Header Ads

BIRTHDAY PARTY BENDI YA FM ACADEMIA AGOSTI 21






BIRTHDAY PARTY  BENDI YA  FM ACADEMIA  AGOSTI 21

Na Happiness Katabazi
BENDI ya FM Academia "Wazee wa Ngwasuma" , Agosti 21 Mwaka huu, itafanya sherehe  ya kukata na Shoka  ya kukumbuka kuanzishwa  kwake miaka 18 iliyopita.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi,  Mhasibu wa Bendi hiyo, Calvin Mkinga alisema sherehe hiyo ambayo imepewa jina la Birthday Party FM Academia Band ,itafanyika tarehe hiyo saa moja usiku Katika ukumbi wa Arcad House Mikocheni Dar Es Salaam, na kwamba Maandalizi yote yameishakamilika.

Mkinga alisema kiingilio ni Sh. 10,000 na kwamba siku hiyo ambayo itakuwa ni siku ya Ijumaa, wimbo mpya wa Dada wewe uliotungwa na mwanamuziki King Blaise ambao utaanza kupigwa kwenye redio mbalimbali leo utatambulishwa rasmi siku hiyo pamoja na nyimbo nyingine  na akawaomba mashabiki na wapenzi wa Bendi hiyo kujitokeza kwa Wingi ili waje kusherehekea pamoja sherehe hiyo ya kihistoria.

"FM Academia inajisikia  faraja sana kuona BendI hiyo inatimiza Miaka 18 kwasababu ni umri mkubwa na kuna baadhi ya bendi zilitamani zitimize umri hiyo zilishindwa na kufa mapema kwasababu ya kushindwa kuimiri Changamoto mbalimbali.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
8/8/2015.



No comments:

Powered by Blogger.