MAHAKAMA YAKATAA KUMWONDOLEA DPP NGUVU YA KUZUIA DHAMANA KESI ZA UHUJUMU UCHUMI
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama ya Rufani nchini imekataa kutamka Kuwa Kifungu cha 36(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ,sura ya 200 ya Mwaka 2002 kinachompa mamlaka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuzuia dhamana kwa washitakiwa wa kesi za Uhujumu uchumi kinavunja ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 .
Kifungu hicho cha 36(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ,kinampa mamlaka Mkurugenzi wa Mashitaka ( DPP), Kuwasilisha hati ya Kuzuia dhamana kwa sababu ya maslahi ya taifa kwa mshitakiwa anayekabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi na Mahakama Inakuwa haina mamlaka ya Kuzuia hati hiyo ya DPP. Ibara ya 13(2) (a) ya Katiba ya nchi inatoa Haki ya mshitakiwa kupata dhamana.
Hukumu hiyo ya kihistoria Imetolewa Februali 21 Mwaka huu na jopo la Majaji wa tatu wa mahakama hiyo ya juu nchini, Mbarouk Mbarouk ,Mziray na Mkuye Katika rufaa ya jinai namba 252 ya Mwaka 2016 iliyokuwa imekatwa na Mwomba rufaa ,Emmanuel Simforiani Massawe dhidi ya Jamhuri iliyokuwa ikipinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam , wa Aprili 12 Mwaka 2016 Katika ombi dogo la kesi ya jinai Na.51 ya Mwaka 2016 .
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilitupilia mbali ombi la Massawe lilokuwa likiomba mahakama hiyo impatie dhamana katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwasababu dhamana ni haki yake Kikatiba na kwamba anaomba mahakama hiyo itupilie mbali hati ya DPP aliyoiwasilisha chini ya kifungu cha 36(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ,ambacho DDP alikitumia kumfungia dhamana yake kwasababu makosa anayoshitakiwa nayo yana dhamana ambapo Mahakama Kuu ilikataa kumpatia dhamana Massawe kwasababu Kifungo hicho kinampa mamlaka DPP ya Kuzuia dhamana kwa washitakiwa wa Kesi za uhujumu uchumi kwa maslahi ya taifa.
Massawe ambaye alikuwa akitetewa na wakili Dk. Lugemeleza Nshalla ,Fulgence Massawe na Jeremiah Mtobesya ni Mwanasheria wa Reli Asset Holding Company ambaye pia alikuwa akishitakiwa kwa kosa la matumizi Mabaya ya madaraka kinyume Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007 na kusababisha serikali Hasara kinyume paraghrafu ya 10(1) ya Jedwari na Kifungu Cha 57(1) na 60(2) ya Sheria ya Uhujumu Uchumi ya Mwaka 2002.
Mawakili wa Mwomba rufaa, Dk.Nshalla na Mtobesya ,Fulgence walipinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu wakakata rufaa Mahakama ya Rufani na kutaja Sababu Sita za kupinga uamuzi ule Kuwa Mahakama Kuu ilikosea kisheria Kusema haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa mshitakiwa pindi tu DPP anapowasilisha hati ya Kuzuia dhamana ya mshitakiwa.
Sababu ya pili Wakili Dk. Nshalla na Mtobesya alidai ,jaji alikosea kisheria kusema kuwa pindi tu DPP anapokuwa amewasilisha mahakamani hati hiyo ya kuzuia dhamana ,mahakama inakuwa haina tena mamlaka ya kusikiliza maombi ya dhamana.
Tatu, Jaji alijielekeza vibaya wakati akitoa uamuzi wake aliposema Mahakama Kuu aipaswi kujua kilichopo nyuma ya pazia ya hiyo Hati ya DPP ya kufunga dhamana.
Aidha Jaji huyo wa Mahakama Kuu alijielekeza vibaya kisheria kukataa kumpatia dhamana mteja wao (Mwomba rufaa) kwa kigezo cha kulinda usalama na maslahi ya Jamhuri ya Muungano kwasababu dhamana ni haki ya Kikatiba.
Sababu ya Sita ,Mawakili Hao walidai Jaji Huyo alikosea kisheria kwasababu alishindwa kuzingatia uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam ,Katika Kesi Madai namba 29 ya Mwaka 2015 iliyokuwa imefunguliwa na Wakili Jeremiah Mtobesya dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo Mtobebesya aliomba Mahakama hiyo itamke kuwa Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai ,kinachompa mamlaka DPP Kumfungia mshitakiwa dhamana ni kinyume na Katiba ambapo Mahakama hiyo ilitamka Kifungu hicho kinakwenda kinyume na Ibara ya 13 (6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 .
Itakumbukwa Kuwa Januari 31 Mwaka 2018 , Mahakama ya Rufani chini ya jopo la majaji sita ilitupilia Mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Jeremiah Mtobesya ambapo Mahakama hiyo ya Rufaa ilisisitiza Kuwa Kifungu hicho cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinafunja Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya nchi.
Kwa mujibu wa nakala hiyo ya hukumu ambayo ninayo, upande wa Jamhuri ulikuwa ukiongozwa na Wakili Mkuu wa serikali, Tumaini Kweka aliyekuwa akisaidiwa na Beata Kitau na Faraji Nguka walipangua hoja za Mawakili wa Mwomba rufaa kama ifuatavyo.
Wakili wa serikali Kweka alisema anaomba rufaa hiyo it upwe kwasababu hoja ya Mawakili wa Mwomba rufaa iliyotumia maamuzi ya Kesi ya Mtobesya haina mantiki yoyote Katika shauri Hilo kwasababu Kesi ya Mtobesya iliyotolewa uamuzi Mahakama Kuu ilikuwa ni Kesi ya Kikatiba na rufaa hii ya Mwomba rufaa ( Massawe) siyo Kesi ya Kikatiba na Jamii ya Kesi ya jinai na kusisitiza Kuwa DPP anayomamlaka ya Kuzuia dhamana ya mshitakiwa kwa maslahi ya sera ya nchi.
Wakitoa hukumu ya rufaa hiyo ya jinai Jopo Hilo la Majaji watu ,Jaji Mziray alisema kwanza wanataka Ieleweke Kuwa Mahakama hiyo Katika shauri Hilo lilokuwa Mbele Yao lilikuwa siyo Kesi ya Kikatiba ..
'Kesi iliyokuwa mbele yetu ilikuwa ni rufaa ya Kesi ya jinai ambayo Mwomba rufaa (Massawe) alikuwa akiomba Mahakama Kuu impatie dhamana ikakataa kumpatia kwasababu DPP aliwasilisha hati ya Kuzuia dhamana kwa kutumia Kifungu cha 36(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ndipo Mwomba rufaa Huyo akakata rufaa Mahakama ya Rufaa kuomba apatiwe dhamana ....hivyo tunasisitiza Kesi hii siyo ya Kikatiba ni rufaa ya Kesi ya jinai' alisema Jaji Mkuye.
Jaji Mziray alisema jopo Hilo linatupilia Mbali hoja ya Mawakili wa Mwomba rufaa kuwa mwomba rufaa akupewa Haki ya kusikilizwa na Mahakama Kuu wakati DPP alipowasilisha hati ya kumfungia dhamana na kwa mujibu wa rekodi iliyopo mahakamani hapo (Memorundum of Appeal ) inaonyesha Mwomba rufaa (Rufaa)alipewa nafasi na Mahakama Kuu ya kusikilizwa na kwamba pindi DPP anapowasilisha hati hiyo ya Kufunga dhamana ,Mahakama Inakuwa haina mamlaka ya kutoa dhamana kwa mshitakiwa hivyo Mahakama Kuu ilikuwa sahihi kukataa kumpatia dhamana mshitakiwa kwasababu DPP aliwasilisha hati ya Kufunga dhamana .
Alisema Kesi ya DPP dhidi ya NURU DIRIE imeweka msimamo wa kisheria kuhusu hati ya DPP ya Kufunga dhamana kwa kutumia Kifungu hicho cha 36(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi na kwamba DPP atalazimika kuzingatia vitu hivi vitatu ambavyo ni 1. DPP lazima hiyo hati yake iwe Katika mfumo wa maandishi (2) Hati hiyo ya DPP ya Kuzuia dhamana aitoe kwaajili ya Usalama na maslahi ya Jamhuri ya Muungano .(3) Hati hiyo ya DPP ya Kuzuia dhamana itatolewa Katika Kesi za jinai ama Katika Kesi ambazo hazijamalizika au rufaa ambazo bado hazijatolewa hukumu.
" Jopo hili linakubaliana na hoja ya Wakili kiongozi wa serikali Tumaini Kweka kesi ya Mtobesya ni kesi ya Kikatiba na kwamba rufaa ya jinai iliyopo mbele yao siyo kesi ya Kikatiba ni rufaa ya kesi ya Jinai Kuwa rufaa hii ya jinai siyo Kesi ya Kikatiba hivyo ....hivyo siyo matakwa ya Kisheria yanamtaka DPP kutoa Sababu za Kuwasilisha hati ya Kumfungia mshitakiwa yoyote dhamana Kwani DPP anachotakiwa ni kuzingatia Usalama au maslahi ya Jamhuri ya Muungano na kwamba hati hiyo ya DPP inaweza kuonekana haina Msingi pale tu itakabothibitika Kuwa aliwasilisha hati hiyo kwania ovu au matumizi Mabaya ya Mahakama kitu ambacho akijawahi kutokea na kuthibitishwa Mbele ya Mahakama na kwasababu hiyo Mahakama hii inatupilia Mbali rufaa hiyo " Alisema Jaji Mziray
Itakumbukwa Kuwa Junuari 31 Mwaka 2018 , Mahakama ya Rufani nchini chini ya jopo la Majaji Sita, hukumu iliyokuwa imekatwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Jeremiah Mtobesya ambapo Mahakama hiyo ya Rufaa ilisisitiza Kuwa Kifungu hicho cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 ambacho kinampa mamlaka (DPP ) Kufunga dhamana ,kinavunja Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya nchi ambayo inatoa Haki ya mshitakiwa kupata dhamana.
Hukumu hiyo ya Kesi ya Kikatiba maarufu kesi ya Mtobesya ilipokelewa kwa Shangwe na wanaharakati na Wanasheria na Mawakili wa kujitegemea ambao wengine walinukuliwa wakipongeza Mahakama ya Rufani Kuwa imetenda na kwamba DPP alikuwa na mamlaka makubwa yanayovunja Katiba ya nchi.
CHANZO: www.katabazihappy.blogspot.com
FACEBOOK: Happy Katabazi
24/2/2018.
No comments:
Post a Comment