Header Ads

TABIA HII ITAKOMA LINI?TABII HII  ITAKOMA LINI?
Na Happiness Katabazi
KWA Miaka zaidi ya Sita  sasa ya Utawala wa Serikali ya awamu ya nne iliyopo madaraka tumeshuhudia baadhi ya viongozi wa juu Katika taifa hili na wananchi wa kawaida sura zao zikipachikwa Katika viwili viwili ambavyo siyo vyao .

Sura za baadhi ya viongozi wakati mwingine zimekuwa zikionekana Kutenda  na matendo machafu sana na kudhalilisha utu wao.

Aliyekuwa wa kwanza Kutengenezewa picha chafu ni Rais Jakaya Kikwete, mwaka 2009 ambayo picha iliyokuwa na sura yake iliwekwa kwenye Mtandao wa  Ze Utamu ambao hivi sasa Mtandao  haupo.

Baadhi ya watu tuliopata bahati ya kuona picha ile tulishtuka na binafsi nilipokuwa Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, niliandika makala ya kumea  picha ile .

Makala ile ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho (WAMILIKI WA ZE UTAMU WASAKWE), ambayo ilichapishwa kwenye gazeti la Tanzania Daima la Aprili 29 mwaka 2009.

Na kweli baada ya saa Chache  Mtandao huo au kuweza kuonekana tena Mtandaoni hadi Leo.

Watengenezaji wa picha hizo,wamekuwa wakiendelea bila kukoma na jana usiku Katika mitandao ya kijamii zimekuwa zikitambazwa picha mbili zenye sura inayofanana na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nnchemba.

 Picha  hiyo ilinisikitisha  na kuanza kuwaarifu watu wangu wa karibu kwa kuwaonyesha hiyo picha na wengine wanafki walijifanya hawataki kuiona na wengine walisikitishwa na wengine walifurahia umdhalilishwaji alivyofanyiwa Nnchemba.

Na wanafki hao ambao wakikataa kuiona picha hiyo yenye sura ya Mwigulu  alivyodhalilishwa, lakini nawafahamu watu Hao ni mabingwa wa kutumia a picha  za utupu na wanazifurahia kimoyo moyo.

Ili makala yangu iwe na kielelezo nimeamua kutumia picha hiyo ambayo inasambazwa  ambayo inaoenekana kufanana na sura ya waziri Mwigulu Kama kielelezo.

Nashauri hata kama unamchukia vipi binadamu mwenzako,tusifikie Hatua ya kufanyia na  hivi, siyo vizuri Kwani tunaowadhalilisha kwa picha hizi Tukumbuke na wao wanastahili Kuwa Kuwa na heshima Mbele ya Jamii.

Tuache unafki na kuficha maovu tuinuke na tukemee vitendo hivi ..Pole Waziri Mwigulu na wengine wote mliopata majeraha kwa kufanyiwa udhalilishwaji   huu.

By Happiness Katabazi
31/1/2015
No comments:

Powered by Blogger.