Header Ads

WAHITIMU MAFUNZO JKT MLICHOKUWA MNAKITAFUTA MMEKIPATANa Happiness Katabazi
FEBRUALI 17 Mwaka huu, niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho : ' WAHITIMU MAFUNZO JKT MNACHOKITAFUTA MTAKIPATA SOON'. 

Februali 23 Mwaka huu, niliandika makala nyingine iliyokuwa na kichwa cha Habari kisemacho : ' WAHITIMU MAFUNZO JKT KUMBUKENI MLIKULA KIAPO CHA UTII'. 

Na leo tena nimejitokeza tena kuandika makala hii yenye kichwa cha habari kisemacho ' WAHITIMU MAFUNZO JKT MLICHOKUWA MNAKITAFUTA MMEKIPATA'.

Makala  zote hizo zinapatika kupitia Blogg yangu ya www.katabazihappy.blogspot.com na ukurasa wangu Facebook: Happy Katabazi.

Kwa kifupi makala zangu zote hizo zilibeba ujumbe wa kukemea vikali tabia chafu na ya kidharimu na ya uvunjwaji wa Sheria za nchi zilizokuwa zilifanywa  na vijana waliotimu Mafunzo ya JKT ambao Februali 15 Mwaka huu, walifanya mkutano na waandishi wa Habari eneo la Msimbazi Center na Kusema kuanzia Februali 23,24,25 watafanya maandamano ya usiku na mchana Jijini Dar es Salaam, kushinikiza waruhusiwe kuonana na Rais Jakaya Kikwete kwasababu hawajapatiwa ajira.

Vijana Hao ambao elimu zao ni ndogo   minawaona uenda wanawazimu kichwani walifikia hatua ya kutoa baadhi ya  Siri za Mafunzo waliyoyapata JKT Mbele ya waandishi wahabari kwakusema Kuwa wamepata Mafunzo ya kijeshi na kutaja aina za silaha nzito wanazoweza kuzitumia na kwamba wanaweza kujiunga na vikundi Vya ugaidi Kama hawajapatiwa ajira wakati wanafahamu wazi Hakuna mkataba wowote waliingia na JKT wala serikali unaonyesha ni lazima serikali iwapatie ajira.

Pia Katika makala zangu hizo mbili ambazo zilizusha  mjadala mkali ambao wananchi wakiwemo wanausalama toka vyombo Vya Ulinzi na Usalama, maofisa wa serikali na wananchi wanaitakia Mema taifa Hilo walinipongeza  sana isipokuwa baadhi ya watu wachache waliojitambulisha Kuwa ni wahitimu wa JKT  walinitishia maisha.

Kwakuwa mimi ni miongoni mwa waandishi wa kike wachache sana nchini ambao ni jasiri  nilikuwa nikiwajibu hivi siwaogopi ,nakuwatajia eneo nilipo wanifuate wanidhuru kama wataweza na nilizaliwa siku moja na siku moja nitakufa na sitishiki na vitisho vyao. 

Niliwakumbusha wahitimu hao  wakumbuke walikula kiapo cha Utii kwa serikali Yao na hivyo hawapaswi kuvunja Sheria za nchi hii ikiwemo kusaliti Viapo vyao kwa kuandamana, Kugoma na kutaka kufanya uhasi .

Kwa nia njema niliwakumbusha kuwa  Mafunzo waliyoyapata kule 'jandoni' yaani JKT yanawataka  wawe na nidhamu na wa watii   viongozi wao Sheria na Jamii kwa ujumla na niliwaambia  kabisa madhara makubwa wanayoweza kuyapata kutokana na matendo Yao ya kiuwenda wazimu ya kutaka kushindana na dola.Hawakutaka kunisikia.

Ushauri wangu kupitia makala hizo waliuupuuza  lakini naamini kuanzia Februali 22,23 na 24 Mwaka huu, watakuwa kimoyo moyo wanakubali sasa Kuwa Mimi nilikuwa ni mtu mwema Kwao   na Laiti wangezingatia  Nasaha zangu katika zile makala yasingewakuta yaliyowakuta leo hii.

