BUNGE LA KATIBA NI 'KOMEDI'?
BUNGE LA KATIBA NI " KOMEDI"
Na Happiness Katabazi
HAKUNA Ubishi kuwa siku hizi ukitaka kucheka, kukereka na kupunguza msongo wa mawazo uliyonayo, ukitaka kujifunza maneno machafu mapya, huna budi kufungulia Televisheni ya Taifa (TBC1), na kuanza kuangalia mijadala ya Bunge la Katiba la Tanzania linavyoendeshwa na jinsi wajumbe wa bunge hilo wanavyochangia kwa kutumia lugha za matusi, zisizonastaa na zinazopolomosha heshima ya bunge hilo na jamii yetu ya Tanzania.
Na Baadhi wananchi wengine wamekuwa wakisema uenda kabla ya bunge hilo kuanza , baadhi ya wajumbe wanakunywa kwanza ‘viroba’ ndiyo wanaingia ndani ya bunge na kuanza kuchangia mjadala kwa kutoa lugha za kejeli, uzushi, kuzomea na kugonga meza ovyo.
Nimeyasema hayo kwasababu tayari baadhi ya wananchi wameisha lipachika bunge la Katiba kuwa ni ‘Komedi’. Kwa wajumbe wa bunge hilo ambao ni watu wazima wenye umri wa zaidi ya miaka 18 , baadhi yao wameshindwa kujiheshimu na kuchunga kauli zao wakati wakichangia mjadala wa mchakato wa kupata Katiba Mpya
Kila kukicha tumesikia wabunge hao wengine wakiwa na umri mdogo wamekuwa wakiwatolea maneno ya ‘shombo’ wajumbe wenzao ambao wamewazidi umri kwa kisingizio kuwa wajumbe hao wenye umri unaowazidi na kuwapita hata wazazi hao wamekuwa wakilidanganya bunge, na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo ambao wanaumri mkubwa nao wamekuwa wakiwatolea maneno yasiyofahaa wajumbe wenzao wenye umri mdogo wachangiapo mjadala huo.
Mila na tamaduni zetu ni mkubwa anamheshimu mdogo na mdogo anamheshimu mkubwa lakini kupitia bunge letu la Katib a’Komedi’, niwazi wajumbe wa bunge hilo wanauzika utamaduni huo na kufanya sasa jamii ya watanzania waanze kuishi kwa kutumia utawawa Kambare kwani baba,mama ,mtoto wa kambare wote wanandevu hakuna wa kumbabaisha mwenzie.
Nia ya Rais Jakaya Kikwete ya kutaka Tanzania iandike Katiba mpya ni njema, ila sasa tunashuhudia baadhi ya wajumbe wa bunge hilo hawataki nia hiyo ikamilike kwa kila siku kuibua mapingamizi na hoja zisizokuwa na kichwa wa miguu hali inayosababisha hivi sasa heshima ya bunge hilo kuporomoka na kuona ni kheri tubakie na Katiba ya zamani ya mwaka 1977 licha ina mapungufu yake kuliko kuletewa Katiba mpya ambayo inaendelea kuandikwa na baadhi ya wajumbe waliokosa adabu, wanatumia lugha za matusi, uzushi kwa kisingizio kuwa eti wanataka serikali mbili wengine wanataka serikali tatu.
Kwa wale tuliopata kuisoma rasimu ya pili ya Katiba, mtakubaliana na mimi rasimu hiyo imeandikwa vitu vingi sana siyo Muungo wa Serikali mbili, Serikali tatu, wala hati ya Muungano pekee.Imeandikwa vitu vingi lakini hatuoni kama baadhi ya wajumbe wanajipa muda wa kuisoma rasmi hiyo yote na kufahamu kilichoandikwa.
Leo hii baadhi ya wajumbe wanaibuka wanasema hati za Muungano mara zimegushiwa, mara hazipo kwa sababu hiyo hakuna muungano.Na mbaya zaidi wanaongea uzushi ndani ya bunge hilo hawatoi vielelezo.Tuwaulize wajumbe wa aina hii hivi siku hati za Muungano zilivyokuwa zinatengenezwa na waliozitengeneza na zikasainiwa na Marehemu Baba wa Taifa Julias Nyerere na Rais wa Zanzibar, Abeid Aman Karume walikuwepo?
