NIMEPONA TATIZO LA MACHO BILA KUVAA MIWANI
NIMEPONA TATIZO LA MACHO BILA KUVAA MIWANI
Na Happiness Katabazi
MEI 16 Mwaka 2017 saa tano asubuhi nilikwenda Katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi ( JWTZ) Lugalo Dar es Salaam ,kwaajili ya kuonana na Daktari wa macho ili anipatie matibabu ya macho yangu ambayo yamenisumbua kwa Takribani Miaka Nane sasa maana nilishaanza kuona ukipofu unaninyemelea kabisa.
Nilipokelewa vizuri katika Hospitali hiyo na baadhi ya maofisa wa JWTZ ambao ni watumishi wa kikosi hicho cha JWTZ ambao ni rafiki zangu kisha nikafuata taratibu zote za kumuona daktari na ilipofika saa 8:11 Alasiri niliingia chumba cha daktari wa macho wa hospitali hiyo ambayo mimi nilizaliwa 25/12/1979 hapo ambaye anaitwa Dk.Seth Japhet .
Dk.Seth alinipokea vizuri nanilipojitambulisha kwakwe kwa Majina yangu yote mawili ( Happiness Katabazi) alinitazama akaanza kucheka sana akaniuliza wewe ni Yule Mwandishi wa habari Happiness Katabazi usiyemuandika Katika makala Mchungaji Antony Lusekelo Kuwa ulimkuta akiwa amelewa na anafanya Fujo ?Nikavuta pumzi ,Kisha nikamjibu ndiyo Mimi.
Dk.Seth alinitaka nianze kujieleza hayo macho yangu yanatatizo gani hadi nikafika hatua ya kujileta Mwenyewe Hospitali kwaajili ya kupata matibabu.
Huku nikicheka ,nikamweleza Kuwa kwa Miaka Saba sasa Macho yangu yamekuwa yakinisumbua sana wakati ninapokuwa eneo lenye Giza na eneo ambalo halina Mwanga wa kutosha wakati wa usiku ambapo eneo Hilo Hilo lenye Giza watu wengine wanatembea na kuona vizuri ila Kwangu Mimi Inakuwa ni tatizo siyoni vizuri.
Mfano usiku unapoingia eneo ambalo lina Giza au Mwanga hafifu macho yangu hayaoni vizuri na ifikapo usiku njiani kama kuna Giza natembea kwa tabu ,Mara kwa Mara najikwaa,napiga watu vikumbo,natembea kwa kunyatanyata maana Sioni Mbali naona Giza.
Nilimweleza Dk.Seth kutokana na tatizo Hilo nilishakwenda Katika Hospitali zenye vitengo vya macho Mara mbili kwa Nyakati tofauti nakufanyiwa vipimo na madaktari wote wa Wawili wa Hospitali hizo mbili tofauti ambazo (Majina yake nayaifadhi) kati ya Mwaka 2009 na 2014 waliniambia macho yangu ni mabovu sana hivyo wakanitaka ninunue miwani nivae haraka sana .
Dk.Seth akanihoji huku anacheka hiyo miwani iko wapi ?Nilimjibu miwani nilishaitupaga nalalani muda mrefu na nilimweleza kabisa niliinunua hiyo miwani ile kwa Sh.150,000 Mwaka 2014 lakini roho yangu ilisita na kunikataza nisivae miwani.
Kweli nikaamua kabisa licha macho yalikuwa yakinitesa eneo lenye Giza na mwanga wa hafifu nilisema kwa jina la Yesu sivai miwani na Mungu anitafutie njia nyingine ya Kuponya hili tatizo la macho ambalo lilinifikisha Hatua ya kuonekana Mimi ni kichekesho Katika eneo la Giza hata kama ni ndani jinsi ninavyotembea kwa kunyatanyata na kujiona siku za Kuwa kipofu zimekaribia .
