KASHFA YA ESCROW ISITUVURUGE
KASHFA YA ESCROW ISITUVURUGE
Na Happiness Katabazi
MIONGONI wa Wimbo unaotamba hapa nchini Homa ya Dengue na kile kinachoitwa eti ni vigogo wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika Katika kashfa ya ufisadi wa Sh Bilioni 200 Katika Akaunti ya Baraza la Usuluhishi la Migogoro ya Kibiashara (ESCROW) ya Benki Kuu (BoT).
Makala yangu itazungumzia Wimbo huo wa pili wa kashfa ya ESCROW ambayo Mbunge wa Kigoma Kusini(NCCR-Mageuzi), David Kafulila amedai Kuwa ndiye yeye ameiibua kashfa hiyo ambapo aliwataja wahusika wakuu wa kashfa hiyo Kuwa ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliachim Maswi, Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba.
Kafulila alisema kuwa ufisadi huo ni lazima mbivu na mbichi zifahamike, na kwamba haungi mkono uamuzi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wa kuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza suala hili kwa kuwa linagusa mamlaka kubwa katika dola, badala yake iundwe Kamati Teule ya Bunge.
Muda mfupi baada ya Kafulila kutoa tuhuma hizo Bunge, hakukubaliana na ombi la Kafulila lililotaka iundwe Kamati Teule ya Bunge na badala yake akaiagiza TAKUKURU na OFISI ha CAG Ifanye uchunguzi wake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo.
Kwa jicho la Sheria tuhuma zilizotolewa na Kafulila zitabaki Kuwa tuhuma, na Kafulila atahesabika kwanza Kuwa yeye ni mtoa taarifa za tuhuma hizo.Hivyo kitendo Cha Kafulila kunukiliwa na Gazeti hili toleo la Jumatano ya wiki hii Kuwa uamuzi huo wa Pinda una Mashaka makubwa na kwamba tuhuma hizo zinahusu viongozi wakubwa wa dola hivyo eti ni Vyema Kamati ya Teule ya Bunge iundwe uchunguze siyoni Kama Ina mantiki.
Kwani TAKUKURU imeanzishwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana Rushwa ya Mwaka 2007 Namba 11/2007.Na kifungu Cha 7 Cha Sheria hiyo kimeanisha Kazi za Takukuru na miongoni mwa Kazi za Takukuru ni kufanya uchunguzi makosa ya kula Njama Kutenda kosa, kuchunguza tuhuma za makosa ya rushwa yanayowahusu maofisa wa serikali.
Aidha Ofisi ya CAG nayoilianzishwa na inayo majukumu yake mengi tu ikiwemo ya kukagua mahesabu Katika Fedha za serikali na imekuwa Ikitimiza majukumu yake na kutoa taarifa zake kwa umma.
Na Taasisi hizo zimeanzishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kafulila ni miongoni mwa wa Bunge wa Bunge Hilo.
Sasa Inashangaza Kama siyo kutisha kumsikiliza mtunga Sheria Huyo Akisema uamuzi huo wa Pinda una Mashaka kwasababu yeye alikuwa akitaka Bunge iunde Kamati Teule.
Kama Kafulila alikuwa Hana Imani na Takukuru, CAG ni kwanini alitoa tuhuma hizo bungeni akitaka mbivu na mbichi sijulikane? Kumbe anaamini Takukuru, CAG ni wa chafu ni kwanini aliibua tuhuma hizo tena akitaka uchunguzi ufanyike? Hivi mwisho wa siku alifikiri Takukuru, CAG hazitausishwa Katika uchunguzi huo.
Tuhuma hizo zinahusu Fedha za serikali , Ofisi ya ya CAG lazima ilihusishwa mAana ipo pale kwa kutazama matumizi ya Fedha za serikali zimetumika Kama iliyokusudiwa?
Maana hata Kama Kamati Teuli ya Bunge ingeundwa Mwisho wa siku ripoti hiyo ya uchunguzi wa Kamati Teuli ya Bunge Ingepelekwa Takukuru au Polisi ili zichunguze kuona je kuna ushahidi wa kutosha wa kuweza kuwafungulia Mashitaka watuhumiwa? maana Polisi na Takukuru Ndio wenye majukumu hayo Kimsingi.
