Header Ads

WAHITIMU MAFUNZO JKT KUMBUKENI MLIKULA KIAPO CHA UTII


WAHITIMU MAFUNZO JKT KUMBUKENI MLIKULA KIAPO CHA UTII

Na Happiness Katabazi
FEBRUALI 15 Mwaka huu, wahitimu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), kupitia Mwenyekiti wa Umoja wao huo,George Mgoba aliutangazia umma Kuwa ikifika Leo Februali 23,23 na 25 Mwaka huu, wahitimu wa Mafunzo ya JKT  watafanya maandamano ya usiku na mchana   kushinikiza kuonana na Rais Jakaya Kikwete ili awasikilize matatizo yanayowakabili ikiwemo ukose tu wa ajira.

Mgoba  ambaye vyombo Vya Habari Vya Juzi na Jana vimeripoti habari iliyowanukuu watu wake wa  karibu ambao walidai  Mgoba Amelazwa Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwasababu alitekwa  na watu wasiyojulikana na kumjeruhi na kumasababishia maumivu makali mwilini Mwake.

Na Tayari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jana amenukuliwa na vyombo Vya Habari akisema amepata  taarifa za tukio Hilo na Ofisi yake inafanya uchunguzi na uchunguzi ukikamilika atatoa taarifa.

Kwa Kuwa kisheria Jeshi la Polisi ndiyo lenye jukumu la Kutolea taarifa matukio ya Uhalifu, hivyo sote Hatuna budi kusubiri taarifa hizo za uchunguzi zitakazotolewa na jeshi la Polisi Kama ni kweli alitekwa na kufanywa unyamana wa na kwanini watu Hao walifikia Hatua hiyo  ya Kutenda hivyo Kama inavyodaiwa.

Pole sana Mgoba Kama kweli umekutwa na mkasa huo.Pole sana ila naamini Kama kweli umefanyiwa unyama huo wahusika watabainika na watachukuliwa Hatua kwasababu Jeshi la Polisi ni Chombo makini na kina uzoefu mkubwa wa kuchunguza matukio ya kihalifu tena zaidi ya tukio Hilo watu wanalodai umetendewa na washitakiwa uwa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Tukiachana na hayo , Turejee Kwenye mada yetu ya Msingi ambayo inawauliza hawa wahitimu wa JKT Leo watafanya yale maandamano Yao Kama walivyotuaidia kwa mbwembwe nyingi licha tayari mpiganisha vita wao (Mgoba) kaisha jeruhiwa na Katibu wao amekamatwa Kabla  ya 'vita 'kuanza?

Inaelezwa Kuwa Askari Wawapo vitani ,Askari mmoja akifa au kujeruhiwa wale Askari waliokuwa salama morali ya kupigana vita ndiyo inapanda na wanazidi kupigana vita kwa  moyo na Nguvu zao zote.

Sasa Leo hii inakuwaje kwa Nyie wahitimu wa JKT ambao mlijinasibu Kuwa mmepata Mafunzo ya kijeshi mna rudi wote mstari wa nyuma Kabla ya tarehe ya kuanza kupigana  'vita 'kuanza kwa kisingizio eti kiongozi wenu ametekwa na kuumizwa?

Ndiyo maƱana Katika makala yangu iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho: ' WAHITIMU MAFUNZO JKT MNACHOKITAUTA MTAKIPATA SOON'. 

Ndani ya makala hiyo nilieleza wazi Nyie  siyo Wanajeshi na hamjapata Mafunzo ya wanayapata Askari wa JWTZ ndiyo mAana kwanza mipango yenu ni dhaifu, hamna nidhamu ya kijeshi na mnadhalilisha wakufunzi wenu waliowafunza JKT na uenda mlijifunza kupigana na mishale.

Baadhi ya watu waliojitambulisha ni wakufunzi wa Mafunzo hayo baada ya kusoma makala hiyo walinipigia simu na kumitolea vitisho na matusi juu, wala sikutishika na wengine baada ya kusikia Mgoba ametendewa unyama walinipigia na kunishukuru kwa kuwataadharisha na kwamba kilichomkuta Mgoba limewaogopesha na hawatashiriki tena maandamano hayo Kwani wamebaini miongoni mwa wakufunzi wa JKT wameanza kusalitiana hivyo hawataki ugomvi na dola wala kuandamana kwanza wanabiashara zao zinawaingizia kipato na kwamba miongoni mwa wahitimu Hao wanaajenda za kutumiwa na baadhi ya vyama Vya siasa kulea vurugu nchini wamewabaini.

Tangu niliposikia Jemedali wao Mgoba Kuwa ametekwa nimejiuliza ,Jemedali gani anatekwa kirahisi  hivyo tena na watu wanaodaiwa ni wanawake?

Nimebaki na Mashaka Je taarifa za kutekwa kwake Je ni Sinema ya Kihindi ambayo Sinema  ya Kihindi ni kawaida stelingi anakufa Badala ya kusave.

Mgoba alidai wanamafunzo ya kijeshi na wameiva kimafunzo inakuwaje alizidiwa akili na Hao watu wasiyojulikana Kumteka kirahisi hivyo wakati yeye ni Jemedali wa Askari wale zaidi ya Miaka 200 ambao walijinasibu Kuwa wanamafunzo ya kijeshi?

Yaani Jemedali gani wa 'vita' anakubali  kuitikia wito wa kila mtu anayemuita na kwenda kuonana nae?

Kama Jemedari 'Mgoba' amekubali kuitikia wito huo ambao tumeelezwa Kuwa ni wa wanawake ni kweli basi Hao watekaji wanawake ni kiboko na wakiamua hata Leo hii kutumia mbinu hiyo hiyo kuwaita baadhi ya wahitimu Hao ,basi watawadhuru   wahitimu wote kwa njia hiyo ya kidharimu.

Mininachofahamu hivi sasa kutekwa wanatekwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino ambao viungo vya ni dili kubwa na serikali na Jamii kwa ujumla Inaangaika  kutokomeza mauji hayo.

Wengine nao baada ya kusikia taarifa Kuwa Mgoba katekwa wakasema amejiteka Hakuna wakumteka na asitake 'kucompite' na albino na kwamba anataka kuaribu vichwa vya habari vya magazeti na kwamba eti Mwenyekiti wa Chama cha Malbino akimsikia hata mwelewa kabisa kwasababu wanaotekwa ni Albino na taifa lipo vitani kulaani mauji  na utekwaji wa Albino  na siyo watu wasiyo na ulemavu wa Ngozi Kama Mgoba .

Wengine wakasema Angekuwa ametekwa  na kutupwa katika machimbo ya madini kama Geita  wangesema wafanyabiashara wa madini walikuwa wanataka kufanyia mwili wake mambo ya kishirikina lakini Mgoba anadai katekwa na kutupwa msitu wa Mkoa wa Pwani ambako hakuna machimbo ya madini kuna machimbo ya Kokoto ,wanapata mashaka na taarifa hizo.

Wasiwasi  wangu kwa wahitimu wa mafunzo ya JKT ambao mnajifanya mnakiherehe na mpo juu juu kama ngoma za daku katika huo umoja wenu wa kujifanya mnaakili zaidi kuliko wale askari wanaolifahamu ndani nje majeshi yetu.

Jitambueni kuwa nyie bado mi watoto wadogo sana, subirini maelekezo kutoka kwa baba yenu (serikali) ,mkitaka kulazimisha kupewa mnachokitaka mtaonekana ni mamluki.

Askari mdogo yaani mwenye Cheo cha chini siku zote anapokea maelekezo na amri kutoka kwa afande wake anayemzidi cheo na anatakiwa atekeleze maelezo hayo.

Hayo mambo ya kulazimisha na vitisho  mnayotaka kufanya siyo mazuri, Kwani Nyie bado ni  watoto wadogo mnataka Kubeba Mzigo mzito ambao hamuuwezi Kuubeba.

Kwanini watu wasianze kuamini mnatumiwa na mabwana Zenu kufanya hayo Mlivyokuwa mmepanga kuyafanya? Siku 'mkifinywa' mtawataja hao mabwana zenu wanaowatumia kufanya hayo mliyokuwa mmepanga kuyafanya Leo.

Mkae mkijua mkivuka mstari serikali itawashughulikia na Hao mabwana Zenu  wanaowatumia siku mkianza kushughulikiwa wasianze Kulalamika Kuwa Jeshi la Polisi limetumia Nguvu nyingi kuwadhibiti wahitimu Mafunzo ya JKT.

Nawashauri achaneni na mawazo hayo ya Kudai kupatiwa kitu kwa mashinikizo mwisho wa siku mtakao kuja kuaribikiwa ni Nyie binafsi siyo siyo mabwana Zenu wanaowatuma kufanya hayo mnayoyafanya.

Mwenye masikio na asikie na atakayeshupaza shingo na ashupaze ,ushauri wangu Ndio huo wahitimu Mafunzo JKT rudini mtaani mkafanyie kazi  ujuzi mlioupata mlipokuwa JKT na sio kujiunga Katika umoja huo ambao nadiriki Kusema Malengo ya umoja huo yatazamwe upya na mamlaka husika kwasababu Tayari kupitia tamko Lao Katika vyombo Vya Habari limeonyesha umoja huo sio wa kuachwa HIvi hivi tu bila kutazwa kwa karibu na vyombo Vya dola.

Pole Mgoba kwa kuugua,Nina Imani waliokufanyia uhuni huo Kama inavyoelezwa na Hao watu wako wakaribu watakamatwa na Sababu ya wewe kufanyiwa hivyo utajulikana.

Waswahili wanamsemo wao usemao 'usiku wa deni haukawii kukucha'.
 Jumatatu Ndio Leo Imefika wale wahitimu wa Mafunzo ya JKT ambao mlinitolea lugha za vitisho kuwa mtaniua,mtanibaka,mkatumia njia ya kijinga kabisa  ya kunitongoza kwa wingi Kwenye Mtandao,na kunisifia Mimi ni mwanamke mrembo mnaitaji kuonana na mimi haraka ili mnidhuru kirahisi bila kufahamu  na Mimi ni 'Mkubwa wa akili' kuliko Nyie , nikawa nawacheka Ujinga. 

 Na hadi Jana usiku mkajitamba Kuwa lazima mtanidhuru na mtaandamana na kwamba Hakuna cha  kuwazuia lazima Leo mtafanya maandamano hamuogopi Polisi Kwani kwenu Nyie 'Polisi ni Raia wakakamavu.

Sasa usiku wa deni ndiyo umeishakucha ingieni uwanjani tuwaone na msitoe kisingizio cha Mwenyekiti wenu anaumwa kuumwa kwake yeye hakuzui mambo mengine ya Jumuiya yenu yasimame  na msipoingia mtaani Leo kufanya hayo maandamano yenu haramu ya usiku na mchana  nitawafananisha na 'mademu' mAana siku zote madem ndiyo wamekuwa na sifa ya kutoa tisho vikubwa lakini wakiminywa au kutishwa kidogo wanafyata Mkia.

Nitoe rai kwa Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi,Jenerali Davis Mwamunyange  atoe tamko la kufunga mjadala huu unaondeshwa na wahitimu wa JKT kwani ni wazi sasa matendo yao yanadhihirisha yanataka kucheza na ofisi ya Yake ya JWTZ nakutaka kumwandikia rekodi mbaya ya kustaafu  kwako.

Sasa ni wazi kupitia Kundi Hilo la vijana waliohitimu JKT kuna siasa chafu nyuma yake ambazo zinadaiwa kufanywa na Chama Kimoja cha siasa ambacho chama hicho kimekuwa ni mahiri sana ya kuratibu migomo,maandamano hapa nchini.

 JKT na JKU ni sehemu ya JWTZ  na kiongozi wa JWTZ ni wewe Mwamunyange .Leo Wahitimu wa JKT wamefanya waliyoyafanya na wameanika nia yao ovyo ya kutaka kusaliti viapo vyao na ukosefu sa adabu ws kuwaamlisha viongozi wao wafanye wanavyotaka wao badala Viongozi waaamlishe wanavyotaka wao, wasipodhibitiwa hawa siajabu kesho tutasikia nao wahitimu JKU nao wakaibuka kwa madai kama haya na kwa njia haramu Kama hizi za kutumia njia haramu za kuingiza siasa chafu kwa kutumia Majina ya majeshi yetu.

Jeshi Lina Sheria  na Mahakama zake  (Court  Martial) .Askari anapokosea kijeshi upelekwa Katika Mahakama hiyo na kuadhibiwa kwa mujibu wa Sheria za kijeshi. Hivyo wahitimu Wa Mafunzo ya JKT msitake kuingiza masuala ya kijeshi uraiani, waende wanawasilishe Madai Yao ambayo wao wanaona ni ya Msingi kule Jeshini tujue Moja.

Uliona wapi mtoto anamtishia nyau baba yake? Nadhani wenye mamlaka watachukua hatua   Leo wamefanya vijana wa JKT Kesho tunaweza kusikia wahitimu wa JKU ,Naomba  hatua zikichukuliwe na hatua zikisha chukuliwa ni wazi wale wanaowatuma watajitokeza kuwatetea.

Wahitimu wa Mafunzo JKT Kumbeni  mlikula kiapo na Askari yoyote anayesaliti kiapo cha utii kwa serikali yake adhabu yake ni moja tu na iko wazi ni kifo.

Uwenda Hilo mmelisahau   ndiyo maana mmeamua kufanya hayo Mlivyokuwa mmepanga kuyafanya Leo .Acheni Kwani ni wazi mtaumia Kwani Tanzania Inaongozwa  kwa mujibu wa Sheria na ni nchi yenye   Amani na Watanzania na vyombo vyao Vya Ulinzi na Usalama hata siku Moja havitakubali kuwaona  Nyie au Mtu yoyote anafanya vitendo Vya kuhatarisha  Usalama wa taifa hili halafu wakawaacha salama lazima watawashughulikia kikamilifu.

Kumbukeni pia Msemo usemao'Nazi haishindani na jiwe,lazima nazi itapasuka itapasuka. 

Hivyo Nyie wahitimu wa mafunzo ya JKT ni Nazi na serikali ni jiwe.Acheni kutumiwa vibaya na Chama hicho cha siasa kwani mwisho wa siku mtakao umia ni Nyie sio wao kwasababu Nyie ndiyo mnaingia mstari wa Mbele wao wanakuwa wamejificha nyuma.

Na kwa taarifa yote mnayoyafanya yanafahamika, ila kwakuwa mnajifanya mmenificha Gizani hamuonekani Kumbe mmenificha Kwenye mawingu mnaonekana.

Acheni wazimu huo nendeni mkafanyekazi za kuwaingizia kipato na kujenga taifa achaneni na tabia ya kutumia utambulisho wa Jeshi kutumiwa kufanya saisa chafu zinazo hatarisha Usalama wa taifa hili.

Mwisho vitisho vyenu dhidi yangu si viogopi,nilishatishiwa sana na watu wenye mabavu zaidi yenu ila kwakuwa nafanyakazi yangu kwa maslahi ya taifa langu na Kutenda haki na kuwarudisha kundi ni Nyie wahitimu wa Mafunzo ya JKT mnaotaka kusaliti Viapo vyenu Vya Utii kwa serikali ya yetu,Mungu atanilinda na wala siwaogopi niwaakikishie nipo imara na ni nafanya mambo yako Kama kawaida.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Februali 23 Mwaka 2015.

No comments:

Powered by Blogger.