Mapema wiki hii Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alifanya mkutano wake na waandishi wa habari na kuwaonyesha hati za Muungano na kusema hati hiyo ni halisi na kwamba Rais Jakaya Kikwete amesikitishwa na uzushi huo kwamba hati hazipo, na lugha za kejeli na matusi.
Minashangaa sana huyo Balozi Sefue anavyosema Rais Kikwete eti amesikitishwa na vitendo hivyo.
Naye Rais Kikwete amenukuliwa juzi akisema kuwa anakerwa na lugha za kejeli , matusi nakuwakejeri waasisi wa taifa hili.
Ni najiuliza Kwa hiyo rais Kikwete akishasikitika ndiyo hao wajumbe wazushi, wanaotoa lugha za kejeli ndiyo wataacha tabia hiyo ambalo linaporomosha heshima ya bunge hilo mbele ya jamii?
Kwa hiyo Rais Kikwete akisikitishwa na lugha hiyo za kejeli zinazotolewa na Hao baadhi ya wabunge la Katiba, ambao watu tunaofikiri sawa sawa HIvi sasa kutokana na vitendo Vya kishenzi na kijani vinavyofanywa ndani ya Bunge na Hao wajumbe HIvi huo mchakato wa kuwapata wajumbe wale ulifanywa na watu wenye akili timamu au wahuni tu?
Maana aingii akilini kabisa kuna baadhi ya wajumbe ambao tangu serikali hii iingie madarakani Desemba 21 mwaka 2005 , wamekuwa wakipinga kila kinachofanywa na serikali hii kiwe kizuri au kibaya na wazushi wakubwa, lakini cha ajabu Rais Kikwete akawateua baadhi ya wanasiasa hao sijui akidhani kwa kuwateua ndio atawafurahisha na wataacha kuzua uongo?
Matokeo yake wajumbe hao wenye tabia hiyo baada ya kufika ndani ya bunge hilo ndiyo kwanza wameendelea na tabia zao ya uzushi, kulazimisha mambo wanayoyataka wao tu na wanataka watu wote waamini yale wanayoyaamini wao na kuzua taftari ma maneno ya shombo ndani ya bunge jambo linalosababisha hivi sasa heshima ya bunge hilo kuanza kuporomoka kwasababu ya vitendo vya kiuni kufanywa na baadhi ya wajumbe ambao wengine ni wateuli wa rais Kikwete.
Wahenga waliwahi Kusema " Mtoto umleavyo ndivyo akuwavyo". Msemo huu umethibitika kwamba Katika Utawala wa serikali awamu ya nne imekuwa ikiwa lea na wakiwa kukumbatia baadhi ya wanasiasa na wanaharakati ambao wamekuwa wakitoa maoni Yao kupitia vyombo Vya Habari, mikutano ya adharani kuzulia uongo na kuwachafua mahasimu wao kisiasa, vyama Vya siasa na wakati mwingine serikali.
Sasa tabia hiyo chafu ya kuzua maneno ya uongo ndiyo Imefikia mahali sasa wajumbe wa Bunge la Katiba kufikia Hatua ya Kusema Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mara imegushiwa Mara haipo wakati ipo.
Kwa hiyo tabia hii Chafu iliyoota mizizi sasa Kwenye vinywa na Fikra Kwa baadhi ya wanasiasa wetu uchwara ya uzishi, upotoshaji kwa kiasi kubwa nadiriki Kusema imelelewa na kukumbatia sana na Utawala wa serikali awamu ya NNE ambayo Katika Utawala awamu ya NNE ndiyo wanasiasa Wengi uchwara hapa nchini ndiyo wamekuwa walitumia mbinu hiyo ya uzishi na uongo Katika hotuba zao kuwadanganya wananchi Katika Mashaka mbalimbali.
Na uthibitisho wa hili ni kitendo Cha baadhi ya wajumbe wa Bunge Hilo kusimama ndani ya Bunge Kusema eti hati ya Muungano haipo , wengine imegushiwa Kumbe hati hiyo ipo.
