Header Ads

HONGERA GEORGE MASAJU KUTEULIWA KUWA MWANASHERIA MKUU WA TANZANIA


HONGERA GEORGE MASAJU KUTEULIWA KUWA MWANASHERIA MKUU TANZANIA 
Na Happiness Katabazi

HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete amemteua aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Mcheche Masaju Kuwa Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Ikulu kwa umma iliyotolewa Leo inasema Masaju  ataapishwa Jumatatu.

Hongera sana Mtani wangu Masaju kwa Kupanda Cheo. Ila Kupanda Cheo kwako huko hivi sasa kutasababisha usionekane tena Katika Mahakama za wazi za Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani nchini kwaajili ya kuendesha Kesi kubwa ambazo Serikali akiwemo Mwanasheria Mkuu alikuwa akishitakiwa.

Masaju ni miongoni mwa Wanasheria wa serikali wazalendo na wanaowaaminiwa kiutendaji na ndiyo maana zilipokuwa zikifunguliwa Kesi ambazo zilikuwa zikivuta hisia za watu Wengi Masaju alikuwa akivaa suti na gauni lake la uwakili na kutinga Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu na kuiendesha Kesi hiyo yeye Mwenyewe akisaidiwana na vijana wake.

Na nilipokuwa Mwandishi wa Habari za mahakamani,nilipokuwa nikimuona Masaju Kubeba gauni jeusi na begi lilokuwa na Nyaraka za kuendeshea Kesi basi nilikuwa Nasema Kimolo moyo Kuwa upande wa wa pili Katika Kesi hiyo ujiandae kikamilifu .

Ushahidi mchache wa haya ninayoyasema kuhusu Masaju ambayo nilikushuhudia kwa macho yangu mwanzo hadi Mwisho ni Rufaa ya Kesi maarufu ya mgombea Binafsi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila Katika Mahakama ya Rufaa nchini Masaju alikuwa kiongozi wa Mawakili wa serikali kuendesha Kesi hiyo ya kihistoria ambayo ikisikilzwa na jopo la Majaji Saba waliokuwa wakiongozwa na Jaji Mkuu wa wakati huo , Agustino Ramadhani,  Masaju alifanikiwa Kujenga hoja na hatimaye jopo lilikubaliana naye na kutengua hukumu ya Mahakama Kuu ambayo iliruhurusu Mgombea Binafsi.

Ushahidi wa pili, ni Mwaka Jana , katika kesi ya Kikatiba Na.24/2013 , Masaju aliwakilisha upande wa Mwanasheria Mkuu Katika Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Kituo ca Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)dhidi ya Waziri Mkuu iliyokuwa ukiomba Mahakama Kuu itoe Tafsiri ya Ibara ya 100 Kuwa wabunge wana Uhuru bila mipaka kwani Pinda alitoa Kauli Bunge akitaka Polisi iwapige wanaovunja Sheria za nchi.

Juni 6 Mwaka 2014 , Jopo la Majaji wa Tatu wa Mahakama Kuu Dar es Salaam, Fakji Jundu, Dk.Fauz Twaibu na Augustine Mwarija walitoa uamuzi wa Kuitupa Kesi hiyo  kwa sababu Imeona walalamikaji walikuwa hawana Haki ya kisheria ya kushitaki Pinda.

Jopo hilo lilitoa uamuzi huo jana ambapo jaji Jaji Jundu alisema anakubaliana na pingamizi la awali lilowasilishwa na wakili wa mdaiwa (Pinda), Ambaye ni Naibu Mwanasheri Mkuu wa Serikali,  George Masaju, AMBAlo lilikuwa likiomba  Mahakama itoe amri ya kuifuta Kesi hiyo kwasababu walalamikaji hawana Haki a kisheria ya kuwashitaki wadaiwa na kwamba Waliokuwa na Haki ya kushitaki Pinda ni wananchi na siyo Taasisi hizo za walalamikaji.
O
LHRC na TLS walimshtakiwa Waziri Mkuu Pinda pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kauli aliyoitoa bungeni Juni 20 mwaka 2013.Ilidaiwa Katika   kipindi cha maswali ya papo kwa papo Waziri Pinda akijibu alisema, ‘ukifanya fujo…unaambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi, utapigwa tu, muwapige tu sababu tumechoka’.

 Jaji Jundu alisema, Masaju Aliwasilisha  pingamizi la awali akiomba  kesi hiyo itupwe kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kuisikiliza, waliofungua hawakustahili kuifungua na iko kwa ajili ya kupoteza MUDa wa Mahakama.

Katika uamuzi huo, majaji walikubaliana na hoja tatu za pingamizi kuwa walalamikaji katika kesi hiyo hawakuwa na haki ya kufungua kesi hiyo na kwamba walikosea taratibu za ufunguaji wa kesi kama hizo kwa kuwa walikiuka amri na kanuni zinazoongoza Mashauri ya Madai (CPC).

Katika hoja ya kwanza kuwa Pinda kama mbunge analindwa na Katiba, jopo hilo lilisema kuwa ni kweli wabunge wanalindwa na Katiba Ibara ya 100 (1) kuhusu haki na upendeleo (Previledge), yaani haki na uhuru wa mjadala na maoni. Hata hivyo, lilikataa hoja za utetezi kuwa wabunge wana kinga isiyo na mipaka ya kutokushtakiwa kwa kauli au jambo lolote walilolitamka bungeni.

“Ibara ya 100(1) ya Katiba haiwezi kujadiliwa mahali popote ikiwemo mahakamani, ibara hiyo inasema kwamba, kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano au katika mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

“Ibara ya 100(2) inaweza kujadiliwa mahakamani, inasema kwamba bila kuathiri katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yoyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.

“Mwananchi mmoja mmoja aliyeathika na jambo lililozungumzwa na mbunge bungeni anaweza kushtaki lakini si taasisi kama ilivyo katika kesi hii,”alisema.
Alisema kutokana na sababu hizo, mahakama inatupilia mbali kesi hiyo kwa sababu waliofungua kesi, LHRC na TLS hawakustahili kisheria kufungua kesi hiyo kwa sababu hawakuathirika.

Kesi ya Tatu ni Kesi iliyofuta hisia za watu Wengi ni Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa Mwaka Jana na Mwandishi wa Habari Saed Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Kubenea alikuwa anaomba Mahakama hiyo itoe amri ya muda ya Kuzuia Bunge  Maalum la Katiba lisiendelee na kazi kwasababu linavunja Sheria .Hata hivyo Masaju aliwasilisha mapingamizi mawili  ambayo yaliomba Mahakama hiyo itupilie Mbali Maombi ya Kubenea Kwani hayana Msingi na Mahakama hiyo ilitupilia mbali Maombi ya Kubenea na Bunge linaendelea na kazi zake.

Mifano ni mingi ya Kuonyesha Masaju Kabla ya kuteuliwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Leo , kuna kazi nzuri ya kuiwakilisha upande wa serikali Katika Kesi mbalimbali mahakamani aliifanya hivyo anastahili.  Hongera sana.

Wosia wangu wa Masaju endelea na msimamo wako ule ule wa kusimamia haki na Kusema ukweli bila woga.Tunaokufahamu Tunaokufahamu Kuwa una sifa hizi. 

Usikubali kuyumbishwa na wanasiasa uchwara yaani baadhi ya wabunge iwe ndani au nje ya Bunge. Kwani ushahidi siyo wa kutafuta watangulizi wako katika Cheo chako kipya cha AG, Johnson Mwanyika, jaji Fredrick Werema waliandamwa sana wakati mwingine kwa tuhuma za kijinga na kizushi tu na hawa wanasiasa uchwara wetu.

Wakianza kukuandama kwa uzushi na ukaona aliokuweka madarakani haonyeshi dalili zote za kudhibiti uzushi huo, fanya Kama alivyofanya Jaji Werema chukua Karamu na karatasi andika barua ya kujiudhuru Kisha nenda kafanye kazi nyingine Kwani hata Bibila ilishaandika Mtu hawezi kuishi kwa Mkate tu.

Masaju mtani wangu usikubali hata kidogo heshima yako ishushwe  na wapuuzi wachache tena kwa uzushi, Linda heshima yako kuliko madaraka uliyonayo Kwani hiki Cheo kipya umekipata pia kutokana na sifa zako za kiutendaji, uadilifu wako usingekuwa na sifa hizo ni wazi ingekuwa ni Ngumu Leo hii kupata hayo madaraka uliyoyapata.


Kwa wabunge misio fahamu Masaju , nataka niwaambie Masaju ni mtu asiye penda kuburuzwa Hasa kuburuzwa na mambumbumbu wa Sheria, ni mtu anayejali haki, ukweli na uwazi na ni Mtu mwenye msimamo.

Sasa ile tabia yenu ya kipuuzi inayofanywa na baadhi ya wabunge na wanasiasa uchwara ya kuingilia kazi za AG, Mtambue mapema Kama Kikwete Katika Kitu yaani Jaji Werema kaweka kitu yaani Masaju. 

Hongera Mtani wangu Masaju, mungu akutangulie Katika majukumu ya Cheo kipya Cha AG licha ulikuwa ukikikaimu.Tenda haki kwa wote na wakati.

Mungu ibariki Tanzania

Chanzo:Facebook:  Happy Katabazi
Januari 3 Mwaka 2015.

No comments:

Powered by Blogger.