TLS KWA NINI LAWRENCE MASHA PEKE YAKE?
Na Happiness Katabazi
AGOSTI 27 Mwaka huu,Chama Cha Wanasheria nchini (TLS), kilitoa taarifa yake kwa vyombo Vya Habari kuhusu Kukamatwa na kuwekwa Katika Gereza la Segerea kwa Mwanasheria Mwenzao Lawrence Masha ambaye ni Mwanachama mpya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anayekabiliwa na Kesi ya kutoa lugha chafu Na.130/2015 kwa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Juma Mashaka na wenzake.
Agosti 25 mwaka huu, Mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema, Wakili wa serikali Mutalemwa Kishenyi alidai Kuwa Kesi hiyo mshitakiwa ametenda kosa Hilo la kutoa lugha chafu kinyume cha Kifungu cha 89(1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.
Wakili Kishenyi alidai Kuwa Agosti 24 Mwaka huu, ndani ya Kituo Cha Polisi Oysterbay Jijini Dar Es Salaam, Masha alitumia lugha chafu dhidi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Juma Mashaka na maofisa wenzake wa Polisi kwa Kuonyesha Kuwa Juma na maofisa wenzake wa Polisi Kuwa ni ' washenzi na waonevu hawana shukrani,huruma wala dini maneno ambayo yalikuwa yanataka kuatarisha Amani na kwamba upelelezi wa shauri bado haujakamilika.
Hata hivyo Masha alikanusha kosa hilo na Hakimu Lema alisema ili mshitakiwa Huyo apate dhamana ni lazima awe na wadhamini Wawili watakao saini bondi ya sh.milioni Moja na barua za utambulisho.
Baada ya Hakimu Huyo kutoa Masharti hayo upande wa jamhuri uliomba muda ukafanye Uhakiki wa barua za wadhamini na muda mahakama wa kufanyakazi saa 9.30 alasiri ulikuwa umemalizika hivyo Hakimu Lema akaairisha Kesi hiyo hadi Septemba 8 Mwaka huu,kwaajili ya kutajwa na akaamuru mshitakiwa apelekwe gerezani kwasababu Masharti ya dhamana bado hayajatimizwa.
Kwanza ieleweke wazi Kuwa dhamana ni mkataba baina ya Mahakama na mshitakiwa.
Mshitakiwa anapotimiza Masharti ya dhamana aliyopewa na Mahakama ndiyo Mahakama umpatia dhamana na mshitakiwa Huyo akishindwa kutimiza Masharti hayo ya dhamana Mahakama haitampatia dhamana.
Barua za wadhamini hizo ufanyiwa uhakiki na Jeshi la Polisi na kisha polisi wanarejesha taarifa za matokeo ya uhakiki huo kwa waendesha mashitaka (Upande wa Jamhuri) .
Na hili zoezi la Uhakiki lilianza kutiliwa Mkazo muda mfupi tu tangu aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashitaka Dk.Eliezer Feleshi alipoteuliwa Kuwa DPP Miaka sana iliyopita.
Kwani Dk.Feleshi ambaye kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu natimu yake wakitilia Mkazo jambo hili la kutaka kila barua za wadhamini zifanyiwe Uhakiki ili wajiridhishe hizo barua ni halisi au feki maana Mimi Binfasi nimekuwa Mwandishi wa Habari za Mahakamani kwa Miaka 16 nimekuwa nikishuhudia baadhi ya wadhamini feki wakiteta mahakamani baa feki ili kuwadhamini washitakiwa na Matokeo yake washitakiwa walipokuwa wakifahaminiwa NA barua hizo feki walikuwa wakikoroka .
Na wakati polisi wanaenda kufanya uhakiki wa barua za wadhamini wa Mshitakiwa Lawrence Masha muda wa Mahakama kufanyakazi ulikuwa umeishamalizika hivyo Hakimu Lema akahairisha Kesi hiyo hadi Septemba 8 Mwaka huu,kwaajili ya kutajwa na akaamuru mshitakiwa apelekwe gerezani kwasababu Masharti ya dhamana bado hayajatimizwa.
Agosti 26 Mwaka huu, Masha alitolewa gerezani na kuletwa Katika Mahakama ya Kisutu kwaajili ya kutimiza mashartia ya dhamana .Kweli alitimiza masharti ya dhamana na Mahakama ikamuachia kwa dhamana.
Itakumbukwa Kuwa Masha aliwahi Kuwa mbunge wa Jimbo la Nyamagana kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na akateuliwa kushika nafasi ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini na kisha kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani lakini hata hivyo Rais Jakaya Kikwete alipofanya Mabadiliko ya Baraza lake la mawaziri alimtupa nje ya Baraza lake la Mawaziri.
Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 ,Masha akigombea Ubunge wa Jimbo la Nyamagana lakini alishindwa na alishindwa .
Agosti Mwaka huu, CCM iliendesha Mchakato wa kura za maoni ndani ya chama kwa ngazi ya Ubunge na udiwani na Masha alikwenda Kugombea Ubunge Katika jimbo la Sengerema akashindwa vibaya na hatimaye William Ngeleja (CCM) aliibuka mshindi na siku Chache baada ya kushindwa Ubunge Jimbo la Sengerema ,Masha alitangaza rasmi kuiama CCM na kujiunga na Chadema.
Turejee Kwenye mada yangu ya Msingi ya Leo ambayo itazungumzia tamko Hilo la TLS Katika aya yake ya mwisho ya tamko lake ambayo inasomeka hivi;
(What TLS disapproves and will challenge is the lawfulness and prudence of the court abdicating its role and allowing the prosecution to deny Mr. Masha the right to enjoy his right to bail).
TLS wanasema Kuwa wamekerwa na kitendo cha Mahakama kuruhusu upande wa Waendesha Mashitaka kuvunja haki ya Mshitakiwa Masha kupata dhamana.
Haki ya Mtu Kuwa huru Imetolewa katia Ibara ya 15 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977,
Lakini Ibara ya 15(2) ya Katiba ya nchi inasema hivi ;
" (2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu-
(a) katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, au
(b) katika kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na mahakama kutokana na shauri au na mtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai".
Kila Kesi Ina mazingira yake na kwa mujibu wa mazingira ya Kesi ya dhamana ya Kesi ya Masha siku ile ya kwanza alipofikishwa mahakamani, Upande wa Jamhuri haukupinga dhamana ,upande wa jamhuri Mbele ya Hakimu Lema uliomba upewe muda wa kwenda kuhakiki barua za wadhamini wa Masha .
Na Hakimu Lema alikubaliana na ombi hilo la upande wa Jamhuri la kwenda kuhakiki barua hizo za wadhamini (verification) ili wajiridhishe Kama hizo barua ni sahihi au laa.
Na muda wa Mahakama ulikuwa umeishamalizika hivyo upande wa jamhuri ulioshindwa kuhakiki muda huo Kabla ya muda wa Mahakama kumalizika na hivyo kusababisha Mahakama kuamuru Masha aende gerezani hadi siku upande wa jamhuri utakapokuwa umekamilisha zoezi kuhakiki barua hizo na Kesho yake Masha aliyetaja Mahakamani hapo akapewa dhamana kwasababu tayari upande wa Mashitaka ulikuwa umekamilisha zoezi la kuhakiki barua za wadhamini wa Mshitakiwa Masha.
Kwa Sababu hiyo napinga hoja ya Chama Cha Wanasheria nchini, inayosema eti Mahakama il iwaruhusu upande wa jamhuri kuvunja Haki ya Masha ya kupata dhamana kwasababu Ibara ya 15(2) ya Katiba ya nchi Inajieleza wazi kabisa Kuwa;
" (2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu-
(a) katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, au
(b) katika kutekeleza hukumu, amri au adhabu iliyotolewa na mahakama kutokana na shauri au na mtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai".
Sasa Mahakama iliamuru Masha apelekwe gerezani siku hiyo kwa mujibu wa Ibara hiyo ya 15(2)(a) ya Kataba ya Nchi .
Na Ieleweke kwamba Katika rekodi ya Mahakama kwa mujibu wa Kesi hiyo Na.130/2015 Jamhuri dhidi ya Lawrence Masha, akuna rekodi inayoonyesha Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), amewasilisha hati ya Kumfungia dhamana Masha .
DPP ,Biswalo Mganga anayo mamlaka hayo ya Kufunga dhamana kwa mshitakiwa yoyote Yule anayekabiliwa na Kesi ambayo ambayo inadhamana kwa mujibu wa Kifungu cha 148(4 ) ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002.
Lakini DPP ,Mganga ajazuia dhamana ya Masha na angependa kufanya hivyo angefanya.
Mhimili wa Mahakama umeanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 107A ya Katiba ya nchi na ndiyo utakuwa na jukumu la kutoa haki. Lakini ibara 107B ya Katiba hiyo Unaizungumzia Uhuru wa Mahakama na inasomeka hivi;
" Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya Katiba na yale ya sheria za nchi.
Sasa Leo hii TLS inapoibuka na Kudai Kuwa Mahakama imeshindwa kutumia mamlaka yake kuwazuia waendesha Mashtika kuvunja Haki ya Masha ya Kuwa huru ,nashindwa kabisa kuielewa TLS Ina ajenda gani na Mshitakiwa Masha hadi kufikia kutoa tamko la aina hiyo ambalo kwakweli halina mantiki yoyote ,na lime acha maswali yasiyokuwa na majibu kwa baadhi ya Wanasheria wenzao,wapenda Haki na Usawa wa Sheria na kuipaka matope Mhimili wa Mahakama na Ofisi ya DPP Kuwa imepindisha Sheria na kupora Haki ya Masha ya Kuwa huru.
Tuiulize TLS kwahiyo TLS Ilitaka Mahakama itoe dhamana kwa mshitakiwa Masha bila Masha kutimiza masharti ya dhamana yaliyotolewa na mahakama?
TLS kwanini mnaishambulia Mahakama na upande wa Mashitaka Katika Kesi hii Moja tu ya Masha?
Mbona huruma hii ambayo mmeionyesha kwa Masha kwa kutaka Sheria ipindishwe ili Masha apewe dhamana Mbona TLS huruma hii ya Uvunjifu wa Sheria hamuionyeshi kwa washitakiwa wengine?
TLS onyesheni ushahidi unaonyesha Waendesha Mashitaka walivunja Haki ya Masha ya Kuwa huru na Mahakama ilishindwa Kuzuia Haki ya Masha ivunjwe na waendesha Mashitaka?
TLS lakini kwa nini iwe kwa Masha tu? Je ni kwa sababu Masha ni Wakili Mwandamizi ?TLS tuelezeni mna maslahi gani na Masha? Mbona wapo wapo Watanzania wengi wanateseka kwa masharti au technicalities za namna hiyo kila siku mahakamani na hamuwwatetei?
Mbona nyie TLS hatujawahi kuwasikia mkiibuka kwenye vyombo vya habari na kutoa tamko la kushutumu Mahakama na ofisi ya DPP kwa kuvunja haki ya kuwa huru za Watanzania hao Kama mlivyojitosa kumtetea Masha wiki iliyopita tena kwa hoja za uongo.
Mbona wakili wa kujitegemea Ademba Agomba, Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Wanawake Taifa (CHADEMA), ambao wanakesi hapo hapo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na walikosa dhamana kwa mazingira kama hayo hayo yaliyotokea kwa Masha, mbona TLS atukuwaona wala kuwasikia kutoa tamko?Maana na hao ni wanasheria wenzenu.
Mbona aliyekuwa waziri wa Fedha,Basil Mramba ,Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona nao walipelekwa gerezani kwa Sababu Kama hiyo ya waendesha Mashitaka katika Kesi ya Masha,Mbona hatukuwasikia TLS mkitoa tamko ?
TLS mnanini na Masha? Kwanini hayo malalamiko yenu hamkuyapeleka rasmi kwa Jaji Mkuu Othaman Chande au Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga ili way afanyiziwe Kazi na kuona kuna hira kweli zilifanywa na watendaji wao wa chini ya Hakimu Lema na waendesha Mashitaka wa Kesi hiyo ?
Hamuoni uamuzi wenu wa kupeleka lalamiko Lenu hiyo ambalo binafsi nasema halina kichwa wa miguu linaweza kuamsha hisia Mbaya baina ya TLS na mahakama na Ofisi ya DPP na washitakiwa wengine Mbali na Masha?
TLS mlichofanya ni 'double standard' , hasa kipindi hiki cha Nchi ipo kwenye kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu.
Umma unaweza kuwaona kuwa mna hisa na mtu fulani kwakuwa labda yuko upinzani au vyovyote vile. Kwa nini wajibu wenu huu Msiufanye siku nyingi na kwa wengine?
Labda sasa kama mnataka kutuambia kuwa ndio mmeanza, lakini kwa sisi wengine hii tunaiona ni nguvu ya soda tu au kuna sababu.
TLS kwa mujibu wa tamko Lenu hiyo mmetuhumu Mahakama wazi wazi Kuwa imeruhusu upande wa Mashitaka Katika Kesi hiyo ya Masha kuvunja Haki ya Uhuru ya Masha.
Sasa Kama mmesema hivyo basi ni wazi Kuwa Mahakama haipo huru kufanyakazi zake na kwamba upande wa Mashitaka ndiyo wenye Nguvu kupita Mhimili wa Mahakama Katika Kesi hiyo ya Masha, maana ni Nyie wenyewe mmesema Mahakama imewaruhusu upande wa jamhuri kuvunja Haki hiyo ya Masha.
Basi pia Mahakama nayo ilivunja mihiko na Katiba ambayo inaitaka Mahakama itoe Haki bila upendeleo wa aina yoyote lakini Mahakama ya Kisutu ikaamua kupora Haki ya Masha ya Kuwa huru .
Sasa Kama ni hivyo mnavyodai,mnafikiri Mahakama ya Kisutu itaweza Kutendea haki Mshitakiwa Masha Katika Kesi hiyo ambayo itakuja kutajwa tena mahakamani hapo Septemba 8 Mwaka huu?
TLS kwa tamko Lenu ambalo Kabla ya kulitoa hamkulifanyia utafiti wa kina na kubaini ukweli ni upi nawashauri aliyeandaa,kuruhusu tamko hili litoke arudi Katika darasa la Sheria akasome .
Maana somo la Legal Reseach ambalo ufundishwa vyuoni kwa wanafunzi wa kozi ya Sheria umtaka Mwanafunzi au msomi wa Sheria asizungumze jambo Kabla hajalifanyia utafiti sasa TLS Katika suala la dhamana ya Mahakama mmekutupuruka ,hamkufanya utafiti Matokeo yake mkatoa tamko la Kusema Haki ya Uhuru wa Masha ilipovunjwa kinyume na Sheria wakati Si kweli.
Chanzo: Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook. Happy Katabazi
0716 774494
1/9/2015.
No comments:
Post a Comment