Header Ads

KWELI INNOCENT MNYUKU 'CHINGA' AMEFARIKI
KWELI INNOCENT  MNYUKU 'CHINGA' AMEFARIKI
Na Happiness Katabazi

NOVEMBA 19 Mwaka 2014 saa 5:11 asubuhi, Nikiwa ofisini Kwangu katika Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Mikocheni Dar Es Salaam,  nikiifungua page yangu ya Facebook ndiyo nikakutana na taarifa ya Tanzia ya kifo Cha Mwanahabari ,Innocent Mnyuku ambayo imewekwa kwenye ukurasa wa mwanadishi wa Habari, Albert  Kawogo.

Nilishikwa na butwaa nisiamini mapema taarifa hiyo na Kuishia kuchangia Katika taarifa hiyo kwa kumwambia  Kawago  Kuwa sina  utani naye lakini baada ya kuendelea kusoma maoni ya watu mbalimbali katika tanzia ile iliyokuwa na picha ya Mnyuku, ikabidi nikubali Kuwa kweli Mnyuku 'Chinga' kafariki Dunia.

Pole sote tulioguswa na msiba huu kwa njia yoyote ile.Pole pia familia yake na wazazi wake.

Binafsi ni miongoni mwa waandishi wa Habari ambao tulifanyakazi  na marehemu Mnyuku Kati ya Mwaka  2000-2003 Katika Gazeti la Mwananchi Enzi hizo Gazeti la Mwananchi Ofisi zake Zikiwa Katika Jengo la CCM Mkoa wa Dar Es Salaam.

Mnyuku alikuwa ni mwanadishi wa Habari za Michezo pamoja na aliyekuwa Mkuu wake wa Kazi ambaye kwasasa ni Marehemu Conrad Dastan 'Kiona Mbali ' au Mzee wa Kamachumu na Charles Mateso.

Mimi Nikiwa Mwandishi wa Habari ngumu ' Hard News' ambaye nilikuwa nawajibika kwa waliokuwa wahariri wangu Revocuts Makaranga ambaye kwasasa ni Mhariri  Mwandamizi  katika Kampuni ya New Habari, na ambaye alinipachika mimi jina la Nyambizi, Muhingo Rweyemamu ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni , Danny Mwakitereko, Theophil  Makunga.

Hata baada ya Mimi na Mnyuku kuama Gazeti la Mwananchi na kwenda kufanyakazi Katika magazeti mengine, tulikuwa tukiendelea kuwasiliana na Mnyuku kupitia Facebook na kutaniana .

Mnyuku Kama Mwandishi  wa Habari za Michezo Enzi hizo nitathamini mchango wake wa kazi ya uandishi wa Habari kwani itakumbukwa Mnyuku mi miongoni mwa waandishi wa habari za michezo wa mwanzo mwamzo kuanza kufanyiakazi gazeti la Mwananchi na miongoni mwa waandishi wa habari wahasisi wa kuandisha makala katika gazeti la Mwanasport.

Mnyuku licha alikuwa akiandikia gazeti la Mwananchi Michezo na lilipoanzishwa gazeti la Mwanasport ,mhariri wa gazeti lile Charles Mateso pia alinipa koramu ambayo nikawa naandika makala zinazohusua masuala ya uhusiano wa kimapenzi.

Nitakumbuka vibweka vya Mnyuku . Maana marehemu Mnyuku yeye alikuwa ni mfupi basi alikuwa akipenda kutumia neno hili kwa kujiami  nanina mjukuu: " MSINIONE MFUPI MKADHANI SIWEZI KUNANIII........ '. Tukawa tunacheka.

Mnyuku alilitumikia taifa hili kupitia Karamu yake na hakuna ubishi Katika Hilo.

Sina mengi ya kumuelezea Mnyuku zaidi ya Kusema hivi ' Kazi ya Mungu haina makosa na uamuzi wa Mungu haukatiwi rufaa'. 

Hivyo basi Mungu ndiye aliyemuumba Mnyuku na akamleta hapa Duniani na Mungu Huyo Huyo ndiyo ameamua kumchukua Mtu wake kwa muda alioutaka yeye licha sisi wanadamu hatujapenda'.

Mbele wewe  Mnyuku'Chinga' ,nyuma yako sisi. Mungu aiweke roho ya marehemu Mnyuku sehemu inayostahili.Amina.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Novemba 19 Mwaka 2014.

No comments:

Powered by Blogger.