MAKONDA TULIA UNYWE DAWA
Na Happiness Katabazi
WIKI Iliyopita Mkuu wa MKoa wa Dar Es Salaam ,Paul Makonda Mara Kadhaa amenukuliwa Katika vyombo Vya Habari akisema yeye amejitahidi kadri ya uwezo wake Kupambana na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo Shisha lakini Jeshi la Polisi limekuwa likisita kuwachukulia Hatua wahusika.
Makonda alitoa tuhuma hizo Mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Katika Uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa upatikanaji wa Umeme Katika Mkoa wa Dar Es Salaam dhidi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda .
Kuwa Mara kwa Mara amekuwa akimuuliza Sirro Kuwa Mbona wananchi wanampatia taarifa wauzaji wa Shisha bado wanatamba na Sirro Amekuwa akimjibu Kuwa Hali ni shwari .
Makonda aliwashushia tuhuma Makamanda hao Wawili Wamelambishwa ile hongo aliyoikata kutoka kwa wafanyabiashara wale wa Shisha ndiyo maana wanasita kuwachukulia Hatua wauzaji wa Shisha.Shisha imepigwa marufuku kutumiwa hapa nchini.
Mkuu Huyo wa Mkoa Alidai kuna wafanyabiashara 10 bila ya kuwataja majina walimfuata wakitaka Kumhonga Sh.Milioni 50 kila mwezi ,lakini alikataa.
Hata hivyo Waziri Mkuu Majaliwa alimtaka Makonda aache Kulalamika badala yake akatekeleze maagizo yanayotolewa na viongozi wa juu wa serikali.
Kauli hiyo Makonda dhidi ya makamanda hao wa polisi imeibua mjadala katika jamii huku wengine wakitofautiana na yeye vikali.
Kwa upande wa Jeshi la polisi Makao Makuu Kamanda Robert Boaz mwishoni mwa wiki alizungumza na umma na akasema taarifa hizo za tuhuma za Rushwa dhidi ya makamanda wa jeshi Lao wamesikia na jeshi hilo limefikia uamuzi wa kuanza kufanyia uchunguzi tuhuma hizo ( Inquiry).
Kwanza Napongeza Hatua hiyo ya Jeshi la Polisi kwa uamuzi huo wa uweledi wa kuchukua Hatua za kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo zilizotolewa barabarani yaani Kwenye vyombo Vya Habari na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam ,Paul Makonda.
Aidha pia Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai 2002 , kinatoa mamlaka kwa Ofisa wa Polisi kuhoji mashahidi,watuhumiwa au mtu yoyote ambaye Polisi inaitaji kupata maelezo yake kutokana na tuhuma au uchunguzi wa jambo lolote .
Hivyo Jeshi la Polisi wapo sahihi kufanyia uchunguzi taarifa hizo zilizotolewa na Makonda wiki iliyopita.
Kifungu cha 7 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 ,kina Mtaka mtu yoyote ambaye anafahamu taarifa za kutendeka au kutaka kutendeka kwa tukio ka Uhalifu apeleke taarifa hizo Katika mamlaka husika za kiserikali ili zifanyiwe Kazi na akishindwa kufanya hivyo atashitakiwa kwa kosa lolote chini ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ya Mwaka 2002.
Tumuulize Makonda yeye Kabla ya ile Sherehe ya Uzinduzi wa Mradi wa umeme aliyotoa tuhuma hizo nzito dhidi ya Makamanda Hao wa Polisi alishazipeleke taarifa hizo za watu wale walifika ofisini kwake kutaka Kumhonga Fedha Katika mamlaka gani za kidola?
Makonda ana anakofia Ya Mkuu wa Mkoa wa Dar e Salaam na kofia ya Pili ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambaye Mkuu wa Mkoa husika ndiyo Mwenyekiti , baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo ni Jeshi la Ulinzi la Wananchi ( JWTZ), Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa ( TISS) ,TAKUKURU ,Uhamiaji ,Magereza na vyombo vingine.
Namuuliza Makonda alivyokuwa akiendesha vikao vya Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwa na kofia ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo alishawahi kuwasilisha taarifa zake hizo za wafanyabiashara 10 aliyodai eti walifika ofisini kwake kutaka Kumhonga Fedha kila mwezi ili aachane na mapambano ya Shisha?
Makonda uliwai Kuwasilisha taarifa Katika Kamati ya Ulinzi na Usalama kuwa Kamanda Sirro anasita kuchukua Hatua dhidi ya wafanyabiashara hao na uenda ile hongo iliyokataa kutoka kwa wafanyabiashara wale wa Shisha uenda imewapitia?
Makonda uliwahi kuwasilisha mezani taarifa Katika Kamati hiyo unayoiongoza Kuwa Jeshi la Polisi kupitia RPC- Sirro amekuwa akikupa taarifa za uongo kuhusu Biashara ya Shisha?
Maana kupitia mahojiano yako na Redio Clouds umesikika ukisema Mara kadhaa umekuwa ukipewa taarifa na Jeshi la Polisi kupitia Kamanda Sirro Kuwa Shisha Hakuna Dar Es Salaam na kwamba Jeshi la Polisi lomefanikiwa Kudhibiti Shisha wakati wewe Makonda umekuwa ukipewa taarifa na wananchi wanaoichukia Shisha Kuwa Shisha ipo ,na ukaenda kukamata na vielelezo unavyo .
Kama uliiwasilisha Taarifa hizo katika Kamati ya Ulinzi na Usalama Tueleze. Taarifa hizo zilijadiliwa ?
Na wajumbe wa Kamati hiyo walijibu nini ulivyosasilisha taarifa hizo walikujibu nini ?Je wajumbe wa Kamati Walisema hawatafanyia Kazi ?Au Walisema watafanyia kazi?Walikupa tarehe ya mwisho ya kujifanyia Kazi 'deadline'?
Nafahamu Hilo Swali kwa mwana Usalama aliyefundwa akafundika hawezi lijibu hadharani ila kwakuwa wewe Makonda ni Mlopokaji na hufahamu majukumu ya kofia zako zote mbili unaweza ni jibu hilo swali.
Au Makonda ndiyo ameamua kuleta Habari zako za Kimbea ,majungu ,kujipendekeza Mbele Waziri Mkuu Majaliwa ?Ili uonekane wewe ni mfanyakazi bora kuliko Jeshi Polisi kupitia makamanda wao Sirro na Kanda ? Upuuzi mtupu.
Je tukisema wale wahongaji hawakurudi tena kukuletea ile Rushwa ndiyo maana umeamua Kusema taarifa hizo hadharani? Mbona walivyokufuata ofisini kwako hukujitokeza hadharani kutuambia kuna wafanyabiashara 10 wa Shisha wamekufuata ofisini kutaka wakuhonge kiasi hicho cha Fedha na ukakataa?
Kama uliamua kunyamaza kimya wakati walipokufuata kutaka kukuhonga Fedha kama unavyodai ,Tukuulize ni kitu sasa kimesukuma utoboe Siri hiyo hadharani hivi sasa?
Hivi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa hasa ya Mkoa wa Dar Es Salaam, Ina uwezekano mkubwa ikawa imefungwa CCTV kamera.
Hivyo ni vyema Makonda atoe ushirikiano atakapotakiwa kufanya hivyo aseme Hao wafanyabiashara wa Shisha walikuja Lini ofisini kwake , ili watu wanaohusika na CCTV Kamera waweze kuwabaini kwa sura ikibidi na mazungumzo Yao ili ithibitike ni kweli walifika ofisini wake?walitaka Kumhonga kiasi hicho cha Fedha ?Na Hao watu 10 wasakwe wako jiwe waseme ni kweli walitaka Kumhonga Makonda kama Makonda alivyodai Mbele ya Umma?
Aiingi akilini Mkuu wa Mkoa mzima anasema wafanyabiashara Hao haramu eti walifika ofisini kwake , anawafahamu kabisa ni wafanyabiashara haramu ,.
Akakaa na kufanya nao mazungumzo ofisini kwake hadi wakamtajia na kiasi cha fedha watawachmpa halafu yeye Mkuu wa Mkoa ambaye lazima Atakuwa na walinzi ashindwe Kuwaeleza walinzi Hao wawakamate wafanyabiashara Hao ambao yeye amejinasibu Kuwa anawajua ni wanafanya Biashara hiyo haramu ya Shisha.
Na katika mtazamo wa yeye kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar Es Salaam, Hilo suala la yeye kutaka kuhongwa kiasi hicho cha Fedha na wafanyabiashara hao haramu 10 Narudia tena kumuuliza aliwasilisha mezani taarifa hiyo ?
Inaoenekana Makonda alikuwa nania ovu ya kutaka kuzipokea maana kama alikuwa hatamani kuzipokea hizo Fedha kwanini hukuwasilisha taarifa hizo za yeye kutaka kuhongwa Kwenye Kamati ya Ulinzi Usalama ya Mkoa ambayo yeye ndiyo Mwenyekiti?
Kwanini umesubiri Waziri Mkuu aje Kwenye sherehe za Uzinduzi wa Maboresho Upatikanaji wa Umeme Dar Es Salaam ,ndiyo useme Hilo?
Makonda kijana mwenzangu umeacha Mashaka mengi sana Katika hili kwa sisi wananchi wako wa Mkoa wa Dar Es Salaam unaotuongoza .
Umeonyesha hujui wajibu wako kwasababu wewe Ndiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na wewe ndiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo .Hufahamu sehemu ya kutoa taarifa au kushitaki ?
Unasubiri shughuli za uzinduzi wa mradi maboresho ya umme ndiyo ushitaki hadharani mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa? Ni dhahiri hutufai maana tayari umeishapata doa.
Nina mashaka na uwezo wake wa kiutendaji na uwezo wake wa kuchanganua mambo.Makonda umetuacha na maswali kama anajua majukumu yake ya Ya kofia ya Mkuu wa Mkoa na kofia ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.
Nashawishika kusema kuwa Makonda kama RC ,Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa ,akiwa pia ndiyo anayesimamia utendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam hafahamu majukumu yake tena hata kwa wale watendaji wake wa Moja kwa Moja yaani wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Na Pia Makonda kupitia matamko yake mbalimbali kuhusu sakata hilo ameonyesha hafahamu Maadili ya Kazi yake Kwani kama Angekuwa anajua Maadili ya kiongozi mwenye hadhi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa asingethubutu kupayuka Yale aliyoyatamka hadharani dhidi ya Kamanda Sirro na Kaganda pia asingethubutu kwenda Redio Clouds kwenda kuzungumzia ule upuuzi aliouongea kupitia Redio hiyo.
Nasema ni upuuzi kwasababu Makonda kama Kweli an ajitambua yeye ni nani,ana madarakani siku ile ile aliposikia Waziri Mkuu Majaliwa alivyomshushua mbele za watu kwa kumtaka Makonda aache kulalamika afanyekazi na atekeleze maagizo toka viongozi wa juu, alivyosikia Kamanda Sirro alipozungumza na waandishi wa habari akisema kuwa operesheni ya kukamata waharifu wa makosa ya aina mbalimbali ikiwemo wauza dawa mbalimbali za kulevya imekuwa ikifanyika na inaendelea kufanyika na kwamba majarada ya uchunguzi wa watuhumiwa hao polisi wameyapeleka ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwaajiili ya hatua zaidi za kisheria na tayari na maana polisi hawana mamlaka ya kufungulia washitakiwa kesi za jinai mahakamani mwenye jukumu hilo ni Mkurugenzi wa Mashitaka ( DPP) .
Na ni kweli kifungu cha 9 cha Sheria ya Taifa ya Huduma ya Uendeshaji wa mashauri ya Jinai Na. 27 ya Mwaka 2008 , inasema DPP ndiyo mwenye Mahakama ya Kufungua na kuendesha Kesi za jinai mahakamani kwaniaba ya serikali.
Na aliposikia Jeshi la Polisi Makao Makuu Kupitia Kamanda Robert Boaz Kuwa
Jeshi la Polisi limeanza kufanyia uchunguzi wa shutuma za Makonda dhidi ya Makamanda wake Sirro na Kaganda, RC -Makonda angefunga mdomo wake kwa kunyamaza kimya kimya lakini sijui ni Utoto ,ulimbukeni akaendelea kuongea tu Mara kuhojiwa Redio Clouds Mara kunukuliwa na Gazeti moja akitamba Kuwa ataendelea kuwachongea. Aibu gani hii jamani!
Ni wakati mwafaka wa Makonda arudishwe darsani ili akapewe mafunzo yatakayomwezeka kufahamu majukumu yake ya Uenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na majukumu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Waswahili wanasema Dalili za Mvua ni Mawingu. Hivyo kama Leo hii Mwenyekiti Huyo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama RC Makonda ameshindwa kutumia majukwaa sahihi ( Proper Forum) yakupeleka malalamiko yake badala yake anatumia vyombo Vya Habari na kusubiri kudandia mkutano wa Waziri Mkuu kulalama tena mambo mengi ambayo ambayo yanapandikiza Chuki baina ya wananchi na Jeshi la Polisi Kuwa Jeshi la Polisi ndiyo linalowalea wauza Shisha kwasababu ha liwachukulii Hatua basi ipo siku Makonda Atakuja kuropoka mambo Siri ya vikao Vya Kamati ya Ulinzi Usalama kupitia Vyombo Vya Bahari kwa Lengo la kutaka kujionyesha yeye ni mchapakazi kuliko watumishi wengine wowote .
Na ushahidi ni Yale mahojiano aliyoyafanya a Redio Clouds ambayo Clip yake ninayo ambayo Makonda kwa kinywa Chake anamtuhumu Sirro ambaye ni mjumbe wake wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Kuwa amekuwa alimpa taarifa za uongo kuhusu Biashara ya haramu ya Shisha.
Sasa kama Mwenyekiti wa Kamati hiyo analalamikia mjumbe wake wa Kamati hiyo hadharani tena Kwa zaidi ya Mara Moja , ni wazi RC Makonda Hana Imani na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam ambalo ndilo Hilo Hilo Askari wake wanamlinda nyumbani anakoishi na ofisini.
