Header Ads

SHYROSE BANJI JIEPUSHE NA TUHUMA CHAFU


SHYROSE BANJI JIEPUSHE NA TUHUMA CHAFU
Na Happiness Katabazi
WASWAHILI wanamsemo wao mmoja usemao ' anaye jamba lazima atakunya tu'.

Msemo huo una una Tafsiri nyingi tu ikiwemo Kuwa unawaweza Kuwa unapenda matendo maovu lakini kwasababu una Nguvu za aina fulani unatumia kujisafisha Mbele ya hadhara Kuwa hujatenda maovu hayo lakini ukae ukifahamu ipo siku ukweli utaanikwa hadharani na itabainika Kuwa ni kweli MTu Yule aliyekuwa akikanusha tuhuma zile ni muongo na kwamba ni kweli alitenda makosa hayo anayekabili nayo.

Nimeamua kuanza na Msemo huo kwasababu nafikiri kila kukicha sasa baadhi ya vyombo Vya Habari vimekuwa vikiandika baadhi ya Habari mbaya zinazomuhusu Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji.

Banji ambaye licha ni Mbunge wa Bunge hilo, pia Mwandishi wa Habari Kitaaluma wa muda mrefu.

Miongoni mwa tuhuma zisizopendeza ambazo zinaelekezwa moja kwa Moja Banji,Moja ni ile tuhuma ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya Kijamii Kuwa ni za utovu wa nidhamu kwamba Banji alitoa lugha ya matusi dhidi ya baadhi ya wabunge wenzake wa Afrika Mashariki akiwa eti amelewa Pombe ndani ya Ndege Hali iliyosabisha baadhi ya wabunge wa Bunge Hilo kutaka ashughulikiwe.


Tuhuma nyingine ni kwamba tulimshuhudia Banji mapema Mwaka Mwaka huu akirushiana vijembe na Waziri wa Wizara ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta ' Mzee Sugu' , ambaye Sitta aliibuka na kusema Banji Hana mamlaka ya kumnyoshea kidole wala Wizara yake kwa Sababu Banji ni miongoni wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ni Mtoro  yaani ahudhurii  ipasavyo vikao Vya Kamati na Bunge Hilo.

Tuhuma Nyingine ambayo imeibuka HIvi sasa ni kwamba Banji ampiga mbunge mwenzie wa Bunge Hilo kutoka Tanzania, Ndelakindo Kessy.

Ibara ya 13 (5) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 , inasema mtuhumiwa anayetuhumiwa  Kutenda makosa ya jinai asichukuliwe au kutendewa Kama Ana hatia hadi pale Mahakama itakapokuja kumkuta na hatia.

Hivyo na Mimi Katika makala hii niliyomwandikia dada yangu, mwanahabari mwenzangu Banji imezingatia matakwa ya Ibara hiyo, hivyo simchukili  Banji Kuwa Ana hatia Katika tuhuma hizo zote zinazomkabili hadi pale mamlaka husika zitakapokuja kumuona Ana hatia.

Namfahamu Banji tangu enzi zile 'tunasaka Nyoka' wote mtaani yaani kusaka Habari, pia namfahamu Banji Enzi zile akiwa Kiongozi wa Timu ya Waandishi wa Habari Wanawake (Taswa Queen), Ofisa Uhusiano wa City Water na Benki ya NMB.

Ni mwanamke ambaye ameangaika hadi kufika hapo alipofikia ,Nampongeza Katika Hilo.

Leo Banji Kama nitakukwaza naomba nisamehe  bure Kwani Mimi siyo mnafki na siogopi Kusema kile ninachokiona Kina faida kwa wahusika .

Banji Utakumbuka ulivyoanza harakati zako za kutaka uongozi ndani ya CCM ,Ubunge wa Jimbo Kinondoni na nafasi nyingine nyingi tu lakini kura hazikutosha na hukufanikiwa kupata nafasi hizo.

Kumbe Mungu aliruhusu ukose hizo nafasi ili uje uchaguliwe Kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.Wanahabari wenzako tunapokutakia Mema tulifurahi kwa kuchaguliwa kwako Kuwa Mbunge wa Bunge la EAC siyo tu ni sifa kwa Familia yako pia ni sifa kwa waandishi wa Habari ,wanawakd Kuwa miongoni mwa wa wabunge wa Bunge la EAC ni mwanahabari na mwanamke mwenzetu ambaye ni Banji.

Sasa inapotokea tena tuhuma Kama hizi zinakuandama mfululizo ,watu tunaofikiri sawa sawa lazima tushituke na tuliulize Kulikoni Banji?Mbona unaandamwa na tuhuma mpya mfululizo kiasi hicho?

Ni kweli Banji amekuwa akijitokeza hadharani kuzinaka tuhuma hizo.Lakini Mimi binafsi SINA ushahidi unaonyesha Tuhuma hizo ni za ukweli au uongo.

Ila najiuliza ni kwanini basi Banji kila kukicha anaandamwa na tuhuma mpya? Je ni kweli Banji anatenda matendo hayo machafu ila amekuwa ni mahiri kukanusha tuhuma hizo pindi zinapovujishwa kwenye vyombo Vya Habari na mitandao ya kijamii?

Tumuulize Banji ,je ana Mpango wa kutaka Kugombea Urais, Ubunge au Udiwani ?.

Maana nchi hii hivi sasa wanasiasa wetu Wengi wamefilisika kimkakati ,kimbinu za kuwadhohofisha maadui wao wa kisiasa hasa wale wanaotaka Kugombea pamoja Katika Ngazi ya urais, Ubunge na udiwani kwa kuamua kwatumia baadhi ya wapambe ambao wabambwe wao wamekuwa na kazi Moja tu ya Kutengeneza fitna,uzushi,majungu dhidi ya hasimu wao na Kisha wapambe Hao wamekuwa wasambaza majungu hayo kupitia Mtandao ya kijamii na kwatumia baadhi ya waandishi wa Habari wasiyojua ajenda iliyopo nyuma ya Habari hizo kuwachafua wenzao.

Nasema Hilo kwasababu ndiyo wanasiasa wetu na sisi wanahabari tulipolifikisha taifa letu hapa lilipo kwa baadhi ya watu Kuwa na tabia za kishenzi za kuzushiana taarifa za uongo na kuchafuliana majina Lengo likiwa ni Moja kuaminisha umma Kuwa Fulani aliyechafuliwa kwenye mitandao na magazeti na wakati mwingine ni Habari za uongo tu, Kuwa hafai kupewa madaraka Fulani hata kidogo kwasababu Hana nidhamu, mwizi na fisadi.Dhambi sana na ni ukatiri pia.

Kama ni kweli Banji unafanya Vituko HIvi Leo hii ni Mara ya pili nakushauri, achana na vitendo HIvi Kwani kaa chumbani peke yako, jitafakari ulipo toka, ulipo sasa na unakokwenda. 

Nayafahamu baadhi ya mapungufu yako  wewe na Ndelakindo Kessy na Mimi Kama binadamu kuna watu wanayafahamu mapungufu yangu sikatai. 

Nakushauri Banji jiepushe kukaliabia ya kufanya mambo ambayo yataendelea Kuwa Chanzo Cha wewe kuibuliwa tuhuma mpya kila kukicha.

Maana sikufichi huku mitaani kuna baadhi ya watu wameanza kuziamini hizo tuhuma Kuwa ni za kweli kwasababu eti wa nafahamu baadhi ya rekodi ya matendo yako.

 Sijapendezwa na mtazamo huu Kwani pia unahusishwa Moja kwa Moja na taaluma ya wanahabari Kuwa Banji ni mwanahabari amepewa nafasi hiyo ya Ubunge lakini anafanya vitendo Vya kihuni.

Binafsi naamini Kama ulitenda vitendo hivyo ,ulitenda Kama wewe binafsi na siyo kwa Kofia ya Ubunge, Uandishi wa Habari. 

Wanawake Watanzaia ni miongoni mwa wanawake Dunia ambao tumekuwa tukipigania Usawa Katika madaraka na kweli Katika Utawala wa serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, wanawake wengine wameshika nafasi nyingi za uongozi ndani na nje ya serikali ni jambo la kujivunia sana kwa wanawake sasa inapotokea Nyie baadhi ya viongozi wanawake mnaanza kutuhumiwa Kuwa mnatenda matendo yasiyofaaa Mkae mkijua mnawapa nafasi ya wanaume Kusema kuendeleza kasumba ya kumuona Mwanamke hafai kupewa madaraka kwasababu Hao waliopewa madaraka wameonyesha kushindwa kujiheshimu. 

Banji  jitambue Kuwa wewe ni kiongozi  na kukubali Kuwa kuna baadhi ya mambo Unatakiwa usifanye hadharani.

Mfano kiongozi aliyefundwa akafundika huwezi kumkuta akivaa nguo za ovyo ovyo barabarani, kujihusisha na ulevi wa vilevi vilivyopigwa marufuku na sheria za nchi, kutoa lugha chafu Mbele za watu ,kupigana hadharani na mambo mengine yasiyofaha. 

Ieleweke Kuwa hayo matendo simaanishi yanafanywa na Banji.
Mwisho nimalizie kwa kumuasa dada yangu Kitaaluma Banji ajitambue Kuwa yeye ni kiongozi  Kama kweli  anatenda matendo aache kwani yatamletea madhara makubwa sana  na kuporomosha heshima yake na ninamshauri afanye utafiti ni kwanini anaandamwa na tuhuma hizo mfululizo na ni wakina nani wanasambaza taarifa hizo  kwa Malengo gani.

Je ni baadhi ya wabunge wenzake wake Bunge la Afrika Mashariki wanaotoka Tanzania au ni wabunge wenzake wa Bunge la Afrika Mashariki wanaotokea nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki? 
Na ujiulize  ni kwanini wakuandame wewe tu   kila kukicha kwa tuhuma na wabunge wenzako  wanawake wa Bunge Hilo toka Tanzania Kama Angella Kiziga na wengine hawaandamwi na tuhuma Kama hizo?  Kwanini ni wewe Banji  tu? Kumbuka  Msemo usemao ' Mke wa Mfalme hata kiwi kutuhumiwa'.

Pole sana Banji kwa kupitia Kipindi hicho kigumu ila rejea Msemo huu ' aliye jamba atakunya tu'.  Hivyo Kama kweli Banji unafanya upuuzi huu halafu unajitokeza hadharani mapema unakanusha , basi tambua ipo siku ukweli utajulikana Kuwa ni kweli Banji anatenda matendo hayo na tutakupuuza.

Chanzo: Facebook.Happy Katabazi,
Novemba 20 Mwaka 2014No comments:

Powered by Blogger.