Mabalaha  yote yanayowakumba sasa ya Kukamatwa msobemsobe ,kulazwa maabusu  za polisi, kufunguliwa Kesi za jinai mahakamani na kufungiwa dhamana na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kutibiwa  chini ya Ulinzi Mkali wa Polisi, Kuanza kuishi kwa  Mashaka Kama 'wanaoga  barazani ' kwasababu dola linawaandama   yasingewafika.

Ila kwakuwa kwanza walinidharu na kuniona mi ni chizi na kuniita mwanamke Malaya , sina akili nilisema sawa Kwani Tayari nilishajua  vijana wanachezea Moto na hawafiiki Mbali watanasa kwenye nyavu na kweli wamenasana kwenye nyavu tena chap chap.

Kwani   Februali 15 Mwaka huu ,ndipo walipoanza mbio zao za Marathoni za kulichokoza dola kwa kufanya mkutano na waandishi wa Habari  nakuanika mikakati yao ya jinsi ya kuvunja sheria za nchi.

 Kesho yake Februali 16 mwaka huu,  Mungu alimlaani mwenyekiti wa Umoja wa wahitimu hao George Mgoba ambapo watu wasiofahamika  'watoto wa Mbwa'  Walimteka  kwa siku tatu na kumfanyizia.Na Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi wa kubaini tukio Hilo ni la kweli au ni Sinema ya Kihindi imetengenezwa na Mgoba na wenzake.


Februali 22 Mwaka huu, wahitimu hao tena waliitisha mkutano na waandishi habari eneo la  Msimbazi Center na kutaka iundwe Tume huru ya kuchunguza nani alimteka Mgoba na kwamba Machi 23 Mwaka huu hawataandamana tena wanajipa muda wa kwenda kujipanga zaidi. 

Na kwa wahitimu hawa mi nalazimika Kuwaita ni wendawazimu walipomaliza mkutano huo na wakatoka eneo la walilofanyia mkutano na kuanza safati ya kuelekea hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa Mgoba huku wakiwa wengi hali iliyosababisha  Polisi kuwazuia getini kuingia kumuona Mgoba na Polisi kuimarisha Ulinzi eneo Hilo na kuwakamata baadhi ya wahitimu na kwenda kuwaifadhi Katika Kituo Central.

Ilipofika Februali 23 Mwaka huu, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova  aka ' Marketing Officer '  wa Jeshi la Polisi alifanya  mkutano na waandishi wahabari na Kusema Kuwa kwanza Jeshi lake linafanya uchunguzi kujua ninani alimteka Mgoba na Je ni kweli alitekwa Kama alivyodi , akawataka wahitimu wa Mafunzo ya JKT kuanzia siku hiyo wakome kabisa kufanya maandamano wala mikutano Jijini Dar es Salaam na kwamba  wanawashirikiria wahitimu Kadhaa kwa makosa ya kufanya mikusanyiko haramu na uchochezi na kumtaka Makamu Mwenyekiti wa umoja wa wahitimu hao Kokote alipo  ajisalimishe Mara Moja Katika Kituo chochote cha Polisi.

Tamko Hilo la Marketing Officer wa Jeshi la Polisi Yaani Kamanda Kova  liliwadhiirishia sasa serikali Imechoka na vitendo vyao na imeanza kuwashughulikia Hali iliyosababisha Kunywea kabisa na adabu zao Kuzitia mfukoni.

Minasema asante sana vyombo vyote Vya serikali vilivyofanya kazi usiku na mchana hadi mkafanikiwa kuwasambaratisha hawa wahitimu wa JKT Kwani Katika makala zangu zile mbili niliomba sana serikali kupitia mamlaka zake ziamke usingizini zianze ' kutroti' na wahitimu hao wa JKT ambao wamekosa adabu na nidhamu.

