye amekuwa akiwasiliana namimi na kunipongeza kwa makala zangu kwani angekosa amani.
Kwa mujibu wa wale watu Saba niliyowakuta eneo la tukio saa 12 asubuhi walinieleza Mzee wa Upako asubuhi hiyo alikuwa anatoka alikokuwa atatokea ndiyo muda huo alikuwa akirudi nyumbani kwake ndipo aliposimamisha Gari lake Hilo Mbele ya geti ya nyumba Na.KAW/MZA 1348 ambapo ndani ya geti Hilo kuna walinzi alianza kujibizana na walinzi akidai wamekuwa wakimkebehi yeye hafai Kuwa Mchungaji kwasababu ni Mlevi kupita kiasi.
Nilimsii sana hadi saa Moja asubuhi ikanikuta eneo Hilo la tukio huku Mvua ikitunyeshea nikimwomba alisikiliza aache kutukana,kufoka Katika eneo la nyumba ya watu kwasababu yeye ni mtumishi wa Mungu anajidhalilisha ,a avunje Sheria za nchi Kwani kutoa lugha chafu ni kosa la jinai,na pia kuziba njia ili watu wasipite kwasababu eti anaugomvi na wale watu siyo ustaarabu na anavunja Haki za watu wengine za kwenda Kokote watakako Katika eneo hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sasa yeye Mzee wa Upako kwa kitendo Chake kile kuegesha Gari katikati ya barabara ile nyembamba ni kuvunja Haki za watu wengine wanatumia usafiri wa Magari Katika barabara ile wasiende wanakotaka kwenda kwaajili yake na kweli alifanikiwa Kuzuia Magari yasipitr eneo Hilo kwa zaidi ya muda Kadhaa huku Mvua ikinyesha.
Baadae alinisikia huku akiwa ameloana maana Mvua ilionyeshea alikuwa akisikika akinuka kileo huku akiyumbayumba akafungua Gari lake akatoa Kikapu kilichokuwa kinachupa za Maji ya Kunywa ,kavaa viatu Vya wazi na kashika miwani huku akiwa amekunja suruali.
Nikamsaidia Kubeba Kikapu kwenda nyumbani kwake ambapo ni jirani kabisa na eneo la tukio huku tukinyeshewa na Mvua tutafika nyumbani kwake tukufunguliwa geti na vijana wake nikamuingiza hadi ndani ya geti la nyumba yake .
Vijana wake wakatupokea Mzee wa Upako akaweka chini kile Kikapu akaanza Kuwaeleza vijana wake Kuwa yeye hata siku Moja hataki kudharauliwa,kuonewa na anapambana .
Akasema anaishukuru kwa kumfikisha nyumbani kwake salama ila akaniambia ananiheshimu sana Mimi ni kama binti yake .Ila anarudi Kupambana .Nikamsiii sana Aiingie ndani akalale kwanini yeye mwenyewe ndiyo ameniambia muda ule wa asubuhi ndiyo alikuwa akirudi nyumbani kwake akitokea katika matembezi yake ya jioni lakini akakakata akaanza Kuwaeleza vijana wake amefanyiwa vurugu.
Vijana wake wale walivyokosa akili na busara waka pandisha Mori wanamtaka Mzee wa Upako warudi akawaonyeshe Hilo eneo wanajibu mapigo.
Mimi ndiyo nilikuwa nimeshika ufunguo Gari la Mzee wa Upako na miwani yake .Nikawataka wale vija na wake waache upumbavu huo Mzee wa Upako ni mtu mashughuli nchini na kiongozi wa kidini wasiruhusu tena baba Yao kurudi tena eneo la tukio kwenda tena kufanya Fujo siyo vizuri Kwani mwisho wa siku Atakayedhalilika ni baba Yao.
Nikawataka wale vijana wasikilize ushauri wangu wamfungie ndani Baba yao ( Mchungaji Lusekelo ) a kalale Kwani anaonekana amechoka sana hajapumzika maana kanieleza alfajiri ile ndiyo anarudi nyumbani kwake.
