Header Ads

WAANDISHI WA HABARI WAKIWA KAZINI


Pichani nipo na Mwanahabari mwenzagu toka gazeti la The Citzen,Bernad James, nje ya jesngo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam,kufuatilia wa kesi ya madai iliyofunguliwa Ijumaa ya Oktoba 5 mwaka 2007, na vyama vinne vya siasa dhidi ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. James ni mwandishi mwenzangu ninayeripoti naye kesi mbalimbali katika mahakama hiyo.(Picha na Kassim Mbarouk wa Gazeti la Mwananchi).

16 comments:

Simon Kitururu said...

Poa sana Mkikutana!

Endeleeni kutupa habari kubwa kuliko! Si mnajua jinsi gani habari ndogo kuliko zinavyotawala?

Anonymous said...

Wewe dada ni CUF, kama siyo CUF basi wewe ni wa Kabwe, sababu unapamba sana wapinzani, mbona uangalii shilingi pande zote mbili? unajua napenda sana mada zako, baya zaidi ni kuwa kila mara you just focus kwenya party moja and not both side. Wewe ni mwandishi mzuri sana, unatakiwa kuonyesha mabaya ya upinzani pia... I'm not CCM even CUF, mimi ni mtanzania niliohukana utanzania wangu na sasa ni raia wa Norway.

Anonymous said...

Naungana kabisa na anonymous wa hapo juu, dada huyu ni mwandishi mzuri sana, lakini anapamba sana upinzani, nadhani anaweza kuwa mwandishi mzuri kama ataweza kuwa na balance kuliko kuwa upande mmoja. Namfagilia sana, habari zake ni nzuri sana.... na dada huyu ni shujaa sana. Dada be balance not only CUF and Chadema tupatie habari za vyama vingine.

Anonymous said...

nyinyi mmezoea kusifia upuuzi huyu dada ana uhuru wa kutoa ukweli na uwazi wa maisha ya kila siku.Nyie mnaonekana mkipewa mapambo feki kauli za viongozi wetu mnafurahia sana hivi hamuoni mtanzania wa kawaida anumia sana hapo cuf au chadema imetoka wapi?Na bila watu kama huyu dada mtu wa kawaida atajuaje utata unaowekwa na mtu kama KINGUNGE asiyeona na kutaka kujua kuwa hata warusi aliposomea wamebadilika ndugu zangu KUWENI WAWAZI HAIWAGHARIMU CHOCHOTE.
Bro MUGA LONDON

Anonymous said...

Ni mitizamo tu, na vijimambo pia. Keep it up

Anonymous said...

We non wa kwanza na wa pili: Mnahoji kuwa huyu dada anaandika makala za upande mmoja tu, mmetembelea makala zake zote kwenye blog yake mkadhibitisha madai yenu? Nawashauri mtembelee blog yake mtakuta makala zinazohusu vyama vingine vya upinzani na hata kuipongeza serikali pale inapofanya mazuri. Mungu mbariki dada huyu aendelee kutuletea vitu adimu.

Anonymous said...

Salaam!

Nawashukuru wadau wote mnafuatilia mada zangu na kuikubali kazi yangu.Changamoto mlizonipatia na ahidi kuzifanyiakazi. Endeleeni kufuatilia mada zangu nami nawaakikishia sitachoka kuwahabarisha.

Tchao

Egidio Ndabagoye said...

Kazi nzuri sana.Kuna wakati unaweza kutafuta kizuri cha sehemu fulani ukakosa.

Mimi naona poa tu hao CCM walaghai kama nini wanafanya mambo kwa maslahi yao na familia zao,hawajui kuwa sisi ndio tumewaweka hapo juu na wakati wowote tukiamka tunashusha!

Happy Kaza buti!

Rashid Mkwinda said...

Kazi nzuri dadaa waache waseme kalamu ndizo zinazofanya kazi wamesahau hata mheshimiwa alitumia kalamu kama risasi ya kuingilia huko ILIKO LULU kunako wafanya wote wakimbilie

Rashid Mkwinda said...