Baadhi ya wahitimu  walinipigia simu nakuniita  Mimi ni   Malaya na hawara yangu  yangu Rais Jakaya Kikwete,Nina utaka  UDC  sina akili na matusi ya kila aina na vitisho Vya kila aina.

Sasa serikali imeishawabananisha kila kona na kuwadhoofisha  na wengine ndiyo mmefunguliwa Kesi na dhamana mmemfungiwa, mmepelekwa gerezani hadi siku DPP atakapojisikia  kuondoa mahakamani hati ya kuwafungia dhamana.

Binafsi sina Shaka kule magerezani mlikopelekwa Jana kuna  mahabusu wanaume wanatabia za kibazazi  wamewapokea  kwa shangwe na sijui kama mtasalimika. 

Hatutaka kusikia Mkilalamika   mahakamani Kama wale viongozi wa dini ya Kiislamu  ambao walikuwa wakijifanya vijogoo kule Zanzibar ambao ni viongozi wa Mihadhara  ya Kiislamu UAMSHO, wanaokabiliwa na Kesi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,walalamika sana Kuwa wamelawitiwa na kuaribiwa vibaya sehemu za Siri wakiwa gerezani .

Je hadi sasa mazito yaliyowafika na jinsi mlivyosambaratishwa na mnaendelea kushughulikiwa, bado mnaendelea na msimamo wenu wa kuniona Mimi ni Malaya Sina na  na mwendawazi?

Kwa upupu huo ambao Tayari serikali kupitia Kamanda  Kova na Manjagu wake ,  DPP- Biswalo Mganga wamewamwagia na unawawasha hivi sasa mnajikuna Umesababisha mfyate mkia, bado tu mnaendelea kunichukulia Mimi sina akili?

Hakuna Mashaka wala ubishi Mimi Happiness Katabazi  ni mwanamke  jasiri sana, nina akili kuwazidi Nyie wendawazimu ambao licha mlipitia Mafunzo ya uaskari nimewatikisa vizuri sana na kufanikiwa kuwavuruga akili zenu ,kusambaratisha mipango yenu hadi hivi  sasa mmeishia kuanza kutumia mbinu za kunipigia simu na kunitumia SMS za maswali ya kipuuzi ambazo zina lengo la kunidadisi Mimi ni nani? 

Kwa akili Zenu Fupi mna mbinu Zenu za kijinga nawaakikishia hamtakaa mfanikiwe hicho  mnachotaka kunifanyia  maana mnatumia mbinu za kijinga jinga Kutafuta taarifa zangu mbinu ambayo hata mwanangu Queen 'Malkia' hawezi kuzitumia  Kutafuta taarifa za Mtu.

Aliyewaambia Nina Shida ya Kuwa na bwana lofa   Katika Kipindi hiki cha Takribani wiki Moja tangu nilipoandika jumla ya makala Tatu kwa mpigo zinazokemea matendo yenu nyie baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya JKT ya Uvunjifu wa nani? 

Aliyewaambia Mimi nataka kuolewa na mwanamme ambaye tayari mwanaume huyo ameishautangazia  umma Kuwa Hana ajira, mgomvi kwa serikali ,anakubali kutumiwa na wanasiasa ambao ni wanaume wenzake nani?Tena mnikome sina Fedha za kulea mwanaume  ambaye Hana ajira na Hana nidhamu na anayehatarisha Usalama wa nchi.Mnikome.

Mlisema Mimi misina akili kwasababu zile makala zangu zimewakera, minasisitiza Mimi Nina akili nyingi sana kuliko Nyie Kwani Mimi sasa Naishi huru Nyie mnaishi Kwa Mashaka kwa kuhofia kushughulikiwa na dola.