Kweli Mei 16 Mwaka huu, Mungu alisikia kilio changu na kwa uweza wake nilijikuta naenda Hospitali ya Jeshi Lugalo na nikakutana na Dk.Seth ambaye kwanza kabisa naomba nimuombe msamaha Dk.Seth kwasababu wakati akinipima macho alikuwa akinipima Taratibu mno na alichukua zaidi ya saa 1:30 .
Kimoyo moyo Nikawa namlaumu Dk.Seth Kuwa mkono wake mzito, anafanya Kazi Taratibu Kwani Mimi nilikuwa nataka nikitoka hapo Hospitali niende Kazini kwangu Mikocheni Kisha jioni niende zangu GYM nikafanye mazoezi ya viungo kama kawaida yangu.
Baada ya kumaliza kumpatia historia ya tatizo langu la macho, alianza kunipima macho yangu Taratibu bila haraka kwakuniweka vifaa Kwenye macho huku akivibadilisha na akawa ananitaka nisome maandishi yaliyokuwa yametundikwa mbele ukutani .Nikafanya hivyo kama alivyonielekeza.
Alipomaliza kunipima hiyo awamu ya kwanza ,Dk.Seth akaingia awamu ya pili ya upimaji wa macho yangu ambapo hiyo awamu ya pili alininyunyizia dawa ya Matone ndani ya macho yangu na Alipomaliza akanitaka nikaa nje ya chumba anachopimia macho na nifumbe macho yangu nisifumbue hadi dakika 25 zipite ataniita tena Nirudi ndani ya hicho chumba aendelee kunifanyia vipimo Vya macho.Nilitii maelekezo yako.
Kweli Nilifanya hivyo huku nikiwa na baadhi ya Wanajeshi na manesi ambao ni marafiki zangu wakinicheka na kunitania Kuwa ndiyo Tayari nimeishakuwa kipofu.
Baada ya dakika 25 kumalizika Mwanajeshi mmoja alinishika mkono huku nimefumba macho hadi ndani ya chumba cha Dk.Seth nikaa Kwenye Kiti , Dk.Seth akanitaka nifumbue macho nikafumbua.
Tukaingia awamu ya Tatu ya matibabu ambayo Dk.Seth alichukua tena vifaa akaziwekea Kwenye macho yangu na kunitaka nisome maandishi yaliyokuwa yamebandikwa ukutani ni kayasoma vizuri.
Baada ya dakika 10 kupita Dk.Seth akaniondoa Katika hicho chumba akaniamishia Katika chumba kingine ambacho kilikuwa kimefungwa vifaa Vya kupima wagonjwa wa macho kilikuwa na Giza Kwani alikuwa amezima taa.
Tukaingia awamu ya nne ya Upimaji ndani ya chumba hicho ambacho alinivaisha vifaa Vya kupimia macho Kwenye macho yangu na kusogeza zile mashine za kupimia macho karibu kabisa na macho yangu ambazo zilikuwa Mbele yangu.
Alivyomaliza awamu hiyo ya nne ya matibabu, aliwasha taa ndani ya chumba hicho kukawa na Mwanga akanitaka Nije Kwenye viti vilivyokuwa Kwenye meza ya kuzungumzia mgonjwa na Daktari anieleze alichokibaini Katika macho yangu baada ya kufanya vipimo vyote hivyo.
Dk.Seth ambaye siyo mzungumzaji sana kama Mimi Kwani wakati wote Mimi ndiyo nilikuwa natawala mjadala kwasababu napenda kudadisi vitu hivyo nilikuwa namchimba anieleze mambo mbalimbali yahusianoyo na macho bila kujua.
Nilienda kukaa nae meza Moja Katika hicho chumba ambapo Anaongea kwa Taratibu akasema amebaini macho yangu bado hayajafikia Hatua ya kutakiwa nivae miwani na uchunguzi wake wa kitabibu umebaini tatizo langu la kushindwa kuona vizuri Gizani ,usiku ni kwasababu ninakabiliwa na upungufu mkubwa VITAMIN A mwilini na kwamba upungufu huo ndiyo umenisababishia matatizo hayo.
