Header Ads

MKURUGENZI TANESCO,MKEWE KORTINI



Na Happiness Katabazi
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), ilimfikisha Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Da es Salaam, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme(TANESCO), William Mhando na Mkewe Eva Mhando pamoja na maofisa wengine wa serikali makosa mbalimbali likiwemo kosa la matumizi Mabaya ya madaraka na kughushi.

Mbali na Mhando na Mkewe ambao wanatetewa na wakili wa kujitegemea Jamhuri Johnson, washitakiwa wengine ni Francis Machalange ambaye ni Mhasibu Mkuu wa Tanesco,Sophia Misidai  ambaye ni Mhasibu Mkuu  na Naftali Kisinga  ambaye ni Ofisa Ugavi wa Shirika Hilo.

Mwendesha Mashitaka wa TAkukuru, Leonard Swai , Mbele  ya Hakimu Mkazi Frank Moshi alidai kosa la kwanza linamkabili Mhando peke yake ambalo  ni kosa la matumizi Mabaya ya madaraka  kinyume na Kifungu Cha 31 haSheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Kuwa Kati ya Aprili Mosi na Desemba 31  Mwaka 2011 huko Tanesco makao makuu, Akiwa ni mwajiriwa  na mwenye wadhifa huo wakati akienda majukumu yake Kwa makusudi  alishindwa kutaka maslahi yake kuhusiana na kampuni ya usambazaji wa Santa Clara , kampuni ambayo wakurugenzi wake ni Mke wake Eva Mhando na watoto wake , kitendo ambacho kilisababisha  kampuni ya Santa Clara kupewa mkataba wa kusambaza vifaa Vya Ofisi kwa Tanesco vyenye Thamani sh.884,550,000 KWA kukiuka Maadili ya Tanesco na Sheria ya uongozi wa Maadili ya umma na kusababisha kampuni hiyo kupata faida I siyo halali ya sh. 31,747,000.

Wakili wa Swai akili taja kosa la pili ambalo  ni kwaajili ya Eva Mhando, ni kughushi kinyume na Kifungu Cha 333,337 Cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002, Kuwa Kati ya Januari 6 na Julai  30 ya Mwaka 2011 , Katika sehemu zisizojulikana ndani ya Dar es salaam,  KWA Dhamira ya kughushi ripoti ya ukaguzi wa mahesabu  kwamba ilikaguliwa na kampuni ya  Finx Capital  House kwamba kampuni ya ya Sant Lara ilikaguliwa Mwaka 2010 jambo alilokuwa akijua ni uongo.

kosa la Tatu ni la kughushi pia ambalo  linamkabili  Eva,  Kuwa Kati Agosti 9 Mwaka 2011 Jijini Dar es Salaam, KWA Dhamira ya kughushi hati ya kuamisha hisa kwa Lengo la Kuonyesha kwamba aliamisha hisa zake 200 zenye Thamani ya sh.10,000 Kwenye kampuni inayoitwa Sant Clara KWA  Eveta John Shing'oma. Huku akijua ni uongo.

Swai alikutana kosa jingine AMBAlo linamkabili Eva kuwa ni la Kuwasilisha Nyakirang'ani za uongo Kinyume na Kifungu Cha 342 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002, Kuwa Kati ya Agosti 5 Mwaka 2011 , Makao Makuu ya Tanesco, akijua ni uongo aliwasilisha Nyaraka hizo zilizoghushiwa Kwa Katibu wa Bodi yaTenda ya Tanesco, ile taarifa ya Fedha ilikuonyesha  kampuni ya Sant Clara  KWA Kuonyesha kwamba ripoti hiyo ya mahesabu iliandaliwa na Finx Capital Houes ambayo ilikaguliwa taarifa ya Fedha ya Sant Clara Kwa Desemba 2010 suala AMBAlo akijua ni uongo.

