Header Ads

KESI YA PONDA YADODA DAR


KESI YA PONDA YADODA DAR 
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imearisha Kesi ya kuomba Kesi ya uchochezi ilipofunguliwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro isimame hadi rufaa iliyokatwa na Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, kwasababu upande wa mlalamikaji(Ponda), haujapewa majibu  na upande wa jamhuri.

Ponda aliwasilisha mahakamani hapo ombi la Kuomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia Kesi ya ya uchochezi inayomkabili Morogoro ,isiendelee kusikilizwa hadi pale rufaa yake aliyoikata mapema Mwaka Jana ya Kapinga hukumu iliyotolewa Na Mahakama ya Kisutu Mei 9 Mwaka Jana, ambayo ilimtia hatiani Kwa kosa la kuingia Kwa jinai Katika Kiwanja Cha Markas Chang' ombe, ambapo Mahakama hiyo ilimfunga Kifungo Cha nje Cha Mwaka mmoja, lakini Agosti Mwaka Jana, alifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro akikabiliwa na Kesi mpya ya uchochezi na kutenda kosa wakati yupo chini ya uangalizi wa Kifungo Cha Mwaka mmoja nje.

Wakili Mwandamizi wa serikali Bernad Kongora ambapo katika kesi hiyo. Upande wa jamhuri ni mdaiwa, Mbele ya Jaji  Lawrence Kaduri alidai Kuwa Kesi  hiliyo ilikuja kwaajili ya kutajwa na kwamba hata hivyo upande wa Mawakili wa Ponda umedai hapo Tayari kwaajili ya kuendelea kwasababu bado hawajapatiwa Hati kinzani na upande wa jamhuri.

Wakili Kongora alidai wao Tayari walishawasilisha hati kinzani mahakamani ,na kwamba Tayari upande wa jamhuri umewasilisha pingamizi la kupinga ombi Hilo la Ponda na Jaji Kaduri aliarisha Kesi hiyo hadi Juni 16 Mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kusikilizwa, hata hivyo Ponda na kuwepo mahakamani.

Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com
Mei 30 Mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.