Header Ads

HASSANOR WA COREFA APANGUA KESI YA KWANZAHASSANOR  WA COREFA APANGUA KESI YA KWANZA 
Na Happiness Katabazi

HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Da es Salaam, ilimwachiria huru Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Soka Mkoa wa Pwani(COREFA), Hassan  Othaman  Hassan " Hassanoo"  Na wenzake ambao waliokuwa wakikabiliwa na Kesi ya jinai namba  209/2011 ya wizi wa madini aina ya Kopa  yenye Thamani ya sh.milioni 400 kwa maelezo kwa upande wa jamhuri umeshindwa kuthibiisha kesi hiyo.

Katika Hague nyingine nudge,Jamaa ,wanachama wa COREFA, wanahabari walilalamikia Hatua ha Hakimu Fimbo kutoa hukumu ya Kesi Katika chemba Hali iliyosababisha wanahabari, na watu wengine Wengi kushindwa kuingia Kwenye chemba hiyo kusikiliza hukumu hiyo  ambayo ilisababisha umati wa watu kufurika Mahakamani hapo tangu asubuhi na kumshaur Hakimu Huyo ajue kusoma baraka za nyakati na Gazeti Hilo lilishuhudia Kumbi za wazi za Mahakama hiyo Zikiwa wazi Hali iliyosababisha watu kuhoji ni kwanini Hakimu Huyo ameshindea kusoma hukumu hiyo Kwenye Kumbi wa wazi.

Hukumu hiyo ambayo imeandaliwa na Hakimu Mkazi Devota Kisoka na kusomwa kwa niaba yake na Hakimu Mkazi Sundi Fimbo , alianza kwa kuikumbusha Mahakama kuwa washitakiwa waliokuwa wakikabiliwa na jumla ya makosa Tatu ya kula Njama,kupatiakana na Mali wizi ambayo ni madini ya Kopa na wizi wa madini hayo.

Hakimu Fimbo Alisema Kabla Mahakama kutoa hukumu yake ilijiuliza maswali matatu ambayo , je washitakiwa waliokuwa Njama Kutenda kosa?, je ni kweli washitakiwa walikutwa na Mali ya wizi? Na je ni kweli washitakiwa waliiba madini hayo?.

Alisema Katika swali la kwanza la Kama kweli washitakiwa walikula Njama, Mahakama Imeona upande wa jamhuri katika harakati zake za kataka kuthibitisha Kesi yake ulileta jumla mashahidi 13', Mahakama Imeona upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi wa kuthibitisha washitakiwa walitenda kosa kwani Hakuna ushahidi uliotelewa unaonyesha washitakiwa waliwai kukukutana na wakapanga Njama za Kutenda makosa hayo.

Hakimu Fimbo Alisema kuhusu swali la pili la endapo washitakiwa walipatikana na Mali ya wizi, Hakimu Huyo Alisema awali Kesi hiyo ilipofunguliwa ilikuwa na jumla ya washitakiwa wa nane lakini baadae mshitakwa mmoja (said.mohamed) alifutiwa Kesi hiyo na mkurugenzi wa mashitaka(DDP),Dk.Eliezer Feleshi.

"Mahakama hii ilitegemea Dereva wa roli ambayo Kopa iliyokuwa Kwenye roli Alegre mahakamani na upande wa jamhuri ili aje atoe ushahidi, lakini hakuweza kuletwa kutoa ushahidi  " Alisema Hakimu Fimbo.

Kuhusu swali la Tatu Hakimu Fimbo Alisema Mahakama ilijiuliza Kama kweli washitakiwa waliiba madini hayo ya Kopa, Alisema mshitakwa wa kwanza na wa pili(Wambura na HASSANOR) hawakupaswa mashitakiwa kwa kosa Hilo la Tatu la wizi kwasababu wao siyo Wamiliki wa godauni la  na kwamba hawakuwepo siku ya tukio na mmilikk wa godauni hakuwepo siku ya tukio na pande zote haikuwa na ubishi Katika hilo na Hakuna Shahidi wa upande wa jamhuri Aliyewaona washitakiwa wakiiba madini hayo ya Kopa.

  "Kwa maelezo hayo hapo juu Mahakama hii inawaachiria HURU washitakiwa wote kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha Kesi yake" Alisema Hakimu Fimbo.
Itakumbukwa kuwa Desemba 24 Mwaka Jana, JAJI wa maHakama Kuu kanda ya Dar es. salaam, zainabu mruke. Alitupilia Mbali ombi la HASSANOR lililokuwa linaimba Mahakama Kuu impatie dhamana Katika Kesi nyingine inayomkabilk ya kusafirisha pembe za ndovu kwenda Hong Kong China zenye Thamani ya sh billioni  1.1 ambayo ipo Kwenye Mahakama ya Kisutu pia.

JAJI mruke Alisema Amekataa Kumpa dhamana kwasababu  HASSANOR ambaye wakati yupo nje kwa dhamana kwa Kesi aliyoshinda Jana ya wizi wa Kopa, aliterate makosa ya kusafirisha Pemba za ndovu na hivyo alimnyima dhamana na hadi sasa HASSANOR anaishi Katika gereza la keko wakati waliokuwa washitakiwa wenzake Katika Kesi waliyoshinda Jana ya wizi wa Kopa Dk.Najim na Wambura Mahenge waliokuwa nje kwa dhamana.

Licha ya HASSANOR kushinda Kesi hiyo Moja back Anakabiliwa na Kesi nyingine hivyo HASSANOR amerejeshwa gerezani.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 2013

No comments:

Powered by Blogger.