Hawa jamaa wawili vp mie nashindwa kuwalewa ndio maana wameamua kuficha majina yao, hivi utasifia upuuzi??? kama kusifiwa mbona wamesifiwa zaidi ya miaka 40 na bado hali yetu ya uchumi iko pale pale ilhali tuna rasilimali zinazouzwa nje ya nchi, mikataba feki na mambo kadha wa kadha huku akina mama wakilala mzungu wa nne mahospitalini,elimu duni huduma duni za maji safi na mambo chungu nzima ambayo m2 mwenye akili atamaizi bila kuambiwa.

Mie nadhani hawa jamaa wamelalia masikio nadhani likiingia giza husahau hata midomo yao na kuinngiza matonge puani....yaah ndivyo ilivyo kwani uongo kama hukijui hata kimvuli chako unaweza kutumbukiza tonge mdomoni wakati giza limeingia?? acheni mambo yenu yasiyokuwa na mantiki kusifia vinavyohitaji kurekebishwa.

Kwa kweli watu wa dizaini hii wakiwa karibu unaweza hata kuwachapa bakora maana hawajui kabisa kinachoendelea katika nchi yao wamekalia majungu na fitina na kukataa kuelezwa ukweli.

Mie wananiudhiiii natamani kutema mate chini hivi hawa wakoje hawaa wako dunia gani hawa, hawaoni wenzao walivyosambaa nchi nzima kujaribu kuwarekebisha wananchi ambao wameamka kifikra, angalia hata sehemu zingine wanaanza kuzomewa, ikifika hali hii ni hatari tena sijui 2010 itakuwaje, maana hata Mheshimiwa JK keshaona dalili za kushindwa siku moja si mmemsikia alivyonukuliwa na vyombo vya habari magazeti ya leo leo??

Rashid Mkwinda said...

Hawa jamaa wawili vp mie nashindwa kuwalewa ndio maana wameamua kuficha majina yao, hivi utasifia upuuzi??? kama kusifiwa mbona wamesifiwa zaidi ya miaka 40 na bado hali yetu ya uchumi iko pale pale ilhali tuna rasilimali zinazouzwa nje ya nchi, mikataba feki na mambo kadha wa kadha huku akina mama wakilala mzungu wa nne mahospitalini,elimu duni huduma duni za maji safi na mambo chungu nzima ambayo m2 mwenye akili atamaizi bila kuambiwa.

Mie nadhani hawa jamaa wamelalia masikio nadhani likiingia giza husahau hata midomo yao na kuinngiza matonge puani....yaah ndivyo ilivyo kwani uongo kama hukijui hata kimvuli chako unaweza kutumbukiza tonge mdomoni wakati giza limeingia?? acheni mambo yenu yasiyokuwa na mantiki kusifia vinavyohitaji kurekebishwa.

Kwa kweli watu wa dizaini hii wakiwa karibu unaweza hata kuwachapa bakora maana hawajui kabisa kinachoendelea katika nchi yao wamekalia majungu na fitina na kukataa kuelezwa ukweli.

Mie wananiudhiiii natamani kutema mate chini hivi hawa wakoje hawaa wako dunia gani hawa, hawaoni wenzao walivyosambaa nchi nzima kujaribu kuwarekebisha wananchi ambao wameamka kifikra, angalia hata sehemu zingine wanaanza kuzomewa, ikifika hali hii ni hatari tena sijui 2010 itakuwaje, maana hata Mheshimiwa JK keshaona dalili za kushindwa siku moja si mmemsikia alivyonukuliwa na vyombo vya habari magazeti ya leo leo??

Anonymous said...

NILIANZA KUFATILIA MAKALA ZA HII BLOG KUTOKA KULE KWA HAKI NGOWI, KAZI NZURI UNAFANYAA DADA KAZANAA KWA MAKALA ZAKO MOTOMOTO

Anonymous said...

Mimi ni anonyomous wa tatu, kuna jamaa ameongelea uchumi hapo chini, mzee tunaweza ongelea hili la uchumi kwa undani kabisa siyo kusema tu, tema mate yako chini, who cares.... wewe kwanza hata darasa la saba ujamaliza... Wewe Rashid Mkindwa, naomba kama unataka ongelea uchumi basi tuongee kwa hilo.... again I repeat... dada huyo hayupo fear... mimi sikuongolea CCM wala nini na wala sipo CCM na sina mpango huo, cha msingi nataka dada huyu awe fear for other parties such as NCCR and vyama vingine....narudia tena dada huyu awe fear tu, siyo kila mara Mbowe and Zibwe sijui nani huyu...wajomba changieni mimi ni Nic hapa Norway

Said Michael said...

Ohoooo!!!! We Nic wa Norway:
Kashfa za nini tena? Mara oh! Umeishia la ngapi..., yanatuhusu nini sisi hayo? Tuwe wastaarabu katika kuchangia mawazo, Unaweza ukasoma kwa kuhesabu madarasa na vyeti kibaaao! Lakini usielimike. Jambo la msingi hapa ni kueleweshana tu na si kushfiana jamani au sio?

Anonymous said...

anonymous namba tatu unaandika ili ujulikane na wewe upo au...? unaposema dada huyu hayuko fear una maana gani? neno fear waweza kulilinganisha na maneno dread,terror,horror,fright,panic,trepidation na apprehension. kama unamaanisha huyu dada si mwoga hapo unasema ukweli. lakini kama ulimaanisha anapendelea upande mmoja kama wanavyosema wenzako wawili, basi hata kiingereza hukijui japo unatukana wenzako kwamba elimu yao ndogo. acheni upuuzi, uchafu wa watawala sharti uanikwe juani na kufanya hivyo si kupendelea hata kidogo.
Happy,usiogope kelele za chura hasa wanaokana uraia kisha wakajidai eti wanapenda kujua habari za tanzania na wana uchungu na nchi hii.huo ni uanafiki uliokithiri,songa mbele dada yetu.
KAHANGWA

Rashid Mkwinda said...

Mimi naitwa Rashid Mkwinda, sio mkindwa kama ulivyoandika

Mara nyingi muungwana akivuliwa nguo huchutama!!!!! huo ni msemo wa wahenga na mara nyingi wahenga hunena kile chenye maana, kejeli matusi na maneno ya bezo mara nyingi huwa hayaoneshi mustakabali wa ujuaji bali hunasibu ujinga ambao mara nyingi matunda yake huwa ni jazba zisizo kuwa na maana yoyote.

Ukweli mara nyingi unapodhihiri huwachoma wale wenye kedi bezo na fitina lukuki ambazo kwazo ndizo chimbuko la ukiritimba ambao huwapa kiburi baadhi ya watu ambao hudhani kuwa siku zote kila mtu ni mjinga mfano wake.

Nakumbuka msemo wa wahenga waliosema kuwa, iwapo utakuwa mtoni umechojoa nguo zako na baadaye mwendawazimu akaja kuchukua nguo zako na kutimua nazo, iwapo wewe uliye mtoni utaamua kumfukuza yule mwenda wazimu wewe uliye mtupu ndiye utakayeonekana mwenda wazimu na yule mwenda wazimu ndiye atakayeonekana mzima.

Kikubwa ni kwamba tunashukuru ujumbe umewafikia walengwa na hii ni dalili kuwa kisu kimegusa mfupa na maumivu yake ndiyo hayo watu wanakurupuka katika blogu na kuanza kutoa kejeli.

Naamini kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji, kalamu bado zitaendelea kufanya kazi, lakini kwanini basi unajificha jina lako hii ndio dalili ya majungu mara nyingi anayepigana vita kinafiki hupenda kujificha ili asionekane jitokeze basi tukuone kama kweli wewe ni mwanaume.

Powered by Blogger.