WAFUASI WA PONDA WAPUNGUZIWA ADHABU
Na Happiness Katabazi
MAHAKAM A Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetengua adhabu ya
kifungo cha mwaka mmoja jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar
es Salaam Machi 21 mwaka huu,dhidi ya wafuasi 52 wa Sheikh Ponda Issa
Ponda kwasababu adhabu hiyo ilitolewa
kinyume na sheria husika.
Hukumu ya Rufaa hiyo
ilitolewa jana asubuhi na Jaji Salvatory Bongole ambaye alisema Agosti 12 mwaka huu alisikiliza hoja za wakili wa waomba rufaa(Mohamed
Tibanyendera) na hoja zilizotolewa na mawakili wa serikali Peter Njike ambapo wakili Wakili
Tibanyendera alikilichambua kosa la kula njama kutenda kosa kinyume na kifungu 384
cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, kosa la pili ni la kufanya
mkusanyiko haramu kinyume na kifungu cha 74 na 75 cha sheria hiyo ambavyo
vinasomwa pamoja na kifungu cha 43(2)(4) na 46 cha Sheria ya Jeshi la Polisi ya
mwaka 2002.
‘Kwa masikitiko makubwa tu
nasema kosa la kula njama halikuthibitika, na hakimu Fimbo alikosea
kuwatia hatiani kwa kosa la kula njama kwa kutumia kifungu hicho cha 384 cha
sheria ya Kanuni ya adhabu. Na kwa mujibu wa kifungu cha 46 cha Sheria ya Jeshi
la Polisi ya mwaka 2002,inasema wazi kabisa mtu anayekutwa na hatia ya kutenda
kosa la mkusanyiko haramu atapaswa alipe faini ya Sh.50,000 au kwenda jela
miezi mitatu au vyote pamoja:
‘Lakini tunashangaa huyu hakimu
Fimbo ameto adhabu ya juu kabisa ya mwaka mmoja jela..sijui hiyo sheria
ameipata wapi?Tunaomba mahakama hii itengue hukumu hiyo kwani inadosari nyingi
za kisheria na hakukuwa na ushahidi wowote wakuweza kuishawishi mahakama hiyo
iwatie hatiani waomba rufaa”alidai wakili Tibanyendera.
Kwa upande wake wakili wa serikali Njike aliiomba mahakama
isitengue hukumu hiyo kwasababu hukumu ile ya Mahakama ya Kisutu ilikuwa sahihi
kisheria na kwamba upande wa jamhuri ulileta ushahidi mzito ambao uliishawishi
mahakama ya Kisutu kuwatia hatiani washitakiwa hao kwa makosa matatu ya kula
njama, kufanya maandamano haramu na kukaidi amri ya jeshi la Polisi.
Akitoa hukumu ya Rufaa hiyo jana Jaji Bongole alisema anakubaliana na wakili wa
waomba rufaa kuwa hakimu Fimbo alikosoea kuwatia hatiani katika kosa la kwanza
la kula njama, kwani hakukuwepo na ushahidi unaonyesha washitakiwa walitenda
kosa hilo la kuja njama kutenda kosa hivyo mahakama yake inawaachiria huru
washitakiwa hao katika kosa hilo la kwanza la kula njama kwasababu hakukuwa na
ushahidi wa kuwatia hatiani.
Aidha jaji Bongole alisema hakubaliani na ombi la waomba rufaa lilotaka mahakama
iwaachiriwe katika kosa la pili la kufanya maandamano haramu kwenda katika
ofisi za Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi kushinikiza DPP
amwachirie huru Ponda aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya wizi wa malighafi na
uchochezi katika Mahahakam ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambayo ilimhukumu kifungo
cha nje cha mwaka mmoja.
“Mahakama hii imekataa kuwaachiria huru katika kosa la pili
la kufanya maandamano haramu kwenda ofisi ya DPP na pia imekataa kuwaachiria
huru katika kosa la tatu na kukaidi amri ya jeshi la polisi iliyowataka
watawanyike kwasababu , upande wa
jamhuri uliweza kuleta ushahidi ambao umedhibitisha waomba rufaa walitenda
makosa hayo mawili na kwamba Mahakama Kuu inawatia hatiani kwa makosa hayo na
kusema kuwa mahakama ya Kisutu ilikuwa sahihi kuwatia hatiani katika makosa
hayo”alisema Jaji Bongole.
Hata hivyo Jaji Bongole alisema pamoja na mahakama yake
kuwatia hatiani katika makosa hayo mawili ambapo kwa mujibu wa Sheria ya polisi
, mtu anayepatikana na hatia katika makosa hayo anapewe adhabu ya ya kutumikia kifungo cha miezi mitatu jela na
faini ya Sh. 50,000 na kwamba mahakama yake inawapatia adhabu kwasababu ndiyo adhabu iliwekwa na Sheria ya
Jeshi la Polisi hivyo hakimu wa Mahakama ya Kisutu alikosoea kuwapatia adhabu
ya kifungo cha mwaka mmoja.\
Aidha Jaji Bongole alisema licha mahakama yake imewapatia
adhabu hiyo, pia mahakama yake imeona washitakiwa ambao walikuwa wakitumikia
adhabu ya mwaka mmoja gerezani tayari wameishakaa gerezani muda mrefu na adhabu
ya kisheria kwa mujibu wa makosa hayo ya miezi mitatu imeishapita , hivyo
mahakama yake inawaachiria huru ila kama waomba rufaa hao wanakesi nyingine,
waendelee kushikiliwa na mamlaka nyingi.
Hata hivyo gazeti hili saa nne asubuhi lilishuhudia waomba
rufaa hao wakipakizwa kwenye basi la jeshi la Magereza na kurudishwa gerezani hadi pale mahakama
itakapopelekea hati inayoonyesha waomba rufaa hao wameachiwa na Mahakama
hiyo.Hata hivyo ulinzi ulikuwa umeimalishwa na hapakuwepo na vurugu zozote.
Kesi hiyo ya
kihistoria ilifunguliwa rasmi katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Februali 18 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi
Sundi Fimbo, na siku hiyo hiyo upande wa
jamhuri ukasema upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na Februali 19 mwaka huu,upande wa jamhuri
uliwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao na shahidi wa kwanza wa upande wa
Jamhuri ambaye ni Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Hemed Msangi
alianza kutoa ushahidi wake hadi Februali 26 mwaka huu, upande wa jamhuri
ulipofunga ushahidi wake ,washitakiwa wakaanza kujitetea na Februali 19 mwaka
huu,Na Machi 21 mwaka huu, Mahakam a hiyo ilimaliza kusikiliza kesi hiyo kwa Mahakama
hiyo kutoka hukumu yake ambapo iliwahukumu kwenda jela mwaka mmoja kwa makosa
hayo ya kula njama, kufanya maandamano haramu na kukaidi amri ya jeshi la
polisi iliyowataka watawanyike.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Oktoba 22 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment