HAPPY BIRTHDAY CCM 38YRS
Na Happiness Katabazi
LEO Februali 5 Mwaka huu, Chama cha Mapinduzi (CCM), chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete ,kinatimiza umri wa Miaka 38 tangu kilipoanzishwa rasmi Februali 2 Mwaka 1977.
Kwa Mwaka huu,CCM iliamua kusherehekea sikukuu hiyo Februali Mosi Mwaka huu ambazo Kitaifa sherehe hizo zilifanyika Mkoani Ruvuma na Kauli mbiu ya sherehe hizo ilikuwa ilisema ; ' Umoja ni ushindi ,Katiba yetu nchi yetu'.
Napenda kuipongeza CCM ambacho ndicho Chama kikongwe hapa nchini kwa kutimiza umri huo mkubwa na ninakiombea Afya na umri mrefu ili kiweze kupata tena ridhaa ya wananchi Katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka 2015 , ili kwa awamu nyingine kiweze kukamata dola.
Hakuna ubishi kwamba CCM imefanya mambo mengi makubwa ndani na nje ya nchi na kwa hapa nchini bado sijaona Chama cha upinzani ambacho kimeonyesha wa vitendo Dhamira ya dhati ya kuing'oa CCM madarakani zaidi ya vyama hivyo Vya upinzani kutumia vyombo Vya Habari na mitandao ya kijamii Kuonyesha vimedhamiria jambo ambalo siyo kweli.
Bado vi nacheza 'makida makida kwenye bakuli la mlenda' kwasababu ya uzandiki,unafki miongoni mwao na kutokuwa na ushirikiano wa kweli kwasababu baadhi ya viongozi wa vyama hivyo Vya siasa wametawali wa na Choyo, ubinfasi ,tamaa ya madaraka na wamekuwa wakiamasisha wafausi wao kutenda matendo ya uvunjifu wa sheria kama maandamano haramu,.
Baadhi ha vyama Vya upinzani hapa kwetu havina umoja wa kweli , vinachekeana vijino Pembe Hali inayosababisha CCM kutumia mwanya huo kuwachisha kila chaguzi.
Wakati Hali ni hiyo ndani ya vyama Vya upinzani ,pia ndani ya CCM hivi sasa kuna baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakijihusisha na vitendo Vya Vya utovu Maadili, majungu,fitna, uzushi,uongo chuki, tamaa ya madaraka, uvunjwaji wa Kanuni na taratibu za chama , Rushwa Hali iliyosababisha baadhi ya wananchi kuichukia CCM kwasababu ya vitendo hivyo .
CCM imekuwa ikijitadi kuwachukulia Hatua baadhi ya watuhumiwa kupitia vikao vyao na mfano mzuri ni Kamati ya Maadili ya CCM ilipowachukulia Hatua wanachama wake kwa kuanza kampeni za urais mapema Kabla ya tarehe iliyopangwaa na CCM, Kamati Kuu iliyoketi Zanzibar ilipopitisha azimio kuwataka wanachama wake waliotajwa Kwenye zogo la Akaunti ya Escrow.
Binafsi nimepata fursa ya kuzunguka Mara nne nchi hii Katika Miaka tofauti, ni wazi wale ambao nao wamepata fursa ya kuizunguka nchi hii watakubaliana nami kwamba ni kweli hatua za maendeleo zimepigwa na serikali inayoongozwa na CCM.
Kwasababu barabara Kuu nyingi za rami kuunganisha Mkoa na Mkoa zimejengwa, umeme umesambazwa katika baadhi ya vijiji,shule nyingi za msingi na serikali na Vyuo Vikuu zimejengwa na Ofisi za serikali nyingi za ngazi za Wilaya zimejengwa,Hospitali na za hati ukilinganisha na Miaka ya nyuma licha bado zinatakiwa kuboreshwa zaidi.
Aidha naiomba CCM ipitishe kwa haki na mwenye sifa sitahiki mgombea urais ,wabunge na madiwani Katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu, wasipitishe wagombea wa ovyo ovyo ambao mwisho wa siku wanaweza kukiletea Chama madhara na kuitumbisha nchini.
Nitimishe kwa kuitakia maazimisho mema ya Miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM na CCM ,ijitathimini na kuboresha madhaifu iliyonayo.Ila leo CCM ikisherehekea Miaka 38 ya kuzaliwa kwake ,haina budi kumkumbuka pia Mhasisi wa CCM, marehemu Julius Nyerere na waasisi wenzake Kwani wakifanyakazi kazi kubwa kukianzisha hicho.Happy Birthday CCM 38yrs.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
Februali 5 Mwaka 2015
No comments:
Post a Comment