Header Ads

KWAHERI BARAKA KARASHANI 'KAKA YANGE'


KWA HERI  BARAKA KARASHANI 'KAKA YANGE'
Na Happiness Katabazi
SAA  7:53  Leo mchana Nikiwa nimeshuka kwenye Gari ili niingii kwenye geti la Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo , Dar es Salaam, kwaajili ya kwenda kumtazama Kaka yangu Baraka Karashani ambaye alilazwa Hospitalini hapo tangu mwishoni mwa wiki iliyopita
Nilijikuta napekua simu yangu ya mkononi na ghafla niliona picha ya Baraka Karashani kwenye ukurasa wa Mdogo wangu ambaye ni Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mtanzania ,Patricia Kimelemeta ,Kabla sijaisoma ile picha nikajiridhisha Tayari Baraka ambaye naye alikuwa ni Mwandishi wa habari za michezo na burudani ameishakufa Leo.

Nilifikia uamuzi huo wa kuamini bila kusoma kwasababu Kutwa nzima ya Jana wazazi wa baraka ambao ni ndugu zangu yaani baba yake Mzazi ambaye ni Mwandishi wa Habari Mkongwe nchini, Phili Karashani na Mkewe wote ni ndugu zangu na baraka tumekuwa nae tangu tunasoma hadi Leo  hii kwasababu wote sisi ni Wanyambo tunatokea Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera.

Mama yangu Mzazi ambaye anafanyakazi Katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, Jana ndiyo alinipigia simu mchana kunieleza Kuwa kaka yangu Baraka anaumwa sana na nifanye juu chini niende kumuona.Nilisikitika sana na nilishindwa kwenda kumuona kwasababu nilikuwa natakiwa kuhudhuria vipi id darasani nikasema Leo mchana Kabla sijaenda darasani niende kumtazama Baraka.

Mama yangu Mzazi Leo asubuhi alinisisitiza sana nisiache Kuja kumuona kaka Yangu Baraka kwasababu Ana Hali Mbaya sana na lolote linaweza kutokea. Na akasema tumeweke kwenye Maombi na kwamba yeye Jana alichokifanya aliyoigiza simu Mchungaji Bruno Kinunda wa Kanisa la Elshadai la Boko Basiaya,Dar Es Salaam, ambaye alimuwekea simu Baraka sikioni na Mchungaji Huyo alimwombea Baraka ambaye alikuwa hajitambui.

Jana mchana niliwasiliana  kwa simu NA Mke wa Baraka yaani mama Bonny na kumuuliza Hali ikoje akaniambia Hali ni Mbaya wifi Hana la Kusema na amemwachia Mungu nikamwambia nitaenda kumuona ila nikamtaka asizime simu yake Kwani Tayari nimeisha mwambia Mke wa Mwandishi wa Habari Mahamoud Zuberi yaani Dina Ismail ambaye ni Mwandishi wa habari kuhusu Hali ya Baraka na kwamba watakuja kumuona na kweli Jana nilimweleza Dinna taarifa hizo Na kumtaka  amweleze Mahamoud Zuberi Kwani ni rafiki yake pia, na Kisha nikaipiga rafiki yake mwingine Baraka , Alfred Lucas ambaye ni mwandishi wa habari Mwandamizi wa Gazeti la Jamhuri bila mafanikio Kwani simu yake ilikuwa haipatikani.

Nikampigia tena Mke wa Baraka kumweleza nimemtafuta Alfred Lucas kwenye simu bila mafanikio na yeye akasema yangu asubuhi amekuwa akimpigia simu Mke wa Alfred ( Happiness), simu yake haipokelewi.

Kweli Leo mchana Nikiwa Katika Ofisi Kwangu Chuo Kikuu Cha Bagamoyo ,Mikocheni baada ya kufanya majukumu yangu na kujikuta nikiandika makala Fupi ya Tanzia ya kifo Cha Mwandishi mwingine wa Michezo, Innocent Mnyuku, nikaanza safari ya kuelekea Hospitali ya Lugalo kwaajili ya kumuona Baraka lakini wakati nafika maeneo hayo ya Hospitali ya Lugalo ndiyo nikapata taarifa kwenye ukurasa wa Facebook ya Patricia Kimelemeta Kuwa kaka Baraka amefariki.

Nilinyong'onyea na kuamua kurudi kwenye Gari nakuanza kulia Mwenyewe ,machungu yalipoisha niliishia kujiiambia Kuwa lazima nikubali Kuwa tarehe ya Leo ya Novemba 19 Mwaka 2014 ni siku Mbaya Kwangu na kwa wengine wenye mahusiano na marehemu Baraka na Mnyuku.

Nikapiga Moyo Kondo na nikakubaliana na Hali halisi Kuwa ni kweli Baraka amefariki Dunia.

Nimeanza kumfahamu Barakawakati akisoma shule ya Msingi,sekondari, shule,kufanyakazi ya uandishi wa Habari Katika Gazeti la Dimba na Mtanzania.

Licha Baraka alikuwa na elimu ndogo ,Baraka alikuwa Akizungumza Lugha ya Kiingereza  kwa ufasaha kuliko waandishi Wengi wakiwemo waandishi wa Habari za Michezo wakati huo.

Nje ya uandishi wa Habari za Michezo Baraka,amekuwa akifanyakazi za Puplic Relation officer Katika maeno mbalimbali .

Namfahamu vizuri sana Baraka.Baraka Umeniuma sana, umefariki wakati watoto wako wakiwa wana umri Mdogo wanakutegemea. Umemuacha peke yake mkeo ambaye Mimi nilishiriki ku kushinikiza Uishi nae NA Kisha mkaja Kufunga ndoa Kwani ulikuwa unasitasita kutaka kukataa kuishi Kama Mke na mume Mke ambaye Kumbe Leo hii Katika ugonjwa amekusitiri.

Mabaya uliyoyafanya hatutayafuata,mazuri uliyoyaacha tutafuata.Utakumbukwa sana  Na kaka yako Magezi, Kagina, Koku,Bahati.Baba yako Mzee Phili Karashani na mama yako, mjomba wako Thadeo Katabazi ambaye ni Baba yangu Mzazi ambaye ilipenda kumuita jina la ' Babu Zungurusha' kwasababu Baraka ,Mzee Karashani, Kagina na walikuwa wakipenda kwenda Kunywa Pombe kwenye Grocery  iitwayo kwa 'Rose' , wakazi wa Sinza C, Mwenge Kijijini, Uwanja wa Fisi , wapata vileo,wanahabari wenzio, na vilivyo kuwa Vyanzo vyako Vya Habari Enzi ukiwa Mwandishi wa Habari yaani aliyekuwa Katibu wa Timu ya Simba, Michael Wambura, Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo Ally Choki.

Baraka Katika Maisha yake alikuwa akiniambia alikuwa akimpenda sana mwanamuziki wa muziki wa dansi Ally Choki na Michael Wambura na Kama dada wa Harusi ya Baraka , nakumbuka Wambura alitoa mchango mkubwa ikiwemo suti ya Harusi alilovaa baraka Katika siku ya Harusi yake ambayo tulisherehekea Katika Sisimizi Bara ambayo ,Bara hiyo imekufa HIvi sasa.

Mungu aiweke roho ya marehemu Baraka mahali panapostahili.Tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi.Hatuwezi kupingana na uamuzi wa Mungu kwasababu uamuzi wake haukatiwi rufaa.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Novemba 19 mwaka 2014.No comments:

Powered by Blogger.