Mbona serikali hii imeishawahi kuyafungia baadhi ya magazeti kwa kile ilichodai kuwa magazeti hayo yamekuwa yakiandika habari ambazo zinaleta uchochezi na uhasama katika jamii?.
Kwanini baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kwa ushabiki wao wa kijinga tu wa kundi moja linataka serikali mbili jingine linataka serikali tatu lifikie sehemu ya kufanya vitendo vya kulidhalilisha bunge letu mbele ya walipa kodi?
Hata kama hati zilizotolewa na Balozi Sefue ni halisi au zimegushiwa hao walisema hati za muungano hazipo na zimeghushiwa wanaweza kuzitambua? .Tukubaliane kimsingi si kila nyaraka ya serikali inatakiwa kuwekwa wazi.Nyaraka zingine hazistahili kuwekwa adharani.
Siku zote wananchi wataendelea kuzieheshimu na kuziogopa mahakama licha mahakama zetu nyingi hazina mazingira mazuri ya ofisi kwasababu mahakimu na majaji wanaoendesha kesi wanajiheshimu wawapo mahakamani wakiendesha kesi.Wakati kesi zikiendeshwa hutakuta mtu akipokea simu, wala kuchati wala kupigana picha na kisha picha kuweka kwenye simu wakati kesi zikiendelea.
Lakini hivi sasa tunashuhudia baadhi ya wajumbe wa bunge la Katiba wakati bunge hilo likiendelea wakitumia Ipad na simu zao kuchati na kupigana picha.Hivi tujiulize muda wa kufuatilia kwa makini hoja zinazotolewa na wajumbe wenzao wanaupata wapi?Maana muda wote wapo bize na simu?
Na nina mshangaa sana huyu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba,Samuel Sitta ambaye ni msomi wa sheria anashindwa kupiga marufuku ufedhuli huu ambao nao unaporomosha heshima ya bunge hilo ambalo hivi sasa huku mitaani limepewa jina la utani la ‘Komedi’.
Kwa uhuni huu unaofanywa na baadhi ya wajumbe wa bunge la Katiba wa kuibua hoja za uzushi, kejeli,matusi ambazo zimesababisha baadhi ya wajumbe hao wamekosa adabu wanaacha bila kuchukuliwa hatua, kunanifanya sasa nione ni kheri tuendelee kutumia Katiba ya zamani ya mwaka 1977 ambayo ni kweli ina mapungufu ambayo yanaweza kurekebishwa kuliko kuja kutumia hiyo Katiba mpya ambayo inaendelea kutengenezwa na hawa baadhi wajumbe ambao wakati wanaitengeneza walikuwa wakitumia lugha chafu na uzushi.
Katiba Mpya sio itaji muhimu sana kama lilivyoitaji la serikali kutoa hela kununua madawa mengi kuweka mahospitalini, kujenga miundombinu,kutengeneza wodi za kuzaliwa wa kinamama, kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa UTI ambao hivi sasa umeanza kuwa tishio kubwa hapa nchini.
Kama kweli tunataka kutengeneza hiyo Katiba mpya, wale wajumbe wa bunge hilo ambao kisheria sisi tunasema wao siyo wa mwisho wa kutengeneza Katiba mpya ,wajiheshimu na watimize jukumu lao hilo kwa nidhamu bila kuvunja heshima ya bunge hilo na kupotosha jamii.
Ni ajabu sana wajumbe wa bunge la Katiba kutaka kuparurana kuhusu mchakato wa kupata Katiba mpya, wakati sisi tuliosoma somo la Katiba tumefundishwa kuna hatua kadhaa za kufikia kutengeneza Katiba mpya. Hatua ya kwanza ni Tume kukusanya maoni ya wananchi, tume kuyaweka kwenye maandishi maoni hayo(rasimu), Bunge la Katiba kuijadili rasimu husika kama bunge linavyofanya sasa, kisha yaliyojadiliwa na Bunge yapelekwe kwa kwa wananchi wayapigie kura za ndio au hapana.
Sasa nyie wajumbe mnaotaka kuparulana kwa kisingizio cha kutaka serikali mbili, mara tatu make mkijua bunge siyo chombo cha mwisho ya kutengeneza Katiba mpya.
0716 774494
www.katabazihappy.blogspot.com
Aprili 19 Mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment