UKAWA SASA NI ZAMU YENU KULIA
Na Happiness Katabazi
KWA Takribani Miezi miwili sasa vyama vinavyounda UKAWA vimekuwa vikipata dhoruba Kali kutoka kwa baadhi ya waliokuwa Viongozi wa juu wa UKAWA kuamua kuachia madaraka vyama vyao Vya siasa walivyokuwa wakivitumikia sambamba na wanachama wao.
Tumewashuhudia waliokuwa Majemedali wa UKAWA ambaye aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba kuamua ukajiudhuru wadhifa wake huo ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Waziri Mkuu aliyejidhuru Edward Lowassa kujiunga na Chadema na siku tatu baadae kutangazwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na hivyo Kuwa mgombea urais kupitia UKAWA unaunganisha vyama vinne Vya siasa ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD.
Septemba Mosi Mwaka huu, aliyekuwa Jemedari wa UKAWA na Chadema, Dk.Wilbroad Slaa alijitokeza hadharani mbele ya waandishi wa Habari uliofanyika Katika Hoteli ya Serena Dar Es Salaam na kuibua tuhuma nyingi kwa viongozi wa Chadema,UKAWA na kukanusha tamko la Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe ambalo alitamkia umma Kuwa Chama kimeamua kumpumzisha Dk.Slaa kwasababu alikuwa Haifiki Lowassa kujiunga na Chadema.
Dk.Slaa yeye alisema anakanusha taarifa Kuwa alikuwa likizo,Bali yeye aliandika barua ya kustaafu siasa Julai 27 Mwaka huu.Hivyo Si kweli Kuwa alikuwa likizo Kama ilivyokuwa ikidaiwa na baadhi ya watu na Mbowe ambaye alidai Dk.Slaa amepumzishwa na Chama.
Pia tulishuhudia aliyekuwa Mwanachama mkereketwa wa muda mrefu wa CUF, Juma Duni Haji Akiama CUF na kuamia Chadema na siku hiyo hiyo akamtangazwa Kuwa mgombea mwenza wa Chadema na mgombea urais akatangazwa Kuwa ni Edward Lowassa ambaye alijiunga na Chadema ndani ya siku Tatu na ndani ya siku hiyo akapewa Kadi ya uanachama na jina lake kupitishwa Kuwa mgombea urais. Kioja cha aina yake.
Pia tulishuhudia baadhi ya waliokuwa wabunge wa Chadema ,Said Khalif, Chiku Abwao na baadhi ya wananchi wengine wakiama Chadema kwenda ACT na Magale Shibuda ambaye alikuwa Chadema amekihama Chama hicho kwa Kusema Kuwa amechoshwa na siasa za Amira zinazoendeshwa na Chadema licha Shibuda ajasema amejiunga na Chama gani.
Na Baadhi ya walioshindwa Katika kura za maoni za Ubunge CCM wakiamia Chadema na siku Chache baadae wakaamua kuhama Chadema na kurudi CCM akiwemo Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sikonge( CCM), Said Mkumba.
Ester Bulaya ambaye alikuwa mbunge Viti Maalum CCM aliamua kuondoka CCM kwa mbwembwe Kabla ya kura za maoni ndani ya CCM kupigwa na kuamia Chadema na hivi sasa ni mgombea Ubunge Jimbo la Bunda na wachambuzi wa mambo wanatabiri Bulaya hawezi kumshinda mgombea Ubunge wa CCM wa jimbo Hilo Steven Wassira.
Na tangu Dk.Slaa ,Septemba Mosi azungumze na waandishi wa Habari Mara mbili wiki iliyopita na kueleza mambo mambo mbalimbali yaliyosababisha afikie uamuzi wa kustaafu Siasa ndani ya Chadema tena wakati wa kipindi hiki kigumu cha kampeni za Uchaguzi Mkuu Unaotarajia kufanyika Oktoba 25 Mwaka huu.
Ni wazi maelezo yaliyotolewa na Dk.Slaa kwa siku tatu tofauti na Telebisheni tatu tofauti yaani mara ya kwanza Dk.Slaa alizungumza na umma Septemba Mosi, mara pili Dk.Slaa alifanya mahojiano maalum na Televisheni ya Star TV Septemba 4 na Septemba 6 katika Azam TV.
Kishindo cha Dk.Slaa tumekiona na tunazidi kukiona Kwani baada ya kutoa hotuba yake tumeshuhudia baadhi ya wanachama waliojitambulisha ni Chadema Katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Tabora,Dar Es Salaam, wakifanya maandamano ya kuunga mkono hotuba ya Dk.Slaa na wengine wakichana na kuchoma Moto Kadi na Kudai Kuwa wa akihama Chama hicho wanajiunga na CCM na ACT.
Hotuba ile ya Dk.Slaa pia umesababisha baadhi ya watu waliokuwa wakiunga mkono UKAWA na Chadema kukata tamaa ,na hata wale waliokuwa wakereketwa wa Chadema na UKAWA kwa ujumla huku mitaani wamepooza sana yale makeke na zile tambo zao na matumaini ya Lowassa na UKAWA kwenda Ikulu zimeyeyuka kabisa.
Binafsi napenda kujadili na kufuatilia mambo ya siasa sana hapa nchini na Mara nyingi napenda kuzungumza na watu wa vyama vyote na wasiyo navyama kuhusu Mitazamo Yao ya masuala ya kisiasa tena uwa napenda kukaa Katika vijiwe ,mikusanyiko ya watu na kujadiliana masuala hayo ya siasa kwa njia ya simu na mitandao ya kijamii.
Nimejiridhisha Kuwa wale Watani zangu waliokuwa wakiunga mkono UKAWA kwa Nguvu zote wamepoaaa baada ya Dk.Slaa kutoa hotuba yake.
Nimekuwa nikiwahoji kwanini wamenyong'onyea ghafla hivyo baada ya Dk.Slaa kurusha makombora kwa Chadema?.wanaishia Kunijibu HIvi: "Dk.Slaa amenukuliwa na CCM ili aje kutuaribia UKAWA yetu.Na kweli hotuba yake imesababisha kutuvunja moyo kabisa.
Wana UKAWA wengine Watani zangu wanasema kwanini Slaa asingesama hayo mapema ?Kwanini kayasema sasa wakati Kampeni zimeanza?ana Hasira za kukosa kupitishwa Kuwa mgombea urais.
Lakini wote hao hawataki kuzungumzia hoja zilizotolewa na Dk.Slaa ni za kweli au uongo.Wao wanaishia Kusema Slaa anatumika na CCM.Dk.Harrsion Mwakyemba alikutana naye kwa Sababu gani? Wewe CCM Ndio maana una muunga mkono Dk.Slaa.
Na hata Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia alidai anamjibu Slaa ameshindwa Kupangua hoja za Slaa alizozitoa Septemba Mosi Mwaka huu, na Ndio maana Septemba 4 Mwaka huu, Dk.Slaa alisisitiza Kuwa hoja zake bado hazijajibiwa na kumrushia Kijembe Mbatia Kuwa " pilipili asiyoila inamuwashia nini?. Kwasababu Dk.Slaa akumtaja Mbatia.
Itakumbukwa Kuwa kwa Miaka Kadhaa Katika Kipindi hii cha Serikali ya awamu ya nne inyoongozwa na Rais Jakaya Kikwete imekuwa ikaishambuliwa na wapinzani, wana CCM wenyewe na wananchi wa kawaida ni serikali na Chama cha mafisadi na kweli baadhi ya viongozi wa Chadema walikuwa wakimasisha wafuasi wao wawaite na wa wazomee wafuasi wa CCM Katika mikutano Yao na misafara Yao ,mitandao ya kijamii,kwenye vyombo vya habari kwa kuwaita ni Mafisadi .
Kweli agizo la baadhi ya viongozi wa Chadema lilitekelezwa kikamilifu na wafuasi Wengi wa Chadema na wananchi wengine kwa kuamini CCM ni Chama Cha Mafisadi Hali iliyosababisha baadhi ya wananchi kuondoa Imani kwa CCM na CCM kuchokwa na baadhi ya watu.
Pia ndani ya CCM Kukazuka Makundi yanayohasimiana vibaya Hali ambayo ilisababisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kukemea Hali hiyo ambayo ilisababisha wana CCM wakutoaminiana hata kumwachia Mwanachama mwenzio glasi ya Maji anaogopa .
Si hayo tu wakati CCM ikiwa Katika vuguvugu la kumpata mgombea urais wao ,wabunge na udiwani mwaka huu napo kulikuwa na mtifuano miongoni mwa wana CCM.
