Header Ads

WAKILI RUTAGATINA ASHINDA RUFAA YAKE

WAKILI RUTAGATINA ASHINDA RUFAA
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE Mahakama ya Rufaa nchini, imetengua hukumu ya Mahakama Kuu Kanda a Dar es Salaam, ya Septemba 6 Mwaka 2006 ambayo ilitupilia Mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na Wakili wa kujitegemea Christian  Rutagatina Kapinga Kapinga uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Mawakili ambayo Kamati hiyo ilimwondoa Kwenye orodha ya Mawakili nchini.

Hukumu ya rufaa hiyo Na.46/2012 ilitolewa jopo la Majaji wa Tatu wa Mahakama ya Rufaa Stephen Bwana, Sauda Mjasiri na Januari Msoffe .Rufaa hiyo Iliikatwa na Rutagatina aliyekuwa akitetewa na wakili George Kilindu dhidi ya Kamati ya Maadili ya Mawakili na Clavery Ngalapa Mwaka 2012.

jaji Bwana Alisema Rutagatina aliwasilisha jumla ya Sababu Sita za Kapinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyotupa RUFAA yake,AMBAPO Sababu ya kwanza ni kwamba Majaji wa Mahakama Kuu waliopo sea kisheria na kimaelezo kukubali mamlaka yasiyosahihi  ambayo yaliyotolewa na mrufani(Rutagatina).

Sababu nyingine ni mahakama Kuu  Walikosea kisheria kukata kukubali Haki ya Msingi ya mrufani, kwamba Mahakama Kuu ilikosea kisheria Kwa kushindwa kutoa hukumu yake kutumia ushahidi thabiti wa tuhuma zilizokiwa zinamkabili mrufani bila kuachakazi mashaka, na kwamba Mahakama ile ilikosea kisheria Kwa kushindwa kutumia ushahidi unaonyesha Majina ya wa maofisa wa Mahakama ambao mdaiwa  wa pili ( Ngalapa) alidai Kuwa mrufani alimtaka ampatie Fedha ili akawape maofisa wa Mahakama Kama rushwa ili wamsaidie Kwenye Kesi yake. Na kwamba adhabu aliyopewa mrufani ya kuondolewa Kwenye orodha ya Mawakili nchini ni kubwa.

Jaji Bwana Alisema amepitia hoja za pande zote mbili ambapo mdaiwa wa kwanza awatete wa na Wakili Mwandamizi wa serikali Vicent  Tangho , mahakama yake imeamua kukubaliana na hoja za mrufani kwamba utaratibu uliotumika kuendesha shauri Hilo Katika Kamati ya Maadili ya Mawakili na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ulikiuka Sheria na Kanuni inayotaka     
Mahakama au Kamati ya Maadili Imtie Mtu hatiani KWA makosa anayokabiliwa nayo bila Kaacha Mashaka yoyote lakini KWA mazingira ya shauri Hilo, Kamati ya Maadili ya Mawakili na Mahakama Kuu ilishindwa kuzingatia kanuni hiyo ambayo inakataza kumtia MTu hatiani wakati kuna Mashaka.

"Mahakama hii inatamka Kuwa  mrufani (Rutagatina),ameathirika  kwa Miaka Tisa sasa  kutokana na hukumu hizo mbili ambazo ni hukumu ambazo zimevunja Sheria  na kwasababu hiyo Mahakama hii inakubali RUFAA yake na inatambua hukumu ya Mahakama Kuu" Alisema Jaji Bwana.

Novemba 18 Mwaka  2005 , Kamati ya Maadili ya Mawakili  nchini, ilimvua  uwakili Rutagatina , baada ya kumkuta na hatia ya kosa kuvunja  Maadili ya uwakili.
Clavely Ngalapa , alikuwa ni mteja wa mrufani , ndiye  aliyewasilisha  malala ipo  Kwenye Kamati hiyo. Ngalapa  alidai Kuwa Wakili Huyo (Rutagatina) alimtaka atoe  rushwa  kwa  jaji  na maharani wa Mahakama Kuu  Katika Kesi ya Madai Namba 393/1998 ambayo Wakili Huyo alikuwa akimtetea  mteja Huyo.

Septemba 6 Mwaka 2006 , jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, lilokuwa likiongozwa na Jaji Augustine Shangwa, Jaji Juxon Mlai (Mstaafu),  Na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Kwa sasa William Mandia , Alisema yeye  Kuwa yeye  na wenzake wamepitia Kwa kina ombi la Rufaa ya Rutagatina kuhusu hukumu iliyotolewa Novemba 18 Mwaka 2005  na Kamati ya Maadili ya Mawakili , na wameikataa  Rufaa yake Kwasababu wamebaini Mrufani alivunja mabadili ya uwakili.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 6 Mwaka 2014.No comments:

Powered by Blogger.