PROFESA ABDALLAH SAFARI
Na Happiness Katabazi
PROFESA SAFFARI ni Mbobezi,Mhadhiri wa Fani ya Sheria na Mwandishi wa vitabu vingi tu.
Nakushukuru Mzee wangu Profesa Safari kwakuikubali makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho , (RAIS AANZE KUREJESHA NYUMBA YAKE SERIKALINI) , iliyochapichwa na Gazeti la Tanzania Daima 13/3/2008.
Ambayo aliichukua na kutumia maudhui ya makala yangu hiyo katika ukurasa wa nne wa kitabu chako kiitwacho ( HAJA YA KUWA NA TUME HURU YA UCHAGUZI YA TAIFA TANZANIA).
Nimepata fursa ya kukisoma kitabu hicho chote chenye kurasa 34 ambacho alinipatia jana nilipomtembelea ofisini kwake Dar es Salaam na kubadilishana nae mawazo, nimejifunza mambo mengi.
Aidha kesho nitaanza kukisoma kitabu chake kingine kiitwacho (PROSECUTION AND DEFENCE OF CRIMINAL CASES).
Safari ambaye ni Profesa wa Sheria ni miongoni mwa wahadhiri wa chache nchini ambao wameandika na wanaendelea kuandika vitabu vingi nchini.
Amewahi andika kitabu ambacho kimetumika kufundishia shule ya msingi na sekondari na hivi sasa anaandika kamusi ya Lugha ya kisheria kwa kutumia lugha ya kiswahili pia anaandaa kitabu cha changamoto alizokutana nazo wakati akiwa wakili amenidokezea baadhi ya mambo aliyoyasema atayaweka kwakweli yatatufundisha sisi wanasheria wachanga.
Safari pia amewahi kuwa wakili wa serikali ,wakili wa kujitegemea ambaye ameendesha kesi nyingi maarufu nchini pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Diplomasia.
Jana nilifurahi sana nilivyofika ofisini kwake na kupiga nae stori nyingi sana za kisiasa,kisheria kwani wakati nilopokuwa Mwandishi wa habari katika magazeti,Mzee Safari tulikuwa tukikutana nae mahakamani anakuja kutetea wateja wake katika kesi mbalimbali na mimi nilikuwa nikienda mahakamani kuandika habari za mahakamani.
Mungu akupe maisha marefu Mzee wangu Profesa Abdallah Safari.
Ms.Happiness Katabazi ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi na Mwanasheria.
13/2/2018.
No comments:
Post a Comment