Ili Mimi niwapatie ule ufunguo wa Gari la baba Yao ili wao vijana ndiyo n uongozane nao Mimi nikawaonyeshe eneo la tukio na Gari lilipoegeshwa Katikati ya barabara ,wale vijana walinijibu ' uwa hawatakagi Ujinga'.
Haraka sana wakanitaka niwape funguo nikawapa , huku Mzee wa Upako akiiondoka hapo ndani kwake kurudi Katika eneo la tukio Kujibu mapigo huku Mzee wa Upako akiwa miguu peku ,vile viatu vyake Vya wazi ( Open Shoes ) Nikiwa nimevishika Mimi wakitembea Mwendo haraka na vijana wake ambapo njia nzima Mzee wa Upako alikuwa akifoka .
Na alipofika tena eneo la tukio la wale vijana wake huku Mimi Nikiwa nimebeba Open Shoes zake ambazo nimezipiga picha .Tayari kulikuwa kumeishapambazuka watu wamejaa anaendelea kufoka Magari hawawezi kupita kwasababu Mchungaji Lusekelo aligoma kuondoa Gari lake katikati ya barabara huku akisema siondoi Hilo Gari hadi Rais John Magufuli na RPC Simon Sirro waje ndiyo wataliondoa Hilo Gari.
Nilisikitika sana Kwani jitihada zangu za Kuzuia Mchungaji Lusekelo asidhalilike Mbele ya umati wa watu kadri kinavyozidi kupambazuka Kwani watu walizidi kujaa na kumshuhudia Vituko alivyokuwa akivifanya ambavyo Mtumishi wa Mungu hapaswi kufinya.
Nikahamua kukaa Mbali kujifanya natuma SMS Katika simu yangu Kumbe napiga picha vile viatu vyake alivyoniachia ,na Gari yake iliyokuwa imageshwa katikati ya barabara Mbele ya geti la nyumba Na.KAW/MZA 1348 ambapo tukio Hilo la aina yake lilitokea hadi saa mbili asubuhi Jana .
Hata Hivyo wale wale vijana wake walinishuku napiga picha tukio lile walitaka kunipiga kisa napiga picha baba Yao.
Makusudi Niliamua kukanusha Kuwa sijapiga picha na kusingizia Mimi Nina matatizo ya macho hivyo nilikuwa Nasoma SMS lazima simu niinue juu na nisiongeze karibu na macho yangu.
Mmoja wa kijana wake akanitishia kunipiga ikabidi nimbadilikie na kumtaka kwanza anikome, cha pili jeuri ya kunipiga Hana,Tatu yeye ni shetani ndiyo maana wameshindwa kumshawishi Mzee wao aache kufanya Fujo Mbele ya umati wa watu wakati baba Yao Huyo ni kiongozi wa kiroho anajishushia heshima.Akawa mpole.
Akageuka pembeni nikawaweka mkono wangu nyuma nikairusha simu yangu kwa nyuma Kwenye majani na kulikuwa majani yanaunywevu wa Maji ya Mvua ili hata akitaka kunipora simu aikose.
Kijana Yule alivyoona sijamuogopa Akaamua kuondoka nilipokuwa nimesimama mimi na akasogea eneo la tukio na kumshuhudia Mzee wao Mchungaji Lusekelo akizidi kufoka nikageuka nyuma haraka nikaokota simu yangu nikaenda kusogea Mbali nikampa mwanamke mmoja anafanyakazi chuoni kwetu anishikie tukasogea mbali aneo la tukio tukasoma mbele ya geti la Redio Times na kuendelea Kutizima Sinema yote ilivyokuwa ikiendelea..
Kumbe vile vitendo vilivyokuwa vikifanywa na Mchungaji Lusekelo Jana Mbele ya Hadhara viliwakera wakazi wa eneo hilo na watumiaji wa eneo hilo licha ni la makazi ya watu lina ofisini pia na chuo wakaamua kupiga simu polisi kwa siri .
Baada ya muda mfupi polisi wa Kituo cha Kawe walifika eneo la tukio na kushuhudia tukio hilo na kuondoka na Mchungaji Lusekelo na kwenda kumuifadhi ndani ya kituo hicho kwa muda .
Hata hivyo taarifa toka ndani ya Kituo hicho zilieleza Kuwa licha ya Mchungaji Lusekelo kuifadhiwa ndani ya Kituo hicho aliendelea kutoa lugha zisizo na staha kwa baadhi ya Askari Polisi ambao walikuwa wakimshangaa Kuwa imekuwaje yeye ni mtumishi wa Mungu halafu amekunywa Pombe kiasi kile na anatoa lugha zisizo na staha .
Hata hivyo mchana wa jana kuna taarifa ambazo sikuwa nimedhinitisha Kuwa Mchungaji Lusekelo alihamishwa pale Kituo cha Polisi Kawe na kupelekwa Katika Kituo kingine.
Kwa mujibu maelezo hayo ya tukio Hilo la ' Sinema ya Bure' nililolishuhudia kwa macho yaliyokuwa yanafanywa na Mchungaji Lusekelo huku akiwa Katika Hali isiyokawaida kwa zaidi ya saa mbili ya kufoka na kutoa lugha chafu na kuleta Usumbufu Katika eneo la nyumba ya jirani yake limenifundisha mambo mengi ikiwemo Mimi Leo kukubaliana ule usemi usemao ' Mungu adhihakiwi' Kwani ukimdhihaki atakuumbua.
Mchungaji Lusekelo ni muhubiri maarufu nchini na ana waumini wengi sana nchini ndani na nje ya nchi na wamekuwa wakimuamini na hata serikali ya sasa inayoongozwa na Rais John Magufuli Inamuamimi na hata Rais Magufuli Mwenyewe siyo Siri anamuamini mtumishi huyu wa Mungu Mchungaji wa Lusekelo na alishampongeza Lusekelo kwa Kazi nzuri anayoifanya ya kutoa huduma ya Kiroho kwa Watanzania ambao ni waumini wake .
Juni 5 mwaka huu, Rais Magufuli alipofanya ziara ya kushitukiza katika kanisa hilo ambapo alienda kwaajili ya kusali katika kanisa linaloongozwa na Mchungaji Lusekelo na Rais Magufuli akatumia fursa hiyo kuzungumza kanisani hapo eneo la Ubungo Kibangu na alisema
Kwa mamlaka aliyonayo ameishaagiza mamlaka zake zianze Kujenga barabara Inayopita Katika Kanisa la Mzee wa Upako ili waumini na wananchi wa eneo wasiendelee kupata tabu kwasababu barabara ile ni Mbaya sana.
Hata hivyo baadhi ya watu walipinga uamuzi huo wa Rais Magufuli na walidai uamuzi huo ni wa upendeleo waziwazi na wakukurupuka.
Licha ya Lusekelo ya Kuwa na heshima kubwa nchini hadi Rais Magufuli Akaamua kwenda kusali kanisani kwake lakini Jana alishindwa kutunza Umaarufu,heshima yake aliyokuwa Katika Jamii kama kiongozi wa Kanisa lenye waumini Wengi Akaamua kuporomosha matusi hadharani ,kuyumbayumba wakati amesimama Na kutembea Mithili ya mtu aliyelemewa na kilevi. Uzuni.
Vituko vile alivyovifaya Jana Mchungaji Lusekelo pia vimenifundisha Mimi binafsi Kuwa kuanzia Jana niache tabia ya Kuwa mgumu kuamini baadhi ya taarifa za mambo machafu yanayofanywa na baadhi ya watumishi wa Mungu.
Miezi mitatu iliyopita kuna watu Wawili toka vyombo Vya Ulinzi na Usalama walinieleza Huyo Mchungaji Lusekelo ni Mlevi mzuri tu wa Pombe aina ya Konyagi na walishamnasa katika matukio mawili akiwa hoi kwa kilevi ,kwakeli nilikuwa mgumu kuwakubali maelezo hayo kwasababu kwanza sikuamini na niliwaona wale maofisa ni wazushi .
Ila Jana asubuhi nilichokiona kilichokuwa kikifanywa na Mzee wa Upako Mbele ya umati watu ,nilikubaliana na Yale waliyonieleza watu wale na nikachukua simu nikamupigia mmoja baada ya mwingine na kuwaambia kweli waliyonieleza Leo Mungu amenileta eneo la tukio nithibitishe Yale waliyonieleza.
Hata hivyo mama yangu Mzazi kwa zaidi ya Miaka minne sasa tukikaa wote sebuleni tukiwa tunaangalia Kipindi cha Mchungaji Lusekelo kinachorushwa na Channel Ten ,mama amekuwa akiniambia huyu Mzee wa Upako ana michango ana maanisha Kuwa licha ni Mchungaji ila bado anafanya mambo ya kidunia ambayo Mungu hayapendi.
Basi mama akisema hivyo namwambia aache hiyo tabia ya kumsema Mzee wa Upako kwasababu Hana ushahidi.Mama anasema haya anafunga mdomo ila ipo siku Mungu atamuanika hadharani ndipo nitakapoamini.
Kweli kupitia tukio la Jana aliyofanya Mchungaji Lusekelo ,Nimelazimika kukubaliana na maneno ya Mama yangu Mzazi kuhusu Mzee wa Upako Kuwa licha ni mtumishi wa Mungu bado anafanya matendo ambayo Mungu hawataki mfano Fujo, kutoa lugha zisizonastaa,kulipa kisasi wakati Mungu anatutaka tusamehe ,tusi lipe kisasi kwa watesi wetu lakini Mchungaji Lusekelo alishindwa kuwasamehe watesi wake na Akaamua Kupambana na maneno makali huku alipokuwa Kaipamba nao wakiwa wanamtazama hawamjibu.
Lusekelo ni binadamu kama Sisi ila tofauti yetu yeye amejipambanua kama mtumishi wa Mungu ambaye ni kiongozi wa Kiroho hivyo Hakupaswa kufanya Yale yote aliyoyatenda Jana ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu ambayo kwa kiasi Fulani yanavuruga akili na akili zangu za kawaida Jana jioni maana sikutengemea kumkuta kiongozi wa dini akiwa Katika Hali kama ile aliyokuwa nayo Mzee wa Upako na kufanya matendo Yale ambayo huwafanywa na watu wasiyo na hofu na Mungu na hawajishina neno la Mungu.
Hata hivyo Fedhea iliyomkuta Jana Mchungaji Lusekelo pia naweza Kusema licha Mimi nilikuwa anajitahidi kumuokoa Lusekeo asidhidi Kuaibika Mbele ya watu Wengi Kumbe Mungu naye aliamua kuruhusu mtumishi wake Huyo wa Mungu adhalike Mbele ya watu Wengi ili watu wa mjue Kuwa mtumishi Huyo wa Mungu ambaye Kutwa analia ubiri neno lake naye Si mtakatifu na kwamba anayefanya Mambo ambayo Mungu ameyakataza.Na kweli Mungu Jana kumdhalilisha kweupe Lusekelo. Uzuni.
Nilikuwa najiuliza hivi ndiyo mmoja wa waumini wake angepata fursa ya kushuhudia Vituko alivyokuwa akivifanya Mchungaji Lusekelo Jana au kama Alikuwepo muumini Akawa anashuhudia tukio lile ,wamejisikiaje?
Hata hivyo tukio la Jana pia limenifanya nikubaliane na Kauli ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipokuwa madarakani alisema hivi : ' Kuna baadhi ya viongozi wa dini Si wa safi,ni wachafu na wengine wanauza dawa za kulevya'.
Nimuulize Mchungaji Lusekelo hivi kupitia tukio hili ,atapata wapi tena ujasiri wa kusimama madhabau ni kuwataka waumini wake wasitumie vileo,wasilipize Ubaya kwa Ubaya ,wasiingie Katika vita ya maneno na watesi wao?
Sikutaka kuandika makala hii ila ni mejikuta nikijiuliza ni kwanini Mungu alipenda nikutane na Mchungaji Lusekelo kwa mara ya kwanza ana kwa ana akiwa katika hali ile na akiwa anafanya matendo yale ya kishetani?
