Header Ads

' PANYA ROAD ' MNALAANA







'PANYA ROAD ' MNALAANA

Na Happiness Katabazi
WATOTO wa Mjini wanasema  ' mtafuta Fedha siyo mhuni'.  Kwa asilimia Fulani anakubaliana na Msemo huu Kuwa mtu  yoyote anayetafuta Fedha kwa njia yoyote ile siyo mhuni.

Mtu yoyote anayetafuta Fedha ni lazima ameisha Keti Kitako na kuchora ramani  vizuri tu kwamba nikienda kufanya tukio sehemu Fulani au kumpora Fulani nitapata Fedha au mali.

Sasa Mtu wa aina hiyo huwezi Kusema kirahisi rahisi Kuwa ni mhuni tu halafu tu kaishia hapo. Na ukiifuatilia taarifa za Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kwa Kipindi chote Cha Mwaka Jana utabaini Kuwa Panya Road wanaenda kufanya Uhalifu sehemu ambazo wanajua watapata Fedha na mali iwe simu, Fedha kidogo.  

Nimelazimika kutumia Msemo huu kwa Sababu makala yangu ya Leo ambayo ni fupi nitajadili vitendo Vya kihalifu vilivyofanywa na kikundi maarufu Cha waporaji hapa Dar es Salaam, ' Panya Road'.

Kikundi hiki ambavyo Mwaka jana kuliibuka kwa kasi lakini Jeshi la Polisi lilijitahidi kupunguza makali Yao Lakini Jana Januari 2 Mwaka huu, kikundi hicho kilifanya balaa la kuvamia mitaani likiwa na silaha za Jadi na kufanya Uhalifu ikiwemo kupora mali za watu na kuhatarisha Usalama wa watu na mali zao.

Kwanza kabisa nataka ni wakumbushe Kuwa Leo ni Mara yangu ya pili kuandika makala ya kukuamasisha Jeshi la Polisi liwashughulike kikundi hiki Cha Panya Road, Mara ya kwanza kuandika ilikuwa ni Mwaka Jana.

Panya Road kadri siku zinavyozidi zaidi kusongwa Mbele nalazimika kuona hawa siyo wahuni ni wasaka Fedha kwa njia haramu na ni watu wenye akili timamu na wanafahamu wanachokifanya.

Maana kwa watu tunaofikiri sawa sawa tunajiuliza hawa Panya Road walikaa  wapi, saa ngapi, wakaamua kupanga Njama za kufanya Uhalifu Jana Kama walivyofanya?

Huo ujasiri wa kufanya huo Uhalifu adharani wanapata wapi?Je hawa Panya Road hatuoni Kama kuna sehemu uwa wanakutana na kupeana Mafunzo ya kutumia silaha  za Jadi, jinsi ya kuvamia eneo, Maana Inaitaji roho ya ujasiri kuamua Kujitoa Mhanga kumvamia mtu usiyemjua na kuanza kumpora.

Ombi langu kwa vyombo Vya dola kuelekeze pia Nguvu zake kwa hawa Panya Road , maana Dalili zinaonyesha wazi siyo watu wa kudekezwa tena na kuchekewa na dhana ya kuwaita Panya Road ni wahuni kuanzia Leo ikome, watazamwe kwa karibu na vyombo ya dola .Bado Nina Imani na vyombo vyetu Vya Ulinzi na Usalama, Kwani Vikiamua kufanya kazi yake vinafanya.

Hakika Jana Uvumi Kuwa   Panya Road  eti umeliteka Jiji la Dar es Salaam kwa kulivamia na kufanya Uhalifu,ulisababisha hofu na taharuki kubwa miongoni mwa wakazi wa baadhi ya vitongoji ambavyo Kumbe havikuvamiwa na Panya Road.

Huku Mitaa ya Sinza Mugabe baada ya Uvumi huo kusambaa kulisababisha maduka ,bar, Kufungwa na baadhi ya watu kuvuka barabara Kuwa nyeupe ,watu kuvuka barabara bila kuangalia kushoto na kulia kwa Sababu watu walililazimika kuwa na nidhamu ,kurudi mapema majumbani mwao na kulala mapema kwa lazima kwa hofu ya Panya Road. 

Kila siku kupitia makala zangu nimekuwa nikikemea tabia ya baadhi ya Watanzania kujigeuza wasemaji wa Jeshi la Polisi, waandishi wa Habari kuamua kutumia mitandao ya kijamii kusambaza taarifa za uzushi Hali iliyosababisha Jana watu kuishi kwa hofu Kumbe Panya Road kuna maeneo walikuwa hawayajavamia.

Hii tabia ya uzushi ni Mbaya sana na Ina madhara makubwa sana na wakati tabia hii ya uzushi kupitia mitandao inaendelea vyombo vyenye mamlaka kudhibiti taarifa za kizushi Katika mitandao vipo vimelala usingizi wa pono.

Namalizia kwa Kusema Panya Road siyo wa huni,ni wasaka Fedha kwa njia haramu na msaka fedha huwezi kumuita mhuni. Panya Road Mnalaana.

Chanzo: Facebook: Happiness Katabazi
Januari 3 Mwaka 2015.







No comments:

Powered by Blogger.