Lakini hata kama ni kweli Kamanda Sirro alikuwa akikupa taarifa za uongo kuhusu Shisha ,Sirro na wewe Makonda wote ni wateule wa Rais John Magufuli .
Je Makonda ulishawahi pia kwenda kumweleza Rais Magufuli,au boss wa Sirro ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Kuwa Sirro amekuwa akikupa taarifa za uongo na auridhishwi na Utendaji wake?
Makonda umedai Jeshi la Polisi limekuwa likisita kuchukulia Hatua wafanyabiashara haramu ya dawa za kulevya, hivyo Jeshi la Polisi Leo Hii likiibuka na takwimu za Kuonyesha Jeshi Hilo limekuwa likichukua Hatua Kabla hata ya wewe kufikiri wa au wewe kufikiria utakuja Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam sura yako Utaiweka wapi?
Maana Mimi ni shahidi mahakamani nimekuwa nikishuhudia Mkurugenzi wa Mashitaka aliwashitaki watuhumiwa mbalimbali wa makosa ya dawa kulevya ambao Chanzo cha washitakiwa Hao kushitakiwa ni walidaiwa Kutenda makosa hayo na walikamatwa na Jeshi la Polisi.
Elewa Uhalifu ulikuwepo toka enzi na Enzi na serikali ya awamu ya tano imeukuta na itauacha na haiwezi kuukomoesha maana kila kukicha wahalifu wanabuni mbinu mpya za kufanya Uhalifu.
Hivyo hata wewe Makonda Biashara ya dawa kulevya umeikuta hapa Dar Es Salaam na Duniani kwa ujumla.
Usijidanganye Huna Nguvu wala mamlaka ya Kupambana nayo kwasababu Huna Mafunzo ya kutambua hizi dawa za kulevya, kukamata wenye hiyo taaluma wapo ndani ya Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Kuthibiti Dawa za Kulevya Chenye Ofisi zake Barabara ya Kilwa Dar es Salaam.
Umejitapa kupitia Redio Clouds Kuwa umekamata dawa za kulevya aina ya Shisha . Mina Kuuliza una Hakika gani hizo ni dawa za kulevya?
Hivi hizo unazodai ni Shisha ulizokimata zikichukuliwa zikapelekwa kwa wataalamu wakazikagua kitaalamu Kisha wakaja kutoa ripoti Kuwa hizo siyo Dawa za kulevya utasema nini?Acha wenye taaluma za Kupambana na dawa za kulevya wafanyakazi Yao.Wewe taaluma hiyo Huna.
Mkuu wa Mkoa Mzima unaacha kushughulika na mambo makubwa makubwa unaamua kujigeuza 'korokoroni 'unaenda kukamata Shisha na vifaa Vya Kuvutia Shisha wakati Polisi wenye vyeo Vya chini wa kufanyakazi ya ukamataji wapo na wala hawakueleza wameshindwa kukamata hivyo wa naomba utasaidie.
Hivi Hao wahalifu wa Shisha unaowafuata hadi Kwenye vijiwe vyao Vya Kuvuta Shisha na bangi wakikumwagia Kinyesi usoni utalia na nani?
Fanyakazi yako uliyotumwa na vyombo Vya Ulinzi na Usalama ambayo ndiyo wenye taaluma ya Ulinzi na Usalama wafanyakazi Yao kwa Uhuru .Heshimu wakubwa wako ,Chagua matamshi ya kuzungumza Mbele ya hadhara dhidi ya viongozi wenzako.
We bado ni kijana Mdogo sana bado unaitaji kulelewa na wanasiasa wenzako,wanausalama hivyo haina maana wewe kujiingiza Katika msuguano na Jeshi la Polisi kupitia Kamanda Sirro na Kaganda. Kushangaa siku Moja kitendo hicho kikaja kukugharimu.
Aidha Makonda kaa chini ujitathimini na utafakari hicho ulichokifanya ambacho kutokana na matamshi yako ambacho kimezusha mjadala na kufanya watu Tutulie Mashaka uwezo wa Utendaji wako .
Kisha wewe binafsi ujiulize Je ulikuwa sahihi wakati ukifanya hayo uliyoyafanya kwa mujibu wa maadili ya kofia zako mbili za kimadaraka? Kisha ujipime wewe mwenyewe mwisho uchukue maamuzi.
Nimalize makala hii kwa kukushauri Makonda Kuwa ' Usiwe na haraka kuliko Upesi'. Mji huu wa Dar Es Salaam Una Masharti hadi ufanikiwe ,sio kuvaa Masharti /Suti ukajiona wa maana . Acha tabia na kutaka kujipatia Umaarufu wa chee kwa mambo yasiyo na tija .
Naomba kutoa hoja.
Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.com
0716 774494
21/11/2016
No comments:
Post a Comment