Kwanini Mungu asingepanga nikutane na Mchungaji Lusekelo akiwa Mzima ananukia harufu ya mafuta mazuri badala ya halufu ya kileo na akiwa anafokea na kutoa lugha chafu dhidi ya jirani yake na kuziba njia na kusababisha kuziba njia kwa muda na hali ya sintofahamu ?
Na Kwani Mungu asinge ya kuruhusu waandishi wa Habari wengine nchini asubuhi ile washuhudie tukio Lile isipokuwa Mwandishi wa Habari Mimi Happiness Katabazi?
Nikahitimisha kwa Kusema huyu ni Mungu ndiyo ananisukuma niandike makala hii ambayo imeanika matendo hayo ya kishetani yaliyotendwa na Mchungakondoo wake Lusekelo ili watu matendo anayoyatenda nje ya madhabau, wapi me Je kiongozi wa kidini anafaa kuendelea tena kulitangaza neno la Mungu na kuongoza waumini wake?
Nikajikuta nachukua Kompyuta na kuacha kwenda GYM kufanya mazoezi ya viungo Jana jioni nikaa chini hadi usiku wa manane kuandika makala ambayo nimeimaliza kuiandika saa Tisa usiku wa kuamkia Leo .
Kwa kupitia makala hii ambayo itamfedhehesha Lusekelo kwa kiasi Fulani na Imani kwa baadhi ya watumishi wa Mungu itazidi kutiliwa Shaka lakini neno la Mungu litasimama .
Uenda makala hii akiisoma anaweza kuachana na matendo yasiyompendeza Mungu Kwani yeye Lusekelo ni mtumishi Mungu anapaswa asitende mat endo ya kishetani kama hayo aliyoyafanya jana badala yake abaki na kazi moja ya kumtumikia Mungu tu .Na ni aomba iwe hivyo.
Kwani hata EZEKIELI 3:19 Katika Biblia inasema , " Lakini ukimwonya mtu Mbaya ,wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake Mbaya ,atakufa Katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.
Hivyo kupitia kitabu maneno hayo yaliyopo Katika kitabu cha Ezekiel ,Mimi nimeitimiza wajibu wangu kwako wewe Mtumishi wa Mungu Lusekelo kukuonea ili uache michanganyo ya mambo ya kidunia badala yake Ubaki na jambo Moja tu la kumtumikia Mungu.
Kumbuka Biblia inasema Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu na hata michanganyo.Ukiamua kumtumaini / kumtumikia basi uyafuate na uyatii maandiko yake Kwani Mungu anauwezo wa kukuinua na kukushusha .
Lusekelo Mungu ameinua huduma yako lakini sasa umeanza kurudi nyuma ,u na michanganyo kama hiyo.Siyo vizuri .Mungu hapendi.
Nina Hakika ungekuwa mzima usingetenda matendo ya kishetani uliyoyatenda Jana asubuhi Mbele ya kadamnasi .Au ulivamiwa na mapepo ndiyo ya kwakutuma utende ushetani ule ambao ulikufedheesha ?Kwa lugha nyepesi ulikuwa umepata kileo .
Ingia ndani tubu kwa Mungu wako atakusamehe songa Mbele ila tu wale watu wote waliokushuhudia Jana ukiwa Katika Hali ile na kufanya vitendo vile Vya kishetani siyo rahisi tena kuiamini huduma ya Kimungu unayoitoa.Nisamehe sana.Licha Nitaendelea kukuheshimu na kukupenda.
Kama kweli Mchungaji Lusekelo umeitwa na Mungu umtumikie ,sikutegemea kabisa mimi binafsi au umati ule watu huku ukiwa umelewa Pombe na huku hujavaa viatu ukifanya ushetani ule hadharani tena asubuhi asubuhi. Inatisha.
Mchungaji Luseleko kama kweli umeweza Kutenda ushetani huo wa kuporomosha matusi hadharani ,nakuwa Katika Hali ile isiyoyakawaida ambayo unafahamu Mungu hataki matendo Yale ,Kesho wewe utashindwa kuingia tamaa ya kufanya mambo yasiyompendeza Mungu kama kwenda kufanya matendo ya kishirikina ili uwapumbaze waumini wako waendelee kuamini Kuwa ni mtumishi safi wa Mungu Kumbe unatenda matendo sirini yasiyompendeza Mungu?
