KAMISHNA JENERALI JUMA MALEWA ,STAHIMILI
Na Happiness Katabazi
LEO Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemtimua kikaoni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Dk.Juma Malewa kwa kile alichodai amechelewa kufika katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Kitendo hicho ambacho si cha kiungwana kilichofanywa na Waziri Lugola dhidi ya Kamishna Jenerali Dk.Malewa kimewasikitisha watu nikiwemo mimi.
Waziri Lugola amemtimua Kamishna Malewa huku akiwa anarekodiwa na vyombo vya habari.
Lugola ambaye Julai Mosi mwaka huu,aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani amesikika na kuoneka katika video akimtimua Kamishna Jenerali Malewa atoke ukumbini kwasababu amechelewa na hakutaka kumsamehe wala kumsikiliza Dk.Malewa kwani Lugola alikuwa akisikika akisema askari wamefundishwa nidhamu ,aliagiza mlango ufungwe na akashangaa nani kafungua mlango akaingia.
Lugola huyu ambaye aliwahi kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa ya kuomba rushwa lakini baadae Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ,Biswalo Mganga alitumia kifungu cha 91 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai akamfutia kesi hiyo.
Siyo hali ya kawaida kiongozi wa kijeshi kuchelewa kufika eneo la tukio kama baadhi walivyo viongozi wa kisiasa.
Kiongozi mwenye busara na anayefikiria sawa sawa kabla ya kufikia uamuzi wa kumtimua tena mkuu wa Jeshi la Magereza Malewa tena mbele ya waandishi wa habari ama angemuacha Malewa aingie mkutano uishe amuite ofisini amwadhibu kiofisi bila hata watu wengine kujua au amuulize nikwanini amechelewa ili wakati anamuuliza TV zimmulike vizuri aonekane ni mchapakazi sanaa maana chakula cha Wanasiasa ni vyombo vya habari.
Hilo mwenzetu huyu Lugola ambaye amekuja moto wizara ya mambo ya ndani lakini ni lazima atapoa tu kwani hii ndio Tanzania zaidi aijuavyo kaishia kumfokea mwanaume mwenzie Malewa dunia kupitia vyombo vya habari tumeshuhudia akimfokea tena kwa kumtaka atoke nje na kwamba askari wamefundishwa nidhamu hamtaki katika mkutano wake na afande Malewa kwa unyenyekevu huku akimulikwa na TV akaondoka.
Hivi wewe Waziri Lugola ulivyosema askari wamefundishwa nidhamu wakati ukimtimua Mkuu huyo wa Jeshi la Magereza Dr.Malewa ndio unamaanisha huyu Kamishna Jenerali Malewa ambaye ni mkuu wa Jeshi la Magereza hana nidhamu?
We Waziri Lugola hivi ikitokea Malewa akija kuulizwa na aliyemteua au mamlaka zingine ni kwanini alichelewa Malewa akatoa sababu ambazo ni Za msingi kabisa utaitisha tena mkutano wa vyombo vya habari kumsafisha?
Kwanini Lugola kama nia yako ni safi kabisa kwa Malewa ukuona haja yakumvumilia aingie mkutano mmalize umuite ofisini umwadhibu kama unayomadaraka ya kumwadhibu?
Kwanini umeona fahari sana kumdhalilisha hivyo na kiongozi mkubwa wa jeshi letu mbele ya uso wa dunia leo umemuhukumu bila kumpa nafasi ya kujieleza kuwa nimchelewaji na kumtimua kama mtoto mdogo mbele ya vyombo vya habari vikimulika?
Umepata faida gani kwa kitendo hicho ambacho wewe unadhani umeshinda kumbe aliyedhalilika na kuonekana mweu ni wewe?
Lugola hivi huu ujasiri wa kumtimua kama kibaka Kamishna Jenerali Jeshi la Magereza ambaye ni mteule wa rais kama wewe umeupata wapi? Umetumwa?
Mtu mwenye cheo cha Kamishna Jenerali wa Jeshi ana wasaidizi,walinzi,washauri,msafara wake na pia ndio mtoa maamuzi wa jeshi la Magereza ktk mambo mbalimbali hivi kabla ya kumtimua kama kibaka kiongozi huyo kwanini ukutaka kujipa muda kwanza kutafakari ni kwanini amechelewa?Badala yake ukamtimua kama mvamiaji ?
Lugola ulivyokuwa polisi hukuwahi kufikia kufikia cheo cha Kamishna Jenerali kama alichonacho Dk.Malewa basi leo kabla ya kufikia hatua ya kumtimua Kamishna Jenerali Malewa kwa dharau vile ukutafakari basi kidogo kuwa licha wewe hivi sasa ni waziri lakini yule Malewa amekuzidi cheo katika jeshi uone haja basi ya kumpa heshima yake ?
