Header Ads

UB YAMSHUKURU KIKWETE






Na Happiness Katabazi
UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB), umemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuwateua wajumbe wawili wa Bunge la Katiba kutoka katika chuo hicho.
 Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, Naibu Mkuu wa chuo hicho, anayeshughulikia Fedha na Utawala, Dk. Elifuraha Mtaro, aliwataja wajumbe hao kuwa ni Profesa Costa Mahalu na Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Dk. Natujwa Mvungi.
Dk. Mtaro alisema wabunge hao wawili ni waajiriwa wa UB, licha ya kuteuliwa kupitia makundi mawili tofauti.
Alisema Balozi Mahalu aliteuliwa kutoka kwenye kundi la dini na Dk. Natujwa ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katika, marehemu Dk. Sengondo Mvungi, amepitia kundi la elimu.
“Kwa niaba ya uongozi wa UB, tunamshukuru Rais Kikwete kwa kuwateua wafanyakazi wetu wawili kwani uteuzi huo ni ishara tosha ana imani nao na pia ni sifa pia kwa UB kwa kutoa wasomi wawili wa sheria kwenda kuungana na wenzao katika Bunge la Katiba,” alisema Dk. Mtaro.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano. Februali 12 Mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.