SHITAKA la tano KWA Eva ambaye ni Mke wa Mhando,ni la kujatia Fedha KWA njia ya udanganyifu kinyume na Kifungu cha302 chaSheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka2002', Kati ya Aprili Moja na Oktoba 31 Mwaka 2011, Akiwa Mkurugenzk Mtendaji wa Sant Clara KWA nia ya Kudanganya alijatia sh 31,747,000 kutoka Tanesco kupitia Usambazi wa vifaa Vya ofisi KWA    Tanesco baada ya Kuwasilisha Nyaraka za uongo ambazo ni ripoti ya ukaguzi wa Fedha KWA Mwaka 2007/2008 na orodha ya mi katana mikubwa ya Miaka miwili kuanzia Mwaka 2011  kwa Katibu  wa Bodi ya Tendaya Tanesco Kwa Lengo la Kuonyesha kwamba kampuni ya Santa Clara ilikuwa Imetimiza vigezo Vya awali Vya kupewa Tenda ya usambazaji wa vifaa Vya ofisi KWA Mwaka 2011 KWA Tanesco.

Kosa la Sita KWA kwaajili ya mshitakiwa Francis Mchalange, Sophia Misidai na Naftali Kisinga.ALILItaja kosa Hilo Kuwa ni la matumizi Mabaya a madaraka kinyume na Kifungu Cha 31 Cha Kupambana na Kuzuia Rushwa ya Mwaka 2007.

Kuwa  Oktoba  17 Mwaka 2011,  Katika Makao makuu Tanesco, wakiwa ni waajiliwe wa Tanesco Kama Wahasib wa Kuu wa Tanesco na Afisa Ugavi , na wakiwa wajumbe wa Kamati  ya Kutathimini Tenda Na. PA/001/11/HQ/G/011 kwaajili ya usambazaji wa OFISI KWA Mwaka wa Fedha Kama ilivyopitishwa na Mtendaji Mkuu wa Tanesco Katika kutekeleza majukumu Yao, KWA kukusudia walitumia vibaya madaraka Yao KWA kutoa maelezo ya uongo kwa avoid ya Tenda KWA  Lengo la Kuonyesha Kuwa Kampuni ya Sant Clara ni kampuni bora na inavigezo ambayo ilistahili kupewa hiyo Tenda kusambaza vifaa Vya ofisi hapo Tanesco ,kitendo kilichosababisba kampuni ya Sant Clara kupewa kampuni ya kusambaza vifaa Vya ofisi Kwa Tanesco, vyenye Thamani ya sh 884,550 ,000 KWA kuvunja Sheria na kufanya kampuni ya Sant Clara kujipatia faida I siyo halali kiasi Cha sh 31,747,000 na kwamba upelelezi wa Kesi hiyo umekamilika.

Hata hivyo washitakiwa wote walikana Mashitaka na Hakimu Moshi Alisema ili washitakiwa wa late dhamana ni lazima kila mmoja awe na wadhamini Wawili wa kuaminika ambao watasaini bondi ya Sh.milioni nane kwa kila mmoja na kwamba mshitakiwa yote hata ruhusiwa kutoka  nje ya Dar e salaam bila Kibali, na washitakiwa Hao walitimiza Masharti hayo lakini Wakili Swai aliomba Mahakama. Iarishe Kesi Kwa MUDa ili waende kuakiki barua za wadhamini na Hakimu Moshi akaamuru washitakiwa wapelekwe mahabusu ya Mahakama hiyo hadi saa Saba mchana ili Mahakama ije kuona Kama wadhamini Hao wanataka Katika Ofisi  walizozisema.

Ilipofika saa Saba washitakiwa Hao walirejeshwa tena kizimbani ambao Wakili Takukuru, Swai alidai Kuwa Tayari wameishakamilisha uchunguzi wao kuhusu barua za wadhamini wa washitakiwa na kwamba ni kweli wadhamini Hao ni wadhamini wa kuaminika na kuomba Mahakama iwapatie DHA

KWA upande wake Hakimu Moshi aliwapatia DHAMANA washitakiwa Hao na akaairisha Kesi hiyo hadi Juni 13 Mwaka huu, Kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Katika hatua nyingine wafanyakazi wa Tanesco ndio wamejitokeza kuwadhamini washitakiwa wote isipokuwa mshitakiwa Machalange naye mdhami Mmoja aliyemdhamini ni mfanyakazi wa Tanesco na mmoja ni mtumishi wa mahakama.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 27 Mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.