TANGULIA 'KIFAA' AFANDE MWAUZI
TANGULIA 'KIFAA' AFANDE MWAUZI
Na Happiness Katabazi
JANA mchana maofisa wa tatu wa ngazi ya juu Jeshi la Polisi ambao ni marafiki zangu katika mazungumzo nao ya kawaida tu walinijulisha kuwa wamefiwa na mfanyakazi mwenzao ambaye ni Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi (SACP) Lutenta Modest Mwauzi ambaye alifariki Juni 12 Mwaka huu na akazikwa Jana Kijijini Kwao Ibwera,Bukoba Mkoani Kagera.
Taarifa hizo zilisababisha siku nzima ya Jana nikose na nimwage Machozi kwasababu SACP- Mwauzi licha ni ' Nshomile ' mwenzangu pia aliwahi Kuwa mwalimu wangu wa kozi ya Sheria ngazi ya Cheti.
Kwa Tuliofundishwa na mwalimu wa SACP -Mwauzi ' Kifaa' enzi hizo wakifundisha pamoja na Afande Nasser Mwakambonja ambaye ni ofisi wa Juu wa Jeshi la Polisi na ni Mwanasheria Kitaaluma .
Alishawahi Kuwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Sheria Jeshi la Polisi, mratibu wa silaha ndogondogo small arms and light weapons ,
Afande Mwakambonja na Afande Nasser Mwakambonja waliopata fursa ya kufundishwa nao somo la Criminal Law na Criminal Procedure walipata fursa Adimu ya kuwafahamu Polisi wanapokuwa wakifanyakazi zao kwasababu masomo hayo mawili Tulifundishwa na maofisa Hao wa Polisi ambazo Sheria hizo ndiyo zinaongoza makosa yote ya jinai ambayo makosa yote ya jinai yanashughulikiwa na Taasisi kama Jeshi la Polisi mfano kukamata,kuhoji na kupeleleza .Kifngu cha 10 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 inatoa jukumu Hilo kwa Ofisa wa Polisi.
SACP- Mwauzi ' Kifaa' ,kifo Chako Mimi binafsi kimeniuzunisha sana tena Kwani Natambua mchango wako Katika elimu ya Sheria ya nchi hii , na mchango wako Katika taifa hili.
Mwauzi ni Ofisa wa Polisi alikuwa siyo mtu wa kujikweza na hata ungekutana naye mitaani usingefikiri ni Polisi mwenye Cheo cha juu ndani Aidha alipenda utani sana.
Nitaendelea kukumbuka ule usemi wako wako iliyowahi kuniambia hivi ; " Ukiwa mwimbaji Kwaya lazima uje kutabasamu". Kila nikikumbukaga huo Msemo wako nacheka sana.
Nilizoea nikifika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar Es Salaam,Kwenye majukumu yangu pia nilikuwa nikipita Ofisini wake kumsalimia sasa kwakuwa umefariki Duniani ndiyo sitakuona tena.Nimeumia sana.
Aidha SACP-Lutenta Mwauzi Mbaye ni Mwanasheria Kitaaluma Utakumbukwa sana ' wagonga fegi ' wenzio.
Pole Jeshi la Polisi ,familia, ndugu Jamaa na marafiki kwa kuondokewa na Mpendwa wetu SACP - Mwauzi.
Mungu aiweke roho ya SACP-Mwauzi Mahali panapostahili.
Mwandishi wa Makala hii ni ;
Ofisa Habari wa University of Bagamoyo(UoB)
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
16/6/2017
No comments:
Post a Comment