Lakini baada CCM kupitisha Majina ya wagombea wake wa urais,ubunge,udiwani uhasama wa kisiasa ndani ya CCM baina ya wana CCM kwa wana CCM umekwisha,wamekuwa wakitu Kimoja wameamua kuwaunga wagombea wote wa lipitishwa na CCM ilikuisaidia CCM ishinde kwa kishindo Oktoba 25 Mwaka huu.
Leo hii Katika Kipindi hiki cha kampeni hatujasikia Mwana CCM yoyote akijitokeza hadharani kumrushia makombora Mwana CCM mwenzake ,tunachokiona hivi sasa wana CCM kuanzia ngazi ya Taifa wamekuwa kitu Kimoja wanashirikiana kumuangamiza adui wao wa kisiasa UKAWA majukwaani,Kwenye mitandao na vyombo Vya Habari .
Na wakati CCM Ilipitia Kipindi hicho kigumu vyama Vya upinzani vilikuwa vikifurahishwa na mtifuano huo uliokuwa ukiikumba CCM ,serikali ikiwemo Chadema ,CUF vilikuwa vikishangilia sana na Kusema CCM na serikali yake hatakiwi na wanachi wanamchukia na imemeguka vipande vipande haifai kuendelea kuwepo madarakani.
Lakini mabalaa hayo yaliyokuwa yakiiandama CCM sasa hivi yameikumba Chadema,CUF.
Kwasababu baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wanahama vyama na kutoa tuhuma mbaya dhidi ya vyama walivyovihama, baadhi ya wanachama hasa waliojitambulisha Kuwa wanachama wa Chadema wiki hii Tumewashuhudia wakifanya maandamano Katika Mikoa mbalimbali wakiunga mkono hotuba ya Dk.Slaa na wanatangaza kuhama Chadema kwa kile walichokieleza Mbowe amemkaribisha mtuhumiwa wa ufisadi(Lowassa) ,hivyo anakiua Chama.
Pia tumeshuhudia baadhi ya wana UKAWA wakishindwa kukubaliana makubaliano waliyoyaingia baina ya vyama hivyo vinne ambapo Moja ya makubaliano Yao ni mgawanyo wa majimbo na kwamba mgombea wa Chama Fulani mfano wa Chadema akipitishwa Kugombea Jimbo la Ubungo ,basi mgombea wa CUF,NLD,NCCR haruhusiwi Kugombea nafasi hiyo.
Lakini tumeshuhudia huko Masasi Katika mkutano wa mgombea Mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji mkutano ulivunjika baada ya Kuzuka kwa tafrani ya wananchi wa Masasi kupinga mgombea Ubunge (NLD), Emmanuel Makaidi kunadiwa Kuwa ndiye mgombea Ubunge wa jimbo Hilo ambapo wananchi wa eneo walitaka asiendelee kuomba kura jukwaani na kwamba mgombea wanaotaka wao ni mgombea Ubunge wa CUF.
Hali hiyo pia imejitokeza Katika jimbo la Segerea ambapo UKAWA imepitisha mgombea Ubunge ,Julias Mtatiro lakini mgombea Ubunge aliyepitishwa na Chadema naye anaendelea na harakati zake za kulitwaa jimbo Hilo Hali inayosababisha Mtatiro Kulalamika kupitia mitandao ya kijamii Kuwa mwanamama huyo wa Chadema , Ana vurugu na haheshimu makubaliano ya UKAWA.
Vivyo hivyo jimbo la Ubungo, UKAWA imepitisha mgombea Ubunge wa Chadema, Saed Kubenea lakini wiki iliyopita tulivyoamka asubuhi Kwenye Nguzo za umeme zilizokuwa zimebandikwa picha za Kubenea ,juu yake zimeandikwa picha za mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CUF ,Mashaka Ngole Vichekesho.
Pia Inaelezwa zaidi ya majimbo 20 likiwemo jimbo la Nkenge Mkoani Kagera pia kuna mvutano kwasababu vyama vinavyounda UKAWA vimeshindwa kuheshimu makubaliano ya kuachiana majimbo.
Uongozi wa UKAWA ulipitisha Majina ya wagombea lakini baadhi ya wagombea toka vyama vingine nao ambao Majina Yao haya kupishwa na uongozi wa UKAWA wamegoma kuwaachia majimbo wagombea waliopitishwa na uongozi wa UKAWA.
Kitendo hicho ni cha kihuni na I imethibitisha ndani ya UKAWA kuna wahuni ambao hawaheshimu maagizo ya wakuu wao wa UKAWA na pia viongozi wa UKAWA nao ni wa dhahifu na hawafai kupewa nchi kuongoza kwasababu haiwezekani uongozi wa juu wa UKAWA uingie makubaliano ya kuachiana majimbo Kisha atokee mtu Kwenye hicho Chama ayakiuke na asichukuliwe hatua.
Na madhara ya kushindwa kuheshimu makubaliano hayo ya kugawana majimbo kwa UKAWA, ni UKAWA watapoteza majimbo mengi sana na hivyo kuipa CCM nafasi ya Kuwanyakua majimbo mengi kirahisi.
Lengo la UKAWA la kugawana majimbo ni kutaka Yule mgombea toka Chama Kimoja kilichomo Kwenye UKAWA jina lake likipitishwa mfano mgombea Ubunge kwa tiketi ya CUF jina lake likipitishwa na UKAWA Kugombea Ubunge basi vyama vingine Kama NCCR Mageuzi,Chadema,NLD vishirikiane naye Katika kampeni ili ashinde na akishinda UKAWA ndio Inakuwa imeshinda.
Sasa Hilo limeshindikana mapema kabisa,UKAWA hivi sasa wamekuwa Kama Mbuzi aliyekata Kamba anaenda njia anayejijua Mwenyewe,ule umoja wa kweli Katika ngazi ya Ubunge kwa baadhi ya majimbo hakuna na wanamfuatilia siasa za nchi hii ha watabisha.
Ndio maana siku zote nasema bado sijaona Chama CHA upinzani hapa nchini ambacho kipo Siriasi kuiondoa serikali ya CCM madaraka maana vyama vyama Vya upinzani licha wakati mwingine vimekuwa vikifanyakazi nzuri ,vimekuwa vikifanya mzaa na vimejaa wahuni wengi .
Aidha lile balaa la zomeazomea lilokuwa likiwakumba vi kiongozi wa CCM sasa hivi limeamia kwa viongozi wa Chadema Kwani tumeshuhudia Mgombea Mwenza wa Chadema,Katika ziara yake ya Kampeni Katika Mikoa ya Kusini akizomewa na wananchi.
Naye mgombea Ubunge NCCR Mageuzi Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila naye mwishoni mwa wiki wakati akinadiwa na Lowassa alizomewa.
Na baadhi ya wananchi wamekuwa wakiwashambulia viongozi wa Chadema na UKAWA Kuwa UKAWA na Chadema imepoteza mwelekeo kitendo ambacho hapo nyuma kilikuwa akuna kwani baadhi ya wananchi walikuwa waliaminishwa Chadema ni Chama cha Ukombozi na kina viongozi malaika ambao ni watu safi hawana dosari wala Kutenda makosa jambo ambalo kweli.
Hivi karibuni tumeshuhudia Katika mitandao ya kijamii idadi ya wakosoaji wa Chadema na UKAWA ikiongezeka ukilinganisha na Kipindi cha nyuma kwani watu waliokuwa wakuonyesha ni wafuasi wa Chadema Kutwa nzima walikuwa wameiteka mitandao hiyo na shughuli Yao kubwa kuipaka matope CCM,serikali na viongozi wake na walifanikiwa kwa kiasi Fulani ila kwasababu kasi ya wafuasi hao wa Chadema Mtandao ambao baadhi Yao walikuwa wakitumia hata lugha za matusi dhidi ya wale waliokuwa wakosoaji wa Chadema umepungua sana sana.
Maana wale nao waliochoshwa na uzushi huo wafuasi Hao wa Chadema nao wameamua kutumia mitandao hiyo hiyo Kujibu mapigo kwa lugha za kistaarabu.
Yale yaliyokuwa yakipingwa na Chadema Kuwa CCM Imechoka ,imelegea na watu hawataki ndiyo maana itumia wasanii wengi ,inatumia mabasi na maroli Kubeba watu kuwaletea uwanjani , nao mchezo huo hivi sasa Chadema unaoufanya vizuri sana nayo inaleta wananchi Kwenye mikutano yake kwa maroli na inaleta wasanii pia Katika mikutano Yao ya kampeni.
Unafki wa aina hiyo nayo ni Sababu pia ya watu wanaofikiri sawa kuiona Chadema nao sio watu wanaoamika na ni wanafki maana CCM ikifanya hayo Chadema inakosoa ila Chadema Mbona inafanya hayo hayo?
