MAHALU HURU TENA
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemfutia Rufaa ya jinai iliyokuwa ikimkabili Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Grace Martin kwasababu Mkata rufaa ambaye ni Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi han haja ya kuendelea na rufaa hiyo.
Mwaka 2012 DPP-Dk.Feleshi kupitia Wakili mwandamizi wa serikali Oswald Tibabyemkomya alikata rufaa Mahakama Kuu Kapinga hukumu iliyotolewa na Aliyekuwa Hakimu Mkuu Mfawidhi Elvin Mugeta, Agosti 9 Mwaka 2012 Katika Kesi ya uhujumu uchumi Na.1/2007 iliyokuwa ikiwakabili wajibu rufaa ambapo Hakimu Mugeta alimwachiria Huru Mahalu na grace baada ya kuwaona hawana Hatia Katika Kesi iliyokuwa ikiwakabili.
Amri ya kuondolewa rufaa hiyo ilitolewa Jana na JAJI John Utamwa ambaye Alisema Mahakama yake inatumia Ibara ya 108 (2)ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 , kukubali ombi la DPP ambapo DPP aliwasilisha ombi la kuiandika rufaa yake dhidi ya wa jibu rufaa chini ya Kifungu Cha 386(1) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002.
Ibara ya 108(2) ya Katiba ya nchi inasomeka HIvi: ' Iwapo Katiba hii au Sheria nyingine yoyote haikutamka wazi kwamba shauri la aina iliyotajwa. Mahususi litasikilizwa kwanza Katika Mahakama ngapi iliyotajwa mahususi kwaajili hiyo, basi Mahakamu Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kila shauri la aina hiyo.Hali Kadhalika Mahakama Kuu itakuwa na uwezo wa kutekeleza shughuli yoyote ambapo kwa mujibu wa mila za kisheria zilizotumika Tanzania shughuli ya aina hiyo kwa kawaida hutekelezwa na Mahakama Kuu.
Isipokuwa kwamba Masharti ya Ibara hii ndogo yatatumika bila ya kuathiri mamlaka Mahakama ya Rufaa ya Tanzania Kama ilivyoelekezwa Katika Katiba hii au Katika Sheria nyingine".
Jaji Utamwa alisema Kwakuwa Kifungu Cha 386(1) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 ikampa madaraka DPP , kuondoa rufaa wakati wowote Kabla ya rufaa, Mahakama yake inalikubali ombi Hilo la DPP la kuondoa rufaa hiyo mahakamani na kwamba kuanzia sasa Mahalu na wenzake wapo huru.
Amri ambayo ilipokelewa kwa Furaha na Grace na wakili wao Beatus Malima licha Mahalu ambaye Mjumbe wa Bunge la Katiba hakuwepo mahakamani , ambapo Wakili Malima Alisema amefurahishwa na amri hiyo ya MahakamA na pia amepongeza uamuzi huo wa DPP. Dk.Feleshi kwa kuwaondolea rufaa hiyo wateja wake na kwamba kwa amri hiyo ya Mahakama ni wazi sasa wateja wake wanakuua Huru kulitumikia taifa Lao kwa kasi mpya baada ya kukumbuka na Kesi hiyo kwa Miaka Saba sasa.
Agosti 9 Mwaka 2012 Aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Elvin Mugeta alimwachishakazi Huru Baloz Mahalu na Grace waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Euro milioni mbili kutokana na ushahidi wa jamhuri kushindwa kuwatia hatiani.
Hukumu hiyo hiyo ilitqfsiriwa i kama ni kubwagwa kwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kutokana na hatua ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa kukubali kupanda kizimbani na kumtetea Mahalu dhidi ya serikali, tukio ambalo ni la kwanza katika historia ya nchi hii. Hukumu hiyo ya kihistoria ya kesi ya uhujumu uchumi Na.1/2007 .
Washtakiwa hao waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka sita walikuwa wanatetewa na mawakili Mabere Marando, Alex Mgongolwa, Beatus Malima na Cuthert Tenga na upande wa Jamhuri ulikuwa ukiwakilishwa na Ben Lincoln na Vicent Haule toka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Ponsia Lukosi toka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).
Aliyaja makosa hayo kuwa ni kula njama, kutumia nyaraka za manunuzi ya jengo la ubalozi ili kumdanganya mwajiri wao serikali, wizi wa Euro milioni 2,065,827 na kuisababishia serikali hasara.
Kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 22 mwaka 2007.
Ili kuithibisha kesi yao, upande wa Jamhuri ilileta jumla ya mashahidi saba wakati upande wa utetezi ulileta mashahidi watatu akiwemo Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Mei 8 mwaka 2012, upande wa utetezi ulifunga ushahidi wake baada ya Grace kumaliza kujitetea. Mei 7 mwaka 2012,Mahalu ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu kipya cha Bagamoyo cha jijini Dar es Salaam alimaliza kujitetea na siku hiyo ndiyo Rais Mkapa aliandika historia mpya nchini kwa upande wa marais ambapo alifika mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake katika kesi hiyo. Julai 16 mwaka 2009, Jaji Sivangilwa Mwangesi ambaye ndiye alikuwa akiisilikiza kesi hiyo tangu ilipofunguliwa mwaka 2007 alitoa uamuzi wake ambapo aliwaona washitakiwa hao wana kesi ya kujibu. Machi 25 mwaka 2011.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Mei 10 Mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment