Header Ads

CUF MMEMWELEWA RAIS KIKWETE?
*KASEMA MAANDAMO YENU YALIKUWA BATIRI

Na Happiness Katabazi
FEBRUALI 3 Mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alisema tukio la kupigwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na wafuasi wake na Polisi  Januari 27 Mwaka huu, tukio Hilo limetokea kwasababu  nchi Inaongozwa kwa Utawala wa Sheria  na atakaye kiuka  atakumbana na mkondo wa Sheria.

Rais Kikwete alisema aliyasema hayo Jana Ikulu Dar es Salaam, alipokuwa Akizungumza  na waandishi wa Habari  baada ya kufanya mazungumzo  ya Faragha  na mgeni  wake Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano.

Rasi Gauck pamoja na mambo mengine amempongeza Kikwete kwa kukuza Utawala wa Sheria na ameaidi nchi yake kukuza ushirikiano Katika Nyanja ya kiuchumi. Asante sana Rais wa Ujerumani kwa kuliona Hilo na ahadi hiyo kwa taifa Letu ambayo ni miongoni mwa Mataifa ambayo yapo Kwenye kundi la nchi zinazoendelea.Karibu Tanzania.

Kwa Kauli hiyo ya Rais Kikwete ni wazi itawakera wafuasi wa CUF ,lakini kwa Tafsiri ya wazi kabisa ni kwamba rais Kasema maandamano Yale yaliyosababishwa wafuasi wa CUF kula kisago ni Matokeo ya kuvunja Sheria za nchi.Wangetii Sheria za nchi iliyowataka wasiandamane wasingekula kisago.

Itakumbukwa Kuwa Januari tukio Hilo litokee Januaria 27 Mwaka huu, nimeishaiandika makala zenye vichwa Vya Habari vifuatavyo: Profesa Lipumba umebug men, Askari Shupavu ni Yule aliye pita Depo, Weli Spana ni dawa tosha ya wanasiasa wakorofi, Polisi Temeke Mmetufurahisha Watanzania wenye akili timamu, Ni Profesa Lipumba au ni Profesa Lipumbafu? , CUF Mmemwelewa Rais Kikwete ?

Jana asubuhi naliandika makala iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho ' Ni Profesa Lipumba au ni Profesa Lipumbafu?.Hakika makala hiyo  ilionekana   kuwakera sana baadhi ya wafuasi wa CUF ambao wameshindwa Kujibu hoja zilizomo ndani ya makala wameishia kutoa  lugha chafu, vitisho, kunitengenezea picha chafu na kuaidi kuendelea kukusanya picha zangu kuzitengenezea picha za utupu huku wakiwa wamefura kwa hasira kwa lengo la kunikata makala ya kuacha kuandika.

Kwa kweli minilipokuwa naona hizo picha,maneno ya matusi nilikuwa nacheka sina mbavu  maana siku zote mtu aliyefirisika kihoja anaishia kutumia lugha chafu.Hali inayosababisha yeye kuonekana ni punguani na kunizidishia Umaarufu.Na vitendo hivyo vimedhiirisha wazi ujumbe wa makala hiyo umewagusa wahusika vilivyo na wametikisika.

Kwa Kuwa makala zangu zote hizo za tukio la Januari 27  Mwaka huu, pamoja na mambo mengine zilikuwa zinataka Utawala wa Sheria uzingatiwe na kwamba maandamano Yale yalikuwa haramu mkanipinga lakini Jana Amir Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni ' The Big Boss' wa Mapolisi  ambaye Lipumba Jumapili iliyopita alisema anaenda kuonana na Kikwete kumweleza jinsi Polisi walivyowafanyia ubabe  Tayari nayeye Jana Amekata mzizi wa fitna kwamba Polisi walikuwa na haki ya kufanya walivyofanya kwasababu CUF mlivunja Sheria na ndiyo maana mkakumbana na Kadhia ile.

Hivyo namshauri msomi wa Kimataifa Lipumba ile nia yake ya kumtafuta Rais Kikwete ili ampeleke ' Umbea' wa Temeke a ifute Manaa tamko la Jana la Kikwete ni Kama imeishatoa Lipumba asiende ofisini kwake Ikulu kupelekea porojo zile na kwa tamko Hilo la Kikwete endapo Lipumba akilazimisha kwenda Ikulu uwenda akajikuta anambulia 'Buti'.

Kilichopo sasa ni Mzee wangu Lipumba ,tuliza kitenesi ,kaa na Mawakili wake ili waone ni jinsi gani wanaweza kukunasua wewe na wafuasi wako wenye Kesi zinazowakabili.Rais Kikwete hati kusaidia tangu Jana nimekueleza kupitia makala yangu sijui uliniona muongo lakini mchana wa Jana baada ya Rais  Kikwete kutoa tamko lile naona kimoyo moyo utakuwa ulikubaliana na Mimi Kuwa nilikuwa sahihi nilipo kushauri uliangaijd kwenda kumuona kwasababu Kikwete ni muumini wa Utawala wa Sheria na mwana Usalama na siku zote wanausalama uwa wasalitiani.

Hongera Kikwete kwa kutoa Kauli hiyo adharani tena Mbele ya rais wa Ujerumani Kwani 'Message Sent' , ndani na nje ya nchi Kuwa wewe ukiwa ndiyo rais wa Tanzania umesema maandamano Yale yalikiuka Sheria za nchi.

Hivyo kwa wale watakao kerekwa watukane lakini usiku watalala na Maisha yataendelea lakini ukweli mchungu ndiyo huo.

Mwisho , napenda kutoa raia yangu kwa raia kutii Sheria bila shuruti na vyombo Vya dola likiwemo Jeshi la Polisi lifanye kazi yake kwa mujibu wa Sheria bila kumuonea mtu wa Kupendelea Vyama. Msikatishwe tamaa na maneno ya kebehi yanayotolewa na baadhi ya watu wanaoshabikia matendo ya Uvunjifu wa Sheria bila shuruti.

Mungu ibariki Tanzania 

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Februali 4 Mwaka 2015.

No comments:

Powered by Blogger.