Header Ads

WAHITIMU MAFUNZO JKT MNACHOKITAFUTA MTAKIPATA 'SOON'


Na Happiness Katabazi
VYOMBO Vya Habari nchini, Juzi na Jana viliripoti Habari Isemayo ,vijana waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wanatarajia kufanya maandamano ya siku tatu mfululizo usiku na mchana jijini Dar es Salaam kuanzia Jumatatu ijayo, kushinikiza kuonana na Rais Jakaya Kikwete kumweleza matatizo ya ajira wanayokabiliana nayo.

Wahitimu hao Februali 15 Mwaka huu,  walifanya mkutano katika eneo la Msimbazi Centre, Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Vijana waliohitimu mafunzo ya JKT, George Mgoba alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiomba kukutana na  Rais ili wamueleze matatizo wanayokumbana nayo, lakini wamekuwa wakipewa ahadi za uongo na Katibu Mkuu wa Rais.
“Tumeomba mara nyingi kukutana na Rais na tumekuwa tukiandika barua, lakini hatujibiwi chochote. Tunajua hizi ni njama tu za watu wachache wanaozuia tusionane na Rais,” alidai Mgoba.
Alidai kuwa wameandika barua nyingine na hivi karibuni  Katibu wa Rais aliwapigia simu kuwa wafike Februari 10 ili waonane na Rais na walipofika,  hawakufanikiwa kumuona Katibu huyo.
Akizungumzia  sababu za kutaka kuonana na Rais, alidai ni kutaka kujua hatma yao ya kutopatiwa ajira kutokana na mafunzo ya kijeshi waliyoyapata. “Sisi tumepatiwa mafunzo ya kijeshi na sasa tupo uraiani kwa ajili gani? Hawa wote unaowaona ni askari tayari ” alidai.
Mkutano wao uliwakutanisha pamoja ili kuweka mikakati yao ikiwa ni pamoja na kufanya maandamano ifikapo Jumatatu kama serikali haijajibu, kama itawaajiri au hapana. Walidai endapo jibu halitapatikana, basi watafanya maandamano ya siku tatu mfululizo hadi ombi lao la kumwona Rais lifanikiwe.
Makamu Mwenyekiti, Paral Kiwango, alisema jambo hilo linaonekana kuwa na upendeleo mkubwa, kwani wenzao wa upande wa Zanzibar wote waliomaliza mafunzo ya JKT, wanapatiwa ajira. Alihoji iweje  vijana wa Bara wametelekezwa?
“Wenzetu wa upande wa Zanzibar wakimaliza mafunzo wote wanaajiriwa, lakini sisi Tanzania Bara hakuna anayetujali na kututhamini,” alidai Kiwango.
Kwa upande wake, Katibu wao Liwus Emmaneul amesema kuna fursa nyingi za ajira hapa nchini kama vile TANAPA na sehemu zingine, ambazo wao wanaweza kufanya kazi; lakini wanaoajiriwa kule ni watu wengine wasiokuwa hata na ujuzi, huku wao wakitelekezwa na wakiomba ajira kule hawathaminiwi, kama watu wenye maadili na mafunzo.

Binafsi sitaki unafki wala simuogopi mtu yoyote anayetaka kuvunja au aliyevunja  Sheria za nchi  nitasema.

Napinga uamuzi huo wa wahitimu Hao wa JKT wa  kutaka kuandama siku Tatu mfululizo wakishinikiza kutaka kuonana na Rais Kikwete eti kwa Kigezo Kuwa hawajapatiwa ajira.

Imekuwa ikielezwa Kuwa baadhi ya Malengo   ya Mafunzo JKT kwa vijana wake ni Hali ya serikali ya taifa lolote kutaka kuvuna Nguvu  la vijana wake  kwa maslahi ya taifa lao.

Serikali inavuna Nguvu ya  vijana wake wawapo katika mafunzo ya kujitolea ya JKT  ili Badaa ya Mafunzo hayo vijana hao waje kulijenga taifa Lao kwakutumia ujuzi walioupata uraiani walipokuwa Katika Mafunzo Katika makambi mbalimbali ya JKT.

Mafunzo hayo siyo ya lazima, ni ya kujitolea.Na mwisho wa Mafunzo hayo pia mshiriki  wa mafunzo ya JKT ndiyo anapata faida kubwa baada ya Kuwa amefundishwa Mafunzo ya stadi za kazi.

Stadi za kazi ambazo  ni Ufundi ,ufugaji, Ukulima, nidhamu, ujasiliamali ,uvumilivu Katika Hali yoyote ile.  Wawapo mafunzoni wanafundishwa  kujiendesha kimaisha kupitia elimu ya stadi ya kazi waliyoipata mafunzoni.

Ikitokea siku Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, JWTZ na Magereza wanaitaji kuajiri watu basi majeshi hayo uchukua wahitimu wachache waliopita kozi ya JKT na kuwaajiri katika  majeshi hayo na Kabla ya kuwaajili uwapitisha kwanza Depo za majeshi hayo na wakifuzu ndiyo upata ajira ndani ya majeshi husika. Majeshi hayo hayachukui wahitimu wote waliopita JKT.

Wahitimu wa mafunzo ya JKT ,katu hawafundishwi kupigana vita wala kufanya maandamano haramu ya kushinikiza wapatie ajira,waonane na Rais Kikwete,kuvunja Sheria za nchi na JKTwala kuwaonea donge wahitimu wenzao toka Zanzibar.Kama mnaona wenzenu wanafaidi basi amieni Zanzibar.

Kwanza watuambie huo uhalali wa wao kuandamana wamepata wapi?
Nyie  wahitimu wa mafunzo ya JKT ile fomu mliyopewa na JKT  mjaze wakati mnaingia mafunzoni na mlipokuwa mnamaliza, hiyo fomu kuna sehemu yoyote inaonyesha   Kuwa Mhitimu yoyote wa JKT akihitimu Mafunzo ya JKT ni lazima atapatiwa ajira na serikali?Tuonyesheni.Jibu ni Hakuna.

Yaani kuudhuria Mafunzo ya muda mfupi tu ya JKT ndiyo imekuwa nongwa na kujitia  wazimu wa kushinikiza mmepewe ajira kwa njia ya mashinikizo ya kuandamana na kutoa vitisho kwa serikali?

Aliyewaambia Rais Kikwete anatembea na ajira za watu walioitimu mafunzo ya JKT mfukoni nani? Ina maana hadi sasa hamfahamu mfumo unaotumiwa na serikali kutoa ajira? Siyo bure mnalenu jambo na litabainika tu.Na mnachokitafuta mtakipata.

Kuna Watanzania wanashahada zaidi ya Moja   bado hawajapata ajira na hata elimu ya stadi za kazi Kama Nyie lakini hata siku Moja hatujawasikia wakiwa na nia Kama yenu ya Kutaka Kutenda jinai ya kutaka kuandamana siku Tatu mfululizo na kushinikiza kuonana na rais muda wanaoutaka wao.

Yaani Nyie kupiga paredi la JKT tu na kuvaa Maganga ya JKT na kwenda kuishi muda mfupi Katika makambi ya JKT kwaajili ya kuudhulia Mafunzo basi imekuwa nongwa mnaanza kutishia Usalama taifa Lenu eti mtaandamana siku Tatu mfululizo usiku na mchana.

Aliyewaambia ajira zipo serikali tu ninani? Hivi Watanzania wote hapa wanaofanya kazi na kutunza familia zao wana ajira za serikali?Siyo kweli.

Mbona mnataka Kuwa wa binafsi hivyo, mmepewa Mafunzo ya stadi za kazi bure wakati wenzenu Mafunzo hayo wanalipia Karo kubwa Katika chuo cha Ufundi VETA, badala ya Nyie Leo hii Kutafuta mitaji kwa njia halali ili muweze kutumia ujuzi mlioupata Katika Mafunzo ya JKT, mnaishia kuamasisha kukutana kushinikiza kukutana na rais na kukusudia kufanya maandamano ya siku Tatu mfululizo.

Hata Kama kweli kuna MTu anataka Kuwasaidia, kwa vitisho hivyo mlivyoviweka ,sia atakataa makusudi kuwasaidia ili hawaone mwisho wenu mtafanya nini .

Maana ni Nyie ndiyo wenye Shida lakini mmeonyesha kwanza hamna nidhamu,subira na mmeshindwa hata kumfuata Mkuu wa JKT kumweleza matatizo yenu ili yeye atafikishe sehemu husika.

Na kwa tabia hizo ndiyo maana vijana hatuaminiwi kwasababu Hatuna subira, uvumilivu na hatutaki kufuata utaratibu.Tunakosa vitu Vingi Vya mAana vijana kwasababu tu Wengi wetu Hatuna nidhamu, subira tuna papara sana.

Mnamtishia nani nyau?mnajitapa mmepatiwa Mafunzo ya kijeshi,nani aliwapatia Nyie Mafunzo ya kijeshi? HIvi nyie mngekuwa mmepatiwa mafunzo ya kijeshi hasa mngefanya wazimu huo mnaoufanya? 

Mmejinasibu wenyewe  Kuwa  mmepata  Mafunzo ya kijeshi na Kuwa  wahitimu wa mafunzo hayo toka Zanzibar wanapata upendeleo Nyie wa Tanzania Bara hampati,basi Kama vipi ingieni kabisa msituni tujue Moja Halafu muone mtakachokutana nacho huko Msituni.

Maana kwa wahitimu Kama Nyie kutangaza tena kupitia vyombo Vya Habari Kuwa makusudia kufanya maandamano kwa siku Tatu mfululizo tena usiku na mchana, hii Kauli siyo ya kupuuzwa na wapenda Amani  wa nchi hii hata kidogo, inatakiwa ifanyiwe kazi na aliyetoa hiyo Kauli aitiwe na mamlaka husika akahojiwe alikuwa anamaanisha nini.

Maana hata Hilo Jeshi la Polisi haliwezi kutoa Kibali cha kundi lolote liwe Chama cha siasa ,wahitimu wa Mafunzo ya JKT kuandamana kwa siku Tatu mfululizo tena usiku na mchana.  

Wanajeshi wetu ni watu wenye nidhamu ya hali ya juu na wamefundwa wakafundika na linasifika ndani na nje ya nchi  ndiyo maana hata siku moja hatujawahi kuwasikia wakifanya huo wazimu wenu wa kutwa kurandaranda  Ikulu na kutangaza kutaka kufanya maandamano ya siku tatu mfululizo Jijini Dar es Salaam eti kushinikiza kuonana na rais.

Mnawaadaa  watu huko  mitaani Kuwa Nyie ni Wanajeshi,Nyie siyo Wanajeshi kwani hata mafunzo ya kupigana vita hamjafundishwa na Kama kweli mngelikuwa ni Wanajeshi siku ile ya Februali 15 Mwaka huu,pale ukumbi wa Msimbazi Center ,mlivyokuwa mnabwabwaja mngekuwa mmeishakamatwa muda mrefu na kushitakiwa kwa kosa la uani.

Mwanajeshi hasa akitaka kufanya lake hatumii mbinu ya kipuuzi Kama mliyoitumia  Nyie ya kuitisha mkutano na vyombo Vya Habari na kutangaza mikakati yenu ya Siri adharani mapema Kabla ya kutimiza adhima yenu  na bila kujua Tayari mmeisha mpa faida adui yenu ambae ni wazalendo wa kweli wa taifa hili na wanausalama wa taifa hili.

Nyie ni 'Makorokoroni'  na ndiyo maana Leo hii Hamuwezi kwenda kufayakazi wanaofanya kazi Askari wa JWTZ. 

Na haya ndiyo madhara ya majeshi yetu kuokotaokota watu mitaani Kumbe wanatabia mbovu wanaingizwa Kwenye makambi ya majeshi yetu mwisho wa siku ndiyo wanakuwa Kama hawa na wengine Kutwa kuchukua Rushwa mitaani, kuuza meno ya Tembo na kushirikiana na wahalifu kufanya Uhalifu.

Nyie siyo Wanajeshi kamili na wala hamkupewa Mafunzo ya kivita, mlienda kupewa Mafunzo ambayo siyo ya kupigana vita .Nyie ni wana mazoezi tu yaani watu Jogging kama Happiness Katabazi, hamjala viapo kama walivyokula wanajeshi, ni Makorokoroni na wala msitutishe na mnachokitafuta mtakipata 'soon'.

Na baadhi ya watu waliohitimu Mafunzo ya JKT wenye akili timamu ,wazalendo kwa taifa Lao na wala hawakubali kutumiwa na vyama Vya siasa ,elimu ya stadi za kazi zimewasaidia sana Kwani wamekuwa wajasiriamali wengine ni Mafundi selemara,wachoma chips na walinzi wa makampuni binafsi na washokaji nguo na wa kulima wazuri.