Mlisema Mimi sina akili na mwendawazimu na Malaya ,Minasema Nina akili sana ndiyo maana kupitia makala zangu kuhusu Nyie, sijafunguliwa Kesi za jinai, Polisi hawajanikamata wala kunisaka zaidi ya kunipa BIG UP kwa makala nzuri, DDP hajanifungulia Kesi na kunifungia  dhamana na wala siishi gerezani Kama mlivyoanza kuishi gerezani Jana .

Haya Nyie wenye akili timamu Leo hii kikowapi Mbona inaelezwa mlivyokuwa mlivyotiwa nguvuni na wanaume wenzenu mlikuwa mnaangua kilio na kuomba msamehewe msipelekwe mahakamani na gerezani?


Hapo Mwendawazimu ni Katabazi au Nyie wahitimu wa Mafunzo ya JKT? Jibu ni Jepesi ni baadhi ya wahitimu wa Mafunzo ya JKT ndiyo wendawazimu na ndiyo maana dola linawashughulikia kikamilifu wao na siyo Happiness Katabazi.

Mlivyoona makala zimeandikwa na mwanamke yaani mimi kwasababu napenda kujipodoa ,mimi raia nyie mmepitia mafunzo ya JKT basi mkanichukulia 'poa'? Hivi mnafahamu kuwa nipo kwenye taaluma ya uandishi wa kwa miaka 15 sasa?  Na Karamu yangu ni Kali sana makala zangu mbili mlizozibeza zimekuwa ni Moja ya Kisu kilichotumika kuwachinja Nyie ? Ndio mjifunze kuwa karamu ina nguvu.

Msimdharau Mtu  msiyemjua, na kumbukeni Kuwa Mwanamke ana Nguvu sana katika mambo mengi tu .Mwanamke anaweza Kujenga famila au Kuibomoa.Mwanamke pia  anaweza  hata Kuaribu kazi ya mume wake.

Sasa kwa taarifa yenu kutokana na ufedhuli wenu mliyoufanya  hata majeshi yetu hayawezi  kuwapa ajira kwasababu mmethibitisha Pasipo Shaka kwamba hamna nidhamu na hampaswi tena  kuaminiwa  kupewa kazi hizo za kijeshi Kwani endapo mkipewa mnaweza kukodisha silaha zetu kwa wahalifu ili wa zifanyie  Uhalifu au mvujishe Siri za Jeshi kwa maadui zetu. 

 Mbona Nyie Askari wa JKT mliojifanya mnaakili Mbona mnaishia gerezani na Kesi ya jinai mmefunguliwa na mmeishakuwa watumwa wa Mahakama? 

Na makala zangu zimemchangia na zitaendelea kutoa hamasa kwa vyombo vya dola vizidi kuwashughulikia  kikamilifu ili mpone huo wendawazimu wenu unaowasumbua vichwani ambao ulikuwa unawatuma kufanya vurugu na kukiuka viapo mlivyokula na mafunzo mliyofunzwa mafunzo JKT.

Askari gani mmepita JKT mlivyo rejea  uraiani mnakubali  kutumiwa kirahisi na  wanasiasa  toka Chama Kimoja cha siasa ambacho Chama hicho kimekuwa na rekodi ya kufanya maandamano na vurugu kila kukicha.

Hivi hamkumjua  Hao wanasiasa  ndiyo  tabia zao za Kupenda kuwatumia hata wanafunzi wa baadhi ya vyuo vikuu wafanye migomo na wanafunzi wakigoma na kupigwa na Polisi na kufikishwa mahakamani yeye wao wakaa Mbali? 

Leo ni familia Zenu na wazazi wenu ndiyo wanaangaika kuwaletea Chakula gerezani na kuwafanya wakose Furaha na Amani ndani ya mioyo Yao kwasababu mmefunguliwa Kesi na mnaishi gerezani.

Askari gani mnakubali kurubuniwa na Raia kirahisi namna hii? Ndiyo aliwaaidi Kuwa eti uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu, Chama chao kitakamata  dola na Nyie ndiyo mtakuwa Jeshi jipya la serikali ya Chama hicho ambacho kwa sasa ni Chama cha upinzani.

Haya tambo Zenu, vibweka vyenu ,mikwara yenu imeishia wapi hivi sasa? Mbona mmekuwa wapole ghafla?Si mlitutangazia kuwa ni mmepata mafunzo ya kijeshi na mnaweza kutumia silaha.

Sasa inakuwaje askari nyie wenye mafunzo ya kijeshi mnadai kiongozi wenu ameweza kutekwa  kilaini  na wanawake,  polisi ambao hawana mafunzo Ya kijeshi wanafanikiwa kuwakamata kiraini kama wanakamata Kuku Bandani? Ni kihoja cha aina yake.

Haya wale mabwana zenu waliokuwa  wanawatumia kwa Siri na Nyie mkakubali kugeuzwa geuzwa Kama Chapati na bwana Zenu   yaani wanasiasa  ili muanzishe vurugu hapa nchini, Mbona hajajiokeza Kuwatetea au kumpelekea uji  au supu ,Mgoba Hospitalini au Kuwapeleka Chakula gerezani wale wahitimu wa JKT walipelekwa gerezani Jana?

Ndiyo mkome  na ndiyo muwajue wanasiasa uchwara wa nchi hii walivyo na roho mbaya za kupenda kuwatumia vibaya watoto wawenzao wafanye vurugu ili wapate umaarufu katika siasa na pindi dola ikibaini njama hiyo ikaanza kuwashughulikia wanasiasa hao uwa wanakaa mbali utafikiri hakuwatuma kufanya matendo yale.

Chezea Kamanda Kova aka 'Marketing Officer  wa Jeshi la Polisi'? lazima utadeki Bahari na kweli wahitimu wa JKT mmedeki Bahari. 

Poleni sana kwa mazito yakiyowakuta na yatakayoendelea kuwakuta baadhi ya wahitimu mafunzo JKT na ndiyo muanze sasa Kuwa wapenzi wa makala zangu Kwani  licha ya Mimi Kuwa Mwandishi wa Habari  pia ni msomi wa Sheria hivyo makala zangu nyingi zinasisitiza watu kuheshimu Utawala wa Sheria Kwani Kifungu cha 8 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Mwaka 2002, inasema kutojua Sheria sio kinga ya kutoadhibiwa.

 Wahitimu wa Mafunzo ya JKT mlichokuwa Mnakitafuta mmekipata.Hongera DPP - Mganga, Kamanda Kova na vyombo vyote Vya Ulinzi na Usalama kuwapatia kile walichokuwa wakikitafuta wahitimu Kwa Takribani wiki Moja.

Maana walichokuwa wakitafuta ni kulala selo za Polisi na kweli baadhi Yao wamelala, kufunguliwa Kesi ya jinai kweli wamefunguliwa Kesi ya jinai Jana ,na walikuwa wanahamu kubwa sana ya kwenda kuishi gerezani na kupata ajira gerezani  ili waweze kulala mabazazi ,wash enzi wa tabia na kweli DPP - Mganga amewatimizia Haja Yao ya Kupenda kwenda kulala gerezani DPP amewafungia dhamana. 

Asante sana DPP- Mganga umenifurahisha sana kwa uamuzi huo wa kisheria wa kuwafungia dhamana washitakiwa Hao kwasababu Kifungu cha 148(4) cha   Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002, kinakupa mamlaka wewe  DPP  Kuwasilisha mahakamani kwa maandishi hati ya kumfungia  dhamana kwa maslahi ya taifa mshitakiwa yoyote anayekabiliwa na Kesi ya jinai ambayo ina dhamana.

Itakumbukwa kifungu hicho cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, kilitumiwa na aliyekuwa DDP- Dk.Eliezer Feleshi  a mbaye hivi sasa ni  Jaji wa Mahakama Kuu Kamda ya Dar es Salaam, kati Kesi ya uchochezi Na.245/2012 Jamhuri dhidi ya Sheikh Ponda na wenzake 49 Katika Mahakama ya Kisutu .

Kesi hiyo ilifunguliwa rasmi Oktoba 18 Mwaka 2012 na ikimalizika rasmi Mei 9 Mwaka 2013 ,Ponda Kipindi chote hicho alikuwa akiishie gerezani kwasababu DPP alimfungia dhamana na aliachiwa siku hiyo ya Mei  9 mwaka 2013 siku hukumu ya kesi hiyo ilipotolewa ambapo alitiwa hatiani kwa kosa moja tu la kuingia kwa jinai katika kiwanja cha Chang'ombe Markaz ambapo alifungwa kifungo cha mwaka mmoja nje.

Hata hivyo Ponda alikataka rufaa   Mahakama Kuu Kanda a Dar es Salaam kupinga hukumu ya Mahakama ya Kisutu,ameweza kushinda rufaa yake mwaka 2014 Kwani Mahakama Kuu imetengua hukumu ya Mahakama ya Kisutu iliyomfunga Kifungo cha Mwaka mmoja .

Hata hivyo  Agosti mwaka 2013 DPP alimfungulia kesi mpya ya uchochezi Ponda inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro na DPP  Akawasilisha tena hati ya kumfungia dhamana Hali nayosababisha hadi sasa Ponda kuendelea kusota Katika Gereza la Segerea na siku ya Kesi yake anasafirishwa hadi Mkoani Morogoro chini ya Ulinzi Mkali.

Safi sana DPP- Mganga ,lazima wavunja Sheria watambue upo na na hutasita kutumia Kifungu hicho kwa washitakiwa wowote na ulipoteuliwa Kuwa DPP niliandika makala ya kukuelezea wewe ni MTu wa aina gani sasa nafikiri hawa makorokoro hawakuisoma ndiyo maana wakawa wanaovunja Sheria za nchi na kusahau nchi hii Inaongozwa kwa mujibu wa Sheria.

Wahitimu Mafunzo JKT ' washitakiwa ' ile Ikulu mliyokuwa mnataka kwenda mmekwenda sasa tena bila maandamano Kwani basi la Jeshi la Magereza limewaogopesha lifti hadi Ikulu(Gerezani).

Na bila Shaka mmeishaonana na Rais wa Ikulu hiyo ambaye ni Bwana Jela na na ni naimani  ameishawapatia ajira mliyokuwa Mnaitafuta kwa njia haramu.

Naamini tutakuwa tu naonana Katika likizo yenu fupi ambayo ni ya saa Chache kila baada siku 14 kuanzia Leo pale kwa Pilato Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mtakuwa mkitusimulia mnaendeleaje na ajira yenu mpya na jinsi mnavyoifanya huko gerezani na Hali hii ya Joto Kali bila Shaka mnajituma sana.

Embu nyie wahitimu wa JKT 'washitakiwa' wa kumbukeni na wahitimu wenzenu mliokuwa mna watetee Katika umoja wenu nawao ili Polisi, DPP na bwana Jela waweze Kuwapa ajira gerezani Badala ya kufanyiwa usajili na kuonekana wanasifa Kama Zenu za kupewa ajira gerezani.

Hakika mmeishia onyesha mna sifa ya kupata ajira gerezani ajira ambayo mnaijua  nyie ,hongereni kwa kupata ajira ndani ya Gereza.Hongereni sana.

Ila nawashangaa mmeupoteza muda wenu mwingi kushiriki mafunzo ya JKT Kama mngefahamu mapema   Moja kwa Moja gerezani kwa kutumia njia hii mliyoingilia jana gerezani na bwana jela akawapa ajira nafikiri hadi KWA muda wote huo ningekuwa mmepata na Promosheni.

Hata hivyo hamjachelewa sana kwa Sababu tangu Jana mlipofikishwa  gerezani mmepata Mafunzo mapya kutoka kwa walimu wanaoitwa NYAPARA .Nyapara hawapatikani JKT wala sehemu nyingine yoyote isipokuwa Magerezani.Hongereni sana.
 
Namalizia Kwa Kusema Kuwa wale mabwana waliokuwa wanawatuma Kutafuta hiyo Kazi ya kwenda gerezani, Mtakapostaafu yaani kutoka gerezani mtawapelekea Habari Kamili Kuwa hiyo Kazi mliyoipata huko gerezani ni kanzi bomba sana. Naamini hivi  sasa  mmekuwa watamu Kama  Mcharo.

Mnaleta ujasiri wa Albino wa kutembea usiku tena katika mikoa ya Kanda ya Ziwa peke yako  lazima utekwe ,ukatwe viungo na uuwawe kikatiri.Ndiyo Nyie wahitimu wa JKT mlikuwa mnalichezea dola limewashughulikia. 

Kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  hadi jeshi la Magereza  yaani jeshi la kulinda Wafungwa na mahabusu ,hiyo ni ajira nzuri kwenu  ambayo mlikuwa mkiisaka kwa udi na uvumba na vitisho.

Kwa kuwa serikali ya awamu ya Profesa Jakaya Kikwete ni sikivu sana na inawapenda mno Jana imeamua kuwapatia ajira hiyo rasmi huko Katika Gereza la Segerea.Hongera serikali kwa kutekeleza ombi la wahitimu Hao wa Mafunzo ya JKT kwa vitendo.

Hongereni kwa kupata ajira hiyo ambayo Hakuna Shaka mlikuwa mkiitafuta sana na kweli Mungu Amesikia kilio chenu.

 Washindi  wa mbio za Marathoni kutoka Msimbazi  Center, Msitu Kibaha ,  Hospitali ya Taifa Muhimbili, Central Polisi ,Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  Mpaka Gereza la Segerea   wajulikana jana nao Si wengine ni viongozi wa umoja usiyo rasmi  wa wahitimu wa JKT wa wahitimu wa JKT nao ni Mgoba  ambaye amecheza filamu ya Kihindi na wenzake ambayo stering uwa anakufa, Makamu Mwenyekiti Parali Kiwango, Katibu Linus Steven na wahitimu wengine Emmanuel Mwasyembe, Ridhiwani Ngowi na Jacob Mang’wita.

Mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi  mawakili wa serikali Wakili wa Serikali,  Nassoro Katuga akisaidiwa na Tumaini Kweka, Hellen Moshi, Janethroza Kitali na Inspekta Jackson Chidunda,  walidai   kuwa Februari 15 mwaka huu katika eneo la Msimbazi Centre, Ilala Dar es Salaam, washitakiwa walipanga njama za kutenda kosa.
 
Alidai siku hiyo katika eneo hilo, walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kuandamana kwenda kwa Rais kulazimisha wapewe ajira katika utumishi wa umma, jambo ambalo ni kinyume cha sheria na lingesababisha uvunjifu wa amani. 

Walikana shitaka na upande wa jamhuri ukasema upelelezi bado haujakamilika na kwamba DPP amewasilisha hati ya kuwafungia dhamana na Hakimu Moshi akesema kwa Kuwa DPP amewasilisha hati hiyo Mahakama yake imefungwa mikono haiwezi kuwapatia dhamana hiyo akaamuru washitakiwa wote wapelekwe gerezani hadi Machi 6 itakapokuja kwaajili ya kutajwa.

Nyie vinara wa wahitimu wa Mafunzo ya JKT  Kuanzia   jana mnaitwa ' Wajelajela Gwaaa'. Mlichokuwa   mnakitafuta mmekipata tena haraka sana,hongereni.Kazaneni sana huko gerezani.Ajira za kumwaga Tanzania na atakae ajira na aje.

Mungu Ibariki Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Februali 25 Mwaka 2015.

No comments:

Powered by Blogger.