Header Ads

MARANDA MGONJWA KALAZWA MOI


Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,Jana ilishindwa kuendelea kusikiliza utetezi wa Kesi ya wizi wa sh.milioni 400 Katika Akaunti ya Madeni ya Nje Katika Benki Kuu , inayomkabili Kada wa CCM, Rajabu Maranda na wenzake kwasababu Maranda ni mgonjwa na Amelazwa Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Eva Nkya, mshitakiwa Farijala Hussein  aliomba Mahakama Kesi hiyo Kuwa Kesi hiyo Jana ilikuwa KWAAJILi ya washitakiwa KUJITETEA lakini anaomba wasijitetee kwasababu mshitakiwa mmoja(Maranda) ambaye ni mfungwa Katika GEREZA Ukonga HIvi sasa Amelazwa Katika Hospitali ya Muhimbili kwaajili ya matibabu.
Ombi Hilo lilikubaliwa na Hakimu Nkya na akaairisha Kesi hiyo hadi MACHI 10  Mwaka huu.

Maranda na Farijala hadi sasa wameishahukumiwa Katika Kesi Tatu tofauti za EPA na WANAISHI gerezani huku Kesi zao nyingine zikiendelee mahakamani hapo.

Katika Hatua nyingine Mahakama hiyo Imeiatisha Kesi ya matumizi Mabaya ya madaraka inayomkabili ALIYEKUWA MKURUGENZI wa TBS, EKEREGE hadi Aproli 8 Mwaka huu.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima Machi 7 Mwaka 2014


No comments:

Powered by Blogger.