Header Ads

POLISI TEMEKE MMETUFURAHISHA WATANZANIA WENYE AKILI TIMAMU


Na Happiness Katabazi

JANUARI 27 Mwaka huu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke lilifanikiwa kuwadhibiti na kuwatawanya Waandamaji haramu wa Chama cha Wananchi CUF, na kuwashushua kisago kitakatifu wafuasi wale waliokuwa wamekaidi amri ya Jeshi ka Polisi iliyokuwa imeyapiga marufuku maandamano na mkutano ule.

Nimetazama zaidi ya Mara 20 video ya jinsi Jeshi la Polisi Temeke ' lilivyowachangamkia' yaani kuwashushia kipigo wavunja sheria wale , Nimefikia uamuzi wa kukubali Kuwa  Polisi Temeke siku ile walifanyakazi Yao ipasavyo na wanastahili pongezi .

Na siyo Siri hiyo video nimekuwa nikiisambaza kwa vijana ambao nawafahamu ni malimbukeni wa siasa za vyama Vya upinzani kwa makusudi ili waone faida waliyoipata wafuasi wenzao wa CUF walivyochezea kisago 'heavy',.

Vijana  wote na wengine ni watu wazima baada ya kumaliza kutazama video ile wameniakikishia Kuwa Kamwe hawatashiriki,wala kusogelea  maandamano haramu mAana video ile inayoonyesha jinsi Polisi walivyokuwa wakiwashushia kisago Waandamaji imewafundisha Kuwa Polisi siyo watu wa kuwachezea ovyo na kwa upande wa wanawake wamesema kupitia video hiyo hawapo Tayari kuingia Kwenye mahusiano ya kimapenzi na Askari Polisi maana ukimchokoza anaweza kuitoa roho yako kwa kipigo haraka sana.

Baadhi ya watu wamenukuliwa wakilalamika kwenye tafrani lile kuna mwanamke alipigwa na kudhalilshwa na polisin, minamuuliza mwanamke yule Kama alikwenda Kwenye maandamano Yale balaa lile la kipigo lingemkuta?Lisenge mkuta.Wanawake wenzake walikuwa Kwenye shughuli za kimaendeleo na wengine walikuwa wamekwenda VICOBA kuurejesha Marejesho Yao ,yeye akaona ni bora aende Kutenda jinai na akaishia kuchezea kichapo.

Mwanamke Yule na wenzake walijifanya wapo  juu juu Kama 'Ngoma za Daku 'kwa kushiriki maandamano haramu ya CUF kule Temeke Matokeo yake ukaambulia kipigo na Kesi juu.

Kwa kisago kile wewe mwanamke unapaswa ujiulize ni kwanini Mke wa Mwenyekiti wako wa CUF,Profesa Ibrahim Lipumba hakushiriki maandamano Yale haramu?

Nimesema kipondo kile kimenifurahisha mimi na watanzania wote wenye akili timamu na wanaochukia vitendo vya uvunjifu sheria kwani tayari huku  mitaani ,video hiyo inayosambazwa Kwenye mitandao ya kijamii imeishatoa Funzo kwa wale wasiyotaka kutii Sheria bila shuruti na pia imetoa Funzo kwa wale ambao hawapo karibu na walinzi wa vyombo Vya Ulinzi na Usalama Kuwa Askari wa Jeshi lolote siyo raia Mwenzenu na msipende kuwazoea zoea na kuwadharau .

Nimalizie kwa kuliombea Jeshi la Polisi pia liwageukie wafanyabiashara ambao HIvi sasa wamejigeuza miungu watu wanaamka asubuhi wanaamua Kufunga maduka ,hawatoi huduma eti wamegoma kwasababu mashine wanazouziwa na TRA ni za gharama sana na eti hawakupewa Mafunzo ya jinsi kuzitumia.

Tumeshuhudia tumepata Usumbufu mkubwa kutoka tabia hii chafu inayofanana na baadhi ya wafanyabiashara Dar es Salaam, Mwanza na kwingineko.

Minasema HIvi Kama mfanyabiashara anaona hawezi kumudu kununua hiyo mashine ambayo serikali inamtaka aitumie, basi aache kabisa kufanya biashara tumjue ,kuliko kila siku wanajifanya wanamsimamo wa kujifanya watagoma, wakifikisww kidogo wanafungua maduka.

Hawa nao pia wanastahili Kutiwa adabu kidogo ili akili iwakae sawa.Maana huo mchezo wao unasababisha shughuli za kiuchumi kwa baadhi ya watu kutikisika kwaajili ya mchezo huo.

Namalizia kwa kulipongeza Jeshi la Mkoa wa Kipolisi Temeke Dar es Dar es Salaam,   unaongozwa na Kamanda  Kihenya Kihenya mmenifurahisha sana Mimi binafsi,mwanangu Queen 'Malkia' ambaye ni 'Mke Mdogo'wa Boss wenu wa zamani IGP- Said Mwema kwa kutoa dozi nzito kwa wavunja Sheria wale. Wa CUF ambayo CUF Ng'ang'ari ya miaka ya 1995-2002 siyo CUF ya leo CUF ya leo ni sawa na joko la kibisa halina meno.Mungu awabariki sana Polisi Temeke.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Januari 31 Mwaka 2015.

No comments:

Powered by Blogger.