Header Ads

UB KUTENGA ' DK.MVUNGI DAY'UB KUTENGA 'Dk.MVUNGI DAY ' 
Na Happiness Katabazi(UB)
MAKAMAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Profesa Costa Ricky Mahalu amesema uongozi wa chuo hicho utawasilisha ombi Katika Seneti ya chuo hicho la kuomba Novemba 12 ya kila Mwaka iwe ni siku ya 'Dk.Sengondo Mvungi Day'.

Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi, Profesa Mahalu alisema Leo Novemba 12 Mwaka huu, marehemu anatimiza mwaka mmoja tangu afariki Nchini Afrika Kusini akikopelekwa kwaajili ya matibabu ambayo yalisababishwa na majeraha makubwa aliyoyapata sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya usiku wa kuamkia  Novemba 3 Mwaka 2013 ,wahalifu kuvamia nyumbani kwake Kibamba Dar es Salaam na kumjeruhi vibaya.

Balozi Mahalu alisema  Dk.Mvungi ambaye alikuwa ni miongoni mwa waasisi wa chuo hicho na Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia Taaluma wa kwanza ,wafanyakazi na marafiki wa chuo hicho wataendelea kumkumbuka na kuendeleza mazuri aliyoyaacha.

" Hakika Jina la Marehumu Dk.Mvungi litabaki Kuwa ni alama ya UB Kwani alitoa mchango mkubwa na Kuwa miongoni mwa waasisi wa  UB;

" Hivyo ndiyo  maana nasema Menejimenti ya chuo itapeleka ombi kwenye Seneti ya UB ambayo Mwenyekiti wake ni Jaji wa Mahakama ya Rufani nchini, Stephen Bwana..linalotaka kila Novemba 12 ya kila Mwaka Katika Jumuiya ya wana  UB, iwe ni siku ya Dk.Mvungi yaani Dk.Mvungi Day  na kwamba siku hiyo kutakuwa kukifanyika shughuli mbalimbali za kumkumbuka Marehemu kwa mchango wake.' alisema Profesa Mahalu.

Pro.Mahalu alisema UB ilivyoanzishwa rasmi Mwaka 2011 Katika Mwaka wa masomo 2011/2012 ilikuwa na jumla ya wanafunzi 64 .Mwaka 2012/2013 ilipata wanafunzi 154 , Mwaka 2013/2014 idadi ya wanafunzi iliongezeka na kufikia 234, na mwaka wa masomo ulioanza rasmi Novemba 3 mwaka huu ,wa 2014/2015 idadi imeongezeka na kufanya chuo kuwa na wanafunzi  254  ambao hadi kufikia jana walikuwa wamesajiliwa.

Chanzo: Ofisi ya Uhusiano
Chuo Kikuu Cha Bagamoyo ( UB)
Novemba 12 Mwaka 2014.


No comments:

Powered by Blogger.