CATHERINE KYAMBIKI AWASHA MOTO KANISA LA ELSHADAI TEMPLE INTERNATIONAL
*JUNI 28 KUZINDUA ALBAMU YA NANE
Na Happiness Katabazi
MSANII maarufu wa Njimbo za Injili nchini, Catherine Kyambiki leo amekonga nyoyo za waumini wa Kanisa la Maombi la Elshadai Tample International lililopo Boko Basiahaya Dar es Salaam,baada ya kuimba wimbo wake maarufu ujulikanao kwa jina la Yesu anaweza Yote.
Sambamba na hilo, Kyambiki Juni 28 mwaka huu ,anatarajia kuzindua albamu yake nane itakayojulikana kwa jina la Ameniponya Bwana Yesu katika Hoteli ya Land Mark Dar es Salaam, ambapo hadi sasa mwanamuziki wa muziki wa Injili Mike Karambai ,Mike Froloy kutoka nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo,Judie Babie toka Uganda na waimbaji wengine wa hapa nchini wameishathibitisha kumsindikiza katika uzinduzi huo.
Kyambiki ambaye jumla ana albamu nane za nyimbo za Injili,leo ni Jumapili ya kwanza kufika katika ibada inayoendeshwa na kanisa hilo ambalo linaongozwa na Kanali mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi(JWTZ), Nabii Bruno Kinunda, pamoja na kushuhudia mambo makubwa aliyomtendea Mungu kupitia maombi aliyoyaomba kanisani hapo mapema wiki hii na Nabii Kinunca kanisani hapo ambapo alisema kwa hisia kuwa " Unapokuwa na Nabii mtu mzima Relax' na kwamba amethibitisha Mungu anamtumia Nabii Kinunda na kuaidi kuwa kwa kipindi cha mwezi mmoja atakuwa akisali kanisani hapo.
Kyambiki ambaye alikuwa akitoa ushuhuda wake huku akionyesha hisia kali na kusema kuwa alipata majaribu katika siku za karibuni na kwa bahati nzuri alikutana na mama mmoja ambaye alikuwa hamfahamu kabisa nakatika maongezi mama huyo ambaye ni Mzee wa Kanisa hilo akamtaka aende kwenye maombi katioa kanisa hilo na majaribu yake yote yatakiwsha na kweli Alhamisi ya wiki hii alifika kwenye maombj kanisani hapo na kuonana na Nabii Kinunda na kumsali nae pamoja na kwamba hivi sasa vile vikwazo vimeondoka na kwamba jana alifika hapo kumshuhudia Mungu na kukiri kuwa ni kweli Tanzania kuna Manabii wa ukweli na kuwashaurj wale wote wasumbukao na mizigo waende kuombewa.
Baada ya Kyambiki kumaliza kutoa ushuhuda huo Kyambiki aliomba atumbuize pamoja na kwaya ya kanisa hilo ambapo alipanda jukwaani na kuanza kuimba wimbo wake wa Yesu anaweza Yote ,hali iliyosababisha waumini kuinuka kwenye viti kwa shangawe huku wakienda kumtunza fedha na kuimba nae pamoja.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kanisani hapo alisema amefurahi kusali kanisani hapo na kwamba ametambua kuna uwepo Mkubwa wa Mungu.
Awali Nabii Kinunda akifundisha somo la leo ambalo linasema Yesu Kristo amepaa mbinguni ambalo linapatikana katika kitabu cha Matendo ya Mitume 8:11 .
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Mei 3 mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment