Header Ads

MAPYA YAIBUKA KESI YA GHOROFA DAR



Na Happiness Katabazi
MAWAKILI wa upande wa utetezi Katika kesi ya Mauji yaliyosababishwa na kuangukiwa na ghorofa lilikuwa MTAA wa Indra Gandhi Dar es Salaam, inayomkabili Mkurugenzi wa zamani wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime(61) na wenzake wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ,ilifutwa Kesi hiyo kwasababu hati ya Mashitaka Ina dosari za kisheria.

Mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka Mawakili wa Washitakiwa John Mhozya na Ndurumah Majembe Jana waliwasilisha ombi Hilo Jana  hoja zao jana ambapo Wakili , Mhozya aliomba  mahakama kuiangalia kwa umakini hati ya mashtaka inayomkabili mteja wake , Fuime  kwa madai ni batili kwa kuwa haikidhi matakwa ya sheria.
 
Wakili Mhozya alidai Kuwa Sheria   inaitaka hati ya mashtaka  kuwa na viashiria vya kosa  ambalo mshtakiwa anashtakiwa nalo, na kwamba mteja wao ameshtakiwa na Kesi ya Mauji  ila hati ya mashtaka iliyopo mahakamani haina viashiria vinavyoonyesha  kosa hilo Hali nayoifanya hat hiyo ionekane ni Batiri kisheria.
 
Awali Kabla ya Wakili Mhozya kuwasilisha hoja hiyo, Hakimu Kisoka alimweleza Wakili Huyo  kuwa jalada halisi la kesi hiyo limeitwa Mahakama  Kuu hata hivyo wakili huyo aliieleza mahakama kitu ambacho kimesababisha liitwe huko akimuhusu mteja wake na kuomba kuendelea kuwasilisha hoja yake.
 
Hakimu Kisoka alimpa nafasi hiyo ya kumsikiliza lakini Wakati wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard Kongola  alipinga  kwa madai kuwa  mahakama hiyo ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza wala kusuluhisha chochote kwa sababu kesi ipo hapo kwa ajili ya taratibu za awali tu na kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza Kesi ya Mauji.
 
Baada ya kutoa maelezo hayo, Hakimu Kisoka alimtaka wampe nafasi ya  kumsikiliza Mhozya, kitendo ambacho Kongola alikataa na kudai kuwa hata jibu chochote na  na wakili huyo wa serikali alidai kuwa atatoka   nje ya mahakama wakati kesi hiyo ikiendelea
 
Hata hivyo Hakimu Kisoka alimtaka wakili Kongola kutulia ili aweze kumsikiliza Wakili Mhozya anaongea nini.
 
Kutokana na kitendo hicho, Wakili Majembe  aliiomba mahakama kuzuia uvunjifu wa sheria kwa watu wa kawaida na  wale wa serikali mahakamani  na kuongeza kuwa katika kusoma kwake  na uzoefu aliokuwa nao hajawahi kuona mahali popote  hicho kinachodaiwa na upande wa mashtaka.
 
Majembe alidai kuwa Mahakama inauwezo wa kuangalia kwa umakini kosa ili kujiridhisha  kwa kuwa uhuru wa mtu ni muhimu  na jela ni mbaya,  leo mteja wetu, Fuime ameshtakiwa kwa kosa la mauaji kesho anaweza kubadilishiwa likawa la kutakatisha fedha na baadaye hata kubaka.

Aidha Hakimu Kisoka aliarisha Kesi hiyo hadi  Mei 19 Mwaka huu, AMBAPO Atakuja kutolea uamuzi wa ombi lilowasilishwa na Mhozya.
 
Fuime na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 27 ya mauaji  yaliyotokea katika mtaa wa Indira Gandh, yaliyotokana na kuporomoka jengo la ghorofa 16.Washtakiwa wengine ni mfanyabiashara na mmiliki wa jengo hilo Radha Hussein Radha, Diwani katika Manispaa ya Kinondoni,  Ibrahim Mohamed maarufu kama Kisoki (59),  Mhandisi Charles Salu (48), Mhandisi wa Majengo Godluck Sylivester (35)  na Mkurugenzi Mkuu wa Mkaguzi wa Majengo, Willibrod Wilbard (42).

Washtakiwa wengine ni Mhandisi Mohamed Swaburi (61), Mhandisi Mshauri, Zonazea Oushoudada (60), Mkadiriaji Majenzi, Vedasto Nziko (59), Msanifu Majengo, Michael Hema (59), Msajili Msaidizi AQRB, Albert Mnuo na Ofisa Mkuu Mtekelezaji OJoseph Ringo.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Mei 7 Mwaka 2014
 
 
 
 
 
 
 
 
 

No comments:

Powered by Blogger.