" Happiness,naheshimu taaluma yangu ya udaktari wa macho na jinai tendea haki kweli kweli.....sitakuandikia uvae miwani kwasababu uchunguzi wa vipimo haujanionyesha Unatakiwa uvae miwani kwasasa ,wewe una upungufu wa VITAMIN A mwilini hivyo nakuandikia vidonge vyenye vitamin na Madini mbalimbali ukameze jumla ni vidonge 90 " alisema Dk.Seth.
Dk.Seth ambaye alichukua zaidi ya dakika tano kutafakari kunichagulia vidonge vitakavyonifaa ambayo siyo tu vina ' Vitamin A 'peke yake ,akafungua makabrasha yake akasema ameamua kunichagulia dawa hii ambayo siyo dawa ni virutubisho inaitwa ONCE A DAY ( Vitamins and Food Supplements ) akasema Kwenye Bima ya Afya pia ipo .
Katika mazungumzo yetu nilimweleza Mimi uwa Nina desturi ya kumeza ( Food Supplement) yaani virutubisho vyenye baadhi ya vitamin ila hivyo virutubisho havina Vitamin A.
Akanipongeza Kwa Hilo akaniambia hiyo ya ONCE A DAY ambayo box moja lina jumla ya vidonge 30 aliyoniandikia ina mchanganyiko wa vitamin nyingi na Madini mbalimbali ambayo binadamu anatakiwa awe nayo mwilini na kwamba madini ,vitamini baadhi zikikosekana mwilini binadamu Huyo lazima atapatwa na tatizo la kiafya na ni wachache Wanaofahamu Hilo Kwani Wengi hawafahamu Umuhimu wa Food Supplement and Mineral .
Baada ya Kumaliza kuniandikia hivyo vidonge ,akaniambia ile dawa ya macho aliyoniwekea Machoni iliyokuwa kwa mtindo wa kimiminika Katika awamu ya pili ya matibabu kwa siku nne kuanzia siku hiyo aliyoniwekea Machoni sitaweza kusoma maandishi madogo Kwenye simu,kompyuta,hata karatasi ila nitaweza kutembea na kweli Hilo likatokea tangu Jumanne jioni ya (16/5/2017) nilipomaliza kupata matibabu nikaenda Duka la madawa la Nakiete lililopo Mwenge Dar es Salaam, nakuchukua hizo ONCE A DAY boxi tatu.
Siku ya Ijumaa ya 19/5/2017 macho yangu yakaanza kuona Mbali Na uwezo wa kuona hata Kwenye Mwanga ukaongezeka kupita siku zile ambazo nilikuwa sijapewa Tiba hiyo na Dk.Seth wa Hospitali ya Jeshi Lugalo.
Kwa kweli nilimshukuru Mungu kwakunikutanisha na Dk. Seth ambaye yeye alipingana na maamuzi ya madaktari wenzake wa Hospitali zingine ambao wao walivyonipima Miaka ya nyuma kwa tatizo Hilo Hilo la Mimi kushindwa kuona Gizani ambao wao walisema tatizo langu linanitaka nivae miwani uamuzi ambao hata Mimi nilipatwa Mara mbili lakini Dk.Seth akaja na uamuzi wake ambao ulisema macho yangu hayastahili kuvaliwa miwani Kwasabababu tatizo lilokuwa likinisumbua ni upungufu wa VITAMIN A mwili hivyo akanitaka nikale vyakula vinaongeza Vitamin A kwa Wingi mwilini ,pia nianze kumeza ONCE A DAY ili nipate Vitamin A kwa haraka na akanitaka kwa siku Moja nimeze vidonge vitatu yaani asubuhi,mchana na jioni.
Kweli nimemeza vidonge hivyo jumla 90 na tatizo Hilo limekwisha kabisa natembea kwa miguu siku hizi usiku,tena Umbali mrefu bila kupiga watu vikumbo, kuanguka,kujikwaa au kutumbukia Kwenye mashimo maana siyo Siri miguu yangu ina harama nyingi zilizotoka na na kujikwaruza usiku kwasababu ya Macho yangu yalikuwa hayana uwezo wa kuona mbalimbali Nyakati za usiku hasa sehemu yenye Mwanga Hafifu.
Baada ya kupata Tiba hiyo ya kumeza virutubisho hivyo (ONCE A DAY) ambayo imeniponya ,niliwaeleza watu wangu wa karibu Kuwa jamani Nilichojifunza kitu Kimoja Kuwa siyo kila mtu mwenye tatizo la macho anastahili kuandikiwa na Daktari avae miwani, wengine wanaupungufu wa vitamini na Madini mwilini lakini baadhi ya madaktari wasiyo na weledi au tamaa tu ya kutaka kuuza miwani wamekuwa wakiwaandikia wagonjwa wa macho wa kavae miwani wakati hawastahili kuvaa miwani wanau upungufu wa Vitamin A mwilini kama Mimi Happiness Katabazi ambaye madaktari Wawili wa Hospitali mbili tofauti walishawahi kunipima macho tena wala hawa kuchukua muda mrefu kunipima kwa umakini kama alivyonipima Dk.Seth wa Lugalo Hospital ambaye yeye alikataa kunipa miwani akasema sistahili kuvaa miwani bali anastahili kumeza vidonge Vya kuongeza Vitamin A ili viweze kujisaidia macho yangu kuona vizuri.
Mama yangu Mzazi yeye alipimwa akapewa miwani kwasababu hawezi kusoma, kuandika wala kutumia simu bila kuvaa miwani na hata akishavaa miwani ili aanze kutumia simu au kusoma magazeti,Biblia lazima hiyo Biblia ,simu ataisogeza karibu kabisa na Macho huku akiwa amekunja sura ndani ya miwani ndiyo anaweza kusoma.
Mama yangu mzazi ambaye Julai mosi mwaka huu anatimiza umri wa miaka 60 naye ametumia Box mbili za ONCE A DAY hivi sasa ameacha kabisa kuvaa miwani na Kasema havai tena Kwani lishe mbovu zina sababisha baadhi ya watu washindwe kuona halafu madaktari wanawaandikia wavae miwani na Ngozi yake imekaa vizuri tofauti na Kabla hajaanza kutumia ONCE A DAY .
Aidha kuna rafiki yangu ambaye ni Ofisa wa Polisi mstaafu naye alikuwa anavaa miwani Macho yake haya wezi kuona Mbali licha anavaa miwani nikampa Ushuhuda wangu naye akaenda kununua ONCE A DAY anameza na Jana usiku nimewasiliana naye amenieleza hivi sasa Macho yake yana anga za sana kupita zamani na uwezo wa kuona Mbali ,kusoma umeongezeka ukilinganisha na siku za nyuma Kabla ya kuanza kutumia Once A Day hadi anajishangaa.
Hadi Jana usiku niliwasiliana naye Ofisa Huyo wa Polisi mstaafu ambaye asema jana ameanza kutumia box la pili la ONCE A DAY amesema hivi sasa yupo Katika Hatua za mwisho za kuacha kabisa kutumia miwani Kwani macho yake yanaona vizuri hivi sasa kutokana na kumeza vidonge hivyo na kwamba hivi sasa amefikia hatua ya kukaa siku hata tatu bila kuvaa miwani na anaweza kutumia simu ,kusoma maandishi ya mbali na karibu bila Shida yoyote.
Aidha kuna baadhi ya watu ambao nao wana tatizo la macho kama niliyokuwa nayo Mimi nao nimpe washauri licha wanatumia miwani wameze ONCE A DAY Kwani mama yangu Mzazi alikuwa anatumia miwani baada ya kumtaka ameze ONCE A DAY amemeza vidonge 60 ambavyo ni box mbili miwani havai tena na ngozi yake imekaa vizuri tofauti na awali.