Hivi Leo hii watu wakikurushia vijembe Kuwa Sadaka zinazotolewa na waumini wako pia unazitumia Katika ulevi ,Utakataa au utasema wanakuonea wivu?
Pombe inavishawishi Vingi sana na inaweza kumshawishi mtu aliyekunywa kufanya chochote anachokisia ikiwemo hata kufanya zinaa.Hivi ule ushetani ulioutonda Jana wewe Mzee wa Upako ,wakiibuka watu wakisema unywagi Pombe tu pia hata dhambi ya uzinzi unatenda ,utakuja kukataa useme wakuzushie?
Pole waumini wa Kanisa linaloongozwa na Mchungaji Lusekelo Kwa makala hii Kwani nafahamu baadhi yenu itawakwaza ila ndiyo mvumilie ukweli ndiyo huo niliyoohushudia Mimi kwa macho yangu nanilitahidi kumsitili kiongozi wenu ili asidhalilike bila mafanikio na mwisho wa siku nilichoambulia nikutaka kupigwa na vijana wake .
Ila roho yangu nyeupe na wala makala hii haina Lengo la kuwazuia muache kumuabudu Mungu kupitia Kanisa linaloongozwa na Mchungaji Lusekelo.
Namimi ni madhaifu yangu sikatai ila bado sijafikia Hatua ya kama alifikia Lusekelo ya Kuwa mtumishi wa Mungu halafu kufanya matendo hayo ambayo kila Mara amekuwa akisimama madhabauni Kukataza waumini wake wasiyafanye kwasababu Mungu ameyakataza Kumbe yeye Anayafanya .
Lengo la Makala hii ni Kuonyesha Mchungaji Lusekelo ambaye anasimamaga madhabau ni anakemea dhambi Kumbe na yeye anatenda baadhi ya dhambi.Mtaamua wenyewe.Ila nawashauri sote tumuombee maana sote sisi ni binadamu Hakuna Mkamilifu .
Ila kuna utofauti wa upokewaji wa Jamii wa baadhi ya matendo ya dhambi yanayofanywa hadharani na viongozi wa kidini na matendo hayo hayo ya dhambi yakifanywa Na mtu ambaye siyo kiongozi wa kidini.
Mtumishi wa Mungu akitenda dhambi za aina hizo alizozitenda Mzee wa Upako Jana za kutukana ,ulevi Jamii zitaipokea kwa uzito wa aina yake na kwa Mshangao mkubwa sana.
Hakuna ubishi Mchungaji Lusekelo umefedheheka Jana tena sana Katika eneo unaloishi Kawe Beach Karibu Univeristy of Bagamoyo na Redio Times .Kaa utulie,maana Hasira ya Mungu Jana imekushukia ,tubu Mungu atakusaidia uondokane na shetani wa Kupenda Konyagi na aina nyingine za Pombe Kali.
Mchungaji Lusekelo kama utashindwa kuachana na anasa za Dunia basi achana na Kazi ya Mungu ili uwe huru kufanya mambo ya anasa kuliko Jumapili na siku za katikati ya wiki Una Simama madhabauni unaubiri neno la Mungu Kumbe ukitoka madhabauni unaenda kufanya mambo yasiyompendeza Mungu ukiwemo Kunywa Pombe.
Mchungaji Lusekelo jana kweli ilikuwa ni mara yako ya kwanza kunywa pombe kwa kiwango kile hadi zikakutuma kufanya matendo yale hadharani ambayo Mungu hapendi?
Je Mchungaji Lusekelo jana ni mara yako ya kwanza kurudi nyumbani kwako saa moja asubuhi ? Maana miminilikufika nyumbani kwako saa moja asubuhi huku nikiwa nimekubeba baadhi ya vitu vyako kama funguo wa gari ,miwani huku wewe ukiwa umebeba Kikabu chenye chupa za maji ya kunywa ;
Baada ya kufanikiwa kumuondoa Kwenye eneo la tukio la ugomvi uliotokea na Kisha baada ya kukufikisha ndani ya nyumba yako wewe na vijana wako wewe ukatoka miguu pekupeku bila kuvaa viatu maana viatu ulikataa kuvaa nimevishika mkononi mkarudi tena eneo la tukio huku ukiwa Ujavaa viatu unakanyaga matope na Mvua inatunyeshea unafoka Katika nyumba ya jirani yako kuishinikiza walinzi wakifungulie Mlango uwaonyeshe Kazi?
Nakupenda kwasababu unapenda kuzungumza ukweli na mimi naupenda ukweli .
Hivyo nakushauri jirekebishe ,tubu kwa Mungu wako, na ukipata muda omba msamaha majirani zako kwa Usumbufu uliowasababishia Jana asubuhi wakuwazibia njia wenzio wasiende makazini na Magari Yao kwasababu Lako ulilipaki katikati ya barabara kumalizima tangu saa 12 asubuhi hadi saa mbili huku ukisikia hutaliondoa Hilo Gari Hali RPC Sirro,Rais Magufuli waje kuliondoa. Nilikushuhudia ukiyasema haya sina Sababu ya kunisingizia .
Pia Hao vijana wako unaoishi nao hapo ndani baadhi yao wana akili mbovu wote watatu waliotufungulia geti kwasababu wao waliochangia kukurudisha tena eneo la ugomvi Matokeo yake ukaenda kudhalilika zaidi wakati Mimi nilifanikiwa kukuondoa mapema eneo la tukio mapema na watu walikuwa wachache na Magari yalikuwa hawajaanza kupita Wingi Katika njia ile .
Vijana Hao kama wangekubali ana na ushauri wangu niliyotoa wakati nome kufikisha ndani kwako wa kukuingiza ndani na kukufungia na Kisha wao vijana ndiyo ni wapeleke eneo la tukio niwape ufunguo wa Gari la Baba Yao Mchungaji wa Luseko wafike eneo la tukio wachukue Gari walioleta nyumbani bila kujibizana na watu kwani lakini walinipuuza Matokeo yake ndiyo hayo umati ulifurika ukakushuhudia ukibwatuka .
Polisi wa Kituo cha Kawe Dar es Salaam wakaitwa na wasamalia wema kwa siri wa kakukuta eneo la tukio ukibwatuka wakakupeleka kituoni ukiwa bado pombe hazijakuisha ukaifadhiwa Kituo hapo kwa muda ukasababisha hata Polisi ambao walikuwa hawafahamu Kuwa unakunywa Pombe wakajua,wakakudharau maana matendo yako ya Jana yalitukanisha pia watumishi wa Mungu .
Mchungaji Lusekelo na wale vijana wako mngeuzingatia ule ushauri wangu Kuwa uende ndani ukaoge kisha ukalale ile saa Moja asubuhi maana ulikuwa umechoka ungefanikiwa kukwepa Kadhia na Fedhea hiyo.
Mchungaji Lusekelo wewe ni mtumishi wa Mungu ,jiheshimu ,usijaribu kumgeuza Mungu Kuwa ni Mwanasesele labda aoni mambo unayoyafanya Gizani.Mungu siyo Mwanasesele anatuona yote tunayoyafanya hadharani na Gizani Akiamua kukuumbua anakuumbua na wewe Jana ni Mungu Yule ndiyo aliyekuumbua .
Ni itimishe kwa kukubaliana na maneno haya yaliyoandikwa Katika MITHALI 20: 1 Katika Biblia inasema : " Mvinyo hudhihaki ,kileo huleta ugomvi; Nakosaye kwa vitu hivyo Hana Hekima".
Kwasababu maneno hayo yametimia kwa Lusekelo ambaye alikuwa amepata kileo amefanya ugomvi na alipofanya ugomvi Jana alithibitisha umati ule wa watu Hana Hekima Kwani Angekuwa na Hekima asingekubali kufanya ushetani ule ambao umefedheesha Vya kutosha.
Mungu Ibariki Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494.
24/11/2016.
1 comment:
Good writing, but you have a lot of spelling mistakes. Please get a blog editor or read through your article before you post. Punguza makosa ya uandishi na herufi
Post a Comment