Header Ads

JAJI KESI YA SHEIKH PONDA AJITOA


JAJI RUFAA YA PONDA AJITOA
Na Happiness Katabazi
JAJI Shabani Lila wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, Aliyekuwa amepangwa kusikiliza rufaa iliyokuwa imekatwa na Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu , Sheikh Ponda Issa Ponda, amejitoa kusikiliza rufaa hiyo  kwa maelezo Kuwa Dhamira yake inamfanya ajione hawezi kusikiliza rufaa hiyo. 

Jaji Lila alitoa uamuzi huo mwishoni mwa wiki ambapo alisema Dhamira yake haimtumi kusikiliza rufaa hiyo namba 89/2013 iliyokatwa na Mwomba rufaa (Ponda) dhidi ya jamhuri inayo omba Mahakama Kuu itengue hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Mei 9 Mwaka 2013, ambayo ilimtia hatiani kwa kosa Moja la kuingia kwa jinai Katika Kiwanja Cha Chang'ombe Markaz ambapo ilimfunga Kifungo Cha Mwaka mmoja nje na kumtaka  awe mtunza Amani na raia mwema lakini Agosti Mwaka na alikamatwa na kufunguliwa Kesi ya uchochezi kwa Madai ametenda makosa ya uchochezi wakati Akiwa ndani ya Maandalizi ya hukumu hiyo.

"Kwa Dhamira yangu hainitumi kusikiliza rufaa ya Ponda, nimerudisha jarada la rufaa hii  kwa Jaji Mfawidhi ili aweze kumpamga jaji mwingine wa kusikiliza .....na pia nimelikataa ombi la Wakili wa Ponda, Juma Nassor lilokuwa Linaomba Mahakama hii impange Jaji mmoja atayesikiliza rufaa hiyo ya Ponda na ombi lilonalooamba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia Kesi ya uchochezi iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Ponda  Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro isimame hadi rufaa iliyokatwa na Ponda Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, itakaposikilizwa kuamriwa.

Ponda aliwasilisha mahakamani hapo ombi la Kuomba Mahakama hiyo itoe amri ya Kuzuia Kesi ya ya uchochezi inayomkabili Morogoro ,isiendelee kusikilizwa hadi pale rufaa yake aliyoikata mapema Mwaka Jana ya Kapinga hukumu iliyotolewa Na Mahakama ya Kisutu Mei 9 Mwaka Jana, ambayo ilimtia hatiani Kwa kosa la kuingia Kwa jinai Katika Kiwanja Cha Markas Chang' ombe, ambapo Mahakama hiyo ilimfunga Kifungo Cha nje Cha Mwaka mmoja, lakini Agosti Mwaka Jana, alifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro akikabiliwa na Kesi mpya ya uchochezi na kutenda kosa wakati yupo chini ya uangalizi wa Kifungo Cha Mwaka mmoja nje.

Hata hivyo Wakili wa Ponda ,Nassor alimwambia waandishi wa Habari Kuwa licha Jaji Lilla alikataa ombi lake la kuomba Maombi mawili ya mteja wake yapangwe wa jaji mmoja lakini Jaji Mfawidhi ameyapanga Maombi hayo mawili ya Ponda yaani rufaa iliyokatwa na Ponda na ombi la kuomba Kesi ya Uchochezi inayomkabili mTeja wake mkoani Morogoro, yamepangwa kusikilizwa kwa jaji Mmoja aitwaye Lawrnce  Kaduri ombi la kuomba Kesi ya uchochezi iliyofunguliwa Morogoro dhidi ya Ponda itaanza kusikilizwa Agosti 4 mwaka huu na rufaa yake Ponda itakuja kutajwa tarehe hiyo hiyo.

Mapema Juni Mwaka huu, Wakili Mwandamizi wa serikali Bernad Kongora aliwasilisha pingamizi la awali mahakamani Linaomba Mahakama hiyo itupilie Mbali maombi  hayo ya Ponda yanayo omba Mahakama itoe amri ya usikilizwaji wa Kesi ya uchochezi iliyofunguliwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro ya simama hadi rufaa yake itakapoamriwa kwasababu ombi Hilo linalengo ya kuaribu muda wa Mahakama na halina Msingi.

Chanzo: Gazeti La Tanzania Daima la Jumatatu, Juni 30 Mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.