PROFESA MUHONGO UZI NI ULE ULE
Na Happiness Katabazi
ASANTE SANA RAIS JOHN MAGUFULI "NGOSHA" , kwa Kumteua msomi Professa Sospeter Mwijarubi Muhongo Kuwa Waziri wa Nishati na Madini Leo wakati Ulipokuwa ukitangaza Baraza Lako la mawaziri.Ngosha Una akili sana.
Itakumbukwa Kuwa Profesa Muhongo alijihudhuru nafasi ya waziri wa Nishati na Madini Katika serikali ya awamu ya nne iliyokuwa ikiongozwa na rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
Kwa lugha nyepesi Profesa Muhongo alikuwa ni muathirika wa siasa za Chuki, uzushi zilizokuwa zimetamalaki Katika Utawala wa serikali iliopita lakini Ikulu kupitia vyombo vyake ilifanya uchunguzi wake kuhusu Muhongo na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eliachim Maswi ambaye kwasasa ni Katibu Tawala Mkoa wa Manyara kama walikuwa wamehusika Katika skendo ya Escrow na uchunguzi ulionyesha walikuwa hawajahusika licha baadhi ya wanasiasa uchwara ,wafanyabiashara na wananchi walimshikia Bango Kuwa ni fisadi kuusikia.
Siri Siri Muhongo licha ya kupakwa matopwe sana lakini kuna baadhi ya watu ambao hatuna ukaribu naye na wala hatujawahi kuonana naye tulisimama kidete hadharani kumtetea Kuwa anasingiziwa na tulitishiwa lakini mwisho wa siku ripoti ya Ikulu ilikuja kumsafisha na hivyo kumuweka Kwenye rekodi safi na ikawashushua wazushi.
Wito wangu wa Muhongo, kwanza wasamehe watesi wako wote waliokuzulia Janga la Escrow Kwani uteuzi huu ni Ishara kwamba ni bakora ya Mungu dhidi ya watesi wako.
Nenda wizarani kafanye kazi uliyotumwa na rais wako na siyo vinginevyo.
Katumie taaluma ,maarifa yako ,busara na Hekima kuiongoza Wizara hiyo.
Naamini jungu lile la ESCROW ulilopigwa licha lilikuumiza pia limekupa Mafunzo Fulani.Hao ndiyo Binadamu uwaelewe na uwavumilie ila Ishi nao kwa makini.
Sasa wale wachawi "wazushi" mlimzushia Muhongo kuhusu Escrow hadi aka chafuka na akajiudhuru kama mnaubavu wa kufanya uzushi wenu katika Utawala huu wa NGOSHA zusheni tena tuwaone .
Na kitendo hiki cha Magufuli kumteua Muhongo kushika tena nafasi hiyo ya Waziri wa Nishati na Madini kimetoa funzo .
Funzo la kwanza watesi wa Muhongo watambue wao sio Mungu wa kuweza kuzuia mipango la Mungu kwa mtu wake .Watambue Wao binadamu wanapanga yao na Mungu anapanga yake.Jiepusheni na uzushi maana mwisho wa ubaya ni aibu na leo kwa Magufuli kumteua Muhongo kushika tena wizara ya Nishati na Madini ni aibu kwenu.
Rais Magufuli aogopi maneno ya watu na amesikiliza kilio cha baadhi ya watu ambao walikuwa wanapenda sana Muhongo arudishwe katika wizara ile ya Nishati na Madini na mimi nikiwa ni mmoja wao kwasababu Muhongo ni miongoni mwanasiasa wachache sana ambao ni wakweli,wawazi ,wenye misimamo isiyoyumba na ni wazalendo.
Kila la kheri Profesa Muhongo Mungu akutangulie.
Chanzo: Facebook.Happy Katabazi
Blogg:www.katabazihappy.blogspot.com
10/12/2015.
No comments:
Post a Comment