Kwa mabalaa hayo yanayoikumbuka Chadema na vyama vinavyounda UKAWA ni sawa na Kusema hivi ; Mwiba uliokuchoma unaweza kuung'oa ukautupa kisha ukaenda kumchoma mtu mwingine.
Lowassa alipokuwa Mwana CCM alikuwa ni Kama Mwiba unaoichoma CCM kwasababu alikuwa akiandamwa mno na tuhuma za ufisadi CCM ikashindwa 'kukimbia' ikawa Ina Chechemea ,wakaamua kuing'oa Mwiba huo yaani kwa CCM kukataa kupitisha jina Lowassa Kuwa mgombea urais Julai Mwaka huu ,wa kaugua Mwiba ule.
Chadema wakaukanyaga Mwiba ule uliong'olewa Katika mguu wa CCM na kuutupa.Yaani kwa maana Chadema wamemchukua Lowassa hivyo Mwiba huo umewachoma hivi sasa Chadema nayo niachechemea ,haiwezi kufika safari ya Riadha wanayoikimbia kwenda Ikulu.
CCM itakapofika mwisho wa safari yake Oktoba 25 Mwaka huu na kufanikiwa kukamata dola ,Chadema waiombe CCM iwaondolee Mwiba huo ili wakapumzike salama.
Chadema ya Miaka ya nyuma na uchaguzi Mkuu wa 2010 sio Chama ya sasa ambayo ni wazi imenyesha kudhoofu Kwani zile Shangwe na vibweka vilivyokuwa vinafanywa na baadhi ya makada wake Kama aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, Dk.Slaa,John Nyika na Timu Yao hatuvioni kabisa Katika kampeni za Mwaka huu.
Na kuhusu CUF Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu, aitambi tena Kama Miaka ya nyumba ipo kimya CUF hapa Tanzania Bara.Hali inayosababisha kupoteza mvuto kwa vyama hivyo ambavyo ninawafuasi wengi.
Pia Chadema imeanza kupoteza mfuko kwasababu mgombea urais waliomsimamisha Lowass anaandamwa na tuhuma za ufisadi hivyo Chadema imekuwa kukichukua muda Mwingi Kujibu wala wanaomuita mgombea urais wao Lowassa ni fisadi badala ya kunadi sera ili wananchi wawasikilize.
Itakumbukwa Chadema Ndio ilikuwa mstari wa Mbele kumuita Lowassa ni fisadi wakati Lowassa akiwa CCM .Lakini ajabu ni kwamba Chadema hii iliyokuwa iki rushiwa mawe Lowassa Ndio Mbowe na genge lake wamekamribisha Lowassa Chadema licha sio kosa .Wanasiasa jamani Mungu a wasamehe bure.
Aidha jambo jingine linaloendelea mvuto mgombea urais wa UKAWA, ni Mwenendo wa mgombea urais Lowassa kuchukua si chini ya dakika Kumi kuwahutubia wananchi ukilinganisha na wagombea wenzake wa urais Kama John Magufuli ambaye anasimama muda mrefu jukwaani na kueleza mipango yake atakapofanikiwa Kuwa rais wa Tanzania.
Katika mikutano ya kampeni za Lowassa,tumeshuhudia Lowassa Anachukua muda kidogo kuhutubia utafikiri anaenda kuweka Kibwagizo lakini watangulizi wake Ndio wanachukua muda mrefu Kabla ya yeye Kupanda jukwaani kuzungumza kwa kutumia muda mrefu.
Baadhi ya watu huko mitaani ninaozungumza nao wanasema wanakerwa na hiyo Hali Kwani inafanya washindwe kufahamu mengine yaliyofangwa kutekeleza na Lowassa akiwa Rais.
Niitimishe kwa Kusema Kuwa Chadema na UKAWA yenu sasa ni zamu yenu kulia,CCM sasa inacheka.Na ule Mwiba uliokuwa umeichoma CCM ikawa Ina Chechemea kwa zaidi ya Miaka Saba waliung'oa wakautupa sasa umeichoma Chadema na Ukawa hivyo sasa Chadema na Ukawa mnachechemea.
Kwa sababu waswahili wanamsemo wao usemao yaliyomkuta Mamba na Boko pia yatamkuta kwasababu wote wanaishi kwenye maji .UKAWA sasa ni zamu yenu kulia.
Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook.Happy Katabazi
0716 774494
7/9/2015.
No comments:
Post a Comment