Kwa kitendo hiki ulichomfanyia Mkuu huyo wa Magereza ,hivi wale wanaongozwa na kamanda huyo wanamuonaje hivi sasa au wanakuchukuliaje wewe hivi sasa kwa kitendo hicho ambacho mimi nasema sicha kiungwana kwa afande wao Malewa ?
Au wale mahabusu / wafungwa waliopo gerezani ambapo magereza yote yapo chini ya Jeshi la Magereza ambalo jeshi la Magereza linaongozwa na Inspekta Jenerali Malewa wanamtazamaje au wanakuchukuliaje wewe wa kitendo cha kihuni ulichomtendea Dk.Malewa?
Kamanda Malewa nyamaza kaa kimya ila akili kumkichwa Muachie Mungu atakulipia hilo uamini kabisa kwanini namimi nilishakutwa na tukio kama hilo chuoni nilichelewa dakika tano kuingia darasani asubuhi nanilichelewa kwasababu nilitokea hospitali nilikokuwa nimelazwa na mtoto ,nikamwacha mtoto wodini na ndugu yangu amtazame minikawahi chuoni nikitokea wodini huku nikiwa nina uchovu ile nafungua mlango naingia class huyo mwalimu alishika kipaza sauti akanitimua kama alivyokutimua huyo Bwana Lugola kama takataka fulani vile nilimwomba msamaha nakuomba nijieleze alikataaa kunisikiliza nikatoka nikarudi wodini kumuuguza mwanangu Queen nanilimshitakia Mungu amtie adabu huyo mwalimu kwa muda wake na kweli aikuzidi miezi sita mwalimu huyo alikumbwa na skendo mbaya ya fedhea na akatimuliwa kazi kwa fedhea.
Mungu atakulipia madamu aukuwa na dhamira ya kuchelewa katika hicho kikao .
Mtu yoyote mstaarabu na muungwana hatujafurahishwa na hiki kitendo ulichomtendea kiongozi huyu wa Jeshi la Magereza Malewa ambaye kwanza hajawahi kusikika katika jamii kuwa anatuhuma za uhalifu kama tuhuma kupokea au kuomba rushwa kama wewe kwani wewe Lugola Ukiwa mbunge ulishafunguliwaga kesi ya rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kesi yake baadae DPP alikuja kuifuta.
Kuna baadhi ya waliowahi kuwa Mawaziri wa Wizara hiyo ya Mambo ya ndani walivyoingia katika hiyo wizara wakajifanya wajuaji kutwa kutaka askari fulani akamatwe mtovu wa maadili,kuagiza askari polisi fulani wasimamishwe kazi,wachunguzwe.
Nanilikuwa nawaonya nikikutana nao chemba waachane na mambo ya kusikiliza umbea wa mitaani kutoka wapiga kura wao na wapambe wao kwani mwisho wa siku jeshi litabaki kuwa jeshi na wao ni mawaziri tu ni watu wa kupita maarufu kwa jina la "WAPITA NJIA" katika hiyo wizara hawakunisikia mwisho wa siku wale askari waliokuwa ameagiza wachunguzwe wakaonekana na vyombo vya polisi wapo safi, na hao mawaziri enzi za utawala wa Rais Kikwete nao Kikwete alikuja kuwaondoa kwa sababu anazozijua yeye na wengine na uwaziri hivi sasa wanausikia redioni.
Lugola na Malewa wote ni viongozi wa Taifa letu mnaitaji kuheshimiana na sisi tuwaheshimu kama mnamdhaifu yenu malizaneni ndani lakini siyo kwa stahili hii ya leo ya waziri Lugola kumtimua kiongozi huyo wa Jeshi la Magereza kwa mtindo ule ambao auleti picha nzuri kwetu.
Ni itimishe kwa kumwambia Waziri Lugola katika hayo madaraka yako mapya ya Waziri wa Mambo ya Ndani ambayo hata wiki moja ajatimiza tangu apewe madaraka hayo nenda taratibu,hekima na busara vikuongoze.
Acha pupa kwani Mwenye Pupa hali tamu.
Mungu ibariki Tanzania.
Mwandishi wa makala hii ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini na Mwanasheria. .
CHANZO:
www..katabazihappy.blogspot.com
FACE BOOK.Happy Katabazi
0716 774494
6/7/2018
1 comment:
Nimeipenda makala yako hii, kilichofanyika ni bullying, kwa vile huu mtindo wa uongozi kwa bullying unaonekana ndio mtindo wa kisasa, kwanini usiwaumbue viongozi ma bullies wengine wote akiwemo kiongozi za bullying?.
Post a Comment