Header Ads

VIGOGO BARCLAYS WATINGA KIZIMBANI



Na Happiness Katabazi
WATU saba wakiwemo wafanyakazi wawili  wa benki ya  Barclays
Jana wamefikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Da es Salaam, kwa kesi ya  sh. milioni 390.2 kwa kutumia silaha.

WAkili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka akisaidiwa na Mwanaamina Kombakono mbele Hakimu Mkazi Nyigulila Mwaseba aliwataja washitakiwa Hao Kuwa ni   Alune Kasililika (38), Neema Batchu (26) wafanyakazi wa
benki, Kakame Julius (38), Iddy Khamis (32), Sezary Msolopa (31), Boniphace na Muumba (29) na Ruth Macha (30) wafanyabiashara.

Wakili Kweka alidai kuwa washitakiwa hao  wanakabiliwa na mashtaka mawili.
Alidai Kuwa  kuwa katika tarehe tofauti tofauti zisizo fahamika washtakiwa  wakiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam walikula njama ya kwa nia ya kutenda kosa la wizi.

Wakili Kweka akili taja SHITAKA la pili washitakiwa Hao   Aprili 15 mwaka huu, wakiwa Katika eneo la  benki hiyo tawi la Kinondoni, Dar es Salaam waliiba fedha tasilimu sh.
milioni 390.2, Dola za Marekani 55, 000 na Euro 2150 mali ya Barclays na  Kuwa Kabla ya kufanya wizi huo walimtishia kwa silaha
Anifah Ahmad na Anna Tegete ambao ni wafanyakazi wa benki hiyo ili kuweza
kujipatia na kumiliki fedha hizo.

hata hivyo washitakiwa hao walikana mashitaka na Wakili Kweka  alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na wa naomba  tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Mwaseba alisema kwa mujibu wa sheria shtaka la pili halina dhamana,
kwa hiyo washtakiwa wapelekwe gerezani  na Kesi hiyo itaalishwa hadi   Mei 15 Mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Mei  3 Mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.