NILIJIUNGA TENA NA CCM 2011: JAJI AUGUSTINO RAMADHAN
.
Na Happiness Katabazi
MGOMBEA urais wa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania , Augustino Ramadhan amesema alijiunga tena na CCM Septemba Mwaka 2011 Katika Tawi la Chama hicho ,Oysterbay, Jijini Dar es Salaam.
Jaji Ramadhani ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la Anglikana, aliyasema hayo Leo saa Tatu asubuhi wakati akihojiwa na Mwandishi wa Habari hizi Katika mahojiano maalumu .
"Nilijiunga tena kwa Mara ya pili na CCM , Septemba Mwaka 2011 katika Tawi langu la CCM lililopo Oysterbay ,Jijini Dar es Salaam na Mimi naviachia vikao Vya Chama viamue Kama muda huo niliyojiunga tena na CCM Unatosha kuniruhusu kugombea nafasi yoyote Kwenye Chama ikiwemo nafasi hiyo ya Urais au laa" alisema Jaji Ramadhan.
Jaji Ramadhaman alisema anaomba wananchi anafahamu Kuwa Mwaka 1966 akiwa ni Mwanafunzi wa kozi ya Sheria Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kulitokea mgomo wa wanafunzi ambao wanafunzi hao walikuwa wakipinga Masharti ya kujiunga na mafunzo ya National Services Hali iliyosababisha chuo Kufungwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wote kufukuzwa chuo kwasababu ya mgomo ule licha yeye hakuwa miongoni mwa wanafunzi walioanzisha vurugu zile na hivyo kufanya Mwaka mmoja kukaa majumbani.
Alisema Julai Mwaka 1967 ,Chuo Kikuu kilisamehe wanafunzi wote waliokuwa wamefukuzwa Chuo mwaka 1966 kutokana na vurugu zile hivyo na hivyo wakarejea chuoni hapo na kuanza upya Mwaka wa kwanza kozi ya shahada ya Sheria na walivyorejea chuoni wanafunzi Wengi Walikata Kadi na kujiunga na TANU YOUTH LEAGE.
Jaji Ramadhan ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Afrika Ya Haki za Binadamu , alisema alipofika mwaka wa tatu wa kozi yake ya Sheria Mwaka 1969 , Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) , lilitangaza ajira na kwamba yeye alienda kuomba kazi ya jeshi na aliitwa kwenye usahili na wakati alipokuwa akihojiwa katika usahili huo maswali mbalimbali na akawauliza Kuwa yeye ni Mwanachama wa TANU YOUTH LEAGE akawajibu Kuwa ni kweli ni Mwanachama .
Alisema Maofisa wale wa JWTZ wala mwambia hiyo haitoshi wakimtaka awapatie Kadi inayoonyesha yeye ni Mwanachama wa Chama cha TANU ,kadi ambayo halikuwa Hana Hali iliyosababisha Mwaka 1969 kwenda kwenye Tawi la TANU ,Temeke Dar es Salaam , kukata Kadi ya TANU na kuwapatia na hivyo hicho nacho kikawa ni Kigezo cha kupata ajira ya JWTZ hadi anastaafu Kazi ya JWTZ alistaafu akiwa na Cheo cha Brigedia Jenerali wa Jeshi Hilo.
" Nikaendelea Kuwa Mwanachama wa TANU ambapo Mwaka 1977 I kazaliwa CCM Nikiwa na Jaji na Ofisa wa JWTZ hadi Ilipofika Mwaka 1992 , Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho ambapo ziliingizwa Ibara ambazo zilikuwa zinakataza Majaji na Askari Kuwa wanachama wa vyama Vya siasa Ndipo nikipoacha kuwa Mwanachama wa CCM "alisema Jaji Ramadhan.
Aidha alisema Disemba 28 Mwaka 2010 alistaafu rasmi Kazi ya jaji wa Mahakama ya Rufaa akiwa na wadhifa wa Jaji ya Jaji Mkuu wa Tanzania na kwamba Septemba Mwaka 2011 ndipo alipojiunga tena kwa Mara ya pili CCM.
Juni 17 Mwaka 2015 ,Jaji Ramadhan alichukua fomu ya Kugombea nafasi ya urais kupitia CCM, Hali iliyosababisha Kuibuka maswali yasiyo na majibu Kuwa ni lini alijiunga na CCM wakati yeye aliwahi Kuwa jaji.
Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
Juni 18 Mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment