Header Ads

MAHAKAMA YATUPA KESI YA PINDA



MAHAKAMA YATUPA KESI YA PINDA 
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,imetupilia Mbali Kesi ya Madai  ya Tanzania imetupilia mbali kesi dhidi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa sababu Imeona walalamikaji walikuwa hawana Haki ya kisheria ya kushitaki Pinda.

Kesi hiyo Na. 24/2013   ilikuwa ikisikilizwa chini ya jopo la majaji watatu waliokuwa wakiongozwa  Jaji Kiongozi Fakih Jundu, Jaji Dk. Fauz Twaib na Jaji Augustine Mwarija.

Jopo hilo lilitoa uamuzi huo jana ambapo jaji Jaji Jundu alisema anakubaliana na pingamizi la awali lilowasilishwa na wakili wa mdaiwa (Pinda), Ambaye ni Naibu Mwanasheri Mkuu wa Serikali,  George Masaju, AMBAlo lilikuwa likiomba  Mahakama itoe amri ya kuifuta Kesi hiyo kwasababu walalamikaji hawana Haki a kisheria ya kuwashitaki wadaiwa na kwamba Waliokuwa na Haki ya kushitaki Pinda ni wananchi na siyo Taasisi hizo za walalamikaji.
O
LHRC na TLS walimshtakiwa Waziri Mkuu Pinda pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kauli aliyoitoa bungeni Juni 20 mwaka jana.Ilidaiwa Katika   kipindi cha maswali ya papo kwa papo Waziri Pinda akijibu alisema, ‘ukifanya fujo…unaambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi, utapigwa tu, muwapige tu sababu tumechoka’.

 Jaji Jundu alisema, Masaju Aliwasilisha  pingamizi la awali akiomba  kesi hiyo itupwe kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kuisikiliza, waliofungua hawakustahili kuifungua na iko kwa ajili ya kupoteza MUDa wa Mahakama.

Katika uamuzi huo, majaji walikubaliana na hoja tatu za pingamizi kuwa walalamikaji katika kesi hiyo hawakuwa na haki ya kufungua kesi hiyo na kwamba walikosea taratibu za ufunguaji wa kesi kama hizo kwa kuwa walikiuka amri na kanuni zinazoongoza Mashauri ya Madai (CPC).

Katika hoja ya kwanza kuwa Pinda kama mbunge analindwa na Katiba, jopo hilo lilisema kuwa ni kweli wabunge wanalindwa na Katiba Ibara ya 100 (1) kuhusu haki na upendeleo (Previledge), yaani haki na uhuru wa mjadala na maoni. Hata hivyo, lilikataa hoja za utetezi kuwa wabunge wana kinga isiyo na mipaka ya kutokushtakiwa kwa kauli au jambo lolote walilolitamka bungeni.

“Ibara ya 100(1) ya Katiba haiwezi kujadiliwa mahali popote ikiwemo mahakamani, ibara hiyo inasema kwamba, kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano au katika mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

“Ibara ya 100(2) inaweza kujadiliwa mahakamani, inasema kwamba bila kuathiri katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yoyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.

“Mwananchi mmoja mmoja aliyeathika na jambo lililozungumzwa na mbunge bungeni anaweza kushtaki lakini si taasisi kama ilivyo katika kesi hii,”alisema.
Alisema kutokana na sababu hizo, mahakama inatupilia mbali kesi hiyo kwa sababu waliofungua kesi, LHRC na TLS hawakustahili kisheria kufungua kesi hiyo kwa sababu hawakuathirika.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Juni 7 Mwaka 2014



No comments:

Powered by Blogger.