Kwa elimu gani mliyokuwa nayo nyie wahitimu wa mafunzo ya JKT hadi mtake ajira kutoka kwa Rais Ikulu? Ni aina gani hiyo ya ajira mnayoitaka mmpewe na Rais Kikwete?

JKT imewafundisha mafunzo ya stadi za kazi hamtaki kuzitumia, mmebweteka ,mnajazwa ujinga mitaani na watu wasiolitakia mema taifa hili na nyie mnaingia kichwa kichwa mnakubali mnaanza kuzungumza upuuzi wa vitisho Mbele ya vyombo Vya Habari.

Mbona ajira zipo kibao katika mashamba ya Mpunga, Miwa,kuzoa matakataka ,kufagia barabara kwenye makampuni ya Ulinzi ,Mbona hamuendi kuomba ajira huko mnashupalia kwenda Ikulu kumuona rais awape ajira?

Au mmetumwa Nyie na watu wa baya mmdhuru rais wetu ili Tanzania iweke rekodi ya Kufiwa na rais ambaye yupo madarakani?Mkome.

Maana hii kasi yenu ya kushinikiza kuona na rais Kikwete tena nammefika Mbali zaidi mnasema msipoonana naye mtaandamana siku Tatu mfululizo usiku na mchana na mtatumia silaha na kwamba eti mnamafunzo ya kijeshi inatia Mashaka.

Kwa taarifa yenu wananchi tuna haki ya kuonana na rais pale tu wasaidii wake watakapojiridhisha una haki na Dhamira safi ya kumuona lakini kwa Nyie wahitimu wa Mafunzo ya JKT kwakuwa mmeisha onyesha mna dhamira Mbaya siyo Siri nawashawishi wasaidizi wa rais wasikubali kumruhusu rais kuona na wahuni hawa ambao kwanza wamedhlilisha wakufunzi wa JKT waliowafunza Maadili Mema Katika Mafunzo ya JKT ,na tuwaruhusu waende huko mitaani na hayo Mafunzo ya kijeshi na hayo Magobole Kama wanayo tunawaone mwisho wao.

Walinzi wa Rais Kikwete watakuwa ni vichaa Kama watamruhusu Rais akaonane  na Nyie wahuni ambao mmetoa vitisho wakati Nyie Ndio wenye Shida.

Sasa Nyie mlipokutana pale Msimbazi Center ,ambao sijui mnawazimu vichwa ni mwenu badala ya kutumia elimu ya stadi za kazi mliyoipata mkiwa Katika Mafunzo ya JKT mnaanza kujihusisha na vitendo Vya kutaka Kutenda jinai kwa makusudi kwa kisingizio eti Mnazuiwa kumuona rais.

Mkuu wa Wanajeshi wote hapa nchini ni Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ)' Davis Mwamunyange. Kama kweli Nyie wahitimu wa JKT ni Wanajeshi maana mmesema mmepewa Mafunzo ya kijeshi,kwanini hayo malalamiko yenu hamjayapeleka kwanza kwa CDF- Mwamunyange?

Au ndiyo akili zenu fupi  zinawatuma kuamini Kuwa Mwamunyange ameshindwa kazi  na Nyie ndiyo mnaweza kazi? Ndiyo maana Nasema siyo bure mnalenu jambo na litajulikana tu wakati ukifika.

Mnalalamika ajira hamna Ina maana hamna kipato .Swali langu Je hizo Fedha za kununua muda wa maongezi mkawasiliana hadi mkakutana pamoja na nauli za kuwafikisha pale Msimbazi Center ,Fedha za kuandika barua kwenda Ikulu,kuitisha mkutano na waandishi wa Habari mlizipata wapi? Si mmesema mna Hali Ngumu na hamna ajira hizo Fedha za Kuratibu ule mkutano mlizipata wapi?

 Msijifanye wajanja sana kuliko watangulizi wenu ambao waliwatangulia kuudhuria  Mafunzo hayo. Kuna watu wahuni na wajanja kuliko Nyie wanawatazama.

Kuna watu wana akili nyingi kuliko Nyie Kwani Tayari  hizo harakati zenu zimeanza kuhusishwa na siasa chafu Kuwa miongoni mwenu mnatumiwa na wanasiasa kutaka kuleta vurugu hapa nchini kwakisingizio hicho cha kutaka kuonana na rais na ajira.

Kwa kupitia tamko Lenu ni wazi mnania ovu ya kushinikiza mpatiwe  mnachokitaka kwa muda Mnaoutaka Nyie na siyo Ratiba ya rais na tena kwa kutoa vitisho eti mtaandamana siku Tatu mfululizo. 

Ombi langu kwa Jeshi la Polisi lisitoe Kibali cha kuruhusu wahitimu  hawa waandamane maana kupitia matamshi Yao wameonyesha hawana Dhamira njema na taifa hili kwani wao ndio wanashida,wanaomba lakini wakati huo huo wanaomba wanatoa na vitisho.

Kwanza wanadhalilisha Mafunzo waliyoyapata walipokuwa JKT Kuwa wakufunzi wao hawa kuwakuwafunza nidhamu au Kama waliwafunza basi wameamua kukengeuka,na ikitokea waliandamana kwa lazima ,Polisi ipambane nao Kiume na kwa silaha za kutosha maana tayari wameishautangazia umma Kuwa   wamepewa Mafunzo ya kijeshi hivyo wapo timamu.

Pili, Jeshi la JWTZ,JKT Idara ya Usalama wa Taifa  iwatazame kwa karibu sana wahitimu wote walioudhuria mkutano wa wahitimu hao wa JKT ambao walifikia  azimio Hilo la kuitisha maandamano ya siku Tatu mfululizo usiku na mchana.

Kama vijana wenyewe Ndio hawa ambao walipelekwa JKT kufundishwa Maadili Mema,stadi za kazi na kujazwa uzalendo kwa Taifa Lao,Leo hii wao ndiyo watakuwa mstari wa Mbele tena bila woga wanaenda Mbele ya vyombo Vya Habari Kusema wanataka kuandamana maandamano ya siku Tatu mfululizo usiku na mchana kwa kukishinikiza waonane na rais ,Wapewe ajira na wasikilizwe matatizo Yao.Ajabu sana.

Wahitimu hawa Kama wanatakiwa watiwe  adabu mapema na vyombo Vya dola ,basi ipo siku wahitimu hawa wanaweza Kuja kurubuniwa na watu wasiolitakia  Mema taifa letu Wakatisaliti taifa kwa kisingizio tu eti hawajapewa ajira na serikali wakati Hakuna mkataba wowote waliingia na serikali Kuwa wakimaliza Mafunzo ya JKT ni lazima serikali iwapatie ajira.

Ikumbukwe Kuwa Tanzania Kama taifa Mwaka huu tunamambo mawili makubwa Mbele yetu ya kupiga kura za Katiba Pendekezwa na Uchaguzi Mkuu na chaguzi za wagombea urais,ubunge, madiwani ndani ya vyama.Tunataka tufanye mambo hayo kwa Amani na utulivu,hatutaki Fujo. 

Na Ieleweke hivi sasa Vituo Vya Polisi vinavamiwa Mara kwa Mara na wahalifu na kuua Askari na kupora silaha na matukio mbalimbali ya kihalifu yanatokea.

Ndipo tumefika hapo Tulipofika Kama taifa ,baadhi ya raia wamekuwa na ujasiri wa kishetani   hadi hawaogopi tena polisi wala vituo vya polisi.

Hatujui mhasisi wa wazo la kuvamia vituo vya polisi ni nani na alikuwa na malengo gani ya kuasisi wazo hilo ambalo kwakweli linashangaza watu wanaofikiri sawasawa na kubaki kujiuliza huo ujasiri wa kuvamia vituo vya polisi na kuua askari na kupora silaha  raia hawa Watanzania wanaupata wapi?

Nimalizie kwa Kusema baadhi ya wahitimu wa JKT mnaotaka kuandamana mnalenu jambo na mnachokitafuta kwa njia za za kifedhuli  mtakipata.

Nimalizie kwa kumwambia   Mwenyekiti wa Vijana wa waliohitimu Mafunzo ya JKT ,  George Mgoba na wenzake  kuwa Sisi Watanzania tunadesturi ya kunyimana matonge ya ugali ,hatunyimani maneno.

Hivyo siri zenu zitabainika na zikibainika mkianza kushughulikiwa na mamlaka husika ndiyo  mtajua 'kachumbali siyo Mboga ila ina save'.Na mnachokitafuta mtakipata 'soon'.

Mungu ibariki Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Februali 17 Mwaka 2015.No comments:

Powered by Blogger.