MIPANGO YENU YA UDHALIMU DHIDI YANGU NIMEIBAINI
Na Happiness Katabazi
LEO Mchana Mara ya kwanza mtu mwenye namba 0624 317172 alijitambulisha kwa jina la Justine alijitambulisha yeye ni mwanakywa ya wa Kanisa la KKKT Temeke ,wanataka kurekodi video hivyo wamepewa namba yangu ili ni wasaidie kuwaandikia Makala nikamwambia nilishaachaga Kazi Katika magazeti ila msaada nitakao mpa ni kumu unganisha na waandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania ,Happy Mnale akawaandikie hiyo makala Yao.
Nikamtaka anitumie ujumbe mfupi whatsup ili nione namba yake ili nimrushie namba ya Happy Mnale na kweli Nikafanya hivyo nitamtumia .
Baada ya muda mchache mtu Huyo aliyekuwa akijifanya Mwema sana Kwangu na kunisii sana nionane naye Mimi moyo wangu ukawa inasita ,akanipigia tena simu yangu akisema Tayari wameishaonana na Happy Mnale na amewapokea vizuri na wameishafanya mahojiano naye ya makala hivyo hiyo makala itachapishwa Katika Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili ya wiki hii na anaishukuru Sana kwa wema wangu.
Mtu Huyo nikiwa na Askari wa JWTZ ( namuifadhi kwa jina) nikuzungumza naye alipiga tena simu nikakatisha mazungumzo na Askari Huyo wa JWTZ ambaye nilikuwa nazungumza naye nakumpa ushauri wa kitaaluma nisimamisha mazungumzo naye nikapokea simu ya Huyo mtu aliyedai yeye ni mwimbaji wa kwaya ya KKKT akaniuliza mchana ule nikipo wapi nikamjibu Si desturi yangu kutaja sehemu nilipo kama msaada nimeishampa.
Saa Tisa nikiwa na mazungumzo na rafiki yangu ambaye ni mtumishi wa umma Kwenye Gari lake mtu Huyo ( Justine) alipiga simu tena Kabla ya kupokea nilimweleza Huyo dada ambaye ni rafiki yangu Kuwa huyu mtu uenda ametumwa kunidhuru na kuniteka Kwanini analazimisha kuonana na Mimi harakahara kawakati Shida yake nimeishatatulia kama makala nimeishamuunganisha na Mwandishi wa Habari Happy Mnale ,Nikajikuta Nasema YESU ni saidia nikapokea simu yake akasema anaomba aonane namimi nikamsisitiza Aiwezekani.
Saa 12 jioni ya leo roho yangu ikanituma nivunje ratiba yangu ya kwenda mazoezi (GYM) nikaenda kukaa sehemu kubadilishana mawazo nawatu namba hiyo ya ( Justine) ikanitumia ujumbe mfupi ukisema NAWEZA KUKUONA? kwakuwa sikuwa nimeikariri namba yake nimamjibu wewe nani? Hakujibu hadi hivi sasa saa nne usiku.
Saa Mbili usiku Leo nikapokea simu kutoka Mama na Mdogo wangu zikinihoji niko wapi natafutwa vibaya sana nikamatwe wamepewa na watu wameambiwa Kuwa Hao watu walienda hadi Ofisi za Tanzania Daima kuniuliza.
Haraka sana akili ikanituma nimpigie simu Mwandishi wa Habari Happy Mnale kumhoji nakumwonya asijaribu kunificha chochote aseme .
Mnale akasema nikweli Yule mtu niliyemwelekeza kwake mchana ambaye alijitambulisha ni muimba kwaya anaitaji kuandikiwa makala alifika ofisini kwake na akatoa nje ya Ofisi yake akampeleka nje ya Ofisi wa kamuuliza maswali Mnale wakishinikiza Mnale a walete ofisini Kwangu Mnale ni kweli hapajui ofisini Na nikweli Mnale hapajui ofisini Kwangu na Mnale Katika mazungumzo yangu naye alinitaadharisha misiseme hayo waliolezwa na Hao watu ambao wakijitambulisha kwakwe kama ni maofisa wa serikali na vitambulisho wakamuonyesha ila iwe Siri baina ya Mnale na Huyo mtu ambaye kwa mujibu wa Mnale anasema walikuwa ni kundi la watu zaidi ya Watano na wakiwa na mwanamke mmoja.
Mnale najua utachukia kwa kuyaandika yote uliniambia nisiyaandike kuhusu mazungumzo yako na hao watu na mazungumzo yangu mimi na wewe nimelazimika kufanya hii kwasababu ya usalama wangu.
Nimejiuliza kama hao ni maofisa wa serikali kweli na wananitafuta mimi na simu yangu wanayo kwanini hawajanipigia simu kunitaka niende kituo chochote cha polisi kwa mahojiano na hatua zaidi za kisheria?
Kama kweli mtu Huyo mwenye namba hii 0624 317172 ( Justine) aliyejitambulisha ni mwimbaji kwaya anataka kuandikiwa makala ,kama kweli alikuwa nania njema na Mimi Kwanini aendelee kunisumbua Kwenye simu na kwanini afike Ofisi za Gazeti la Tanzania Daima hayo mahojiano ya Makala ha kuyafanya Matokeo yake wamweleze Mnale Kuwa Lengo Lao siyo kuandikiwa makala Lengo ni kumsaka Happiness Katabazi wa mkamate na Mnale asitoe Siri ?
Mungu yupo na naweza na atanilinda na siku zote ananilinda na ndiyo maana mmepanga mipango yenu michafu kwa siri na dhamira yangu ilikuwa ni njema na msaada mlioutaka nikawasaidia ndiyo maana mipango yenu dharimu mliyoipanga kwa siri Mungu ameianika.
Na kwa taarifa yenu wewe Justine ambaye namba yako hivi sasa haipatikani na genge lako Nyie siyo kwanza kunipangia mipango ya kidharimu na kunijia na mbinu za kipuuzi kama hizi lakini Mungu aliniokoa.Amini Mungu yupo na at alisambaratisha mipango yenu.
Nasiwaogopi ,Jeuri yangu ni Yesu na Mkae mkijua na Mimi siyo "Mwepesi kihivyooo" na ndiyo maana majaribo yako yote ya kunishawishi nionane nawewe yameshindikana na ni Mungu wangu aliingilia Kati akasambaratisha mipango yenu.
Nawarahisishia Kazi kama nyie ni wanausalama kweli wa serikali jitajeni Nyie ni wanausalama toka Kituo gani cha Polisi nitakuja Mwenyewe kuliko njia za kipuuzi mnazotumia za kujifanya Kuwa ni watu wa dini kwakuwa mmesikia Mimi nasali basi mkaamua kuiniingilia Gia hiyo.Poleni sana.
Na Nina Mashaka kama Nyie kweli ni wana Usalama kweli wa serikali ila kwa Mungu hamfichi mnafki itabainika kweli Nyie ni wanausalama toka serikalini kama mlivyomweleza Happy Mnale mkataka asinieleze Kuwa Nyie siyo wanausalama ila kwakuwa Mnale ni rafiki yangu nanimepokea Kazi hawezi nificha chochote maana tunasaidiana naye Katika Shida na raha.Mungu amfichi mnafki atawasukuma Mtaje mnachonitafutia.
Mungu ibariki Tanzania
Mwandishi wa Makala hii ni ;
Ofisa Habari wa University of Bagamoyo(UoB) na Mwanasheria
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
23/5/2016.
No comments:
Post a Comment