Header Ads

LOWASSA UNA TATIZONa Happiness Katabazi

LEO  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezindua rasmi kampeni za uchaguzi Mkuu Katika Viwanja Vya Jangwani Dar Es Salaam. Na ukweli kampeni za UKAWA zimefana hongereni sana.

Nimefuatulia kwa makini Uzinduzi huo mwanzo hadi mwisho kupitia Kwenye Televisheni.Nimewasikia wote waliopewa nafasi ya kuzungumza a amezungumza waliyozungumza hata Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye nimemsikia yote aliyoyasema licha yote aliyoyasema Sumaye siyo mapya.

Lakini wenye akili timamu tunayapuuza yote aliyoyasema Sumaye Leo kwasababu Sumaye ambaye  amewahi kugombea urais mara mbili kupitia CCM na hakufanikiwa.

Enzi akiwa   Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu aliwahi kusema "UKITAKA BIASHARA ZAKO ZIKUNYOKEE  VIZURI UJIUNGE NA CCM". Hadi sasa Sumaye hajafuta Kauli hii ambayo ilizua mjadala Mkali nchini.

Nirudi Kwenye mada yangu ya Msingi ya Leo.Mada hiyo nitajadili uamuzi wa Mgombea Urais wa CHADEMA kwa muunganiko wa UKAWA, Edward Lowassa  Leo  saa 11 jioni alipopanda jukwaani kuanza kuhutubia  alisema ameishauriana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe Kuwa asisome hotuba yake ya Uzinduzi wa kampeni hiyo kwasababu eti muda umekwenda na Polisi wa Dar Es Salaam, hawampendi kabisa kwahiyo eti wakizidisha muda Polisi hao watapata Sababu.

Kwasababu hiyo eti Mbowe na viongozi wengine wamemshauri asiisome hiyo hotuba ndefu badala yake hiyo hotuba itawekwa Kwenye Website ili wananchi waisome.

Jamani , hivi huyu Lowassa yupo Siriazi kweli ?Lowassa hayupo Siriazi kuutaka urais wa Tanzania. 

Leo Ndio ilikuwa siku rasmi ya Lowassa ambaye ni mgombea urais kuja  Uwanjani kueleza wanachi atayafanyia nini kupitia Katika kinywa Chake na kuwaomba kura wananchi .

Lakini Lowassa Hilo Leo lime mshinda kashindwa  kueleza kwa wananchi atayafanyia nini na mipango ya serikali yake akafanikiwa Kuwa rais itakuwa ni ipi kwa Sababu dhahifu kabisa.

Mgombea urais kabisa bila aibu Katika mkutano wa Uzinduzi wa kampeni yako bila aibu na woga unasema eti hutasoma hotuba yako badala yake Utaiweka Kwenye website? 

Tumuulize huyu Lowassa ambaye amekuwa akijigamba Kuwa anachukizwa na umaskini na amekuwa akiwa tembelea watu wa Haki ya chini Kwenye masoko .

Sasa Nimuulize hao masikini ambao hawana simu za Smartphone wataweza kuisoma hiyo hotuba yake kupitia website? 

Jibu ni Jepesi Watanzania Wengi hawataisoma hiyo hotuba yako kwa Sababu hata hela za kuweka Bando Kwenye simu hawana uhakika wa kuzipata.

Sasa ikitokea wasikupigie kura za Ndio kwasababu umeshindwa kusimama jukwaani kunadi sera zako utakapoingia Ikulu utawafanyia nini utakuja Kulalamika umeibiwa kura?

Maana hata unapotaka Mwanamke kimapenzi lazima usemezane naye ,umwage sera zako ili akakubali au aukataee wewe Leo Lowassa Hilo limekishinda la kututongoza wananchi wenye akili timamu ili tu kuipigie kura kwasababu dhahifu?

Kama Mbowe na viongozi wenzake walijua muda ni Mdogo, kwanini wasinge panga Ratiba ikaanza mapema ili upate muda mrefu wa kusimama jukwaani usome hotuba yako?

Lowassa unataka kutuchezea akili, yaani unataka tukupe urais wakati umeshindwa kusoma hotuba ya ufunguzi wa kampeni zako? 

Kama ulishauriana na viongozi wa UKAWA usisome hotuba yako ,sasa kulikuwa na maana gani ya kufanya mkutano huo Leo ?Simngeweka hiyo hotuba Kwenye Mtandao tukajua Moja.

Hilo limekushida,Je ikitokea ufanikiwe urais wa Tanzania, licha naamini huwezi kufanikiwa kupata nafasi hiyo unaweza kwenda Umoja wa Mataifa na Kusimama Mbele na kusoma hotuba au mhadhara  kwa Niaba ya Tanzania zaidi ya saa Moja?

Kwanza Ulipaswa uonyeshe kwa vielezo Kuwa ni kweli Polisi Dar Es Salaam wanakuchukia na wanakuchukia kwasababu gani? Lini walianza kukuchukia?

Polisi wakikukataza kisheria kufanya ziara zako ambazo zinahatarisha Usalama wako na kuleta Usumbufu Katika Jamii ndiyo wanakuchukia? 

Lowassa wewe ni kiongozi wa ajabu sana na unageuka kuchekesha Mbele ya watu tunaofikiri sawa sawa.

Leo umetumia dakika nane jukwaani kuzungumza mambo ambayo siyo mapya ,jipya nililoliona ni lile la kumshukuru aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani,Fredrick Sumaye  eti amefanyakazi nzuri sana ya kuwapa vidonge vyao serikali ya CCM.

Hili Mimi Ndio nimeliona jipya kutoka mdomoni mwako kwasababu umemsifia aliyekuwa hasimu wako wa kisiasa Sumaye.

Na pia nimeliona jipya pia kwa mdomo wa Sumaye kutoa maneno ya kujisafisha wewe Lowassa Kuwa ni Msafi wakati ni Sumaye huyu huyu alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanakupiga vijembe.

Sielewi kabisa ni kwanini watu wazima Mmekuwa na tabia za kinafki  mna misimamo  inayoyumbayumba na ya msimamimii maneno yenu?

Itoshe Kusema tu kwa nilichokiona Leo nimeitimisha kwa Kusema mkutano wa Leo wa UKAWA ulikuwa Una sura mbili.

Sura ya kwanza ni ya Uzinduzi wa Kampeni na sura ya pili ni Sumaye kutumika kurusha makombora Moja kwa Moja kwa Rais Jakaya Kikwete na serikali na CCM.

Na kweli Sumaye amefanyakazi hiyo kikamilifu ya kurusha vijembe Kwani watu walikuwa watu livu sana wakamsikiliza na kushangilia licha Lowassa Katika zile dakika zake wakati akizungumza watu baadhi ya wananchi walikuwa hawamsikilizi Kwani walikuwa wakiondoka uwanjani hapo.

Yaani mgombea Urais kabisa wa UKAWA, huyu Lowassa anasimama jukwaani anasema eti akiwa Rais Atalishughulikia Kesi ya Babu Seya,kuwaachiria huyu Masheikh wa UAMSHO  Sheikh Farid na wenzake ambao wapo gerezani,elimu ya Darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu Bure. Kwa hiyo hayo yapo ndani ya Ilani ya UKAWA?

Lowassa Leo Kasema anajua tu ataibiwa kura zake .Sasa Kama unajua utabiwa kura zako kwanini unaendelea kushiriki Katika uchaguzi Mkuu?Maana hadi umediriki Kusema utaibiwa kura Ina maana utashinda.Kwanza Hao watakaokuibia ni wakinanani na kwasababu gani?

Msimnajipata Kuwa UKAWA mmejipanga kisawasawa na kwa upande wa wanausalama mmpo vizuri.Sasa Kama mmejipanga vizuri na wanausalama wa UKAWA wapo imara kwanini uibiwe kura?Basi hamna wanausalama UKAWA?

Hivi Lowassa kwa usanii huu unaoufanya kabisa unaamini utakuwa rais wa Tanzania baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu Oktoba 25 Mwaka huu? Pole sana Lowassa kwasababu huwezi kushinda urais kwa Sababu haupo Siriazi na urais ,unafanya mzaa na usanii wa wazi kabisa.

Lowassa jiulize kwanini Hilo limetokea uliopoanza kuongea wananchi walianza kuondoka Hawakutaka kuusikiliza .Jibu ni Jepesi walilokuwa wanalitajarajia  kutoka kwako hawajalipata  maana umewaambia wakasome Kwenye Mtandao.

Kumekuwa na Madai Kuwa Afya ya Lowassa sio nzuri ,licha yeye Mara kwa Mara amekuwa akikanusha taarifa hizo. Sasa kwa kitendo hicho cha Leo cha kushindwa kusoma hotuba kwa kisingizio cha muda kumalizika.

Je hatuoni hii ni mbinu iliyotumiwa na viongozi wa UKAWA ya kumuepusha Lowassa asisome hotuba hiyo kwasababu hawezi kusimama jukwaani muda mrefu ? Lowassa unatatizo.

Mungu ibariki Tanzania

0716 774494
Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
29/8/2015

No comments:

Powered by Blogger.