DK.GHARIB BILAL SITOKI CCM
DK.GHARIB BILAL  SITOKI  CCM
Na Happiness Katabazi
MAKAMU wa rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk.Mohammed Gharib Bilal amekanusha vikali taarifa za uzushi zinazosambazwa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa anakihama  Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na Mwandishi  wa habari hizi leo Katibu  wa Makamu wa Rais , Zahor Mohamed Haji  kwaniaba ya Dk.Bilal, alisema taarifa hizo ni za uongo na uzushi wa aina yake.
Zahoro alisema Dk.Bilal yupo nchini Uingereza Katika shughuli za Ujenzi wa taifa na wala Hana Mpango wa kuondoka CCM na wanaoeneza uzushi huo wanalao jambo.
Aidha Dk.Bilal alisema yupo imara na mwenye Siha njema   na kuwa hivi sasa anajiandaa  kushiriki kikamilifu kuzunguka Majimbo yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kumnadi  mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,  Dk. John Pombe Magufuli   kwa adhma ya kumsaidia Rais Jakaya Kikwete  aendelee kufanya kazi za kitaifa ili kukipatia CCM ushindi mnono  Katika uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25 Mwaka huu ili Chama hicho kikongwe liendelee kukamata dola.
 Itakumbukwa Kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia mitandao ya kijamii ilikuwa ikisambazwa  taarifa ya uzushi iliyokuwa ikisomeka Kama  ifuatavyo;
"Habari nilizozipata mida hii ni kuwa Makam wa Rais Mh Gharib Bilal kesho saa nne kwenye hoteli ya Serina atazungumza na vyombo vya habari na nyepesi yes I Ni kuwa ataachia nyazifa zake zote na kujiunga UKAWA baada ya kuchoshwa na uhuni Wa CCM.."
Chanzo: www.katabazihappy.blogspot.com
 

 
 
 
No comments:
Post a Comment