Tujiulize ni wangapi kumbe wanatatizo la upungufu wa VItamin A mwilini ambao unasababisha macho yasione vizuri kama mimi ( Happiness) walipimwa na madaktari wakaambiwa wavae miwani wakakubali wanavaa miwani wakati ukweli ni kwamba imekuja kubainika tatizo lao la macho halikustahili kuambiwa wavae miwani?
Hivi daktari unavyompa tiba isiyo sahihi mgonjwa wako ,ufikiri kuwa unamsababishia mathara makubwa huyo mgonjwa wako Mbele ya safari?
Tujiulize mimi ( Happiness ) ningekubaliana na maagizo ya wale madaktari wawili mwaka 2009 na 2014 walionitaka nivae miwani mimi nikagoma leo macho yangu siyangekuwa yameishaaribika bure ? Siyo vizuri baadhi ya madaktari Mnachotufanyia baadhi ya wagonjwa wenu.
Wakati Leo nikitoa Ushuhuda huu kwa umma ,napenda Kusema Kuwa kwanza unapopatwa tatizo mshirikishe Mungu ili akusaidie kutatua tatizo lako kwa kutumia watu waliosahihi hapa duniani kwasababu mimi nilimshirikisha Mungu katika tatizo hilo na kweli akanitafutia mtu "Dk.Seth" akanipa matibabu sahihi ambayo yameniponya.
Aidha nimejifunza pia ukileta ubishi katika katika baadhi ya mambo ,ubishi unalipa / faida wakati mwingine kwasababu bila ya mimi kukaidi maagizo ya wale madaktari wawili waliyonipa kati ya mwaka 2009/ na 2014 walionipima na kuniambia nastahili kuvaa miwani na nikainunua lakini nikagoma kuivaa .
Je ningekuwa nimekubalina nao ningeivaa miaka yote hiyo kumbe tatizo langu limekuja kubainika sikustahili kuvaa miwani leo hii macho yangu siyangekuwa yamearibika kabisa? Ubishi wakati mwingine unalipa .
Lakini kingine Nilichojifunza na ninachotaka Kuwaasa wagonjwa, ndugu wa wagonjwa muwapo mahospitalini waache tabia ya kuwalazimisha madaktari wanachotoka wao na Kuwalazimisha madaktari wawatibie harakaharaka waondoke ,hii tabia tuache Mara Moja haitasaidii zaidi ya kutuaribia Kwani Daktari naye ni binadamu anaweza akakerwa na hiyo tabia akaamua Kumpa huduma mbovu mgonjwa.
Nakemea tabia hiyo kwasababu hata Mimi siku hiyo hiyo ya 16/5/2017 nilipokuwa nikitibiwa macho hospitalini hapo, kimoyo moyo nilikuwa nakereka na Dk.Seth alivyokuwa ananipima macho Taratibu .
Bahati nzuri sikuropoka nilivumilia Kumbe ndiyo Dk.Seth alikuwa ananiponya kwa kutumia Taaluma yake.
Hivyo Tujenge tabia ya kuwapa nafasi madaktari pindi wafanyapo Kazi zao ,tuwavumilie tusiwaingilie wala kuwaharakisha wafanyapo Kazi Yao ya kitabibu.
Kingine Nilichojifunza wakati Leo nikitoa Ushuhuda huu ni kwamba Kuwa siyo kila mtu anayesumbuliwa na ugonjwa wa macho anastahili kuandikiwa na Daktari avae miwani .Kwani Maradhi ya macho yanasababishwa na sababu mbalimbali na matibabu ya macho ni tofauti.
Natoa Rai kwa umma Kuwa makala hii isitafsiliwe Kuwa inaamasisha wagonjwa wa macho waliopimwa wakabainika wana matatizo ya macho Na wakatakiwa wavae miwani na wanavaa miwani hadi sasa waache kuvaa kwasababu ya makala hii imetoa Ushuhuda wa jinsi Mimi, mama yangu Mzazi tulivyopimwa Tunaambiwa tuvae miwani Mimi nikakaidi ila mama yangu Mzazi kwa zaidi ya Miaka Kumi Ana anavaa miwani ila baada ya kutumia ONCE A DAY ameamua kuachana na miwani kwasababu anaona vizuri kuliko hata akivaa hiyo miwani .
Shukurani zangu za dhati nazipeleka Kwa Uongozi wa Kikosi cha 521 Hospitali ya Rufaa ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi ( JWTZ) kinachoongozwa na Brigedia Jenerali Dk.Paul Masawe ambaye kitaaluma ni daktari wa magonjwa moyo ambaye ni miongoni walioniimiza sana nianze kufanya mazoezi ya kupunguza mwili Mwaka 2011 alipokuwa na Cheo Cha kwasababu aliniona na uzito mkubwa sana ,wafanyakazi wa hospitali hiyo na Dk.Seth na Mwenyezi Mungu.
Mungu ampe Afya na Maisha Marefu Dk.Seth Japhet wa Hospital ya Rufaa ya Jeshi Lugalo na ninaamini kupitia Mimi utawaponya Wengi zaidi.
Niitimishe kwa Kusema nilichokigundua Kuwa Kumbe siyo kila mgonjwa anayedai anasumbuliwa na matatizo ya macho basi Daktari anaona Tiba inayomfaa nikimpatia Tiba ya kuvaa miwani tu Kumbe sasa kupitia Ushuhuda wangu huu wa makala hii mtakubaliana na Mimi Kuwa siyo wote wanaovaa miwani ya macho au waliondikiwa wavae miwani ya macho kama Tiba siyo sahihi Kwani wengine hawakustahili kuandikiwa wavae miwani Kwani tatizo Lao la macho ni la kama langu mie ( Happiness) la upungufu mkubwa wa VITAMIN A mwili ambao ulisababisha macho yangu yashindwe kuona sehemu yenye Giza na yenye Mwanga hafifu hivyo madaktari wale wawili walipaswa wanishauri nikale vyakula vyenye Vitamin A au waniandikie nikanunue vidonge vyenye madini na vitamin nimeze ili niongeze vitamini A mwili na baadhi ya madini. Ndugu zanguni Akili Kumkichwa.
Mwandishi wa Makala hii ni ;
Ofisa Habari wa University Of Bagamoyo (UoB ) na Mwanasheria.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
21/6/2017
17 comments:
Umenigusa sana dada Happyness changamoto hiyo iliyokupata ya kuumwa macho nami ninayo.juma3 nami nafika hosp Lugalo.MUNGU Akubariki sana kwa makala hii.
Nimeguswa nduguyangu namm nnamatatizo kama uliokua nayo nna uoni hafifu sioni mbali usiku ndo kabisa naomba msaada wapi naweza kupata hiyo dawa my no 0718586590
Mm macho yangu hayaoni maamdishi madogo
Nimeguswa na ushuuda huu na mim Nina tatizo la macho soon mbali wap hizo daw zinapatikan
Nashukuru kwa taarifa namimi kesho mapema naenda pale Lugalo kumtafuta huyo Dr
Kesho mapema naenda Lugalo kumsaka huyo Dr
Ahsante sana
Asante
Mungu akubariki
Namimi nina shida hiyo hiyo nashukuru kwa ushuhuda wako nitatafuta hizo dawa
Dawa ndo zinaitwa once a day au
Once a day ziko za aina tofauti ipi uliyotumia ww kwa ajili ya macho msaada tafadhali
Tunaomba namba ya huyo Dr.
Nashukuru sana dada, sasa mimi Niko Congo drc, ntaataje hiyo dawa? Naomba namba namba ya sim kwani macho Yana nisumbua kabisa.
Asante Dada Solution tumepata kwa uwezo wake Mungu😀
Shukrani kwa ushauri huu, Mungu ampe maisha marefu huyo Dr. Ili aweze kuponya wengi na kuwa mfano wa ma Dr. wengine ili waweze kutusaidia sote
Asante kwa ushauri wako barikiwa sana tusaidie na picha la box
Post a Comment