Header Ads

MAKONGORO:TURUDISHIENI CHAMA CHETU
".....Sisi  ndio Wazalendo  na sisi wazalendo tunasema hivi mnaetaka kutupora hiki chama wenyewe tupo.Turudishieni  hiki chama na mnapoturudishia  kipitishieni  kwa Makongoro Nyerere.

Sitojiunga hayo makundi  kwanini? Kwasababu  makundi  haya ni makundi ya  watu  wachache . Sisi tuko wengi  kwanini tukajipendekeze kwa wachache?

Turudishieni chama chetu. Tunaataka chama chetu na mtakirudisha tu. Hatununuliki,tuko wengi na jina letu tunaitwa wazalendo.Tupo.Mzalendo haondoki,mzalendo hanunuliki."

Maneno hayo yametamkwa na mgombea urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Makongoro Nyerere ' Mtoto wa Marehemu',.wakati akitangaza nia ya kugombea urais Mwintongo ,Butiama mkoani Mara, 1/6/2015

Binafsi nimeipenda nukuu hiyo.

Imeandaliwa na Happiness Katabazi
Blogg:www.katabazihappy.blogspot.com
Juni 3 mwaka 2015.

No comments:

Powered by Blogger.