Pia Itakumbukwwa kashfa ya wizi Katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), iliibuliwa Bungeni, Kamati ya Teule ya Bunge haikuundwa Matokeo yake Rais Jakaya Kikwete alitenda TIMU ya Uchunguzi wa tuhuma hizo ambayo ilishirikisha polisi, Wanasheria toka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tasisi nyingine za serikali ambayo ilikuwa na Ofisi zake Mikocheni ambapo ili fanyakazi yake vizuri Mwisho wa siku Uchunguzi huo ulimfanya Mkurugenzi wa Mashitaka , Dk.Eliezer Felelshi Kufungua jumla ya Kesi 12 za EPA m Novemba 4 Mwaka 2008 ambapo hadi sasa jumla ya Kesi Nne zimetolewa hukumu na baadhi ya washitakiwa walipatikana na hatia za makosa waliyoshitakiwa na wengine waliachiwa Huru kwasababu ushahidi haukuwagusa.
Mfano mwingine ni tuhuma za mkataba wa kampuni ya Richmond Ambapo kelele zilipigwa na wabunge hadi Kamati Teuli ya Bunge ikaundwa Mwaka 2007 na Mwanzoni Mwaka 2008 Kamati Teuli ikabainika kilikuwa na ouzo Katika mkataba huo na kumtaka Aliyekuwa waziri makuu Edward Lowassa ajipime na Kamati hiyo ikaamuru Wamiliki wa kampuni hiyo Naeem Gire na Mohamed Gire na baadhi ya Maofisa wa serikali wawajibishwe Hali iliyosababisha Lowassa kuwajibika KWA kujiudhuru wadhifa huo ambao alidumu nao KWA Kipindi kifupi sana.
Baada ya ripoti ya Kamat hiyo kusomwa, baadhi ya wabunge kwasababu wanazozitoa wa Wakaanza kuishinikiuza Takukuru iwashitaki watu Hao Hali iliyosababisha Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru , Dk.Edward Hosea na baadhi ya wabunge kuingia Kwenye malumbano Kwani Hosea alikuwa akitaka Takukuru iachwe ifanyekazi yake kwa Uhuru na siyo kuingiliwa na wasiasa Hali iliyosababisha kila kukimbia wabunge Hao Kuwa wanashambulia Takukuru na Hosea kila kukicha Kumbe wabunge Hao walikuwa wananjama zao chafu za kuaribiana kisiasa.
Wananchi ambao walikuwa hawaelewi Njama hiyo waliwaunga mkono wabunge Hao wengine ambao walipachika jina la ' wabunge wanapambana na ufisadi", Leo hii wanasiasa 'Mgambo uchwara' hao wapo kimya utafikiri ufisadi ndani ya nchi hii umekwisha.Dhambi sana.
Mwisho wa siku Takukuru iliamua kumfungulia Kesi ya Madai ya Kutoa taarifa za uongo Kwenye Kikao Cha Tenda Cha Tanesco kuhusu uwezo wa kampuni ya Richmond, mshitakiwa alikuwa ni Neem Gire Mwaka 2012, Hakimu Mkazi wa Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Waliarwande Lema alimuoa Gire Hana Kesi ya Kujibu na Mkurugenzi wa Mashitaka DPP- Dk.Feleshi hakulidhika na uamuzi huo anakimbilia Mahakama Kuu Ambapo Jaji Lawrence Kaduri alitengua uamuzi huo na akaamuru jarada la Kesi hiyo lirudishwe Mahakama ya Kisutu na Gire aanze kujitetea na Gire naye kupitia Wakili wake Alex Mgongolwa hawakubaliani na uamuzi wa Mahakama Kuu, wamekimbilia Mahakama ya Rufaa.
Kwa hiyo binafsi naweza Kusema Kuwa sikubali Kuwa tuhuma ni za kweli na sikatai Kuwa tuhuma hizo zilizoibuliwa na Kafulila Kuwa ni za uongo Katika Hatua hii ya awali.Nasubiri vyombo vyenye mamlaka ya kufanyia uchunguzi itakapokuja kuandika ripoti za uchunguzi wake.
Kwani tuna Mifano hai ambayo inafunza kupitia wanasiasa wetu ambao Walijifanya ni mabingwa wa kuibua kile wanachokiita ufisadi wakati Sheria zote za Tanzania ikiwemo Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002 , haina kosa linaloitwa ufisadi. Sijui wenzetu hawa kosa la ufisadi wanaotaka watu washitakiwa nalo sijui wa alipata wapi Katika Kifungu kipi Cha Sheria.
Mbunge Zitto Kabwe aliuaminisha umma Kuwa Ana ushahidi kuhusu Majina na namba za Akaunti za watu walioficha Fedha nje ya nchi na baadhi ya watu waliomua mini, lakini siku zote njia ya muongo ni Fupi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Werema aliliambia Bunge Kuwa Zitto ni muongo aliwashawahi kumuita Ofisini kwake akimtaka atoe ushahidi chini ya kiapo , Zitto akasema hana ushahidi, na hadi Leo kimya kabisa utafikiri Zitto siyo yeye aliyekuwa akisimama majukwaa akijinadi anaoushahidi wa watu walioficha Fedha nchini Uswiss.
Pia kuna wanasiasa wengine ambao Walijitapa ndani na nje ya Bunge Kuwa wanaushahidi wa Majina ya watu walioiba Fedha za EPA kupitia kampuni a Kagoda hadi Leo hawajaenda kutoa ushahidi thabiti Katika vyombo husika, Wanaishia kubwatuka majukwaani na kuwataka Ujinga huo baadhi ya waandishi wa Habari ambao hawajui kilichopo nyuma ya tuhuma zinazoibuliwaga na baadhi ya wanasiasa wa naandika Habari za kutoa hukumu za upande mmoja.
Wiki iliyopita Spika Anna Makinda Mara Tatu wakati akiendesha Bunge aliwataka baadhi ya wabunge waache kutumiwa na baadhi ya watu walionje ya Bunge Kuja bungeni Kusemea maslahi binafsi ya watu wakiwa tuma na kuwataka wabunge Hao watumie akili zao.
Ushauri huu ni mzito sana kutolewa na Spika Kwa wabunge na Hakuna Shaka Makinda alikuwa anasababu anayoifahamu ndiyo mAana Akaamua kutoa ushauri huo licha Spika Makinda hakutaja jina la Mbunge anayetumiwa.
Hivyo ushauri wangu kwanza kwa waandishi wa Habari wenzangu kuhusu tuhuma hiyo iliyoibuliwa na Kafulila tuwe makini na tusimame Katika Maadili ya taaluma yetu.Kafulila tumemsikia, serikali kupitia Pinda imeishachukua Hatua KWA kuanzia Pinda ameagiza Taasisi hizo mbili zifanyie Kazi tuhuma za Kafulila.
Hivyo ni vyema sasa tuziachie Taasisi hizo zifanyie kazi yake Kwa Uhuru na Mwisho wa siku zije zitoe ripoti yake.Tusikubali ama kutumiwa na wafanyabiashara, wanasiasa, Wanasheria kuwachafua watu wengine wanaotuhumiwa Katika tuhuma hizo na Kafulila isivyohalali Kwani Tayari naona kuna Dalili za wazi ambazo ni chafu za miongoni mwetu kuanzia kutumiwa na Makundi yanayoasimiana Katika kashfa hii.
Pili, Takukuru, CAG visikubali kuingiliwa kufanyakazi yake na Makundi yenye Hira Katika Sakata hili Kwani endapo watakubali kufanyakazi kwa shinikizo la wanasiasa Mwisho wa siku watajikuta wanaumbuka Mbele ya safari Kama serikali ilivyoumbuka Mara mbili Kwenye Kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Ricky Mahalu na Grace Martin Kwani Chanzo kikubwa Cha Kesi hii kilianzia pale Bungeni Mwaka 2004 ambapo wanasiasa uchwara waliliaminisha Bunge na Takukuru Kuwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Costa Mahalu alitafuna Fedha za ujenzi wa Jengo la ubalozi Wa Tanzania nchini Italia kumbe ni uzushi na leo hii wale wanasiasa na baadhi ya wachunguzi wanaona haya.
Tatu , Kafulila kwa Kuwa Tayari umeishanukuliwa ukisema uamuzi wa Pinda una Mashaka nao , ni wazi hata vyombo hivyo va uchunguzi vikitoa Matokeo ya uchunguzi ambao wewe hutapendezewa nao, hutatakubaliana nao.
Basi minakushauri Kafulila tumia Kifungu Cha 99 Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002, kuomba uwe mwendesha Mashitaka Binafsi(Private Prosecutor), ili uweze kuendesha Kesi hiyo mahakamani mAana Tayari umejinasibu Kuwa una ushahidi wa kutosha kuhusu tuhuma hizo.
Ni sisi wenyewe wananchi wa Tanzania Tulitaka nchi yetu iongozwe na Utawala wa Sheria, kwahiyo Takukuru, CAG, Cheo Cha Waziri wa Mkuu na Spika vimeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Hivyo tuheshimu wanapokuwa wanatimiza majukumu Yao na anayeona Hana Imani na vyombo Vya dola, aende kuishi nchi ambazo anaamini vyombo vyao Vya dola vinaaminika.
Na wananchi huko vijiweni Tusikubali kutoa hukumu Kuwa. Fulani n fisadi , hafai kuongoza, afukuzwe Kazi eti tu mwanasiasa Fulani kajitapa kuibua tuhuma za ufisadi.Kwani ni hawa hawa wanasiasa Ndio wamekuwa wakituingiza Kwenye ushabiki wa mambo ya kijinga Mwisho wa siku wanatoa na soremba.
Ni hawa hawa wanasiasa walijiapiza Kuwa kampuni ya Richmond ni ya Kitapeli na ni kampuni ya mfukoni .Wananchi tukaamini Kumbe walikuwa nalo jambo.
Mwisho wa siku kampuni hiyo ikabadilishwa jina ikaitwa Dowans, kelele zikazidi hadi kufikishana mahakamani na Mwisho wa siku Tanesco ikashindwa Kesi iliyoishitaki Dowans kule katika Baraza la Usulushi wa Migogoro ya Kibiashara ya Kimataifa (ICC), Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na Mahakama ya Rufaa Tanzania.Na Tayari Serikali ya Tanzania imeishailipa fidia Dowans.
Kampuni ya Richmond tuliyoaminishwa na wasasiasa uchwara Kuwa ni kampuni ya mfukoni ilibadilishwa toka jina la Richmond Kuja Dowans, na Mwishoe HIvi sasa inaitwa Sympion Power Na inatoa huduma zake kama kawaida na huduma ha kampuni hiyo inatumika .
Na mwaka jana Rais wa Marekani Baraka Obama alivyokuja Tanzania aliizindua kampuni hiyo,na Hao wanasiasa waliotuaminisha uongo kuhusu uwezo wa kampuni hiyo Kuwa ni ya mfukoni nao walikuwepo Kwenye msafara wa ziara hiyo ya Obama kuzindua Sympion .Na leo wanasiasa hao, sanaharakati waliokuwa wakishabikia kuiponda kampuni hiyo leo wapo kimya utafikiri wamefariki Dunia.
Tujifunze kutokana makosa, tusiwe wepesi kuamini kila kitu kinachoibuliwa na baadhi ya wanasiasa wetu uchwara Kwani wengine ni Mavuvuzera wa wafanyabiashara, makampuni na wanasiasa,na makuadi wa Makundi yanayoasimiana Katika magomvi Yao ama ya Kugombea Tenda Fulani, Biashara , urais Mwaka 2014 na kulipizana visasi vitendo ambavyo havina maslahi ya taifa zaidi ya kutaka kuvuruga umoja wetu.Tusiwape nafasi wahuni hawa.
Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Mei 18 mwaka 2014
0716 774494
www.katabazihappy.blospot.com
Facebook: Happy Katabazi
No comments:
Post a Comment