Header Ads

WANAWAKE NA DAWA ZA KUBANA UKE Mhhhh!

WANAWAKE NA DAWA ZA KUBANA UKE Mhhhh! 
Na Happiness Katabazi
NCHI ya Tanzania ni miongoni  mwa nchi ambazo zina baadhi ya wananchi wanaugua aina Mbalimbali ya ugonjwa wa Kansa maarufu Saratani.

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi Mbalimbali za Kimataifa zimejitoa kimasomamaso Kupambana na ugonjwa huo ikiwemo kutoa elimu ya ya kujikinga na ugonjwa Huo,kuamasisha watu wajitokeze kwa Wingi Kwenye  Vituo husika kupimwa ili wajijue mapema kama wana dalili au wameishapata maambukizi ya ugonjwa wa Kansa au laa.

Kutoa   elimu kwa waathirika wa ugonjwa wa Saratani Kuwa  wanatakiwa wafanye nini,nanini wasifanye na ni wapi wanaweza kwenda kupata matibabu.

Lakini kadri siku zinavyozidi kwenda baadhi ya Watanzania wenzetu hususani wanawake wenzangu wanaona jitihada hizo ni sawa na 'kumvalisha Mbu miwani'. Tena hawataki kuzisikia na wameweka masikio pamba.Inatisha sana.

Makala yangu ya Leo nitazungumuzia jinsi baadhi ya wanawake na wasichana walivyoamua kutumia baadhi ya Madawa ambayo mengine hata hayajaandikwa   tarehe Kuwa yalitengenezwa lini,wapi, mwanamke wa aina gani anatakiwa atumie na atumie kwa muda gani na dawa hiyo itamalizika muda wake wa matumizi lini?

Dawa hizo ambazo ni Sabuni  aina Misk Attahar Soap, Misk ambacho kimetengenezwa kwa mtindo wa kimiminika ambacho kimehifadhiwa Katika kichwa ambacho hata jina halijaandikwa, wala il itengenezwa  lini, kiwanda gani , wapi na muda wake wa matumizi unaisha lini?

Ieleweke wazi makala hii haimaanishi Kuwa nimethibitisha matumizi ya dawa hizo nimezigundua  kuwa zina  madhara.Hapana. 

Lengo la makala hii ni kuziuliza  mamlaka husika za serikali je, zinafahamu uwepo wa dawa  hizo?Je serikali inafahamu Kuwa baadhi ya wananchi wake hasa wanawake ndiyo watumiaji wa Kuu wa dawa hizo?

Je dawa hizo ni salama na Hazina viambata vyenye sumu ambazo mwisho wa siku watumiaji watakuja kudhurika?

 Je Tunaruhusiwa kuzitumia dawa hizo bila kuzitilia Mashaka Kuwa mwisho wa siku zinaweza kuleta madhara kwa wanawake Kama Kansa ya shingo ya kizazi ,ngozi na madhara mengine?

Kwa Miezi Sita sasa, nilipata fursa ya kuzungumza na wanawake mbalimbali na wasichana ambao wametumia dawa hizo.

Pia nilipata fursa ya kuzungumza na wauzaji wa dawa hizo kwa Nyakati tofauti ambao kila mmoja wake alinipa maelekezo ya jinsi ya kuzitumia na kunithibitishia Kuwa ni kweli ukitumia dawa hizo sehemu ya uke wa mwanamke  ina bana yaani inageuka Kuwa ndogo.

Wauzaji wa dawa hizo walinielekeza matumizi ya dawa hizo Kuwa hiyo Sabuni, mwanamke ambaye siku Tatu Kabla  ya  kwenda kukutana  kimwili na mwanaume  ,basi mwanamke Huyo anatakiwa akishamaliza kuoga ananawaa sehemu zake za Siri kwa kutumia sabuni hiyo ya Misk Attahar Soap.

Baada ya kunawa sabuni hiyo, misuli yake  ujibana na kufanya eneo lake la uke la mwanamke   kuonekana ni dogo na hivyo siku ya kukutana na mwanamme kimwili;

Mwanaume  Huyo bila kujua nini mwanamke Huyo alitumia Kabla ya kukukutana nae, Kuwa mwanamke huyo jinsia yake ya kike ni nzuri Kwani imebana na watoto wa mjini usema ' Kitu Mnato'', na haingiliwi Mara kwa Mara na wanaume Kumbe mwanamume huyo  Tayari kaishaingizwa 'Chaka'.

Kichupa Chenye maji mekundu, hicho kichupa kwa mujibu wa watumiaji na Wauzaji wamenieleza Kuwa ,maji maji hayo mwanamke hupaka Katika sehemu zake za Siri ili aweze kuondoa harufu Mbaya na pindi apakapo dawa hiyo unukia vizuri na endapo akikutana na mwanamke kimwili,inamshawishi mwanaume Huyo Kupenda kuendelea kufanya tendo Hilo zaidi na zaidi na mwanamke huyo.

Baadhi ya wanawake  wengine Utumia majani ya chai kubana eneo Lao la uke.  Wamenielekeza Kuwa wanachukua majani ya Chai mengi wanayachemsha Kwa kuweka kiasi kidogo Cha maji,majani hayo ya chai ya nachemka hasa, yakishachemka uyaipua na kuyaacha ya Poe.

Nakisha kuyachuja halafu wanayachukua Yale majani wanayaweka Kwenye chupa safi Tayari kwaajili ya matumizi.

Wamenielekeza Kuwa mtumiaji ambaye ni mwanamke anapotaka kwenda kukutana kimwili na mwanaume siku mbili Kabla, basi ulazimika Mara mbili kwa siku kunawa Katika sehemu zake za Siri Maji Yale yaliyochemsha kwa majani ya Chai ambayo uwa ni makali sana huwezi kuyaweka mdomo na hatimaye sehemu yake ya uke ubana na Kuwa ndogo.

Kuhusu hivyo vichupa vitatu vilivyopangana  hivyo kwa mujibu wa wauza duka na watumiaji wanasema majimaji hayo yametengenezwa na zao la  Mchaichai, na Utumiwa na mwanamke Yule ambaye sehemu zake za Siri zina majimaji hivyo , aina hiyo ya dawa inayotengenezwa kwa mchaichai ufanya sehemu zake za Siri mwanamke Huyo Kuwa kavu.

Na kichupa hicho cheupe ambacho kina Maji mazito meupe ambacho hakijaandikwa hata jina ,tarehe ambayo ingeonyesha kimetengezwa wapi na lini ambacho nacho  uitwa Misk, ambacho mwanamke anayetaka kwenda kukutana kimwili na mwanamume saa mbili Kabla  anapaka Katika sehemu yake ya uke tone Moja Kisha avaa  nguo anaenda zake kukutana kimwili na mwanaume Huyo.

Na baadhi ya watumiaji niliongea nao kwa Miezi Sita sasa wameniakikishia Kuwa ni kweli dawa hizo ukizitumia zinabana misuli ya uke na mwanamume uona mwanamke Huyo haingiliwi Mara kwa Mara na wanaume.Kumbe wizi mtupu.

Nimefanikiwa kupata aina hizo za dawa licha kuna baadhi ya wanawake wanaofanya Biashara za nguo kutoa China kuleta Tanzania ,pia wameniambia kuna kifaa kingine ambacho hapa nchini wakikileta kinauzwa Sh.35,000.

Hicho kifaa mwanamke anayetaka kwenda kukutana na mwanamume siku Moja Kabla ukiingiza ndani ya uke kifaa hicho Kwa dakika Kadhaa na Kisha ukitoa na baada ya muda uke wa mwanamke Huyo unakuwa umebana sana.

Lakini hata hivyo Hao watumiaji wa dawa hizo Kwa Nyakati tofauti pamoja na maswali mengine niliyokuwa nikiwauliza ,nilipokuwa nawauliza je tangu walipoanza  kutumia dawa hizo zimeweza kusaidia kuwazuia Waume, wapenzi wao wasiwasaliti Katika mahusiano Yao ya kimapenzi?

Wengine walipandwa na jazba na Kusema licha ya kubana uke wao kwa dawa hizo ,wanaume wao wamekuwa na mahusiano na wanawake wengine Hali iliyosabisha baadhi Yao HIvi sasa kuacha kutumia dawa hizo Kwani wamenitumia Kwa Lengo la Kuwauliza Waume zao lakini Waume zao hawatulii.

Na kwamba walichoamua hivi sasa Fedha zao wanazimalizia Katika kujipambana,kufanya vitu vinavyo starehesha nafsi zao.Lakini Hakuna hata mtumiaji mmoja aliyeniambia amewahi kupata madhara kutoka na matumizi ya dawa hizo, ila hawafahamu siku za usoni uenda wakaja kupata madhara.

Wanawake mnatumia dawa hizi naomba mnisamehe sana kwa haya nitakayoyasema Kama yatawakwaza.Maana miili ni yenu na Fedha za kununulia dawa hizo ni Zenu.

Minajiuliza HIvi hawa wanawake wenzangu ambao wameamua kujilipua na kuanza kutumia dawa hizo ,hivi wanachokitafuta hasa ni kitu gani?

Maana baadhi ya wanawake kwa makusudi tumeamua kuwa 'Maalbino wa Kutengenezwa' yaani kujipaka mikorogo ambayo inachubua ngozi na kutuaribu vibaya sana?

TDFA, Madkatari kila kukicha Maskini ya Mungu wanaelezea madhara ya mikorogo hatusikii na tunawaona wanaowakataza msitumie   mikorogo ni wanasesere na wa nawaonea wivu.

Minasema HIvi hipo siku tutawauguza Maradhi yasiyotibika kutokana na hayo matumizi ya mikorogo na Madawa ya kubana uke  kwa Lengo la kuwaahada  wanaume.

Hivi minikiwaita hawa wanaotumia  dawa hizo ni sawa tu na 'majambazi wasiyotumia  silaha' , nitakuwa nakosea?

Halafu ni wanaume gani Hao mnaowaongopea na hayo Madawa? Ni hawa hawa wanaume waliopo Kwenye kizazi hiki Cha kamasi ukipenga kamasi basi kizazi hicho kinasahaulika?

Ndiyo Mnataka Kuwahadaa kimapenzi hawa wanaume ambao Wengi wao hawana fedha, mabahiri na siku hizi wamepachikwa majina haya 'wanaume suruali,wanaume SACCOS  yaani wakopaji ,hawana Fedha' ili wawape Fedha?

Baadhi ya Wanaume wenyewe huko mitaani siku hizi wengine wanakiri kabisa Kuwa Utawala wa Rais Jakaya Kikwete umeweka mazingira mazuri kwa wanawake Kuwa na kipato na wanawake  Wengi hivi sasa wapo  Katika ngazi za uongozi ukilinganisha na Miaka ya nyuma na wengine wapo Kwenye njia Kuu za uchumi na kwamba   wanawake wengi hivi sasa wanafursa nyingi za kujipatia kipato kuliko wanaume?

Hali imebadilika HIvi sasa baadhi ya wanaume ndiyo wamekuwa mstari wa Mbele kutaka wahongwe  Fedha,mali na wasaidiwe na wanawake.

Kabla ya kuandika makala hii pia nilienda Kuwapelekea wataalamu wa Madawa Wawili wazisome dawa hizo na wazielewe, waliniambia watumiaji wa dawa hizo wanachokitafuta watakipata.

Na wakasema hao wagunduzi wa dawa hizo za kubana uke ni kwanini wasingegundua  dawa za kutibu Ugonjwa wa Ebola!.

Na waliitimisha kwa kutaka serikali kupitia dawa hizo nilizozikusanya ikazifanyie utafiti ili mwisho wa siku serikali itoe Matokeo ya utafiti huo kuwa dawa hizo Hazina madhara au zina madhara kwa watumiaji .

Naomba mamlaka husika itoe tamko kuhusu matumizi ya dawa hizo ni haramu au halali.

Na Kama ni haramu basi wale waliokuwa na fikra za kutaka kuanza kuzitumia wasi thubutu kuzitumia.

Na wale waliokwisha zitumia waendelee au wasiendelee kuzitumia na wale wenye hofu ya matumizi ya dawa hizo Kuwa ni haramu au siyo haramu ,hofu hiyo iwaondokee.

Mwisho, wanawake mjenge tabia za kujiamini na muondokane na muda wote kuwaza mawazo ya kufanya ngono.

Kuna mambo mengi sana ya kufanya ambayo ukiyafanya kikamilifu na unavyopaswa,mtaondokana na balaa hili la matumizi ya dawa hizo za kubana uke ambao Kwa  vinywa vyenu mmekiri Kuwa licha mmekuwa mkitumia dawa hizo ,wapenzi na Waume wenu wamekuwa wakisaliti mapenzi yenu na mwisho wa siku wanaokuja kupata madhara ya Kiafya ni Nyie na Hao wanaume,wapenzi watawatelekeza.

Leo hii kila kukicha tunasikia Kansa inawashambuliwa wanawake sana.Tujiulize ni kwanini inawashambulia sana wanawake tena Kansa ya shingo ya uzazi?

Isije Kuwa matumizi ya Madawa ya kubana uke yanayotumiwa na wanawake na wasichana nayo yanachangia ongezeko Hilo la maambukizi ya Kansa!

Tubabirike, tuache kuiga na tuache kutumia dawa ambazo mwisho wa siku zinaweza Kuja kuleta madhara Katika Afya zetu.

Wakati mwingine Huwanajiuliza ila sipati Jibu Kuwa HIvi hawa wanawake wanautumia mikorogo Kukoboa ngozi zao wakati mikorogo hiyo imekatazwa na wataalamu , HIvi ni wazima kweli kichwani au ni mahayawani?

HIvi Kama siyo uhayawani ,kutojiamini na kutojitambua ni kitu gani?Wataalamu wa Madawa wakiwemo TDFA msitumie Madawa hayo na Jeshi la Polisi inayakamata hizo cream, lotion, sabuni zenye viambata vya sumu kwasababu singlets madhara hawasikii hawa 'Maalbino wa Kutengenezwa' yaani wanawake wanaopaka mikorogo.

 Mbaya zaidi wanawake wengine ni wasomi,wanaume zao ni wasomi na wana familia zinazowategemea.

Kwa makusudi wanakaidi katazo Hilo la wataalamu na serikali ,ndiyo kwanza wanaenda kununua mikorogo na kuendelea kujichubua ngozi zao.

Mindiyo maana nasema hawa 'Maalbino wa Kutengenezwa' siyo wazima Katika ubongo wao, Kwani wanawake Wengi wanajipaka mikorogo HIvi sasa wameishakuwa watumwa wa poda kama Enjoface,Foundation ambazo ujipaka usoni muda wote ili Kuonyesha umma uso wake una rangi sawa ,Hauna mashimo na Hauna Michilizi yakuonyesha Mishipa ya Damu ambayo Mishipa hiyo uwatoka wanawake wanaozidisha matumizi ya mikorogo.

Fedha yako Mwenyewe  Kwanini uruhusu ikuletee madhara na ikutese? Au watumiaji wa mikorogo ni viziwi hawasikiagi TDFA,wataalamu ,Polisi wakiwa watu wasitu mie mikorogo? Au ni vipofu uwa hawaonagi watumiaji wa mikorogo walivyoonza madhara mbalimbali ikiwemo NGOzi zao kuaribika vibaya, kupata madhara ya Figo?

Bado hamjachelewa,acheni matumizi ya Madawa yaliyokatazwa na mamlaka husika Kwani ipo siku mtalia na kusaga meno. Watafuteni wataalamu wa Madawa watawapatia Madawa mazuri tu yasiyo na madhara Kama Lotion mtapaka na ngozi Zenu zitakuwa nzuri tu na kuondoa mikunjo usoni,alama,ngozi itakuwa nzuri.

Mwanamke Kama ni mrembo ni mrembo tu siyo lazima upake mikorogo ya kujichubua ngozi.  Mbona Mimi napaka Lotion aina ya OLAY TOTAL EFFECTS 7in one na bado nakuwa mwanamke mrembo?

Wanawake jengeni utaratibu wa Kuwa na marafiki madaktari, wataalamu wa Madawa waliobobea ambao watakaokuwa wa nawashauri nini mtumie Katika ngozi Zenu na vitu gani msitumie.

Nawaambia hili Kwani Mwenzenu nilibaini Hilo tangu Mwaka Jana, nina mtaalamu wangu wa Madawa ambaye ni mmiliki wa Madukani Pharmacy , Iliyipo Sinza Madukani, Dk.Kessy ndiyo amekuwa Mshauri wangu mkubwa Katika masuala ya Kutengeneza ngozi kwa kunielekeza kitaaluma .' Maalbino wa Kutengenezwa' . Hamjachelewa ,badilikeni sasa.

Mungu Ibariki Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Oktoba 17 Mwaka 2014.No comments:

Powered by Blogger.