GWAJIMA 'MSHENGA' NI MTUMISHI WA MUNGU KWELI?
Na Happiness Katabazi
SEPTEMBA mosi mwaka huu ,aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Dk.Wilbroad Slaa alimrushia tuhuma chafu kiongozi wa Kanisa la ufufuo na uzima Askofu Josephat Gwajima.
Dk.Slaa aliyasema hayo Jana mchana Katika mkutano wake na waandishi wa Habari uliofanyika Katika Hoteli ya Serena Dar Es Salaam.
Mkutano ule wa Dk.Slaa ni wakwanza kufanya tangu alipostaafu rasmi siasa Julai 27 Mwaka huu, baada ya kushindwa kuvumilia na siasa zinazoondelea ndani ya Chadema ambayo alishiriki kukijenga cha hicho kwa muda mrefu .
Nilimfuatilia Dk.Slaa kupitia Televisheni Jana mchana na Jana saa nne usiku hadi saa Saba usiku.Dk.Slaa amezungumza mambo mengi mazito yanayohusu Chadema ilivyokuwa awali na Chadema ya sasa ambayo ameiita imepoteza mwelekeo kwasababu imeamua kufanya machafu yanayofanywa na Chadema ambayo Chadema hiyo hiyo walikuwa wakiyakemea sasa Chadema wameamua kuyafanya wazi wazi.
Tuachane na watu wengine waliotuhumiwa na Dk.Slaa Jana, mada yangu ya Leo itamjadili mtu mmoja tu aliyetuhumiwa pia na Dk.Slaa .Mtu huyo Si mwingine ni Askofu Gwajima ambaye Jana Dk.Slaa amempachika jina la Mshenga.Jina Hilo la Mshenga limenichekesha sana.
Tuhuma hizo za Dk.Slaa dhidi ya Askofu Gwajima minaziita hivi. ( Dk.Slaa kampiga ngumi za mbavu Askofu Gwajima.)
Kweli nimeamini kuwa sio wote waitao bwanabwana watauona ufalme mbinguni.
Ebu Mtumishi wa Mungu Josephat Gwajima ,kama kawaida yako jitokeze Jumapili hii ujibu tuhuma hizi maana madai aliyoyatoa Dk.Slaa jana dhidi yako ni kama ya yameishakuzika ukiwa hai.
Umechafuka sana na sio siri taratibu waumini wako wanaweza kuamua kuacha kukuamini tena na wakalihama Kanisa Lako na usije kumtafuta mchawi maana mchawi ni wewe unaeleta michanganyo katika hekalu la Bwana.
Na ushahidi wa moja kwa moja "Direct evidence" na ushahidi wa mazingira "Circumstantial evidence" unaonyesha unafanya michanganyo ya mambo ya kidunia na Mungu.
Na Mungu hapendi michanganyo na watu wanaofanya matendo yasiyompendeza kwa kutumia mwamvuli wa jina lake lazima atakuumbua tu.
Lakini ni kwanini Askofu Gwajima mtumishi wa Mungu umeshindwa kusimama na kofia moja ya utumishi wa Mungu ukaamua kujiingiza kwa siri katika siasa za makundi ya kumpigani Edward Lowassa alipokuwa CCM na kwenye mkutano wa Lowassa kutangaza nia ha kugombea urais ndani ya CCM ulikwenda kushiriki katika mkutano ule mkoani Arusha kwa kigezo wewe ni mtumishi wa Mungu unaongoza misa ya mkutano ule na kweli uliongoza sala na kuishia kurusha vijembe kwa wasiomtaka Lowassa kwamba wakalambe malimao.
Wakati ukimuunga mkono Lowassa alipokuwa bado CCM pia ulikuwa ukimuunga mkono Chadema na UKAWA kwa ujumla wake huo ukawa unaiunga mkono Chadema na Mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za UKAWA katika viwanja vya Jangwani Agosti 29 mwaka huu,kupitia sala zako ukaonyesha wazi wewe upo upande Lowassa,Chadema na UKAWA kwa ujumla .
Sio kosa kisheria lakini turudi kwenye maadili ya viongozi wa kidini mnaongoza makanisa mnaruhusiwa kweli kuonyesha mnamuunga mkono mgombe yupi NA wachama gani tena hadharani?
Kiongozi wangu wa kanisa la Elshadai la Boko Basiaya Dar es Salaam,Kanali Mstaafu wa JWTZ, Bruno Kinunda anakata viongozi wa makanisa kujionyesha wanaunga mkono mgombea wa chama gani .
Kwani kiongozi wa kidini akifanya hivyo lazima atakuwa anawagawa waumini wake kwani sio waumini wote wanaofika makanisani wanayoyaongoza watakuwa wakimuunga mkono mgombea wa chama anayeungwa mkono na kiongozi wa kanisa aliyeamua kufanya kitendo hicho kisichompendeza Mungu .
Gwajima uliyataka mwenyewe yakufanya michanganyo ya siasa na dini.
Ukawekwa kwapani na wanasiasa akiwemo huyo Dk.Slaa ambae nae alipokuwa Katibu Mkuu Chadema wakashiriki kukutumia na kukugeuza Vuvuzela lao ,wanakufahamu vizuri sana na sasa hivi Slaa ambae alikuja kukutazama hospital ulipolazwa hospitali ya TMJ ametofautiani na wanasiasa wenzake jana kaamua kumwaga yote uliyoshiriki kufanya kwa siri na mwisho wa siku anayeathirika ni Gwajima kwa tuhuma hizi na zile za awali maana usipokaa mbali na wanasiasa waumini wasiopenda kusikia kila siku tuhuma zikielekezwa kwako watalihama kanisa lako.
Gwajima jitokeze utoe ufafanuzi wa tuhuma zilizotolewa na Dk.Slaa jana dhidi yako kuwa wewe ni mshenga wa Lowassa na ulishiriki katika michezo michafu isiyompendeza Mungu ya kupokea fedha wewe na maaskofu wengine.
Ni hatari sana taifa kuwa na viongozi wa dini aina ya Gwajima ambao kila kukicha wanazongwa na tuhuma mbalimbali.
Na ninajiuliza ni kwanini ni askofu Gwajima kila siku na sio watumishi wengine wa Mungu watuhumiwe kila siku tuhuma chafu chafu na za ovyo ovyo Kama hizi?
Mke wa mfalme aitaji kutuhumiwa.Mtumishi wa Mungu hapendezi kila kukicha kuandamwa na tuhuma za ovyo ovyo kama unazoandamwa nazo wewe mara Umepora Mke wa mtu,unatukana watu,umeacha kumtumikia Mungu umejiingiza Kwenye siasa ,unaweza kufufua wafu wakati si kweli na tuhuma nyingine mbalimbali ?
Askofu Gwajima nakushauri sema na Mungu wako .Kaa chini ufunge na kusali ili Mungu akuonyeshe umemkosea wapi ndio maana kila kicha unapata mapigo ya kuelekezewa uchafu kibao,kufunguliwa kesi na tayari baadhi ya watu wameanza kuwa na mashaka nawewe na tunajiuliza Gwajima kweli anamtimikia Mungu?
Na ni nataka ujue wazi kuwa wanasiasa wao wakirushiwa tuhuma hata za uzushi wala hawaathiriki sana Kama utakavyoathirika wewe kiongozi wa dini .Hakuna kitu Kibaya Kama kiongozi wa kidini usiaminiwe na kutiliwa Mashaka na waumini wako au watu wasiyo Sali Katika Kanisa Lako.
Jiadhari na wanasiasa hasa wa nchi hii ,Wengi ni washenzi sana na minafikiri ukubwa fahamu awali ndiyo maana ukaamua kuingia kichwa kichwa na Kujenga mahusiano nayo na wakawa wanakutumia kwa Siri kukamilisha mambo Yao sasa walioshiriki kuutumia akiwemo huyo Dk.Slaa kupitia Chadema amekuvua nguo na bado watakuanika ndiyo utapata akili.
Tunaowafahamu wanasiasa wa nchi hii tunakwenda nao kwa akili sana hatukubaki kuingia 'kwa miguu yote miwili' katika mission zao.Unaingia na mguu lakini wewe Gwajima uliingia mzima mzima tena kwa miguu yote miwili.
Mwisho tunaomba uongozi wa makanisa ambao Dk.Slaa ambaye awali alikuwa ni Padri wa Kanisa Katoriki wamtafute Dk.Slaa awapatie Majina ya hao maaskofu na mapridi walioshiriki kufanya ushetani huo uliolezwa NA Dk,Laa mtoe tamko Kwani tamko la Dk.Slaa Jana limeibua hisia tofauti baadhi ya watu wasiyopenda kwenda makanisani kumuomba Mungu wamesema ndiyo maana hawapendi makanisani kwasababu viongozi wa dini baadhi Yao ni wachafu na pia ni hatari Kuwa na viongozi wa kidini wanaojiusisha na tuhuma za Rushwa .
Na hapa ndipo ninapokubalina na Rais Jakaya Kikwete ambaye aliwai Kusema Kuwa kuna baadhi ya viongozi wa dini wanajihusisha na Biashara ya dawa kulevya.
Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
2/9/2015.
No comments:
Post a Comment